Rufaa kumpinga Mnyika kusikilizwa Disemba 7

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,575
2,000
RUFAA ya kupinga matokeo ya ubunge katika Jimbo la Ubungo iliyokatwa na aliyekuwa mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Hawa Ng’humbi dhidi ya Mbunge wa jimbo hilo John Mnyika itaanza kusikilizwa Desemba 7 mwaka huu katika Mahakama ya Rufaa.

Rufaa hiyo inatarajia kusikilizwa mbele ya jopo la Jaji Salum Massati, Jaji Nathalia Kimaro na Jaji Catherini Oriyo. Ng’humbi alifungua kesi akipinga matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka juzi yaliyompa ushindi Mnyika kwa madai kulikuwa na ukiukwaji wa taratibu, kanuni na sheria za uchaguzi katika uchaguzi huo.

Hata hivyo Mei 24, mwaka huu, Jaji Upendo Msuya wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam alitupilia mbali maombi ya Ngh’umbi na kuthibitisha Mnyika kuwa Mbunge halali wa Jimbo la Ubungo.

Katika kesi hiyo, Ng’humbi aliiomba Mahakama ibatilishe matokeo hayo kwa kuwa uchaguzi haukuwa wa haki, alikuwa na hoja tano ambazo Mnyika alimtuhumu kuuza nyumba za Umoja wa Wanawake (UWT) na kutumia Laptop za Mnyika kuhesabu kura.

Aidha kuingia watu wengi wa Chadema katika chumba cha kuhesabia kura, kuwepo kwa kwa kura hewa 16,000, kukosewa kwa karatasi za kujumlisha kura (form). Katika hukumu hiyo Jaji Msuya alisema Ng’humbi alishindwa kuthibitisha madai yake na kuonesha jinsi yalivyoathiri matokeo ya uchaguzi huo na kutangaza kuwa uchaguzi huo ulikuwa halali.

Alisema maombi kuwa Mahakama hiyo ibatilishe matokeo yaliyompa ushindi Mnyika yametupwa kwa kuwa hakuthibitisha madai yake na kutakiwa kulipa gharama za kesi hiyo pia mashahidi wa mdai hawakuonesha wala kuthibitisha madai yaliyowasilishwa yalitendeka vipi na ni namna gani yaliathiri matokeo ya uchaguzi.

Katika madai kuwa zaidi ya kura 14,000 alizodai hazieleweki zilitoka wapi Jaji alisema alihesabu kura hizo walizopata wagombea wa vyama 16 na kubaini ni kosa tu la kibinadamu na halina uhusiano wowote na Mnyika.

Aliongeza kuwa Fomu namba 24 b ilikuwa na dosari na ndiyo ilikuwa inabishaniwa na Ng’humbi ilikosewa kuandikwa. Kura halali Mnyika aliyetangazwa kuwa ni mshindi alipata kura 66,742 wakati Ng’humbi kura 50,544.

Wagombea wote kura ni 132496. Alisema kuwa katika ushahidi wa mdai hakuonesha ni vipi ongezeko hilo la kura liliathiri matokeo ya uchaguzi na pia mdaiwa Mnyika anahusika vipi na ongezeko hilo.

Chanzo: HabariLeo - Dec 01, 2012
 

AdvocateFi

JF-Expert Member
Jan 15, 2012
11,492
2,000
Hiv Rwakatare upo wapi na wale blue guards wa CHADEMA ili muwahadhibu watu kama hawa wanaofungua kesi za kitoto.
 

TUMBIRI

JF-Expert Member
May 7, 2011
1,933
0
Emu tujikumbushe mtiririko wa kesi yenyewe:-

1. DAI LA KWANZA KURA 14854 HAZIJULIKANI ZILIKOTOKEA WAKATI WA MAJUMUISHO
Wakili upande wa mlalamikaji: Siku ya kutangaza matokeo ulikuwepo?

Hawa: Sikuwepo

Wakili: kwanini hukuwepo kwenye kituo cha majumuisho?

Hawa: wakala wangu alikuwepo

Wakili: je ulisaini form ya matokeo

Hawa: Sikusain

Wakil: inatakiwa kama hujasaini ujaze form je ulisain?

Hawa: Wakala wangu hakupewa

Wakili: Aliomba?

Hawa: Hakuomba

Wakili: Je unafaham tofauti ya kura zako ulizopata na za mh Mnyika ni ngapi baada ya matokeo kutangazwa?

Hawa: ndio nafaham

Wakili: ni ngapi?

Hawa: 16198

Wakili: Madai yako kuwa kuna kura 14854 ambazo kwenye majumuisho hazieleweki zilikotokea....je unadhan kama ukipewa kura zote na kuassume ni zakwako je zitabadili matokeo?

