Rugemalira: IPTL iliokoa fedha za serikali

Nacheka umeniona? Na sijui ni facts gani unataka! Taasisi kama makampuni ya simu zinachangia kama ni sehemu ya kurudisha mapato kwenye jamii (Corporate Social Responsibility), hawa jamaa wamekurupuka hivi majuzi tu, hapo awali walikuwa wapi?

Au fedha ndiyo zinatubabaisha? Naona baadhi yenu mumenijia juu kwa sababu ya vijisenti vya ugoro.
Kwi kwi kwi huna kitu kichwani mkuu, nakuonea huruma kuendelea kuokota maneno ya majukwaani na kwenye vipeperushi vya magazeti ya mafisadi. Unapozungumzia mrejesho wa ushiriki ktk maswala ya kijamii kwa makampuni, haimaanishi kampuni inapaswa kutoa kwa wakati gani. Ila inalazimishwa kushiriki kwa namna na kadri wawezavyo kuisaidia jamii. Kwahiyo PAP kushiriki kutoa misaada kwa wakati huu ni utaratibu tu. Na isitoshe hizo ni fedha zao wanaopaswa kuzitolea macho ni hao waliyokuwa wabia wenzie na siyo wewe.
 
Utacheka sana maana hizo fedha za hao tuliowazungumzia zinatoka kwako wewe na mimi na walipa kodi wa nchi hii.

Endelea tu kucheka halafu ulalamike eti hakuna huduma muhimu wakati watu wanachota mapesa halafu wanajidai kutoa michango minene kwenye taasisi za dini na mayatima kwa kudhania kuwa wanajisafisha.

Cheka sana cheka sana sana sana na wala usinionee huruma bali nakuhurumia wewe uliyevaa miwani ya mbao.
 
Mkuu usipange matumizi kwa pesa ya mtuu
Walw pesa zao na wanamahamuz yao sasa wewe kinakuumaa nini kwa wale kutoa msaada
Acha umbululu wewe
 
Utacheka sana maana hizo fedha za hao tuliowazungumzia zinatoka kwako wewe na mimi na walipa kodi wa nchi hii.

Endelea tu kucheka halafu ulalamike eti hakuna huduma muhimu wakati watu wanachota mapesa halafu wanajidai kutoa michango minene kwenye taasisi za dini na mayatima kwa kudhania kuwa wanajisafisha.

Cheka sana cheka sana sana sana na wala usinionee huruma bali nakuhurumia wewe uliyevaa miwani ya mbao.
mkuu mbona biashara ilishafanyika sasa wewe kinakuumaa nini
 
Hivi Rugemalila mbona watu wanamwonea kinyongo sana, Yakina Jitu Tapel yanaiba hayasemwi kama huyu jamaa aliyetumia ujanja wa kucheza na sheria kikaeleweka, akapata vipesa vya ugolo, hamtaki hata apumue ? mwacheni bwana naye atese kama walivyotesa wa EPA, huyu hajafanya wizi amechezesha sheria sasa kalipwa, ona sasa matunda kamsaidia dada yake Prof Tiba kulipa deni nyumba isiuzwe. Kama wewe ungezipata ungemsaidia nani?
 
Hilo nalo neno
 
IPTL ILIOKOA FEDHA ZA SERIKALI ASEMA RUGEMALIRA

Pia Rugemarila alisisitiza katika maelezo yake hayo kwamba uamuzi wa serikali, akimtaja Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Katibu mkuu wake Eliakim Maswi,kuruhusu fedha hizo zitoke BOT na kumaliza mgogoro zimeiokoa serikali na hasara nyingi ikiwamo kununua umeme wa bei ghali zaidi kutoka sehemu nyingine.

chanzo: Raia Mwema.

