Rushwa na uraia wa Siyoi, CCM watafutana uchawi badala ya kujibu HOJA

Nina marafiki zangu wameoa wazungu na wakati wa kukaribia kujifungua wamekimblkia kujifungua nje kwa mwanamke ili kupata uraia wa kule hapa unanisaidiaje kuelewa Paulss?

Nina imani Paulss anajua vyema how it is. Ni vijimambo vya propaganda tu katika kuhakikisha angalau tunakufa kiume. Uk4zaliwa nchi za watu ujue unakuwa wa huko na ukitaka kuwa siyo wa huko ukifjkisha eighteen ujue una jukumu la kuukana ule wa kule. Vinginevyo ndo haya yanatokea. Tena dogo ana pass mbili kama wahindi wetu. Duh!
 
Nina imani Paulss anajua vyema how it is. Ni vijimambo vya propaganda tu katika kuhakikisha angalau tunakufa kiume. Uk4zaliwa nchi za watu ujue unakuwa wa huko na ukitaka kuwa siyo wa huko ukifjkisha eighteen ujue una jukumu la kuukana ule wa kule. Vinginevyo ndo haya yanatokea. Tena dogo ana pass mbili kama wahindi wetu. Duh!

Hivi ni kweli Siyoi ana pass ya Kenya?. Kama anayo basi Section 14, ya sheria ya uraia inamuondoa, wala hakuna mabishano kama siasa haitatumika. This is a section

(14). The Minister may by order deprive any person, other than a person who is a citizen by birth, of his citizenship of the United Republic if the Minister is satisfied that person has at any time while a citizen of the United Republic and of full age and capacity voluntarily claimed and exercised, in a foreign country, any right available to him under the law of that country, being a right accorded exclusively to its own citizens, and that it is not conducive to the public good that he should continue' to be a citizen of the United Republic.
 
@mtanzania1989, Uraia wa Tanzania hutolewa bila kuangalia kama nchi alikozaliwa mhusika imempa uraia au la. Kwa mfano kama wewe ni Mtanzania na ukamzaa mtoto wako ukiwa Kenya, kwa Tanzania huyo mtoto atahesabika kuwa na uraia wa nchi mbili - Kenya & Tanzania. Kama Kenya watampa mwanao sabuni, au kalamu, au uraia, au maziwa hayo yanaishia huko huko Kenya. Hayana uhusiani wowote na Tanzania. Na mwanao huyo atahesabika kuwa raia wa Tanzania hadi atakapofikisha miaka 18. Baada ya hapo kama anataka kuendelea kuhesabika kama raia wa Tanzania atalazimika kula kiapo cha utii kuukana uraia wa huko alikozaliwa.

Sasa kama nchi alikozaliwa haitoi uraia automatically e.g. Kenya basi ni jukumu la huyo mhusika kutoa UTHIBITHO unaoeleza kuwa hakuwahi kupata uraia kule alikozaliwa. Kumbuka uraia wa Tanzania hautolewi kufuatana na sheria za Kenya.

Kwa kifupi mtu aliyezaliwa nje ya mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (wazazi ni watanzania) na akata kuendelea na uraia wake wa Tanzania baada ya kufikisha miaka 18 basi mtu huyo anatakiwa ama kuukana uraia wa huko alikozaliwa au KUTHIBITISHA kuwa hakuwahi kuwa na uraia wa nchi nyingine (i.e huko alikozaliwa).

Kwa issue ya Sioi alichotakiwa kufanya ni kuleta uthibitisho kuwa hakuwahi kuwa na uraia wa KENYA kwa sababu Kenya hawatoi uraia automatically. Na uthibitisho haimaanishi kuwa mhusika 'atamsimulia' bwana uhamiaji kuwa Kenya hawatoi uraia automatically. Huwezi ku-file hadhithi, hivyo alitakiwa awe na barua toka sehemu inayotambulika kisheria.

Hata hivyo niseme, hii issue ya Sioi inanipa tabu sana. Hiivi ni kweli CCM hawakuona hili? Ile kamati nzito CC hawakuona umuhimu wake? Hata kama watalitatua sasa hivi lakini tayari huyu kijana wameshamchafulia image yake. Au ndio mambo ya kuviziana huko ccm?