Hawa: Hazitabadilisha matokeo

Wakili; kama hazibadili sasa madai yako makubwa hasa ni nini?

Hawa: Madai yangu ni ukiukwaji wa utaratibu wa majumuisho

Wakili: Mh.Mnyika anahusika vipi na huo utaratibu?

Hawa; sijui

Wakili: je,,matokeo yaliyoko kwenye form namba 21 ambayo ni ya matokeo ya jumla ya kwenye vituo yanayoonyesha ulipata kura 50544 unamashaka nayo?

Hawa:Sina mashaka nayo

Wakili:Kama huna mashaka nayo basi hakuna tatizo kwenye ushindi wa Mh.Mnyika

Hawa:sikulalamikia ushindi bali utaratibu

Wakili:Kama ndivyo basi inaonyesha huna imani na tume ya uchaguzi?

Hawa:ninaiman nayo

Wakili:Je Unakumbuka siku ya kuhesabu kura mkurugenzi wa uchaguzi kutoka tume Kiravu alikuwepo?

Hawa:ndio alikuwepo

Wakili:we huoni kama mlikuwa mna bahati ya pekee kuwa na mkurugenzi kwenye kituo chenu cha kuhesabia kura?

Hawa:ndio ni bahati kubwa

Wakili:sasa iweje wewe huna imani na utaratibu uliotumika?

Hawa:kwa kweli hata mm hapo sielewi

2. DAI LA PILI: MALALAMIKO YA VITUO KUWA UAINISHAJI WA KURA KWENYE FOM HAUELEWEKI

Wakili: Je ni vituo vingapi unavyovilalamikia?

Hawa:sijui wakala ndiye aliyeniambia mm sikuwepo

Wakili: Kwenye madai ya awali (Amended Petition) ulisema na ukasaini kuwa ulishuhudia wewe mwennyewe na unajua,,sasa iweje hapa mahakaman unakataa?

Hawa: Sina uhakika kama nilisema hivyo

Wakili: Je..Kingereza unakijua?

Hawa: Najua lakini cha kuokoteza

Wakili:Angalia hii (anampatia Amended petition ya madai yake)

Hawa;(Anaangalia )

Wakili:Je haya madai yaliyoandikwa humu na wakili wako na kusainiwa na wewe unayatambua?

Hawa:Ndio nayatambua

Wakili;sasa mbona unapinga hapa mahakaman kuwa anayejua kila kitu ni wakala ilihali wewe umesaini huu waraka?

Hawa: Ni kutojua sheria tu.

3. DAI LA TATU :KUKASHIFIWA KWENYE MKUTANO WA TAREHE 11/09/2010 KUWA AMEUZA NYUMBA YA UWT

Wakili:je wakati huo Mh.Mnyika anakukashfu ulikuwepo?

Hawa:hapana sikuwepo ila niliambiwa na shahidi wa pili ambaye ni Robert Bondera

Wakili:baada ya kuambiwa ulichukua hatua gani?

Hawa:sikuchukua hatua yeyote na ndio maana nikaileta huku mahakamani

Wakili;je unazijua form za maadili?

Hawa:ndio nazijua

Wakili:je,ulijaza form na kusaini?

Hawa:ndio

Wakili:form zinaelekeza kama mgombea akikashifiwa wakati wa kampeni anatakiwa aandike malalamiko kwa mwenyekiti wa uchaguzi wa jimbo ambaye ni mkurugenzi .Je ulifanya hivyo?

Hawa:sikufanya

Wakili:je tarehe 30/07/2010 ulihojiwa na TAKUKURU kuhusu tuhuma za rushwa na jalada halijafungwa.ni kweli?

Hawa:ahaaa nilihojiwa ,,ni kweli lakini sikuwa na ufaham wa kukumbuka kama limefungwa au bado.

Wakili:wakati wa kipindi cha mijadala ya mchakato majimboni kuna mwananchi alikuuliza juu ya wewe kuhusika na uuzaji wa nyumba ya UWT..Ni kweli?

Hawa:Ndio ni kweli

Wakili;Ulisema utamshtaki,,je ulifanya hivyo?

Hawa;sikufanya hivyo

Wakili:kwa nn hukumshtaki ilihali ulishatangaza hadharani?

Hawa:nilipuuzia kwasababu haikuwa kweli

Wakili:kutokumshtaki kwako huoni kama kuna ukweli ndani yake?

Hawa:si kweli ..mm ndiye ninayesema

Wakili:wakati wa kampen mlikuwa mnaongozwa na nn?

Hawa:Na ratiba ya kampeni za nje

Wakili:je wakati mnapobadili ratiba ya mkutano mnetumia njia gani ya maandishi au simu?

Hawa;Maandishi

Wakili;Unaijua ratiba ya tume kama ukionyeshwa.

