Rufus cuff: Hii ndio smartwatch tunayoitaka?

Millah

JF-Expert Member
Jun 3, 2011
410
195
[h=1]RUFUS CUFF: HII NDIO SAA TUNAYOITAKA?[/h]
  • By Mwandishi Wetu
  • 09:21
  • 0 comments
  • gajeti, Mwanzo, SaaSmartwatch na gajeti nyingine za kuvaa mkononi ziko katika njia panda huku kampuni mbali mbali zikijaribu kutoa mwelekeo ni vipi hasa gajeti hizi ziwe, na nini ziwe zinafanya ili kuwa na matumizi halisi ambayo yatahitaji kila mtumiaji simu aone umuhimu wa kuwa na gajeti hizi. Wakati Pebble walikuwa waanzilishi wa gajeti ya mkononi baada ya kutoa Pebble Watch ya kwanza, Samsung wanaonekana kuongoza soko katika gajeti za aina hii baada ya kutoa Smartwatch mbili na Gear fit ambayo ni gajeti ya mazoezi zaidi ya kuvaa mkononi. Hata hivyo Rufus Lab ambao ni “kickstater” waliojisajili kwenye Indiegogo wanaonekana kufanya jaribio la mabadiliko juu ya ni vipi Smartwatch iwe.


Rufus Cuff inavyoonekana mkononi, hii ndio smartwatch kubwa zaidi Duniani
Gajeti hiyo ambayo imepewa jina la Rufus Cuff inatofauti moja kubwa na gajeti zote za mkononi, tofauti hiyo ni kuwa ina kioo chenye ukubwa wa inchi tatu, je tunahitaji kuvaa saa ya aina hii? Hili ndio swali la msingi, iwapo jibu ni ndio Rufus Lab bila ya shaka itakuwa ni kampuni itakayoingiza mamilioni ya Dola. Rufus Lab walipojisajili kwenye Indiegogo walikuwa na lengo la kukushanya mchango wa Dola za Kimarekani laki mbili, tayari Rufus Lab wameshakusha zaidi ya Dola laki tatu, hivyo ni jambo la uhakika kwamba gajeti hii itaingia sokoni kwa ajili ya mauzo, Rufus Lab washatangaza kwamba Rufus Cuff itaanza kuuzwa mwezi wa tisa mwaka huu.


Kamera ya Rufus Cuff katika chat ya video
Kwa upande wa vielelezo: Rufus Cuff itatumia Android 4.4 kitkat na itakuwa inafanya kazi na saa za Android na iPhone, kwa mara nyingine Windows Phone imeachwa pembeni. Rufus Cuff ambapo kampuni wanayoitengeneza wameitambulisha kama Wrist Communicator badala ya Smartwatch itakuwa na sensa zote zinazotarajiwa kwenyegajeti za aina hii, yaani Bluetooth 4.0, Gyroscope, GPS, WiFi na akselerometa. Itakuwa inachukua app za Android za kawaida, hii inatufanya tushangae ni vipi Rufus Lab wataitofaoutisha na Simu, ili mtumiaji aone kwamba Rufus Lab sio tu kurudia vilivyomo kwenye simu kwenye kifaa chingine. Hii ni changamoto kubwa ambayo kampuni mbali mbali bado zinaonekana kushindwa kufikia ugunduzi wa kutosha. Wengi tunaisubiri wka hamu Rufus Cuff tuone utofauti wake.Rufus Cuff itakuwa tofauti na gajeti nyingizne za mkononi kwa vile kioo chake chenye ukuwba wa inchi tatu kitaruhusu usomaji wa barua pepe, ujumbe mfupi, whatsapp, BBM na aina nyingine za meseji kwa urahisi zaidi, pia itaruhusu utazamaji wa video za youtube, vimeo na hata video zitakazo rekodiwa na Rufus Cuff yenyewe kwa vile gajeti hiyo ina kamera ya mbele, Rufus Lab hawajaeleza uwezo wa kamera yake. Rufus Cuff itakuwa na disk yenye ukuwba wa 16 GB, prosesa aina ya TI ARM, speaker na microphone, hivyo watumiaji wataweza kupigia simu na kupokea bila ya kutumia simu yenyewe.


Rufus Cuff pia itatoa taarifa (notification) mbali mbali, kwa vibration, sauti na hata LED Flashlight. Pia communicator hiyo itakuruhusu kucheza muziki uliomo kwenye Rufus Cuff yenyewe au simu yako, Rufus Cuff inauwezo wa kuzuia maji (water proof) pia itakuwa na kazi zote za kiafnya kama vile kujua kalori zilizounguzwa wakati wa mazoezi, hatua ulizokimbia pamoja na umbali. Pia Rufus Cuff itakuwa na uwezo wa kufanya kazi na gajeti zote zinazofanya kazi na OS ya Android.
Bei ya Rufus Cuff ni ya kuridhisha kiasi kwa vile gajeti hiyo tayari unaweza kuweka oda kwa $279 kwa ajili ya kuletewa gajeti yako baina ya mwezi wa tisa na wa 12 mwaka huu. Wakati bado tunajiuliza kama kweli wanateknolojia wako tayari kuvaa lijidude kubwa kiasi hichi mkononi dalili zinaonyesha kuwa jibu ni “ndio” kwa vile mtandao wa Indiegogo unaonyesha kuwa watu wengi tayari wamesha weka oda ya kifaa hichi.


Chanzo: gajetek habari
 

iMind

JF-Expert Member
Mar 27, 2011
2,194
2,000
Zionism bado as babu itakayonifanya ni undue gaieties hii mañana features sake zote ninazo Keynes simu yangu ya android.
 

Millah

JF-Expert Member
Jun 3, 2011
410
195
Zionism bado as babu itakayonifanya ni undue gaieties hii mañana features sake zote ninazo Keynes simu yangu ya android.

Vile vile unaweza ukasema huoni sababu ya kuwa na iPad kwa vile feature zake zote unazo kwenye iPhone, ua Galaxy Phone na Galaxy tab. It's all about new category gadgets.
 

NullPointer

JF-Expert Member
Feb 7, 2011
3,467
2,000
hiyo smartwatch sijanunua, kubwa hivo sasa si bora niendelee kutumia simu tu, lote hilo unavaa mkononi utaonekana wa ajabu, i think kuna better smartwatches ndogo size nzuri...na nyingine zinakuja mwaka huu pia kama ya motorola ya round inayotumia latest android OS, Google now itarun vizuri sana...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom