Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,042
- 10,787
Mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Pius Luteko mkazi wa kijiji cha Nankanga mkoani Rukwa, ameuawa kwa kukatwa mapanga baada ya kufumaniwa akifanya mapenzi na mke wa mtu.
Akithibitisha kutokea tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa George Kyando amesema tukio hilo lilitokea june 5 mwaka huu majira ya saa 11: 40 baada ya watuhumiwa watatu kumvizia mtu huyo na kufanikiwa kumkuta akifanya tendo la ndoa na mwanamke huyo kwenye pagala na kuchukua hatua ya kumkata mapanga kisogoni na kumsababishia kifo papo hapo.
Kamanda Kyando amesema baada ya kufanya mauaji hayo mmoja kati ya watu walioshiriki kufanya unyama huo alifanikiwa kukimbia na serikali ya kijiji iliwakamata watuhumiwa wawili akiwamo mume wa mwanamke huyo na kuwafikisha polisi.
Chanzo: IPP