Nashukuru kwa ufafanuzi,naomba msaada wa kunifafanulia hili.Iwapo wazazi wa wazazi wako wote wa 2 hawakuwahi kuwa raia wa Tz na walifika TZ kwa VITA KUU ya 2 ya DUNIA,na wakazaliwa wazazi wako hapa Tz kisha ukazaliwa wewe je kuna haja ya KUUKANA URAIA wa nchi ya asili ya babu yako?Ndo uwe raia usiye na UTATA Tz? pls help
 
Ngoja tuone. Mimi nazungumza nikiwa field. Sizioni hizo kura za chadema. Kati ya chaguzi ndogo rahisi ktk kipindi hiki ukiondoa uzini naona ni Arumeru. Hapa naomba slaa apewe usimamizi wa uchaguzi, mbowe awe msimamizi msaidizi, wabunge wote wa chadema wawe wasimamizi kwenye kata, na polisi wote waondoke.

Thubutu! Mwigulu acha utoto, huyo Sioi mwenyewe kama angekuwa mgombea wa Chadema, saa hizi kishatupiliwa mbali. Dunia gani uliwahi kumwona mgombea Uraisi akiteremshwa jukwaani eti na polisi, kwa wenzetu ukishateuliwa rasmi kuwa mgombea wa Uraisi unalindwa kama yai, protocol zote ndani!
 
Tumesema toka mwanzo kwamba Siyao ni Mtanzania na sasa Uhamiaji wamepigilia nyundo.

"Akizungumza na gazeti dada la The Citizen kwa simu kutoka Dar es Salaam jana, Kamishna Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Magnus Ulungi alisema haoni tatizo lolote kuhusu uraia wa Sioi.

Alisema ni kweli kwamba alizaliwa Kenya lakini hiyo haimuondolei haki ya kuwa Mtanzania, wala hana haja ya kuukana uraia wa Kenya ambao hakuwahi kuwa nao.

"Wasichofahamu hao waliotoa pingamizi kwa Sumari ni Sheria ya Uhamiaji. Iko wazi kwamba mtoto aliyezaliwa na wazazi wote Watanzania ana fursa ya kupata uraia wa kurithi kutoka kwa wazazi wake…. hatakiwi kukana uraia ambao hakuwa nao," alisema Ulungi." Kutoka gazeti la mwananchi.
 
Nashukuru kwa ufafanuzi,naomba msaada wa kunifafanulia hili.Iwapo wazazi wa wazazi wako wote wa 2 hawakuwahi kuwa raia wa Tz na walifika TZ kwa VITA KUU ya 2 ya DUNIA,na wakazaliwa wazazi wako hapa Tz kisha ukazaliwa wewe je kuna haja ya KUUKANA URAIA wa nchi ya asili ya babu yako?Ndo uwe raia usiye na UTATA Tz? pls help
Mkuu,

Mimi sio mwanasheria kwahiyo mawazo yangu ni ya jinsi ninavyozielewa sheria kwa juu juu tu.

Kama wazazi wako walizaliwa Tanzania kabla ya siku ya uhuru yaani 9/12/1961 na babu zako huko walikotoka lilikuwa koloni la Mwingereza, basi wazazi wako walikuwa ni Watanzania na wewe hutakiwi kuukana uraia mwingine wowote.

Ila kama babu zako walitoka nchi ambayo haikuwa koloni la Uingereza, hapo kunaweza kuwa na issue. Ushauri wangu ni kwamba waone wanasheria au Uhamiaji.

Wakati mwingine njia rahisi ni wewe kula kiapo cha kuukana uraia wa nchi nyingine yeyote ambayo wewe huijui.
 
Tumesema toka mwanzo kwamba Siyao ni Mtanzania na sasa Uhamiaji wamepigilia nyundo.

"Akizungumza na gazeti dada la The Citizen kwa simu kutoka Dar es Salaam jana, Kamishna Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Magnus Ulungi alisema haoni tatizo lolote kuhusu uraia wa Sioi.

Alisema ni kweli kwamba alizaliwa Kenya lakini hiyo haimuondolei haki ya kuwa Mtanzania, wala hana haja ya kuukana uraia wa Kenya ambao hakuwahi kuwa nao.

“Wasichofahamu hao waliotoa pingamizi kwa Sumari ni Sheria ya Uhamiaji. Iko wazi kwamba mtoto aliyezaliwa na wazazi wote Watanzania ana fursa ya kupata uraia wa kurithi kutoka kwa wazazi wake…. hatakiwi kukana uraia ambao hakuwa nao,” alisema Ulungi." Kutoka gazeti la mwananchi.