Hawa:ndio

Wakili(anampa na kumwambia asome tarehe hiyo 11/09/2010 ambayo anadai kukashifiwa kwenye mkutano Riverside)
Je,,kwenye hii ratiba inaonyesha chadema walikuwa na mkutano sehemu gani?
Hawa:haionyeshi kama walikuwa na mkutano

Wakili:sasa haya madai ya kukashifiwa tarehe hiyo uliyapata wapi wakati umekiri kuwa hawakuwa na mkutano kwa mujibu wa ratiba ya tume ya uchaguzi

Hawa:niliambiwa na shahidi wangu

Wakili:basi shahidi atatuhakikishia ukweli atakapokuja

HAKIMU
Wakili:umesema wakati mnyika anatangaza nia ya kugombea alimkashfu Hawa,,je haya maneno ni sahihi?
shahidi:ndio ni kweli


SIKU NYINGINE
DAI LA KURA HEWA ELFU 15.
SHAHIDI WA HAWA NG'HUMBI.

Wakili; katika chumba cha majumlisho ya jumla, baada ya kumaliza kujumlisha kura vyama shiriki vinapata nakala?
Shahidi: Ndio wanapata.

Wakili: uchaguzi 2010 je vyama vilipata nakala?

Shahidi: ndio, na ni kwa chama changu.

Wakili: je nakala ulizotoa ni sahihi?

Shahidi: ndio, ni sehemu ya nakala

Wakili:huwa mnapewa copy au 0riginal?

Shahidi: tunapewa copy

Wakili: kwanini sasa hapa mahakamani umeleta photocopy badala ya copy ya original?

Shahidi: mi sijui labda umuulize wakili wangu.

Wakili: je kwy fomu ilizoleta mahakamni kuna wakala wa ccm?

Shahidi: ndio

Wakili:je una wasiwasi na wakala wa ccm?

Shahidi:sina wasiwasi

Wakili: anaonyesha fomu ambayo wakala wa ccm katika kituo amesaini. Je aliyesaini ni wa chama gani?

Shahidi: mi sijui sababu sikuwepo.

Wakili: ok

Wakili:je unaudhibitisho juu ya laptop unazodai mnyika amezingiza kwa ajili ya kuhesabia?

Shahidi:sina udhibitisho.

WAKILI WA MLALAMIKIWA.
Wakili: fomu ya matokeo inaonyesha wewe ukusaini, je unaidhibitishia vipi mahakama kama ulikuwepo siku ya majumrisho?

Shahidi: nilikuwepo na mimi nilipewa nakala.

Wakili: bado hujajibu swali, kwa maana hiyo hukuwepo na hayo maneno umeyatunga.

Shahidi; nilikuwepo na hata chama changu kinajua.

Wakili: ulisema mnyika aliingia na wafuasi wake zaidi ya nane, na uliwataja wanne tu, kama ulikuwepo taja na wengine waliobaki?

shahidi: wanatosha hao niliowataja.

Wakili: ulisema mnyika aliingia na wafuasi wake, je kati ya wewe na mnyika nani alianza kuingia ktk chumba cha majumuisho.

Shahidi: mnyika alianza.

Wakili:sasa ulionaje kama mnyika aliingia na wafuasi wake?

Shahidi: kuna baadhi walikuja baada na wengine ni kabla.

Wakili: ulisema wale waliongia walikua wanawazonga wasimamizi, je watu wa usalama hawakuwepo?

Shahidi: ndio walikuwepo.

Wakili: je ulikwenda kuwalalamikia kwa watu wa usalama?

Shahidi: sio jukumu langu.

Wakili: ni jukumu la nani?

Shahidi; msimamizi wa uchaguzi.

Wakili: mlipata bahati ya kuwepo kwa mkurugenzi wa uchaguzi [kiravu] kwa nchi nzima, je naye ulimlalamikia?

Shahidi: nilimlalamikia

Wakili: alikujibu nini?

Shahidi: hakunijibu

Wakili:je wale wafuasi wa mnyika walikua na shughuri gani?

Shahidi: kuwazonga wasimamizi

Wakili: je watu wa usalama hawakuwazuia?

Shahidi: ndio hawakuwazuia

Jaji: umeathiri vp matokeo?

Shahidi: kupatikana kwa kura hewa hizo elfu 15

Wakili: wakati wa kampeni ulisema ratiba ya tume ilikua haifuatwi, je ni kwa chama chako tu au na vingine?

Shahidi; vyama vyote

Wakili: unaushahidi gani kama vyama vingine havifuati?

Shahidi: ilishawahi kutokea kwa mgongano wa kuingiliana kwa mkutano maeneo ya mbezi kati ya ccm naa cdm

Wakili: nani siku hiyo alikua na ratiba ya mkutano kwa mujibu wa ratiba ya tume?