Mapya yaibuka fedha za IPTL

Mwandishi Wetu

Toleo la 371
17 Sep 2014

371_rugemarila.jpg

  • Rugemalira amruka Seth kwa CAG
  • Andrew Chenge ataka asihusishwe

MMOJA wa waliokuwa wamiliki wa Kampuni ya Independent Power (IPTL) amedai hana ushahidi na hakuhusishwa katika uuzaji wa hisa za mbia mwenzake wa kampuni hiyo, uuzaji ambao hatimaye umesababisha kuchotwa kwa mabilioni ya shilingi katika akaunti ya Tegeta Escrow, imefahamika.
Mmiliki huyo ni Mkurugenzi wa Kampuni ya VIP Engineering (VIPEM), James Rugemalira na alitoa maelezo hayo kwenye ofisi za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ambayo inachunguza tukio la kuchotwa kwa fedha hizo zilizokuwa zimehifadhiwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Katika maelezo aliyoyatoa kwa CAG na ambayo Raia Mwema imefanikiwa kupata nakala yake, Rugemalira alieleza kwamba hakushirikishwa wakati mbia mwenzake wa zamani katika IPTL, Kampuni ya Mechmar ya Malaysia, ilipofanya uamuzi wa kuuza hisa zake (asilimia 70) kwa Kampuni ya Pan African Power Solution (PAP) ambayo sasa ndiyo inamiliki IPTL.
“Bwana Rugemalira hakuwa na ushahidi wa kuuzwa kwa hisa za Mechmar kwa PAP ingawa alikwishaona baadhi ya barua za Mechmar kwenda Wizara ya Nishati na Madini.
“Rugemalira hakuhusishwa katika uuzwaji wa Mechmar kwa Piper Link. Wakati wa kusaini transfer tarehe 24/1/2014, kuna document (nyaraka) Bwana Rugemalira aliiona ambayo inaonyesha kununuliwa kwa share (hisa) za Mechmar,” inasema sehemu ya maelezo hayo ya Rugemalira ambayo yamesainiwa naye Septemba 10, mwaka huu.
Rugemalira naye aliuza hisa zake kwa kampuni hiyo ya PAP inayomilikiwa na Harbinder Seth Singh kwa thamani ya dola za Marekani milioni 75 (sawa na shilingi bilioni 123 za Tanzania).
Uuzwaji wa hisa za Mechmar kwa Piper Link na hatimaye PAP, ndiyo uliosababisha Rugemalira auze hisa zake kwa kampuni hiyo; tukio ambalo mwisho wake umewezesha kutolewa kwa fedha katika akaunti ya Tegeta.
Katika maelezo yake kwa CAG, Rugemalira ameeleza kwamba kwa kadri anavyofahamu, alilipwa fedha hizo kwa taratibu halali za kibiashara na kisheria.
Ofisi ya CAG inafanya uchunguzi kutafuta ni kwa vipi kiasi cha shilingi bilioni 200 zilitolewa katika akaunti hiyo ya Tegeta iliyokuwa ikishikiliwa na BoT na kulipwa kwa PAP.
Pia alisisitiza katika maelezo yake hayo kwamba uamuzi wa serikali, akimtaja Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu wake, Eliakim Maswi, kuruhusu fedha hizo zitoke BoT na kumaliza mgogoro zimeiokoa serikali na hasara nyingi ikiwamo kununua umeme wa bei ghali zaidi kutoka sehemu nyingine.
Hata hivyo, maelezo hayo ya Rugemalira yamefunua mapya taarifa kuhusu uhalali hasa wa Singh kupewa hisa za Mechmar na hatimaye kuruhusiwa kuchukua fedha hizo zilizokuwa zimehifadhiwa BoT.
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ambayo ndiyo iliyomwagiza CAG kufanya uchunguzi huo, ilikuwa na wasiwasi kwamba Singh atajipatia kiasi cha shilingi bilioni 200 kwa kununua hisa za Rugemalira.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe, Piperlink ilinunua asilimia 70 ya hisa hizo za Mechmar kwa thamani sawa na shilingi milioni sita za Tanzania lakini nayo ikaziuza kwa PAP kwa thamani ya dola 300,000 (shilingi milioni 500 za Tanzania).
Hata hivyo, wakati Mechmar ikidaiwa kuuza hisa zake hizo mwaka 2010, taarifa zilizopo zinaonyesha kwamba ilikuwa imefilisiwa nchini Malaysia na kwa mujibu wa sheria za nchi za Jumuiya ya Madola, isingewezekana kuruhusiwa kuuza hisa zake.
“Ni kwa njia gani ambako PAP ilichukua hisa za Mechmar katika IPTL mwaka 2010 wakati Mechmar ikiwa inafilisiwa? Sheria za nchi zote ulimwenguni haziruhusu jambo hilo kutokea kwani ni marufuku hisa za kampuni iliyo chini ya muflisi kuuzwa au kufanyiwa biashara yeyote.
“Au, kama wengine wanavyoamini, wakurugenzi wa Mechmar waliwazidi akili wasimamizi wa Malaysia, ikiwa ni pamoja na Mahakama Kuu na kufaulu kuuza hisa zao? Anachoeleza Harbinder ni kuwa Mechmar kwanza iliuza hisa zake katika IPTL kwa kampuni kificho inayoitwa Piper Link, ambayo ilizihifadhi, kwa sababu moja au nyingine, huko British Virgin Islands vya Uingereza,” ilisema taarifa ya Kabwe iliyopelekwa kwa CAG, Machi mwaka huu.
Mmoja wa wabunge waliosimama kidete kutaka fedha zilizotolewa BoT zirudishwe, David Kafulila, alisema haingii akilini kwamba hisa ambazo zimenunuliwa kwa shilingi milioni sita na baadaye milioni 500, zipande thamani ghafla na kufikia mabilioni ya shilingi.
Mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini (NCCR-Mageuzi), alisema suala la PAP kununua hisa za IPTL na hatimaye kupewa mabilioni hayo limegubikwa na rushwa.
Wakati hayo yakiendelea, zimeibuka tuhuma kwamba baadhi ya viongozi wa serikali wamepokea fedha kutoka kwa mmoja wa waliokuwa wamiliki wa IPTL katika mazingira ya kutia shaka.
Taarifa hizo zimeenea katika mitandao mbalimbali ya kijamii huku majina kadhaa ya viongozi wa serikali na wabunge yakitajwa.
Mmoja wa wabunge ambao majina yao yametajwa sana ni Mbunge wa Bariadi Mashariki, Andrew Chenge, ambaye katika mazungumzo yake na gazeti hili amekataa kuzungumzia suala hilo.
“Mimi kwa sasa nashughulika na masuala ya Katiba. Nafanya kazi hadi usiku. Sipendi kujadili mambo yangu binafsi au ya kikazi na vyombo vya habari. Naomba kwenye suala hilo la IPTL mniache,” alisema Chenge.
Chenge ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi wa Katiba ya Bunge la Maalumu la Katiba linaloendelea na vikao vyake mkoani Dodoma.