Mwanzo Ofisa Uhamiaji Mkoa alisema kwa kuwa alikua akiwasilisha kwa CCM, now Kamishna Mkuu anajibu kwa niaba ya CCM, hii ndio Tanzania na hicho ndio chama tawala. Wao ndio wanaamua chekundu kiwe cheusi kwa maslahi yao. Tafsiri ya sheria haifanywi na Kamishna Mkuu bali Mahakama. Let's wait and see. Ila naona hapa mjadala mkuu ni "uraia" issue ya RUSHWA inaonekana kama jambo halali kabisa, hata hao Chadema wamekaa kimya, hawalijadili na hata katika uzinduzi walizungumzia fedha halali za mkutano wa kura za maoni, hawajazungumzia mamilioni ya fedha zilizogawiwa kwa rushwa na hata PCCB kuwakamata wahusika na Sms zenye kuelekeza wapi na vipi watumie fedha. Hii ndio Tanzania, iko siku tutahukumiwa na HISTORIA, tuombe UHAI.
 
Ofisa Uhamiaji alijua kabisa matumizi ya barua yake na alichoandika si siri maana ukiingia katika mtandao hapa Legislation Tanzania (Lexadin) utaziona sheria zote ikiwamo ya uraia ambayo ameinukuu. Haihitaji taaluma ya juu sana kusoma na kuelewa hicho kifungu. Inavyotakiwa hata Chadema wangemwandikia huyo Ofisa Uhamiaji angetakiwa awajibu kama alivyowajibu CCM na kama ambavyo angewajibu waandishi wa habari watakaomuuliza.
Halisi,
Afisa uhamiaji alitoa opinion yake kwa RC. Hiyo barua ilitakiwa iishie hapo. Huko kwenye vikao vya CCM huyo RC angeenda yeye na maelezo aliyoyapata kutoka idara ya uhamiaji, full stop.

Hii ya kupeleka siri za serikali kwenye vikao vya vyama vya siasa ni makosa.

Katika hiyo barua ya huyo ofisa kuna makosa mengi ya utendaji na tafsiri ya sheria. kwa kuianika nje tayari imefanya tafsiri yake iwe tofauti na tafsiri ya mkuu wake wa uhamiaji. Lakini laiti hiyo barua ingebaki ofisini kwa RC haya mambo yote yasingelitokea.

Pia katika hiyo barua huyo ofisa anaongelea sheria in generic terms, hivyo hakutakiwa kuweka jina la Siyoi kwenye hiyo barua. Ukiongelea hypothesis huwezi kuweka jina la mtu maana unakuwa huna facts za kuhalalisha hilo. Kama alitaka kuongelea case ya Siyoi ilitakiwa aombe file lake au alichukue kama liko pale Arusha na kisha ndio aandike hiyo barua in specific terms ikimhusu Siyoi.

Tuna safari ndefu sana kwenye kurekebisha utendaji wa hawa maofisa wetu.

Argument yangu bado ni ile ile huwezi kupambana na uvunjaji wa sheria kwa kuvunja sheria, two evils don't make right. Watanzania wengi hatuna umakini wa kuheshimu sheria zetu na hapo ndipo tatizo linapoanzia. Ndio maana unakuta viongozi wengi tu wanaona ni OK tu kupeperusha siri za serikali kwenye mikutano ya kisiasa na wananchi pamoja na waandishi wa habari tunawashangilia bila kujua madhara yake.
 
Naomba nisitie neno!! Tafsiri ya Kamishna Mkuu, naona inamhusu Siyoi na vigogo wa CCM pekee, maana nina ushahidi wa mamilioni ya watu waliokosa haki yao kwa kuzaliwa nje na kushindwa kuukana uraia wa nchi walikozaliwa ikiwamo Kenya na mmoja namfahamu alinyang'anywa hadi paspoti na hadi sasa anasubiri maombi ya uraia na anaishi kwa kulipia hati ya ukaazi
 
People born outside the United Republic on or after Union Day
6. Every person born outside the United Republic on or after Union
Day shall, with effect from the date of his birth, be deemed to have
become and to have continued to be, and with affect from the commencement
of this Act shall become and continue to be, a citizen of the United Republic
if at the date of his birth his father or mother is or was a citizen Republic on
or after Union of the United Republic otherwise than by descent, subject to the provisions of section 30.

Cessation of dual citizenship
7(1) Any person who, upon the attainment of the age of eighteen
years, is a citizen of the United Republic or was a citizen of the former
Republic of Tanganyika or of the former People's Republic of Zanzibar
and also is or was a citizen of some country other than the United
Republic or either the former Republic of Tanganyika or the former
People's Republic of Zanzibar shall, subject to the provisions of subsection
(8), be deemed to have ceased to be a citizen of the United Republic
upon the specified date unless he previously renounced his citizenship
of that other country, taken tile oath of allegiance and, in the case of
a citizen by descent, made and registered the declaration prescribed by
Parliament regarding his intention as to residence.