Shahidi; cdm

Wakili: je unajua idadi ya fomu ulizoleta hapa mahakamani unazolalamikia.

Shahidi: sio dai langu.

Jaji: aliingia jaji na kusema unapaswa kujibu sababu umeleta hapa mahakamani ni lalamiko.

Shahidi: sijui.

Wakili: moja kati ya kazi ya wakala wa ndani wa majumuisho ni kurekebisha kasoro zilizojitokeza kwenye vituo, ni kweli?

Shahidi: sio

Wakili: wakili akampa fomu asome sehemu ambayo inaelezea moja ya kazi ya wakala na hiyo aliyoisema wakili ipo.

Shahidi: mimi sijui hicho.

Wakili: je unajua tofauti ya kura kati ya mnyika na hawa ng'humbi?

Shahidi: sijui

Wakili: sasa uliwakilisha nini kama hujui?

Shahidi: na ndio maana sikusaini baada ya kuona madudu niliacha.

Wakili: je baada ya kuona kuna kasoro je ulijaza fomu za malalamiko?

Shahidi: hapana

Wakili: kuhusu mnyika kuingiza laptop zake na kuzitumia kwa ajili ya majumuisho, je zilikua ngapi?

Shahidi: tano

Wakili: je alizibeba mwenyewe?

Shahidi: ndio alibeba mwenyewe zote tano.

Wakili: je wakati mnyika anaingiza hizo je za tume zilikua mbovu?

Shahidi: hazikua mbovu, bali zilikua slow.

Wakili: wakati unajielezea mwisho ulisema matokeo yabatilishwe na uchaguzi urudiwe ni kweli?

Shahidi: ndio

Wakili: kwanini uchaguzi urudiwe na si kuhesabiwa tena kura za kwenye mabox, ambazo bado yapo hadi leo yameifadhiwa na tume na utaratibu huu upo?

Shahidi: siwezi kusema kura zihesabiwe wakati nilishasema uchaguzi urudiwe.

Jaji: jaji aliingilia kati na kumwambia shahidi ajibu swali na si maelezo.

Shahidi: sikujua kama utaratibu huo upo.

Wakili: sasa ushajua utaratibu huo upo wa kuhesabiwa kura tena kama kuna utata, je uko tayari?

Shahidi: nipo tayari.

Wakili: ok mh jaji mi nimemaliza.

Jaji: kuna shahidi mwingine

Wakili wa mshitaka: alipaswa kufika lakini hajafika hadi muda huu na hiyo ni kutokana na kuchelewa kupewa ruhusa.

Jaji: je kesho mna uhakika atakuja?

Wakili: ndio mh jaji. Mara wakili aliongea na mgombea [mlalamikaji] na kumpa taarifa wakili kuwa shahi wan ne hawezi kuja amekataa.

Wakili: akatoa taarifa kwa jaji

Jaji: je zaidi ya huyo kuna shahidi mwingine.

Wakili: hakuna, kwa maana hiyo tumefunga mashahidi kwa upande wetu.

Kesi imehairishwa hadi tarehe 29/03/2012 saa tatu asubuhi, mahakama ya kazi iliyopo akiba

SIKU NYINGINE 30/03/2011
Ufafanuzi:

Wakili J- Wakili Mbogolo, wakili mtetezi kwa John John Mnyika

Wakili H- Wakili Maige, wakili wa mshati, Hawa Nghumbi

Wakili G- Wakili Mulokozi, Wakili mtetezi kwa serikali

Wakili J: Ieleze mahakama wewe ni nani?

Mnyika: John John Mnyika, miaka 31, mkristu, mkazi wa Sinza

Wakili J: Unafanya shughuli gani?

Mnyika: Ni mbunge, Mkurugenzi wa chama idara ya habari na uenezi Makao Makuu ya CHADEMA, Mwenyekiti CHADEMA kanda Kinondoni, DSM.

Wakili J: Ulishiriki vipi uchaguzi Mkuu 2010?

Mnyika: Nilikuwa mgombea niliyependekezwa na CHADEMA, na kuteuliwa. Nilishiriki katika kampeni kama mgombea lakini vile vile wakati wa kampeni nilikuwa Kaimu Katibu Mkuu wa CHADEMA Taifa. Pia nililikuwa Katibu wa Timu ya Taifa ya kampeni ya CHADEMA. Nilikuwa mjumbe wa Kamati ya kampeni ya CHADEMA jimbo la Ubungo.

Wakili J: Wagombea walikuwa wangapi?

Mnyika: walikuwa 16

Wakili J: Matokeo?

Mnyika: Nilitangazwa mshindi

Wakili J: Lini na nani alikutangaza?

