Rufaa ya Sioi yatinga NEC

wazazi wako kama ni watanzania na wewe ukazaliwa nje ya Tanzania hiyo haikupi direct citizenship ya Tanzania, kumbuka issue ya AZIZI PREMJI alivuliwa ubunge kwa sababu ya kutoukataa uraia wa sehemu aliyozaliwa mara baada ya kufikisha miaka 18 . ukizaliwa nchi nyingine na wazazi wako hata kama wote wawili ni watanzania utakuwa mtanzania mpaka utakapofikisha miaka 18. hapo utaitajika kuukana uraia wa nchi nyingine na kubakia mtanzania. mwanasheria wa uhamiaji anaelekea kuwa anatumiwa na CCM kwani swala hili liko wazi kabisa kwani mtu yeyote aliywzaliwa kenya miaka hiyo ya nyuma ni mkenya. utanzania wa SIYOI uliisha alipofikisha miaka 18 baada ya hapo alipaswa kuukana uraia wa kenya pamoja na kwamba hakuwahi ku claim uraia wa kenya lakini hakuitaji kufanya hivyo kwani kwa kuzaliwa kwake tu tayari ni mkenya kwahiyo hakupaswa hata ku claim uraia wa kenya. eti kwa kuwa hajawahi kujiita mkenya au kubeba passport ya kenya huko hakumaanishi kuwa uraia wake wa kenya ulikufa mpaka pale tu angekwenda mahakamni kuukana.

Mkuu ingekuwa vizuri kama ungeweka hizo sheria za uhamiaji ili tujadili tujue zimetungwa mwaka gani, kuliko kuongea bila data na facts za kutosha.
 
Chadema kweli mambo magumu kama kweli mnakubalika Arumeru, kwa nini mnapoteza muda wenu na hizo rufaa.
Kwani kukata rufaa anakwenda Nassari? kuna kina Marando ndio wanashughulika nayo mgombea yuko ground.
 
Heading ilinichanganya kidogo "rufaa ya Sioi" kumbe habari yenyewe inahusu "rufaa dhidi ya Sioi".Anyway, asante kwa taarifa
 
Napenda sana jitihada za CDM juu ya swala hilo ila kwakuwa tunao uwezo wa kushinda kwa kura, basi nashauri tusipoteze muda na akili katika kuweka pingamizi badala yake tuweke nguvu na akili yote katika mbinu za ushindi wa kura. Lini fisadi akamtosa fisadi mwenzio? Hawa wote lao moja kama Tendwa yuko radhi kueneza chuki na husda dhidi ya kamanda Lema, leo aseme Siyoi sio raia? Haiwezekani na bado Siyoi atatakatishwa mpaka awe mgombea tu.
Kamanda acha tu CDM wafanye hivyo ili historia/kumbukumbu zikae vizuri, hizi blunders zinazofanywa na CCM ipo siku tu zitatumika kuwahukumu.
 
Vipi kama utata wa uraia ungekuwa ni wa mgombea wa CHADEMA?

Crashwise,

Hata angelikuwa mgombea wa CHADEMA tungelisema hivyo hivyo. Laiti pingamizi dhidi ya Siyoi lingepita ina maana maelfu ya watanzania hasa wale wa mipakani leo wangelikuwa sio Watanzania. Tusichukulie hili jambo kisiasa maana mambo ya uraia yanahusu watu wengi sana.

Sisi tumezaliwa kule mipakani na tunawajua watu wengi sana ambao wana cases kama za Siyao. Kule kwetu ilikuwa kawaida watu wa upande mmoja kwenda upande mwingine kutibiwa/kujifungua.

Hao watu muda wote wamejulikana kama Watanzania kwasababu wamezaliwa na wazazi wote Watanzania, ghafla leo mnataka kusema sio Watanzania?

Maamuzi ya hili pingamizi tayari yametoa ufafanuzi wa maana na Watanzania wenzetu wengi inatakiwa wasiwe na wasiwasi tena maana hata mahakamani reference itakuwa ni haya maamuzi ya Siyoi.
 
Chadema kweli mambo magumu kama kweli mnakubalika Arumeru, kwa nini mnapoteza muda wenu na hizo rufaa.
Haipo hivyo kiongozi, itifaki inapaswa kuzingatiwa, hatuwezi tawaliwa na Mkenya/mchina ilhali tuna wazawa lukuki wapo pale na wamepoteza haki yao ya kugombea jimbo kwa ghilba za kisiasa . Iweje siku zoooote hakuona umuhimu wa kuwa mtanzania, leo hii aone Tanzania ni pazuri????kwanini asigombee kwenye nchi yake???

