Rufaa vigogo wa EPA BoT katika hatua za mwISHO

mwanaizaya

Senior Member
Apr 26, 2008
133
1
Rufaa vigogo wa EPA BoT katika hatua za mwISHO


USIKILIZAJI rufaa za maafisa wa nne wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ambao walipinga adhabu za kuhusishwa kwa tuhuma za ufisadi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), uko katika hatua za mwishoni.


Mchakato huo unaelekea mwisho wakati tayari rufaa za vigogo wanne kati ya sita waliokata rufaa, zikiwa zimeshapitiwa na mwenyekiti wa rufaa ambaye ni Gavana wa Bot, Profesa Benno Ndulu.


Hata hivyo, alipoulizwa Profesa Ndulu kuhusu kupitia sehemu ya rufaa hizo, alisema kiutaratibu hawezi kupitia baadhi ya rufaa na kutoa taarifa.


Profesa Ndulu alifafanua kwamba, taarifa za jumla zitatolewa baada ya kukamilika rufaa zote.


Kwa ufafanuzi, Profesa Ndulu alisema anachofanya ni kuangalia uwiano wa rufaa moja kwenda nyingine hivyo kama ni kukamilika zinapaswa kukamilika zote si moja moja.


"Napitia zote kuangalia uwiano sasa siwezi kusema kuna ambazo zimekamilika," alisema Profesa Ndulu na kuongeza:


"Hapa nashughulika na maisha ya watu. Siwezi kulipua, nafanya kazi kwa umakini, kwa hiyo sijamaliza rufaa, umakini na uangalifu ni muhimu."


Alipoulizwa kwamba, inakuwaje apitie rufaa zote na kufanya uwiano wakati kila mtu kajitetea kwa maslahi yake na pingamizi zake, alijibu: "Sawa, lakini hili jambo lazima kufanya uwiano. Kwa hiyo siwezi kusema zimekwisha, ndiyo maana nasema napitia zote kwa pamoja na kufanya uwiano."


Wakati gavana akisema hayo, taarifa zinaeleza kwamba anachofanya mwenyekiti huyo kwa sasa ni uwiano kuona madai ya kila rufaa zikiwemo hizo nne ambazo tayari.


Chanzo chetu kimetaarifu kuwa baada ya kupitia na kukamilisha gavana ndiyo huangalia uwiano huo kabla ya kutoa maamuzi ya mwisho.


Tuhuma za ufisadi katika EPA ziliibuka katika hesabu za BoT za mwaka 2005/06, baada ya ukaguzi uliofanywa na kampuni ya Ersnt&Young. Awali ukaguzi huo ulifanywa na kampuni ya Deloitte&Touche ya Afrika Kusini, lakini ukasitishwa ghafla.


Mchakato wa kuchukua hatua kwa maafisa hao wa BoT walioshindwa kuwajibika, unakwenda pamoja na hatua kwa mafisadi wengine nje ya benki hiyo kurejesha fedha walizochota kabla ya Oktoba 31, kama Rais Jakaya Kikwete alivyoagiza.
 
Mwizi wa kuku anakamatwa mara moja, wa mabiolioni anapewa mpaka Octoba 31,haki iko wapi jamani,mm!
 
Back
Top Bottom