Rubani na Msaidizi Wake Wanapopitiwa na Usingizi Angani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rubani na Msaidizi Wake Wanapopitiwa na Usingizi Angani

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Aug 19, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Aug 19, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Monday, August 17, 2009 3:12 PM
  Inakuwaje pale rubani na msaidizi wake wanapopitiwa na usingizi na ndege kupita juu ya uwanja wa ndege ambao ilitakiwa kutua? abiria walibaki wakishangaa shangaa wakijiuliza tunaelekea wapi tena. Rubani na msaidizi wake wa ndege ya shirika la ndege la Go! Airlines walipiga mbonji wakati ndege ikiwa angani wakati wakikaribia kufika uwanja wa ndege ambao ndege hiyo ilitakiwa kutua.

  Abiria 43 wa ndege hiyo iliyokuwa ikielekea kwenye kisiwa cha Hawaii kutoka kwenye kisiwa kingine cha Honululu, walibaki wamepigwa na butwaa wasielewe kinachoendelea walipochungulia madirishani na kuona wameupita uwanja wa ndege kwa juu na wameanza kuchanja mbuga kukatiza baharini.

  Rubani huyo na msaidizi wake walizinduka kutoka usingizini baada ya kuamshwa na waongoza ndege kwenye uwanja wa ndege wa Hilo International ambao ndege hiyo ilitakiwa kutua.

  Wakati huo ndege hiyo ilikuwa futi 21,000 toka ardhini na ilikuwa imeshatambaa kilomita 48 kutoka kwenye uwanja wa ndege huo.

  Baada ya kuzinduka marubani hao waliigeuza ndege hiyo na kutua salama kwenye uwanja huo.

  Matokeo ya uchunguzi wa tukio hilo lililotokea mwezi februari mwaka jana, yametolewa wiki hii na bodi ya usalama katika usafirishaji (NTSB) ambayo imethibitisha kwamba marubani hao walilala kutokana na uchovu wa kazi.

  NTSB ilisema kwamba marubani hao walifululiza siku tatu wakiendesha ndege asubuhi kuanzia saa 11 alfajiri.

  NTSB pia ilisema kwamba mbali na uchovu wa kazi, rubani wa ndege hiyo alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa usingizi wa Apnea ambao ulimsababishia awe anasinzia sana nyakati za asubuhi na mchana.
  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=2837054&&Cat=2
   
 2. M

  Magezi JF-Expert Member

  #2
  Aug 19, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Ni mungu tu aliwalinda abiria na siku zao wote zilikuwa bado
   
 3. Gudboy

  Gudboy JF-Expert Member

  #3
  Aug 19, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 799
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  hello ndugu wa JF mimi ni member mpya wa JF na nimefurahishwa sana na hii JF kwa kutupa habari mbalimbali, naombeni muendelee kutupatia habari mbalimbali. ahsanteni
   
 4. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #4
  Aug 19, 2009
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  hii kali ila ndiyo hivyo wale ni binadamu yote yanawezekana. Kumshukuru mungu kabla ya kuanza kazi ni vizuri zaidi.
   
Loading...