Rufaa ya Sioi yatinga NEC | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rufaa ya Sioi yatinga NEC

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by EasyFit, Mar 12, 2012.

 1. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #1
  Mar 12, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Chadema kimekata rufaa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kikitaka kuenguliwa katika uchaguzi huo, mgombea wa CCM, Siyoi Sumari kwa maelezo kwamba si raia wa Tanzania.

  Hatua ya Chadema imekuja saa chache baada ya Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Trasias Kagenzi kutupa mapingamizi yote ya wagombea katika uchaguzi huo mdogo.

  Kwa mujibu wa nyaraka za Chadema, ambazo zina nukuu, barua ya siri ya OfisaUhamiaji Mkoa wa Arusha, D. Namomba kwenda kwa Mkuu wa Mkoa, aliyetaka kujua uraia wa Siyoi, mgombea huyo wa CCM anadaiwa kuzaliwa Thika, Kenya na kunautata kama aliwahi kuukana uraia wake wa awali.

  Meneja wa Kampeni wa Chadema, Vicent Nyerere alisema wana ushahidi kuwa uraiawa Siyoi una tata hivyo, hawakubaliani na uamuzi wa Kagenzi... “Tunakata rufani NEC kwani tuna ushahidi kuwa uraia wa mgombea wa CCM una utata.”

  Source: Mwananchi
   
 2. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #2
  Mar 12, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Imeshakula kwake,sisiemu wamuondoe tu,wapi hussein bashe?
   
 3. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #3
  Mar 12, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Aisee naona wameamua kulindana lakini ukweli utajulika tu mwisho wa siku. Lakini hii yote ni ukosefu wa umakini hivi ingekuwa UK au USA jambo kama hili lisingeachwa kimzaha mzaha namna hii kwa sababu kila kitu kingekuwepo na suala ingekuwa documentation.
   
 4. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #4
  Mar 12, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  :lock1:
   
 5. K

  KAMANDA HANGA Senior Member

  #5
  Mar 12, 2012
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 158
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Napenda sana jitihada za CDM juu ya swala hilo ila kwakuwa tunao uwezo wa kushinda kwa kura, basi nashauri tusipoteze muda na akili katika kuweka pingamizi badala yake tuweke nguvu na akili yote katika mbinu za ushindi wa kura. Lini fisadi akamtosa fisadi mwenzio? Hawa wote lao moja kama Tendwa yuko radhi kueneza chuki na husda dhidi ya kamanda Lema, leo aseme Siyoi sio raia? Haiwezekani na bado Siyoi atatakatishwa mpaka awe mgombea tu.
   
 6. k

  kibananhukhu JF-Expert Member

  #6
  Mar 12, 2012
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 368
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  CDM wakishinda kesi hakuna fursa ya kubadilisha mgombea
   
 7. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #7
  Mar 12, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Sioni mantiki ya rufaa hiyo. Wameru wataamua kwenye box la kura.
   
 8. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #8
  Mar 12, 2012
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Nadhani magamba watapindisha mambo kama kawaida yao
   
 9. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #9
  Mar 12, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Jamani tisichanganye SIASA na SHERIA. Kama CDM RUFAA imejikita kwenye kuzaliwa Kenya, Basi rufaa ya CDM haina mshiko kisheria. Tundu Lissu wasaidie CDM ili wasinekane kituko.

  Kenya kama ilivyo Tanzania kabla ya Katiba mpya ilikuwa hairuhusu dual citizenship. Ili uwe raia wa nchi hizo (TZ & KNY) Lazima mzazi wako mmoja awe RAIA wether by birth or naturalisation. Kuzaliwa tu Tanzania au Kenya kulikuwa hakukufanyi uwe RAIA, tofauti na USA na UK (ingawa siku hizi UK nao wamefuta hiyo sheria kwamba mtoto akizaliwa UK anakuwa Muingereza, because wana Nigeria, Wahindi Paksitani etc walikuwa wana abuse hiyo sheria. Mama akikaribia kujifungua anakimbilia UK ili mtoto apate URAIA).

  Hivyo Kama Siyoi alizaliwa Thika Kenya na wazazi wa kitanzania, yeye ni Mtanzania na hakuwa na haja ya kuukana URAIA wa Kenya because hakuwa RAIA wa Kenya.

  Mimi nilifikiri labda Siyoi ana PASSPORT mbili moja ya Tanzania na ya nchi nyingine. Kama Siyoi ana PASSPORT 2 hiki tu ndiyo kinaweza kuwa kigezo cha kumfanya kutokuwa RAIA wa Tanzania. Kwasababu TZ hairuhusu dual citizenship. Kuwa passport ya nchi nyingine maana yake wewe ni RAIA wa nchi hiyo na automatically unakuwa sio tena raia wa Tanzania, hata kama hukuukana uraioa wa Tanzania. Mnaoishi majuu najua baadhi yenu mpo mmechukuwa passport za nchi hizo kimya kimya, huku mkiwa na passport pia ya Tanzania. It is Illegal and you know it! Labda hapo KATIBA mpya itakaporuhusu dual citizenship.
   