- See more at: Raia Mwema - Mapya yaibuka fedha za IPTL
 
Makala nzuri kweli,nimejifunza vitu vingi kumbe IPTL waliwafanyia ufisadi wa malaysia wenzao katika uuzaji wa hisa,sasa tunachopigia kelele hapa tanzania nini,wakati walifisadiana wenyewe
 
kitu kinachonishangazaga kuhusu wanasiasa wa hapa kwetu ni kupenda kutumia neno ufisadi vibaya katika kujipatia umaarufu
 
IPTL ILIOKOA FEDHA ZA SERIKALI ASEMA RUGEMALIRA

Pia Rugemarila alisisitiza katika maelezo yake hayo kwamba uamuzi wa serikali, akimtaja Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Katibu mkuu wake Eliakim Maswi,kuruhusu fedha hizo zitoke BOT na kumaliza mgogoro zimeiokoa serikali na hasara nyingi ikiwamo kununua umeme wa bei ghali zaidi kutoka sehemu nyingine.

chanzo: Raia Mwema.
Huyo nae ameshatia kibindoni cola milioni 75 anajaribu kumung'unya maneno ili tumwone mwema.
Kama utapeli alishafanya imetosha akae. Kimya
 
Name Hugo nae ameshatia kibindoni cola milioni 75 anajaribu kumung'unya maneno ili tumwone mwema.
Kama utapeli alishafanya imetosha akae. Kimya

utakuwa umesahau hizo pesa aliuza hisa zake 30% kwa kampuni ya PAP, au umesahau alikuwa mbia kwenye iptl
 
hili la rugemalira kutoa fedha limeka sawa kweli ama kuna harufu ya rushwaa ndani yake
 
Kweli labda katoa yeye,maana mchakato mzima wa iptl ulifuata misingi yote ya kisheria na ulikua wazi katika mahakama zetu tukufu hata mkono analijua hilo

Yani team mkono inavyo tapatapa kisa prof muhungo kawapga shini bac wanasumbua hao mpaka kero kwenye mitandao
 
Back
Top Bottom