Hiyo sheria, inatafsiriwa kulingana na mhusika na wakati. Sitii neno, hii ndiyo Tanzania yetu. Tusubiri.
 
Mkuu Kiranga Sioi sio Mkenya...........period
Unaweza kuwa sahihi kusema sio raia wa Tanzania lakini hii haimaanishi ni raia wa Kenya kwakuwa kazaliwa Kenya


Kwamba ni au si Mkenya is a side detail that has little material concerning his eligibility. Our law does not base eligibility on whether one is or is not Kenyan. I was merely giving an account that is in circulation which can be true or not.

To us, and to the legal eligibility concern, it does not matter whether he is Canadian or Kenyan.

What matters is that he is not Tanzanian according to Tanzanian law.

Sasa kama yeye ni Android, Borg au Klingon hilo swala jingine.
 
Mkuu Kiranga Sioi sio Mkenya...........period
Unaweza kuwa sahihi kusema sio raia wa Tanzania lakini hii haimaanishi ni raia wa Kenya kwakuwa kazaliwa Kenya


by mtayeshelwa Nimekuelewa kaka kwa ufafanuzi wako mzuri,CCM wasingekuwa wajinga kiasi hicho kumpitisha mtu asiyekuwa raia kuwa mgombea wao
 
Naomba nisitie neno!! Tafsiri ya Kamishna Mkuu, naona inamhusu Siyoi na vigogo wa CCM pekee, maana nina ushahidi wa mamilioni ya watu waliokosa haki yao kwa kuzaliwa nje na kushindwa kuukana uraia wa nchi walikozaliwa ikiwamo Kenya na mmoja namfahamu alinyang'anywa hadi paspoti na hadi sasa anasubiri maombi ya uraia na anaishi kwa kulipia hati ya ukaazi
Mkuu Halisi,
Mifano ya watu hao unaosema unawajua ndio hasa tunaitaka hapa ili kuweka kila kitu wazi. Mimi nawajua watu wengi sana wenye status kama ya Siyoi na wote ni Watanzania na hawajawahi kukataliwa huduma yoyote ya Tanzania.

Kule kwetu mipakani Kyela, cases kama hizi ziko nyingi tu na sijawahi kuona mtu ambaye kanyimwa uraia au kanyangánywa uraia ambaye ana status kama ya Siyoi. Kama mwenzetu kuna watu unawajua basi lete mfano hata mmoja hapa na tuujadili.

Hili suala hata ukienda kwenye suala la Bashe tulilijadili hivi hivi kama linavyojadiliwa hapa.

Hata hivyo vifungu viwili vya citizen act 1995 ulivyotoa vimejadiliwa mno hapa. Hakuna mahali popote wanapoelezea mtu aliyezaliwa na wazazi wawili ambao wote ni Watanzania. Kwanini watunga sheria hawakuweka hiyo option? Kwa tafsiri yangu binafsi nafikiri waliona hilo ni no brainer, ukizaliwa na wazazi wote wawili ambao ni Watanzania wewe ni mtanzania unless otherwise umechukua au umepewa uraia wa nchi nyingine.

Binafsi ningependa kujua Mtanzania yeyote ambaye kaambiwa kuwa sio Mtanzania mwenye status kama ya Siyoi.
 
Kwamba ni au si Mkenya is a side detail that has little material concerning his eligibility. Our law does not base eligibility on whether one is or is not Kenyan. I was merely giving an account that is in circulation which can be true or not.

To us, and to the legal eligibility concern, it does not matter whether he is Canadian or Kenyan.

What matters is that he is not Tanzanian according to Tanzanian law.

Sasa kama yeye ni Android, Borg au Klingon hilo swala jingine.
Sina matatizo na opinion yako kuwa Sioi sio Mtanzania isipokuwa nilikuwa naweka sawa sentensi ya mwisho kwenye bandiko lako..... that's all mkuu
Hata hivyo ni kifungu gani kuhusu kuzaliwa nje kinasema wazazi wote wawili wakiwa watanzania pia anakuwa sio raia?
Soma hapa

http://www.vijanatz.com:81/governan...ajnisi-katika-jamhuri-ya-muungano-wa-tanzania

Habari ni kwamba Sioi kazaliwa Kenya na hajaukana uraia wa Kenya alipotimiza miaka 18, hivyo ni Mkenya.
 
Back
Top Bottom