Choka fulani lakini si choka mbaya, let alone choka hatari, mi nilifikiri nitakuta mbavu za mbwa hivi.
Maana kuna Choka, Choka Fulani, Choka Mbaya, Choka Hatari na mwisho kabisa huko inakuwa si choka tena kuna Kufa Mtu. Hizo ndizo SI Units za nyumba mbovu kwa mujibu wa redio mbao.
Sasa hii Choka Fulani.
Mara nyingine kuwa na ofisi kama hizi zisizopita uwezo wa wananchi kwa sana ni poa tu, si unaona ofisi haina tofauti sana na nyumba za wananchi zilizo karibu hapo?
Sio mnajenga mkanisa mkuuubwa kama wa Yamoussoukrou unalipita mpaka Basilica la Rome, au kasri kubwa kama la Mzee Mobutu Gbadolite, halafu jirani wananchi wanaishi katika mbavu za mbwa na paa za nyasi.