Rungwe FM imewadia karibuni kusanyiko kubwa

Rungwe FM imewadia karibuni kusanyiko kubwa

Joined
Mar 5, 2012
Posts
90
Reaction score
23
RUNGWE IZIDI KUSONGA MBELE…..UJIO WA REDIO RUNGWE FM
Napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru wote mliondelendelea kutoa maoni yenu kuhuru siku maalumu kwa wana-Rungwe, ndugu zetu wasiotoka Rungwe na Watanzania wote kwa ujumla. Siku yetu kubwa ya wana-Rungwe sasa imewadia. Itafanyika Landmark Hotel-Ibungila Hall(kutokana na sababu za kiufundi-Haitakuwa Diamond Jubilee kama ilivyokusudiwa)…..ITAFANYIKA JUMAPILI, TAREHE 25 MEI, 2014…KUANZIA SAA NANE MCHANA. Kutakuwa na burudani za Injili, za asili ya Unyakyusani, vyakula vya asili ya Kinyakyusa(Kifuge, ilyombo, amasimbi, ingati, nk). Tunategemea kuwa na Viongozi wa dini mbalimbali, ikiwepo watu kama Dr. Alex Malasusa, Askofu Mwakafwila, Mwl. Christopher Mwakasege, Wabunge Prof. Mwakyusa…….Prof. Mwandosya, Dr. Mwakyembe nk….Mkuu wa wilaya ya Rungwe Ndg. Chrispin Meela nk… Wote mnakaribishwa…Pamoja na mambo mengine, siku hii itatumika KUENDESHA HARAMBEE YA UCHANGIAJI WA REDIO RUNGWE FM…….Redio ya kijamii inayolenga kuinua maendeleo ya wilaya ya Rungwe na Tanzania kwa ujumla…. Rungwe ni Wilaya ya pili kuanzishwa nchini. Kwa bahati mbaya mpaka sasa hina Redio ya jamii. Hii hatua itasaidia kuendeleza wilaya yetu, na kutangaza mambo mbalimbali kama vile utalii na fursa mbalimbali zilizomo ndani ya Wilaya ya Rungwe na maeneo jirani…… KADI ZIMEANDALIWA NA KIWANGO CHA CHINI NI LAKI MOJA TU(100,000). KARIBUNI SANA SANA. UCHANGIAJI WA UANZISHWAJI REDIO RUNGWE FM
AKAUNTI! 038201043087; BENKI-NBC-JINA LA AKUNTI-TUKUYU CHRISTIAN FELLOWSHIP
TIGOPESA-0715 441728
MPESA NI 0765 605371

KWA MAWASILIANO ZAIDI
Christopher Andendekisye -Mwenyekiti Kamati-
Daniel Mwamwaja - Mlezi-
Maria Abel - Katibu….0682260435
Joseph Mwakisyala -Katibu Msaidizi- 0656 002540
 
Back
Top Bottom