Ruby - Forever; Wimbo wenye Video "Covers" za Kutosha tu

Shark

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2010
Posts
29,966
Reaction score
30,132
Wadau kwema??

Leo nikiwa nasafiri kutokea Morogoro kuja Dar, njiani kwenye Bus katika video tulizowekewa ni pamoja na ya Msanii anaitwa Ruby, wimbo ni Forever ule Original Version ukiacha remix iliyofanywa na Msanii Chemical.

Sasa basi Video niliyoiona kwa kweli sikua nimeielewa elewa, hata nikadhani labda pengine ni sababu ya uchovu wa safari au nilisinzia. Maana niliekua nikumuona pale hakua Ruby naemjua. Huyu alikua kidogo kibonge japo TV ya kwenye Bus ilikua mbali kidogo lakini nilijihakikishia kua sie yeye.

Kufika home baada ya kupumzika nikasema nifungue Laptop ni-google Video ya huo Wimbo ili nione Video yake aliicheza nani. Yaani kufungua nikakutana na Video "Cover" kama 20 au zaidi hivi zote zimechezwa na Watu mbali mbali. Kuna zilizochezwa mpaka nje ya nchi, vijijini, vikatuni etc. lakini audio imebaki ileile ya Ruby.

Kilichonishangaza ni kua sijaona hata moja ambayo amecheza Mwenyewe Ruby zaidi ya hizo "Covers" zake. Maana katika kufuatilia kwangu kote sijawahi kuona Wimbo wa kibongo wenye Covers ningi namna hii. Hii kitu imenishangaza sana maana nimeshindwa kuelewa nini kilisababisha hivyo. Nimewaza labda ni wimbo mzuri sana kiasi kila alieusikiliza aliamua kuundia story akajirekodi ama vipi.

Pengine tunaweza kusadiana hapa nini kilitokea kwa huu wimbo, ila ni Mzuri pia.
 
RUBY ALITOA TANGAZO WATU WAFANYE VIDEO YA WIMBO ULE,ATAKAESHINDA NDO ITAKUWA VIDEO RASMI NA PIA ATAMPA ZAWADI.
Inawezekana mradi huu uliishia njiani.Usione babu wa kariakoo anatumikishwa fiesta sio kwamba anapenda ila anaogopa kupotea kwenye game kama mwanzo.
 
mambo ya babu wa kariakoo yameingiaje hapa na wakati anayetajwa ni Ruby?
 
Najua aligombana na Clouds last year hakushiriki Fiesta aligoma, ila bado nawaza why Wimbo una Video covers nyingi namna hii then hakuna yake hata moja? What happened?
Aliwaambia watu wafanye hivyo
 
RUBY ALITOA TANGAZO WATU WAFANYE VIDEO YA WIMBO ULE,ATAKAESHINDA NDO ITAKUWA VIDEO RASMI NA PIA ATAMPA ZAWADI.
Inawezekana mradi huu uliishia njiani.Usione babu wa kariakoo anatumikishwa fiesta sio kwamba anapenda ila anaogopa kupotea kwenye game kama mwanzo.
Aliwaambia watu wafanye hivyo
Mmhhh, aisee,
Sikujua hili,
Kumbe ndio maana kukawepo Video za Kutosha tu,
Sasa alishinda nani katika hilo Tangazo??
Na haoni kama ilichangia kumpoteza pia??
Yaani wimbo mzuri afanye yeye lakini kwenye Video waonekane wengine, inakuja kweli hii??
Kwa ambae hamjui akiingi Google anakutana na Video mbali mbali za watu wengine, ye Ruby anajitangaza vipi sasa hapo??
 
RUBY ALITOA TANGAZO WATU WAFANYE VIDEO YA WIMBO ULE,ATAKAESHINDA NDO ITAKUWA VIDEO RASMI NA PIA ATAMPA ZAWADI.
Inawezekana mradi huu uliishia njiani.Usione babu wa kariakoo anatumikishwa fiesta sio kwamba anapenda ila anaogopa kupotea kwenye game kama mwanzo.

Hallelujah
 
Mmhhh, aisee,
Sikujua hili,
Kumbe ndio maana kukawepo Video za Kutosha tu,
Sasa alishinda nani katika hilo Tangazo??
Na haoni kama ilichangia kumpoteza pia??
Yaani wimbo mzuri afanye yeye lakini kwenye Video waonekane wengine, inakuja kweli hii??
Kwa ambae hamjui akiingi Google anakutana na Video mbali mbali za watu wengine, ye Ruby anajitangaza vipi sasa hapo??
Waliomfanyia ubaya ni clouds.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom