Baada ya Dr Kafumu kugoma kukataa rufaa sasa Tume ya taifa ya uchaguzi inatakiwa kuitisha uchaguzi mdogo wa Igunga. CCM wakiwa hawaamini kinachotokea wamebaki wakishangaa wakitafuta mbinu za kuchelewesha uchaguzi.
M4C, Nguvu ya umma na chama cha wananchi Chadema wamejipanga kuchukua jimbo la Igunga kuwahakikishia CCM hawana ngome tena popote. Igunga inakwenda kutoa mwelekeo wa 2015 na hapo ndipo CCM wanataka kutafuta jinsi ya kujificha.
Dr kafumu ameona siasa zimemyeyusha na alitapeliwa ili aondoke madini kwani ni kati ya watu waliokuwa makini na wazalendo, alijitahidi sana kukataa vi-memo vya wizi ila hakujua mbinu chafu, akajikuta kwenye kampeni za rushwa, maneno machafu, ghiliba na udini, huku matapeli wa ccm wakitoa ahadi za hewa na za utengano baina ya dini na dini na koo na koo, leo hii Dr kafumu anaonekana mgeni ndani ya jimbo alilozaliwa.
Kampeni chafu za CCM zilisababisha uzinzi, wizi wa wake za watu, vifo, uharibifu wa mali za raia na matumizi ya silaha za moto kutishia watu na mali zao. Huku Mbunge wa Tabora mjini akiitumia juu ya jukwaa kutishia wapiga kura bastola yake iliyokuwa ikining'inia kiunoni.
Ahadi hewa za Kuwahadaa wananchi bila kafumu hakuna daraja la mbutu na mengine mengi. Dr Kafumu baada ya kuona kachafuliwa vya kutosha sasa atangaza kujikita kwenye taalauma yake na kuachana na siasa. Kibarua hiki kinawafanya CCM ama kutafuta mgombea mwingine au kumrudia Rostam Azizi arudi kugombea Igunga kwani swala la kuvua gamba limekwisha na wamewaangukia wote waliosema ni magamba na kuwaambia zilikuwa kelele za Nape tu. Kwa kuwahakikishia kwamba hakukuwa na swala la kujivua gamba wamemwakikishia RA kwa kuwarusdisha magamba wenzake kwenye kinyang'anyiro cha NEC mzee wa vijisenti na mamvi.
CDM wanasubiria kauli ya Tue ya uchaguzi ili haki itendeke na kura iwe ndio njia pekee ya kuchagua mgombea. ikumbukwe katiba mpya inatakiwa iweke bayana jinsi ya kuendesha mapingamizi ya ubunge badala ya kusubiria kesi muda mrefu ni heri kuweka pingamizi na kusikiliza kesi kabla ya kutangaza mshindi ili kuweza kutangaza mshindi baada ya kila kesi kufungwa na kutoa mwanya wa kutokuwa na kesi mbeleni, hii itasaidia kuwapa wabunge muda wa kufanya kazi na kuepuka gharama nyingi za chaguzi ndogo.
Chief Mkwawa wa Kalenga
Mungu akipenda huwezi badilisha - CDM 2015 Ikulu hakuna wa kuzuia.