Mjuni Lwambo
JF-Expert Member
- Apr 25, 2012
- 9,395
- 8,855
Kwa yeyote mwenye habari kuhusu nini kinaendelea juu ya chadema kukata rufaa katika kesi iliyomuengua ubunge Godbless Jonathan Lema naomba anihabarishe, Kwa mujibu wa gazeti la mwananchi la tarehe 6 april,2012, kulikuwa na mkanganyiko katika hukumu na chadema walitangaza kukata rufaa. Likimnukuu mwanasheria wa upande wa mlalamikiwa bwana method kimomogolo, linasema kuwa Mheshimiwa Lema alipatikana na hatia ya kutenda makosa yanayojulikana kisheria kama illegal campaining( kifungu namba 108) ambayo humruhusu alieenguliwa kugombea tena, lakini katika hali ya kutatanisha katika ku sum up hukumu jaji alimhukumu Lema kwa kutumia makosa yajulikanayo kama illegal practice (kifungu namba 114) ambayo hayamruhusu aliyeenguliwa kugombea tena, hivyo basi kuwa na ulazima wa pekee kwa chadema kukata rufaa. je wameshakata au ni nini kinaendelea?.