Ukitaka kuelewa ubaya wa hili suala chukua mfano ufuatao, siku zooote mkeo huoni umuhimu wako na anakudharau kwa vile hula kazi yenye kipato kizuri, siku umepata kazi yenye pesa mingi, anajifanya anazidisha mikogo na mapenzi juu yake. Unadhan wewe/jamii itamchukuliaje mke wa hivyo????Kimsingi huyo bwana hajavutiwa na wakazi wa Arumeru, kavutiwa na Fedha ya Ubunge, tutemane nae tu, hatukatai CCM kushinda, ishinde ila kwa kufuata taratibu na sheria.
 
Nadhani magamba watapindisha mambo kama kawaida yao

Kuna wadau walilia na Mkwe.re kwamba kamteua mwenyekiti wa tume ambaye ni shemeji yake mamvi! connecting the dots unaona kabisa tume itapindisha kumlinda mkwe!
 
Mkuu Bobouk,
Uraia wa Sioni utaamuliwa kwa kuangalia sheria za Tanzania zinasemaje,Katiba mpya ya Kenya hazitakuwa na nafasi katika maamuzi ya NEC.

Ngongo naomba nikujibu pamoja na Politiki.

Sheria sio mathematics kwamba 2+2 is Always = 4! Ndiyo Uraia wa Sioyi utaamuliwa kwa kufuata SHERIA za Tanzania. Lakini pia utaangalia sheria za URAIA wa Kenya alikozaliwa HASA Kabla ya Katiba mpya. Kwa mfano wakati Siyoi anazaliwa Thika, Kenya ilikuwa hairuhusu dual citizenship. Hivyo Siyoi kuzaliwa Kenya na Wazazi wa Kitanzania kulikuwa hakumfanyi awe RAIA wa Kenya.

Sasa namjibu Politiki ambapo nitakuonesha kuwa sheria za nchi nyingine zinahusika kuaamua uraia wa Siyoi. Mathalani Siyoi kama angezaliwa USA, kwa sheria za USA yeye angekuwa Mmarekani. Kwa sheria zetu za TZ sheria ingemtambua Siyoi kuwa na uraia wa nchi 2 yaani USA na TZ mpaka hapo atakapotimiza miaka 18. Kwakuwa TZ hairuhusu dual citizenship baada miaka 18 kama angetaka awe raia wa TZ basi ingebidi aukane uraia wa USA. Na hii ndiyo iliyomtokea AZIM DEWJI. Lakini kama umezaliwa kwenye nchi ambayo sheria yao hairuhusu kuwa ukizaliwa ktk nchi hiyo automatically unakuwa raia wa nchi hiyo, basi uraia wako ni wa wazazi wako na hapo hakuna cha dual citizenship na huhitaji kuukana uraia wa nchi hiyo uliyozaliwa baada ya miaka 18 because sio raia wa nchi hiyo in the first place.

Kitu ambacho hadi sasa ninaona kinaweza kumnyima Uraia Siyoi ni kama ana passport mbili. Kama anazo basi tayari yeye ni raia pia wa nchi hiyo nyingine ambapo Tanzania haturuhusu dual citizenship hence automatically anakuwa sio raia wa Tanzania.
 
Chadema kweli mambo magumu kama kweli mnakubalika Arumeru, kwa nini mnapoteza muda wenu na hizo rufaa.

cdm inakubalika lakini haki na ukweli lazima uwekwe wazi.Hao wanaoweka wagombea wasio raia ndio wenye matatizo.,
 
Ngongo naomba nikujibu pamoja na Politiki. Kwakuwa TZ hairuhusu dual citizenship baada miaka 18 kama angetaka awe raia wa TZ basi ingebidi aukane uraia wa USA. Na hii ndiyo iliyomtokea AZIM DEWJI.

Ooops Huyo MTU asomeke kama AZIZ PREMJI (former MP for Kigoma) sio AZIM DEWJI. Samahani kwa usumbufu.
 
Napenda sana jitihada za CDM juu ya swala hilo ila kwakuwa tunao uwezo wa kushinda kwa kura, basi nashauri tusipoteze muda na akili katika kuweka pingamizi badala yake tuweke nguvu na akili yote katika mbinu za ushindi wa kura. Lini fisadi akamtosa fisadi mwenzio? Hawa wote lao moja kama Tendwa yuko radhi kueneza chuki na husda dhidi ya kamanda Lema, leo aseme Siyoi sio raia? Haiwezekani na bado Siyoi atatakatishwa mpaka awe mgombea tu.

kamanda hanga umeongea vema.. lakini ni muhimu sana kupigania haki hata kama una nguvu au huna..cdm wanapenda sana taratibu zifuatwe sababu kama kina nape wanavunja sheria hii basi wanaweza kuvunja nyingine wakiamini chadema watapotezea na kupelekea kuathiri ushindi wa chadema..kwa hiyo ni vizuri kuweka njia safi toka mwanzo..
 
Jamani tisichanganye SIASA na SHERIA. Kama CDM RUFAA imejikita kwenye kuzaliwa Kenya, Basi rufaa ya CDM haina mshiko kisheria. Tundu Lissu wasaidie CDM ili wasinekane kituko.

Kenya kama ilivyo Tanzania kabla ya Katiba mpya ilikuwa hairuhusu dual citizenship. Ili uwe raia wa nchi hizo (TZ & KNY) Lazima mzazi wako mmoja awe RAIA wether by birth or naturalisation. Kuzaliwa tu Tanzania au Kenya kulikuwa hakukufanyi uwe RAIA, tofauti na USA na UK (ingawa siku hizi UK nao wamefuta hiyo sheria kwamba mtoto akizaliwa UK anakuwa Muingereza, because wana Nigeria, Wahindi Paksitani etc walikuwa wana abuse hiyo sheria. Mama akikaribia kujifungua anakimbilia UK ili mtoto apate URAIA).

Hivyo Kama Siyoi alizaliwa Thika Kenya na wazazi wa kitanzania, yeye ni Mtanzania na hakuwa na haja ya kuukana URAIA wa Kenya because hakuwa RAIA wa Kenya.

Mimi nilifikiri labda Siyoi ana PASSPORT mbili moja ya Tanzania na ya nchi nyingine. Kama Siyoi ana PASSPORT 2 hiki tu ndiyo kinaweza kuwa kigezo cha kumfanya kutokuwa RAIA wa Tanzania. Kwasababu TZ hairuhusu dual citizenship. Kuwa passport ya nchi nyingine maana yake wewe ni RAIA wa nchi hiyo na automatically unakuwa sio tena raia wa Tanzania, hata kama hukuukana uraioa wa Tanzania. Mnaoishi majuu najua baadhi yenu mpo mmechukuwa passport za nchi hizo kimya kimya, huku mkiwa na passport pia ya Tanzania. It is Illegal and you know it! Labda hapo KATIBA mpya itakaporuhusu dual citizenship.

Kama hujui sheria kuhusiana na uraia wa Tanzania inasemaje si unakaa kimya ndugu ya nini kujiaibisha na maneno mengiutafikiri unaelewa kumbe hamna kitu.kama kitu hujui unauliza si lazima uchangie hapa au unaongeza idadi ya post zako JF?
 
Ngongo naomba nikujibu pamoja na Politiki.

Sheria sio mathematics kwamba 2+2 is Always = 4! Ndiyo Uraia wa Sioyi utaamuliwa kwa kufuata SHERIA za Tanzania. Lakini pia utaangalia sheria za URAIA wa Kenya alikozaliwa HASA Kabla ya Katiba mpya. Kwa mfano wakati Siyoi anazaliwa Thika, Kenya ilikuwa hairuhusu dual citizenship. Hivyo Siyoi kuzaliwa Kenya na Wazazi wa Kitanzania kulikuwa hakumfanyi awe RAIA wa Kenya.

Sasa namjibu Politiki ambapo nitakuonesha kuwa sheria za nchi nyingine zinahusika kuaamua uraia wa Siyoi. Mathalani Siyoi kama angezaliwa USA, kwa sheria za USA yeye angekuwa Mmarekani. Kwa sheria zetu za TZ sheria ingemtambua Siyoi kuwa na uraia wa nchi 2 yaani USA na TZ mpaka hapo atakapotimiza miaka 18. Kwakuwa TZ hairuhusu dual citizenship baada miaka 18 kama angetaka awe raia wa TZ basi ingebidi aukane uraia wa USA. Na hii ndiyo iliyomtokea AZIM DEWJI. Lakini kama umezaliwa kwenye nchi ambayo sheria yao hairuhusu kuwa ukizaliwa ktk nchi hiyo automatically unakuwa raia wa nchi hiyo, basi uraia wako ni wa wazazi wako na hapo hakuna cha dual citizenship na huhitaji kuukana uraia wa nchi hiyo uliyozaliwa baada ya miaka 18 because sio raia wa nchi hiyo in the first place.

