Tanesco ni janga!! Ukifatilia utendaji wa Tanesco, ndio utajua kwa nini?! nchi yetu tunapiga hatua kwa mwendo wa kobe linapokuja suala la maendeleo!
Ni jambo la kusikitisha,!! Unapewa control number unaenda kulipia pesa nyingi tu! kwa ajili ya kuwekewa umeme, shirika wanakueleza kuwa watakuja kukuwekea umeme ndani ya siku sitini za kazi,hizo siku walizokuaidi zinaisha!! bila kuja kumuunganishia mteja umeme!!! Hawatoi taarifa yeyote kwa mteja kumfahamisha kama kuna tatizo lolote, mteja anakaa zaidi ya miezi mitano, bila kuunganishiwa umeme, na hakuna taarifa yeyote na pesa wameshachukua!!!
Shirika linajiendesha kijima sana, ukimsikiliza waziri anavyoongea kwenye vyombo vya habari unabaki unasikitika tu, majigambo mengi, takwimu nyingi ila kwenye ground ni zero kabisa,kama hapa dsm kumuunganishia mteja umeme mnashindwa uko vijijini si ndio aibu tupu?!! Imagine upo mjini miezi mitano huna umeme na umeshalipia, ni mateso. Ukifatilia wanaishia kuchukua number zako za simu na mtaa uliopo basi!hakuna feedback yeyote, hizo pesa mnazotoza watu wakati uwezo wa kusambaza umeme hawana!! Kwanini wasiweke utaratibu kuwa wakiwa tiyali kumuunganishia mtu umeme ndio alipie, kuliko kuchukua pesa ya mtu wanakaa nazo zaidi ya miezi mitano!! Mtu akiamua kuziweka kwenye mzunguko wake wa biashara zingemsaidia, kuliko huu unyang'anyi wanaoendelea kuutumia kupokea pesa za watu ilhali uwezo wa kuunganisha umeme hawana!! Shirika linajiendesha kijima sana, sijui kama lina afsa anaeshughulika na biashara, hio miezi mitano kwa hesabu za kawaida kama wangekuwa wamemuunganisha mtu uyu umeme kwa haraka, iyo miezi mitano angekuwa ametumia umeme kiasi kikubwa ameingizia shirika pesa na pia angekuwa amelipia tozo mbalimbali za serikali kupitia umeme ambao angekuwa ananunua kila mara!!
Shirika linatia aibu sana!! Hii inaonyesha ni jinsi gani watu waliopewa dhamana kuongoza shirika, wamelala usingizi wa pono!! Hakuna uwajibikaji, ukitaka huduma kwa haraka lazima utoe rushwa, ndio wakufanyie kwa haraka!! Ili ni tatizo usipotoa rushwa utasota kwenye giza mpaka ujute!! Ifike mahali mashirika kama haya wapewe wazungu, ili watufundishe namna ya kufanya kazi kwa weredi bila longo longo za sisi watanzania.