Mnyika: Nilitangazwa tarehe 02/11/2010 na Msimamizi wa Uchaguzi, Bwana Nduguru

Wakili J: Mlalamikaji anapinga ushindi na ametoa sababu tano. Tuanze, je kampeni zilikuwa zinaongozwa vipi na kuratibiwa?

Mnyika: Zilikuwa zinaongozwa na nyaraka mbalimbali. 1. Ratiba ya kampeni-ambayo ilikuwa inaonyesha nani anakuwepo wapi 2. Sheria- mbalimbali kama sheria katika uchaguzi 3. Maadili ya uchaguzi-ambayo nilisaini kama mgombea na yalikuwa yanatuongoza. 4. Maelekezo ambayo tume ilitupa wagombea na pia kutoa nakala kwa vyama vya siasa.

Wakili J: Ratiba ya kamepni iliandaliwa na nani?

Mnyika: Katika ndani ya ngazi ya chama kamati ya kampeni tuliandaa mapendekezo ya ratiba kasha tukawasilisha kwa msimamizi wa uchaguzi kwa maandishi. Msimamizi wa uchaguzi akaitisha kikao cha vyama vya siasa. Na baada ya kikao hicho Msimamizi akaleta kwa barua nakala ya ratiba ya kampeni. Ambayo mimi kama mgombea nilipewa nakala na chama vilevile.

Wakili J: Angalia nayaraka hii

Jaji: Ni nini?

Mnyika: Ratiba ya kampeni za uchaguzi manispaa ya Kinondoni.

Wakili J: Mwezi gani?

Mnyika: Septemba, 2010

Wakili J: Unakumbuka mratibu wa kampeni zako?

Mnyika: Ndiyo. Nilikuwa na waratibu wawili. Mratibu Mkuu ambaye tulikuwa tunamwita pia Mwenyekiti, anaitwa Eric Ongara na mwingine Ally Makwilo.

Wakili J: Shahidi alisema mlikuwa wapi Septemba 11, 2010?
Mnyika: Alisema nilikuwa na mkutano eneo la Riverside siku hiyo Septemba 11, 2010 jumapili

Wakili J: Ulitoa matamshi gani?

Mnyika: Nimesikia madai kuwa nilitoa matamshi kuwa yeye ni fisadi

Jaji: yeye nani?

Mnyika: yeye mlalamikaji Hawa Nghumbi ni fisadi kwa kuwa ana tuhuma za kuuza nyumba za UWT

Wakili J: alisema katika mkutano alikuwepo?

Mnyika: alisema hakuwepo ila aliambiwa

Wakili J: Aliambiwa na nani?

Mnyika: alisema aliambiwa na mwanachama wake ambaye alitaja jina hapa mahakamani Mheshimiwa Jaji.

Jaji: alitaja jina gani?

Mnyika: Sikumbuki ila alikuja kutoa ushahidi kama shahidi namba 2 Mheshimiwa Jaji

Wakili J: Unaiambia nini mahakama juu ya hayo?

Mnyika: Aliyosema si ya kweli. Tarehe 11/09/2010 sikuwepo Riverside. Nilikuwa katika mkutano mwingine ya hadhara; asubuhi Ubungo eneo la Msewe-Msikitini. Mchana mpaka jioni; nilihamia kata ya Saranga eneo la Stop-over. Na siku hiyo kwa kumbukumbu zangu ni siku ya jumapili na si jumamosi kama ilivyodaiwa hapa mahakamani mheshimiwa Jaji.

Wakili J: Shahidi #2 alisema ulianza kwa kufanya nini?

Mnyika: Kadiri ya maelezo yake nilianza kwa kutangaza nia ya kugombea ubunge. Na baadae nikaelezea sababu ya kugombea. Baadae akaendelea kutoa maelezo mgombea wa CCM asichaguliwe kwa sababu ni fisadi kutokana na tuhuma kushiriki kuuza nyumba UWT.

Wakili J: Unaielezaje mahakama juu ya hayo?

Mnyika: Maelezo yaliyotolewa na shahidi juu ya mimi kutangaza nia. Maelezo hayo yanadhihirisha kuwa shahidi husika hakuwa akihudhuria mikutano yangu ya kampeni toka kanpeni zilivyoanza rasmi. Kwa sababu mimi nilitangaza nia ya kugombea ubunge mwezi Machi, 2010. Nilitangaza kupitia vyombo vya habari, mkutano ya hadhara na taarifa hiyo nilisambaza katika mitandao ya kijamii kwa maana ya kupitia internet. Rekodi hizi zipo. Hivyo, sikuwa na sababu mwezi wa Septemba baada ya kuwa nimeshapendekezwa na chama na nimeshakwisha kuteuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi na nipo katikati ya kampeni kutangazia wananchi nina nia ya kugombea ubunge ambao nilikuwa nagombea tayari.

Wakili J: mlalamikaji anasema kutokana na kauli hiyo ilipelekea kushindwa

Mnyika: Kwanza sijazitoa kauli hizo. Sikuwepo. Pili, iingie kwenye kumbukumbu ya mahakama yako tukufu Mheshimiwa Jaji mwaka 2010 nilikuwa nagombea kwa mara ya pili. Mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2005 ambapo kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na tume nilipata kura zaidi ya elfu 45. Pia iingie katika kumbukumbu jimbo la Ubungo ndilo jimbo lenye wapiga kura wengi kuliko jimbo jingine lolote Tanzania, wapiga kuwa laki nne na hamsini elfu.

Wakili J: Mahakama ielewe nini wapigakura lakinne na hamsini elfu.

Mnyika: Ielewe kuwa katika kampeni zenye siku 90, zenye kufanywa kwa mikutano katika mitaa mingi ndani ya kata zilizopo kwenye jimbo, mkutano mmoja ieleweke si rahisi kuathiri matokeo.

Wakili J: Hii tuhuma ya kuuza nyumba za UWT ulipata kuisikia?

Mnyika: Ndani ya kumbukumbu zangu Mheshimiwa Jaji, nilipata kuisikia. Mosi, kabla ya kampeni wakati wa kura za ndani za CCM, walikuwa wanatuhumiana wao kwa wao. Na iliandikwa na moja ya vyombo vya habari. Pili, nilisikia moja kwa moja Agosti 28, 2010 wakati mimi na mlalamikaji tukiwa katika kipindi cha mchakato majimboni kilichokuwa kinarushwa moja kwa moja na TBC1, mmoja wa wananchi waliohudhuria alimuuliza swali mlalamikaji Hawa Nghumbi, alimuuliza swali kuhusiana na tuhuma hiyo. Nikawa nimeisikia tena kwa mara nyingine. Na …

Wakili J: Unakumbuka nini?

Mnyika: Nakumbuka aliahidi kwa kurudia mara mbili kwamba atamshtaki aliyetoa tuhuma.

Wakili J: Hapa mahakamani una kumbuka nini juu ya madai hayo alisema?

Mnyika: Hapa mahakamani alisema, hakumshtaki mpaka sasa kwa kuwa alisema madai si ya kweli hivyo akayapuuza.

Wakili J: Mahakama ielewe vipi kuhusiana na tuhuma hizo?

Mnyika: Ningependa mahakama irejee kwenye ukweli kwamba madai yake mimi nilikuwa tarehe 11 Septemba, 2010 siku ya jumapili nilikuwa Riverside nikatoa tuhuma. Na ukweli nilioeleza sikuwapo Septemba 11, 2010 Riverside. Na pia haikuwa siku ya Jumapili kama ilivyodaiwa hapa mahakamani Mheshimiwa Jaji na mlalamikaji na ukweli tuhuma zote hizo zilisemwa kabla ya tarehe hiyo na hakuchukua hatua zozote kuhusiana na hizo tuhuma. Na kwamba kama angekuwa na malalamiko dhidi yangu katika kampeni, wote tulisaini maadili ya uchaguzi. Na maadili hayo yalimpa fursa ya kuwasilisha malalamiko. Nasikumbuki kupewa malalamiko. Hivyo hakutumia fursa hiyo. Pia mkutano mmoja hauwezi kuathiri matokeo kwani kampeni zilifanyika kuanzia Agosti mpaka ukomo wake Oktoba.

Wakili J: Juu ya Majumuisho ya kura. Majumuisho yalifanyika lini?

Mnyika: Tulianza mchakato wa majumuisho Oktoba 31, 2010. Na nasisitiza neno tulianza "mchakato". Usiku wa tarehe 31 saa sita kasoro mimi na wakala wangu tulienda Loyola baada ya kupewa barua. Tulipofika, tuliambiwa tunaanza kupokea matokeo na masanduku.

Jaji: Ulienda na mawakala wako?wangapi? nani?

Mnyika: Mmoja, Bwana Eric Ongara

Mnyika: Nilifika tukakuta eneo la kukaa mawakala. Nikakuta mawakala wengine. Tukaelezwa zoezi la kuhesabu litaendelea, tusubiri kuendelea kupokea vifaa na tukawepo pale usiku mpaka usiku wa manane. Baadae nikatoka na kumwacha wakala wangu.

Jaji: Kwa hiyo ulikuwepo kushuhudia kupokea vifaa?

Mnyika: Ndiyo mheshimiwa Jaji. Na nikatoka baadae nikamwambia wakala wangu anijulishe zikibaki kata chache ili nirudi.

Jaji: asubuhi saa ngapi?