Kitu ambacho hadi sasa ninaona kinaweza kumnyima Uraia Siyoi ni kama ana passport mbili. Kama anazo basi tayari yeye ni raia pia wa nchi hiyo nyingine ambapo Tanzania haturuhusu dual citizenship hence automatically anakuwa sio raia wa Tanzania.

@Bobuk, tusichanganye mambo, sheria ya Tanzania haitoi UBAGUZI. Hakuna mahali sheria inasema kuwa anayetakiwa kuapa ni yule ambaye amezaliwa kwenye nchi ambayo haikumpa uraia. hakuna. Ili mradi umezaliwa nje ya territorial za Republic unatakiwa ama uape au utoe evidence(uthibitisho) kuwa hauna uraia wa nchi nyingine yoyote. Mbele ya sheria za Tanzania aliyezaliwa Kenya na aliyezaliwa USA wote wanakuwa kwenye kundi moja. Foreign citizen until proven otherwise.

Kwa ruhusa ya mdau Jagermaster naomba niweke ufafanuzi wake ili uone exactly tatizo liko wapi.

"Tanzania tuna uraia wa aina tatu,
(1) Uraia wa Kuzaliwa (citizenship by birth)-Huu napatikana kwa mtu yoyote aliyezaliwa Tanzania with a condition that, mzazi mmoja wapo au (wote) awe either raia wa kuzaliwa au raia wa kwandikishwa.

(2) Raia wa kuandikishwa (citizeship by naturalisation)- Huu hupatikana kwa kuomba, ikiwa raia yoyote wa kigeni anayeishi Tanzania kwa muda usiopungua miaka kumi, au pungufu ya hapo kama waziri ataona inafaa, ambaye anania kubaki Tanzania kwa muda wote wa maisha yake. Huu ndio mara nyingi tunauona kwenye magazeti watu wakiomba

(3) Uraia wa kurithi (citizenship by descent)- Huu ni uraia mtu yoyote aliyezaliwa nje ya Tanzania huku wazazi wake wakiwa Watanzania raia wa kuzaliwa au wa kuandikishwa. Watu wanaozaliwa ikiwa wazazi wao wanafanya kazi kwenye balozi hao watu wanahesabika wamezaliwa Tanzania. Pia ileweke kuwa mtu ukizaliwa kwenye chombo cha usafiri (ndege, meli.e.t.c) unahesabika umezaliwa kwenye nchi ambayo hicho chombo kimeandikishwa

Ileweke kuwa sheria ya uraia ya Tanzania, haitambuwi uraia wa nchi mbili au tatu, with exception kwa mtu mwenye uraia wa kurithi. Raia wa kurithi anaruhusiwa kuwa na uraia wa nchi mbili mpaka pale atakapofikisha umri wa miaka kumi na nane (18) anatakiwa kukana uraia wa nchi nyingine na kubaki na uraia wa Tanzania pekee. Hiki kitendo watu wengi hawakifanyi na price yake wanaipata pale wanapotaka uongozi wa kisiasa

Pia hakuna mahara popote pale ambapo sheria ya uraia ya Tanzania inatoa exception katika kukana uraia kwa mtu mwenye uraia wa kurithi, kwamba either kama huyo mtu kazaliwa kwenye nchi ambayo inatoa automatic citizeship kama US au conditional citizeship kama Kenya kwamba aukane uraia wake wa awali au hapana. Sheria ya Tanzania inawataka watu wote wenye uraia wa kurithi kuukana uraia wa nchi walizozaliwa pale wanapofikisha umri wa miaka kumi na nane, without exception kama Mh Mchemba unavyotaka tuamini. Naona hapo Mh umetumia common sence na sio sheria unavyosema, ni vizuri kama ukaweka ushahidi wa hayo mnayoyaamini. Pia sheria inatoa mwanya wa mtu kupewa uraia hata kama hajakana uraia wa nchi nyingine, ikiwa atathibitisha tu kuwa ni vigumu au haiwezekani kukana uraia wa nchi nyingine ambayo inamtambuwa au haimtambui kuwa ni raia wake

