Rukwa: Mwajiri achinjwa akidaiwa mshahara

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Fundi makenika wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa, Cathbert Mwangalaba (47) ameuawa kwa kukatwa mwili wake na kiwiliwili chake, kutenganishwa na kichwa na kitu chenye ncha kali.

Mlinzi ambaye alikuwa ameajiriwa na marehemu anadaiwa kumuua mwajiri wake huyo kwa kumchinja na kiwiliwili chake kutenganishwa na shingo yake.

Anatuhumiwa kutenda ukatili huo, baada ya bosi wake huyo kushindwa kumlipa mshahara wa miezi sita unaofikia Sh 360,000.

Baada ya kumuua, mwili wake ulifukiwa katika shimo lililochimbwa shambani mwake katika Kijiji cha Kaondo Manispaa ya Sumbawanga.

Mlinzi huyo alikuwa akilinda shamba la marehemu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Justine Masonje alithibitisha matukio hayo. Alisema kwamba mauaji ya kikatili ya Mwangalaba, yanadaiwa kufanyika saa 3:00 asubuhi Januari 17, mwaka huu shambani mwake kijijini Kanondo.

Mwili wa marehemu ulibainika ukiwa umeviringishwa katika mfuko wa sandarusi, ukiwa umefukiwa katika shimo lililo ndani ya uzio wa shamba hilo.

Baada ya kuchunguzwa, mwili ulibainika kuwa na majeraha ya kukatwa na kitu chenye ncha kali. Shingo, miguu na kiwiliwili vilikuwa vimetenganishwa.

Mwili wa marehemu uligundulika majira ya saa 11:30 jioni, baada ya ndugu wa marehemu kulitilia shaka shimo ambalo lilikuwa limefukiwa.

“Mtuhumiwa amekamatwa na atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi.

Chanzo: Habari Leo
 
Dah ivi mtu anaanzaje kukata kichwa aisee mimi hata nikinunua nyama buchani kukata siwezi
 
Nafwaaa...ninadaiwa...hivi kitu chenye ncha kali kipoje kimuonekano yaani mapema nichukue tahadhari...kinashukiwa na kutuhumiwa kuleta madhara mengi sana katika jamii...

Everyday is Saturday...........:cool:
 
ni vile si ndugu yako wala huna ukaribu nae basi una toa maoni kama umekatika kichwa

ivi laki 3 na nusu ndo uchukue uhai wa mtu, ili hali ana wategemezi. aya anaenda ishia jera iyo hela kaipata sasa
6 months humpi mtu mshahara wake na bado anakufanyia kazi !!!!...

Sikubaliani na alilofanya lakini kama ni kweli bhasi boss nae hakuwa fair. R.I.P boss
 
inatokea mkuu, sema nahisi marehemu itakuwa alimjibu jamaa vby
 
Fundi makenika wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa, Cathbert Mwangalaba (47) ameuawa kwa kukatwa mwili wake na kiwiliwili chake, kutenganishwa na kichwa na kitu chenye ncha kali.

Mlinzi ambaye alikuwa ameajiriwa na marehemu anadaiwa kumuua mwajiri wake huyo kwa kumchinja na kiwiliwili chake kutenganishwa na shingo yake.

Anatuhumiwa kutenda ukatili huo, baada ya bosi wake huyo kushindwa kumlipa mshahara wa miezi sita unaofikia Sh 360,000.

Baada ya kumuua, mwili wake ulifukiwa katika shimo lililochimbwa shambani mwake katika Kijiji cha Kaondo Manispaa ya Sumbawanga.

Mlinzi huyo alikuwa akilinda shamba la marehemu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Justine Masonje alithibitisha matukio hayo. Alisema kwamba mauaji ya kikatili ya Mwangalaba, yanadaiwa kufanyika saa 3:00 asubuhi Januari 17, mwaka huu shambani mwake kijijini Kanondo.

Mwili wa marehemu ulibainika ukiwa umeviringishwa katika mfuko wa sandarusi, ukiwa umefukiwa katika shimo lililo ndani ya uzio wa shamba hilo.

Baada ya kuchunguzwa, mwili ulibainika kuwa na majeraha ya kukatwa na kitu chenye ncha kali. Shingo, miguu na kiwiliwili vilikuwa vimetenganishwa.

Mwili wa marehemu uligundulika majira ya saa 11:30 jioni, baada ya ndugu wa marehemu kulitilia shaka shimo ambalo lilikuwa limefukiwa.

“Mtuhumiwa amekamatwa na atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi.

Chanzo: Habari Leo
Sasa kama huna hata uwezo wa kulipa TZS 60,000 kwa mwezi unaajiri mlizi wa kulinda nini?
 
Back
Top Bottom