Rushwa ni zao la jamii yetu

Rushwa ni zao la jamii yetu

Right3

Senior Member
Joined
Aug 16, 2015
Posts
194
Reaction score
237
Rushwa inarudisha nyuma maendeleo kutokana na ukweli kwamba mali ambazo zingeweza kukuza uchumi wa taifa zinaishia kwenye mifuko ya watu au kuwapa wageni kwa makubaliano ambayo hayana faida kwa taifa.

Kuna rushwa kubwa na ndogo lakini zote zina madhara na ukiangalia sana wengi wetu tunapenda rushwa tunaweza kuwa wasafi leo kwa kua tu mirija ya rushwa haijatusogelea.

Kwa maoni yangu naona rushwa inatokana na sisi wanajamii wenyewe, kwa mfano;

1. Nikiwa nasoma Chuo nilienda field Ifakara kujifunza kwenye shirika moja lisilo la kiserikali. Siku hiyo tulikua tukienda field nikaonyeshwa mzee mmoja anapasua kuni kwenye gogo fulani nikaambiwa umemuona yule alikua OCD wa hapa alikua anapenda haki sana hakua mla rushwa hata kidogo, alikua mtu mzuri sana ila sasa yuko anaishi maisha ya kawaida anachekwa, maana nilikua nasimuliwa msimuliaji alikua kama anamsikitikia.

Nikajiuliza mimi kama mwanafunzi wa Chuo hichi kisa kinanifundisha nini?
Nikaona kumbe na mimi nikiwa mpenda haki, nisipokula rushwa nikiwa mtu mzuri kwa wanajamii wenzangu ntaishia kupasua magogo nikizeeka sio? Kwa kua mishahara kiukweli hata ya polisi ni midogo sana, nikasema loo hii ni kazi kweli kweli.

Je, ni mara ngapi jamii tumekua tukiwacheka watumishi wastaafu ambao hawakufuja pension wala mishahara isipokua mishahara yao ilikua midogo na matumizi ya muhimu kabisa yalikua mengi kuliko kipato?

Je, ni mara ngapi jamii tumekua tukiwasifia vijana ambao ndani ya miaka 2 ya ajira ana majumba na magari ilhali tukifahamu mshahara wake hauwezi kukidhi kufanya hayo na kuwasema vijana ambao either ni waadirifu au kazi zao hazina mirija ya kupata pesa zisizo halali?

Ni mara ngapi tunekua tukiwasifia wanasiasa fulani kuwa wana ukwasi sio mchezo ilhali hawana vyanzo vinavyoelezeka kusupport ukwasi huo?

Ikitokea mimi na wewe tumepata nafasi ambayo inatoa mwanya wa kuchukua chako mapema na kukufanya usijekupasua magogo hatutachukua mzigo kweli?

Tuko na kazi ngumu kwenye kuitokomeza rushwa kwani hata jamii zetu zinachangia wanajamii tusiwe waafirifu.
 
Rushwa imekuwa ni sehemu ya utamaduni wa nchi hii. Haitishi, haishangazi wala haikeri tena, watanzania wameshakubaliana nayo (Customarily endorsed). Kilichobakia kwenye jamii hii ni kugombaniana nafasi za kula rushwa.

Kuna ofisi fulani nishawahi kufika, kila niliyemkuta alianza kuuliza wewe umeletwa na nani huku. Wakishangaa nimefikaje mle ndani bila mkono wa mdhamini (godfather) maana mle ndani zaidi ya asilimia 85% walikuwa wamepelekwa kwa kupitia vimemo.

Taifa la aina hii linaweza kufika mbali kweli ?
Taifa la Connection...
 
Mfumo mbovu wa CCM hata umlete Biden hawezi kufanya chochote, CCM ipo kwenye damu ndani ya CCM
 
Rushwa hailrudishi maendeleo nyuma. Zaidi zaidi inaweza hata kuyasongesha mbele. Labda useme ni adui wa haki.
 
Rushwa inarudisha nyuma maendeleo kutokana na ukweli kwamba mali ambazo zingeweza kukuza uchumi wa taifa zinaishia kwenye mifuko ya watu au kuwapa wageni kwa makubaliano ambayo hayana faida kwa taifa.

Kuna rushwa kubwa na ndogo lakini zote zina madhara na ukiangalia sana wengi wetu tunapenda rushwa tunaweza kuwa wasafi leo kwa kua tu mirija ya rushwa haijatusogelea.

Kwa maoni yangu naona rushwa inatokana na sisi wanajamii wenyewe, kwa mfano;

1. Nikiwa nasoma Chuo nilienda field Ifakara kujifunza kwenye shirika moja lisilo la kiserikali. Siku hiyo tulikua tukienda field nikaonyeshwa mzee mmoja anapasua kuni kwenye gogo fulani nikaambiwa umemuona yule alikua OCD wa hapa alikua anapenda haki sana hakua mla rushwa hata kidogo, alikua mtu mzuri sana ila sasa yuko anaishi maisha ya kawaida anachekwa, maana nilikua nasimuliwa msimuliaji alikua kama anamsikitikia.

Nikajiuliza mimi kama mwanafunzi wa Chuo hichi kisa kinanifundisha nini?
Nikaona kumbe na mimi nikiwa mpenda haki, nisipokula rushwa nikiwa mtu mzuri kwa wanajamii wenzangu ntaishia kupasua magogo nikizeeka sio? Kwa kua mishahara kiukweli hata ya polisi ni midogo sana, nikasema loo hii ni kazi kweli kweli.

Je, ni mara ngapi jamii tumekua tukiwacheka watumishi wastaafu ambao hawakufuja pension wala mishahara isipokua mishahara yao ilikua midogo na matumizi ya muhimu kabisa yalikua mengi kuliko kipato?

Je, ni mara ngapi jamii tumekua tukiwasifia vijana ambao ndani ya miaka 2 ya ajira ana majumba na magari ilhali tukifahamu mshahara wake hauwezi kukidhi kufanya hayo na kuwasema vijana ambao either ni waadirifu au kazi zao hazina mirija ya kupata pesa zisizo halali?

Ni mara ngapi tunekua tukiwasifia wanasiasa fulani kuwa wana ukwasi sio mchezo ilhali hawana vyanzo vinavyoelezeka kusupport ukwasi huo?

Ikitokea mimi na wewe tumepata nafasi ambayo inatoa mwanya wa kuchukua chako mapema na kukufanya usijekupasua magogo hatutachukua mzigo kweli?

Tuko na kazi ngumu kwenye kuitokomeza rushwa kwani hata jamii zetu zinachangia wanajamii tusiwe waafirifu.
Rushwa ni adui wa haki CCM wanapenda rushwa.
 
Back
Top Bottom