Mnyika: 01/11/2010 around saa nne nikaambiwa nirudi. Nikapokea fomu chache zilizobakia.

Wakili J: Majumuisgho yalianza saa ngapi?

Mnyika: Saa tano asubuhi ndipo majumuisho yalianza Mheshimiwa Jaji.

Wakili J: Ulikuwepo?

Mnyika: Mimi nilikuwepo Mheshimiwa Jaji.

Wakili J: Ulifika na nani?

Mnyika: Mimi nilifika nikiwa mikono mitupu. Na wakala wangu alikuwa tayari ndani.

Wakili J: Umemsikia shahidi yeye alifika saa ngapi?

Mnyika: saa 3 usiku siku ya 01/11/2010

Wakili J: Kati ya wewe na yeye nani alimtangulia mwenzake?

Mnyika: Mara zote yaani 31/10/2010 na 01/11/2010 mimi niliwahi kumtangulia.

Wakili J: Ametoa tuhuma nzito sana, unakumbuka ulisema nini?

Mnyika: Nilikuja na wafuasi nane. Nikiwa nimebeba laptop 5 nimezibeba kwa kuzikumbatia.

Wakili J: laptop?

Mnyika: Madai hayo si kweli mheshimiwa Jaji. Haiwezekani mtu niliyeingia kabla yake awe aliniona nimeingia na laptop. Lakini ukweli wakala wangu Eric Ongara alikuwa na laptop. Huu ni ukweli.

Jaji: Alikuwa na laptop ngapi?

Mnyika: alikuwa na laptop moja mheshimiwa Jaji.

Wakili J: Vipi kuhusu mawakala wengine?

Mnyika: Nilikuta mawakala wengine. Hao walikuwa na laptop. Alex Mayunga wa AFP, alikuwa na laptop na laptop ya wakala wa CHAUSTA anayeitwa Michael John. Nazikumbuka laptop hizo. Tulipoketi, kulikuwa na waangalizi toka kituo cha Haki za Binadamu (LHRC), simkumbuki jina. Kulikuwa na mwangalizi wa Tanganyika Law Society (TLS), John Seka. Hawa waangalizi walikuwa na laptop wanatumia.

Wakili J: Laptop zilikuwa zinatumikaje?

Mnyika: Ni zungumzie mimi na wakala wangu namna alivyokuwa anatumia. Kura zilipigwa kwenye vituo, matokeo yakatangazwa kwenye vituo. Mawakala katika vituo wakapewa nakala ya fomu za matokeo vituo 1013. Sisi kwenye kamati yetu ya kampeni.

Jaji: Walipewa lini?

Mnyika: Wote walipewa 31/10/2010 ila mida ilikuwa imetofautiana. Ila ilipofika saa nne usiku. Tulikuwa na nakala za matokeo ya vituo. Tulipokwenda saa sita kasoro tulikwenda na fomu za matokeo. Wakala wetu aliweza kwenda na watu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi sambamba katika kuhakiki, sisi tulikuwa tunatumia laptop yetu ambayo haikuwa na programu kama yao. Kituo kikiingizwa katika majumuisho nasi tuliingiza katika laptop kujumlisha kadiri ya wakala na taarifa tulizokuwa nazo.

Wakili J: Hivyo hiyo ndiyo kazi ya laptop ilikuwa nayo?

Mnyika: Ndiyo

Wakili J: Mdai anasema ulipika matokeo hewa kwa matumizi ya laptop yako

Mnyika: Nimeeleza awali Mheshimiwa Jaji, matokeo awali yalitangazwa katika vituo. Huwezi kupika matokeo bila kuwa na fomu mbadala na ushahidi mbadala. La pili, laptop ya wakala wangu Mheshimiwa Jaji haikutumiwa na Tume. Hivyo isingeweza kupika matokeo

Wakili J: Sheria inataka wajumlishe kwa njia gani?

Mnyika: Kwa uzoefu wangu wa kisheria kwa kushiriki katika chaguzi na nyaraka za uchaguzi. Hakuna maelezo ya kifaa gani kitumike. Kinachoelezwa katika sheria na maelezo ya vyama kwa wagombea. Msimamizi wa Uchaguzi anapaswa kutaja kwa sauti kura ili wote waweze kujumlisha. Upande mmoja wa nukuu yaani Tume, pia wengine wenye uwezo wa kujumlisha ili waweze kuhakiki ujumlishaji wa matokeo kwa wagombea. Hatua hii ilifatwa pia Loyola

TUMBIRI (PhD In Progree at HULL, CPA(T), MBA(UDSM), Bcom(UDSM), PCM(Mzumbe High School - 2[SUP]nd [/SUP]Best Student in Form Six National Exams),
tumbiri@jamiiforums.com
 

Habarindiyohiyo

JF-Expert Member
Aug 11, 2008
263
0
Rufaa ya Hawa Ng'umbi dhidi ya Mnyika ni kesho kutwa Disemba 7, kwa namna ambavyo Mnyika aliingia na laptop zake na kundi kubwa la watu na kulazimisha tume imeongezee kura hewa zaidi ya 14,000 hatma ya ubunge wake iko mikononi mwa jopo la majaji watatu.