 10. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #10
  Mar 12, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Chadema wameshashindwa mpaka hapo, sasa wanatapatapa.
   
 11. Babuu blessed

  Babuu blessed JF-Expert Member

  #11
  Mar 12, 2012
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 1,340
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Jamani ivi swala la bashe lilikuwa tofauti na la sioi au?mwenye kukumbuka atujuze tuone kama cdm wapo sahihi na cc m wanalindana
   
 12. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #12
  Mar 12, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,798
  Likes Received: 3,883
  Trophy Points: 280
  actually na hapo kwenye passort mbili ndipo kwenye uti wa mgongo wa doccument ya rufaa dhidi ya Sioyi!
   
 13. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #13
  Mar 12, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  maana yake, huoni sababu ya utawala wa sheria

  myopic view
   
 14. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #14
  Mar 12, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,798
  Likes Received: 3,883
  Trophy Points: 280
  vita unatakiwa utumie kila mbinu na silaha uliyo nayo pia uchaguzi lazima ucheze na propaganda, siasa na mambo ya kisheria yote hayo ni malengo ya kupata ushindi, unapoanza kuchokonoa uraia possible yakaibuka mwngine ambayo yanakuwa karata muhimu kwenye kampeni na hatimaye kupatikana ushindi!!
   
 15. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #15
  Mar 12, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Mkuu Bobouk,

  Uraia wa Sioni utaamuliwa kwa kuangalia sheria za Tanzania zinasemaje,Katiba mpya ya Kenya hazitakuwa na nafasi katika maamuzi ya NEC.


   
 16. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #16
  Mar 12, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Mwenyekiti wa NEC ni shemeji yake na EL, Siyoi kaoa kwa bwana EL, Siyoi huyo huyo ndiyo mgombea wa ubunge kupitia CCM. Wakati huo huo, mwenyekiti wa NEC kateuliwa na mwenyekiti wa CCM taifa ambaye ni rafiki yake mkubwa na EL. Hapo ni kutafuta kumbukumbu/ushahidi wa jinsi hawa wazee wanavyobaka taratibu na sheria za nchi ili waweze kushitakika vizuri huko mbeleni, vinginevyo utaratibu ukifuatwa sioni tatizo pingamizi likitupwa.
   
 17. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #17
  Mar 12, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Najua hata CDM wanajua itakuwa ngumu rufaa yao kupita ila nafikiri malengo yao ni haya

  1. Hii ni njia mojawapo ya kueneza habari ili hata yule (mpiga kura) aliyekuwa hajui ajue mgombea wa CCM si raia.
  2. Kuonyesha CDM kinasimamia na kufuata sheria na kuiachia CCM ndio waonekane wamepindisha.
  3. Keep the ball rolling closer to their goal, kuna magoli ya kujifunga.
  4. Keep them busy.
  5. Divide and rule, kwa vile hawako pamoja jambo hili litakuwa linawakumbusha,tumewasikia wao kwa wao wakisema 'tuliwaambia atapingwa'.
   
 18. p

  politiki JF-Expert Member

  #18
  Mar 12, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  wazazi wako kama ni watanzania na wewe ukazaliwa nje ya Tanzania hiyo haikupi direct citizenship ya Tanzania, kumbuka issue ya AZIZI PREMJI alivuliwa ubunge kwa sababu ya kutoukataa uraia wa sehemu aliyozaliwa mara baada ya kufikisha miaka 18 . ukizaliwa nchi nyingine na wazazi wako hata kama wote wawili ni watanzania utakuwa mtanzania mpaka utakapofikisha miaka 18. hapo utaitajika kuukana uraia wa nchi nyingine na kubakia mtanzania. mwanasheria wa uhamiaji anaelekea kuwa anatumiwa na CCM kwani swala hili liko wazi kabisa kwani mtu yeyote aliywzaliwa kenya miaka hiyo ya nyuma ni mkenya. utanzania wa SIYOI uliisha alipofikisha miaka 18 baada ya hapo alipaswa kuukana uraia wa kenya pamoja na kwamba hakuwahi ku claim uraia wa kenya lakini hakuitaji kufanya hivyo kwani kwa kuzaliwa kwake tu tayari ni mkenya kwahiyo hakupaswa hata ku claim uraia wa kenya. eti kwa kuwa hajawahi kujiita mkenya au kubeba passport ya kenya huko hakumaanishi kuwa uraia wake wa kenya ulikufa mpaka pale tu angekwenda mahakamni kuukana.
   
 19. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #19
  Mar 12, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,673
  Trophy Points: 280
  Chadema kweli mambo magumu kama kweli mnakubalika Arumeru, kwa nini mnapoteza muda wenu na hizo rufaa.
   
 20. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #20
  Mar 12, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Exactly Osokoni, vita ni vita hakuna vita ndogo ukishika hata kisu cha mkate ambacho hakina makali kinaweza kukusaidia, tuliona CCM walivyoshupalia hijab kule Igunga baada ya uchaguzi hatujasikia tena. CDM nao watumie hii issue kuirudia rudia hata kwenye majukwaa kama CD iliyokwama.
   
Loading...