Hayo mambo unayoyasema ya mara kupotea mara ukiweka chini ukaweka bakuli ya maji juu coins zinaelea na kurushwa wewe ulionaje wakati unasema haujaigusa?!!! Au ulisimuliwa na huyo kaka yako aliyeruka akili? Haya mambo yana conspiracy nyingi sana ambazo ni ngumu kuconfirm, btw kuna mtu mmoja namfahamu na yeye kutwa kucha kutafuta hayo mapasi na mabirika, kama kweli ndugu zako wanavyo niwaelekeze kwa huyo mtu, kama atakagua nakuona ni vyenyewe wataelewana, lakini angalau wangekuwa wanapiga picha nikimwonesha picha anaweza kuwafuta hukohuko.
Sema sasa, isijekuwa na wewe umeskiza stori tu!
sawa nimekuelewa kwan ukitazama lazima ushike? mm nilizishika zile nyngne za kawaida tu hiyo nyingne awakuniruhusu kabisa kutokana na iman yao inaweza kupotea. kwa kweli ni mda kidogo toka nimeziona had sasa ilikuwa 2011 na sikuwa na sim ya kupiga picha. Ila kitu kinachowafanya washindwe kujitangaza ni kwamba serikal inadai kugawana pasu pasu sasa ndo icho kinachowafanya waogope au wanaweza kutapelewa na watu ambao wapo kwenye system. Sikuwa na interest kabisa na vile nilivyoona. Mm naweza kukuelekeza hawa jamaa walipo sasa hiv huyo mtu kama anatafuta akiulizia hayo maeneo hatawapata tu sawa.
kuna mtu ameniambia nimtafutie hiyo hela ya Rupia yenye picha ya simba na akaniahidi hela nyingi endapo nitafanikiwa kuipata inafanya kazi gani hasa kwa mwenye kuelewa asisite kufunguka kuhusu Rupia ya kijerumani.
It always ends like that! Poa, jumapili njema kaka.
Hawa watafutaji wa rupia akili zao ni kama haziko sawa. Watakwambia story nyingi za kuvutia ila mwisho wa siku hawajui hata wanachokifanya.
Mimi Mtu ananieleza habari ya kutajirika na rupia namwona kama mwendawazimu flani.
Kumbe na wewe umeona mkuu, maelezo yao lazima yajichanganye! Mara eti nikitangaza serikali itataka pasu...utafikiri wamekuta tani nane za dhahanu..lol!
kashakutana na watoto wa mjini wanataka kumuweka sawa,wakimkosa kwenye Rupia watampa deal la Mercury,mjini hapa shauri yako!Mwambie Washawasha
It always ends like that! Poa, jumapili njema kaka.
nimecheka sana mkuu hakuna rupeeee wala nn ni ujinga tu
Alafu hao wanao comment maneno ya wenzao mbona Humu sion wamesema nn? Au ndo bas tu ile ukanushe tu!!? kwel shida sana hawa watu.
Hii mada nimeisoma soma bahadh ya maneno ya watu. Ila kiukwel tanzania kuna sehem kuna maajabu sana jaman msibishe vitu ambavyo ujaviona. Mbeya chuo cha magereza pale kuna miujiza mingi sana pale kwenye mto kiwira sehem ya kijungu na lake ngoz tukuyu ambapo wanadai rupia zipo ila uwez kuthubutu kuingia panatisha sana.
Hiv vitu vipo sana me nimfanyakaz wa kampun moja hapa Tanzania na kaz yangu kubwa nikufanya tasmin sehem mbal mbal ambako miundo mbinu inatazamiwa kupelekwa.
Ki ukwel nimejionea mambo ya ajabu sana na kuna sehemu uwezi kufika bila kuongea na wazee wa kijiji. Mojawapo ni sehem ambapo inasadikika hizo rupia zipo ni sehem nying ambazo jamaa wa nyuma wametaja mbeya, iringa, smbwanga, tabora nk.
Kama kuna mwenyeji wa iringa anaweza kuwa shaidi yangu juu ya yale makabur ambayo yalisumbua sana pale Isimila had kuja ya kuyatoa kujenga hii bara bara mpya. Inasemekana vijana walio bomoa yale makabur wote hayupo hata mmoja.
Kw wale ambao mnatafuta utajir wa rupia achen watu wanakufa sana kila nakoenda unasikia kuna mtu alijaribu kwenda akafarik.
Tufanye kaz tuachane na hizi habar za rupia tulidhike na kile ambacho Mungu ametupa. Anayetafuta rupia ni sawa na anayetafuta uganga.