....ndiyohiyo
 

Matola

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
45,015
2,000
Rufaa ya Hawa Ng'umbi dhidi ya Mnyika ni kesho kutwa Disemba 7, kwa namna ambavyo Mnyika aliingia na laptop zake na kundi kubwa la watu na kulazimisha tume imeongezee kura hewa zaidi ya 14,000 hatma ya ubunge wake iko mikononi mwa jopo la majaji watatu.

....ndiyohiyo
Mbona unaweweseka wewe mbulula? mara unasema Ubunge wa Mnyika kukoma December 7 mara uko mikononi mwa majaji, hivi una uewelewa hata finyu wa kujuwa namna rufaa zinavyosikilizwa na kupangiwa tarehe za kusomewa Hukumu? Kilaza 100% wewe.
 

Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
58,497
2,000
Rufaa ya Hawa Ng'umbi dhidi ya Mnyika ni kesho kutwa Disemba 7, kwa namna ambavyo Mnyika aliingia na laptop zake na kundi kubwa la watu na kulazimisha tume imeongezee kura hewa zaidi ya 14,000 hatma ya ubunge wake iko mikononi mwa jopo la majaji watatu.

....ndiyohiyo

hizi gharama za kufungua kesi mnazoshindwa kwa aibu pesa huwa mnatoa wapi??
 

frema120

JF-Expert Member
Jan 1, 2012
5,099
1,195
Nauliza sheria inasemaje kama mrufani ( hawa) hayupo dunian kesi sindio mwisho wake au ? ( kwan hawa si marehemu?????)

V
SENGEREMA
 

Zogwale

JF-Expert Member
Jul 10, 2008
14,900
2,000
Hivi wana JF hebu tusaidieni hizi pesa za RUFAA za kesi za uchwara kama hizi huwa zinagharamiwa na vyama husika au ni nani? Kwa mantiki hii hizi kesi za SSM hebu sasa muamue kutumia hizi pesa za walipa kodi kwa manufaa ya watanzania. Uchafu mtupu.
 

mayenga

JF-Expert Member
Sep 6, 2009
4,120
2,000
Kwa taarifa za uhakika nilizonazo Hawa Ngumbi ameamua kuondoa rufaa yake Mahakama ya Rufaa,hivyo kusikilizwa kwa rufaa hakupo tena na bwana mdogo Mnyika anapeta mpaka 2015.
 

nyabhingi

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
15,106
2,000
yule mama anapenda kusuguana mabega na dogo mnyika kwenye benchi la mahakama...hii kesi hata ukimpa nchemba aliyekunywa maji ya bendera la kijani na njano na mwenye upeo mdogo anampa ushindi kamanda mnyika!!!kwa sababu kubaka mahkama ni kawaida yenu mnaweza kumrudishia ubunge lema na kutengua kijambazi wa mnyika ili muharibu balance ya hoja nzito bungeni...sh..wa.ini
 

mwemanga

Senior Member
Oct 22, 2012
120
195
Rufaa ya hawa ng'umbi zidi ya john mnyika inaaza kusikilizwa kesho mahakama ya rufaa posta wanachadema wananchi na wapenda mabadiriko wote tufutilie kwa karibu rufaa hiyo.
 

kapya

Senior Member
Oct 5, 2012
153
225
Mnyika hana chake hapo kudadadeki.
watoto wa chichidodo(mang'ula)utawatambua tu(hoja mpauko kinoma)..................kamanda tupo pamoja.....mwache hawa aendelee kuhangaika.....hivi anadai nini hasa,viongozi wengine bana utumbo mtupu..............waiting for 2015
 

frema120

JF-Expert Member
Jan 1, 2012
5,099
1,195
Hawa Ngumbi si marehemu huyu jamani? au? kwa sheria inasemaje hapo kama mrufani ni marehemu msaada kwa hiliiii pls?

V
SENGEREMA
 

MNYISANZU

JF-Expert Member
Oct 21, 2011
7,047
2,000
Hawa Ngumbi si marehemu huyu jamani? au? kwa sheria inasemaje hapo kama mrufani ni marehemu msaada kwa hiliiii pls?

V
SENGEREMA
Mkuu umechanganya. Marehemu ni Hawa Ngulume na si Hawa Ng'humbi. Kuwa makini siku nyingine.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom