Rubani Gower alikufa kishujaa

News TZ

Senior Member
Jun 17, 2015
127
69
2.jpg


Dar es salaam,

Wakati taratibu za kuusafirisha mwili wa rubani Rodgers Gower aliyeuawa na majangili zikiendelea, simulizi za aliyekua naye kwenye helikopta zimesema alikufa kishujaa baada ya kufanikiwa kuifikisha helikopta hiyo chini bila madhara makubwa kwa wenzake.
Wakati hayo yakifahamika, jeshi la polisi limeeleza kuwa linawashikilia watu 6 kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo.

Gower raia wa Uingereza aishiye afrika kusini (37) ambaye alikuwa akiendesha helikopta hiyo aliuawa kwa risasi siku ya Ijumaa akiwa kwenye doria dhidi ya majangili katika pori la akiba la Maswa mkoani Simiyu akiwa na raia wa Afrika kusini, Nick Bester ambaye alinusurika kifo.
Vyombo mbalimbali vya kimataifa vimeelezea siku ya jana kuwa rubani huyo alifariki katika jitihada za kuokoa maisha ya Bester.

Gazeti la The Guardian la Uingereza lilisema baada ya Gower kupigwa risasi mguuni, begani na usoni, alijitahidi kutumia ujuzi wake ili aweze kutua taratibu bila papara.
Gazeti hilo pia lilimkariri manusura huyo akisema Gower aliiongoza helikopta hiyo itue kwenye mti ili kuzuia mlipuko ambao ungegharimu maisha yake.
 
Back
Top Bottom