What about SIYOI?
Kwa kesi ya Siyoi ilivyo, yeye anafall katika category ya tatu yaani raia wa Kurithi kwa kuwa alizaliwa Kenya na wazazi watanzania. Wazazi wake walikuwa hawafanyi kazi za ubalozi huko Kenya wakati jamaa anazaliwa.
Pasipo kujali kuwa either Kenya walikuwa wanamtabua kuwa raia wao au hapana, Tanzania ilikuwa inamtambua Siyoi kama raia wa Kurithi yaani alikuwa na uraia wa Kenya na Tanzania na alivyofikisha umri wa miaka 18 kama alishindwa kuukana uraia wa Kenya alipoteza sifa za kuwa raia wa Tanzania. Kwa mazingira yake kama inaonekana ilikuwa ni vigumu kwa yeye kukana uraia wa Kenya kwa kuwa Kenya walikuwa 'hawamtambui' kama raia, alipaswa kupeleka maelezo hayo idara ya Uhamiaji ili wamwelewe kuwa kwa kesi yake hawezi kukana uraia na wa mpe uraia wa Tanzania

Kwa jinsi nilivyosoma sheria ya uraia ya Kenya, Siyoi pia hana sifa ya kuwa raia wa Kenya kwa umri alionaona. Swali sasa linakuja Siyoi ni raia wa aina gani?
Jibu ni jepesi SIYOI SUMARI hana Uraia wa nchi yoyote ile Duniani (Stateless). Watu wa aina hii wapo wengi tu duniani ambao wanaishi kwa kutokuwa na uraia wa nchi yoyote kisheria. Ila kwa Tanzania I know anything can happen

NB
Issue hii ni tofauti na Kesi ya Ulimwengu, licha ya mwamba wote Siyoi na Generali wanajikuta wanakuwa sio raia wa nchi yoyote ile Duniani, Siyoi anapaswa kuukana uraia wa Kenya, kwa kuwa yeye alishawahi kuwa raia wa kurithi mpaka alipofikisha umri wa miaka 18 ndipo uraia wake ulikoma, Ulimwengu hakuwahi kuwa raia wa Tanzania kwani hata Wazazi wake hawakuwahi kuwa raia wa Tanzania, ndio maana yeye aliambiwa aombe uraia wala hakuambiwa aukane tu uraia wa Rwanda.

Kwa maoni yangu sheria ya Uhamiaji ya Tanzania inamapungufu mengi. Ikifika stage kama hizi ndio mapungufu yake yanaonekana. Kwa mfano mpaka sasa raia yoyote wa kurithi, mwenye mke au mume ambaye sio raia wa Tanzania au ni raia wa kurithi, akizaa mtoto nje ya nchi huyo mtoto anakuwa sio raia wa Tanzania, wala uraia wa kurithi haupati. Itampasa huyo mtoto amuombee uraia wa kwandikishwa kama anataka awe Mtanzania.

Wito kwa Watanzania wote wenye uraia wa kurithi nendeni mkakane uraia wa nchi mlizozaliwa, maana kwamtindo huu mkekalia kuti kavu bila kujiju" (MWISHO WA KUNUKUU).
 
wazazi wako kama ni watanzania na wewe ukazaliwa nje ya Tanzania hiyo haikupi direct citizenship ya Tanzania, kumbuka issue ya AZIZI PREMJI alivuliwa ubunge kwa sababu ya kutoukataa uraia wa sehemu aliyozaliwa mara baada ya kufikisha miaka 18 . ukizaliwa nchi nyingine na wazazi wako hata kama wote wawili ni watanzania utakuwa mtanzania mpaka utakapofikisha miaka 18. hapo utaitajika kuukana uraia wa nchi nyingine na kubakia mtanzania. mwanasheria wa uhamiaji anaelekea kuwa anatumiwa na CCM kwani swala hili liko wazi kabisa kwani mtu yeyote aliywzaliwa kenya miaka hiyo ya nyuma ni mkenya. utanzania wa SIYOI uliisha alipofikisha miaka 18 baada ya hapo alipaswa kuukana uraia wa kenya pamoja na kwamba hakuwahi ku claim uraia wa kenya lakini hakuitaji kufanya hivyo kwani kwa kuzaliwa kwake tu tayari ni mkenya kwahiyo hakupaswa hata ku claim uraia wa kenya. eti kwa kuwa hajawahi kujiita mkenya au kubeba passport ya kenya huko hakumaanishi kuwa uraia wake wa kenya ulikufa mpaka pale tu angekwenda mahakamni kuukana.

Sheria si taarabu. Majibu yako hayo ni mipasho tu ila ukweli wa kisheria ni huo alioeleza hapo juu.
 
Back
Top Bottom