Rubani auchapa usingizi ndani ya ndege

Hata mimi huwa siwaelewi kabisa, eti ajali haina kinga, mara kifo hupangw
Hata mimi huwa siwaelewi kabisa, eti ajali haina kinga, mara kifo hupangwa na Mungu, nk. Hizi zote ni imani kinyume na Kweli hata
Hata mimi huwa siwaelewi kabisa, eti ajali haina kinga, mara kifo hupangwa na Mungu, nk. Hizi zote ni imani kinyume na Kweli hata za huyu Mungu hakika. Tunajidanganya sana.
 
Vipi kabla ya ndege kugunduliwa kwa vijiakili vya wanadamu Sir God alikuwa hawa assign watu wafe kwa ajali za ndege, kwahiyo naye Mungu anabadilisha gia kulingana na maendeleo yetu wanadamu? Duh! Hii kali.
 
Kichekesho.Ndege kubwa katika masafa marefu Pilot ukishaseti computer zako unaweza ukaondoka kwenye cockpit kwa muda.Kweli ushamba ni mzigo.Walidhani ni basi ambalo dereva lazima ashike usukani kila saa.
 
Hii habari niliisoma sehemu,Pilot alilala for 2 hrs! Ila nadhani alikua anajua kua wapo wenye uwezo wa kuiendesha bila uwepo wake,coz kama ni ajali hata yeye ingemkuta coz nae alikua ndani ya hiyo hiyo ndege.
 
Vipi kabla ya ndege kugunduliwa kwa vijiakili vya wanadamu Sir God alikuwa hawa assign watu wafe kwa ajali za ndege, kwahiyo naye Mungu anabadilisha gia kulingana na maendeleo yetu wanadamu? Duh! Hii kali.
Upeo wetu (binaadamu) wa kufikiria ni mdogo sana. hivyo kuna mambo ukiyatafakari huwezi pata majibu yake, na ndio maana Mungu akashusha vitabu vitupe muongozo katika hili. kuna mambo maswali binaadamu hatuna majibu yake,..

nikuulize swali: je ww unalo ini (liver)? ulishawahi kuliona kama unalo? una uhakika wa asilimia ngapi kama unalo?

nadhani swali lako si kuhusu ajali-ndege things, swali lako ni "je Mungu yupo"? ..

 

Kwenye iyo "reference case" ya mid air collision nakumbuka baada ya ripoti ya ajali kutoka yule lawyer muitaliano aliepoteza mke na mtoto kwenye ajali alisafiri kutoka Italia mpaka ujerumani akaja akamchoma kisu na kumuua yule jamaa wa "tower" aliesababisha ajali..

Kwa kuongezea kidogo hapo: kwenye ndege kuna kifaa kinaitwa TCAS - "Traffic Collision Avoidance System" ichi kifaa kinacontrol ajali kama ndege zinasafiri kwenye usawa mmoja..

Ikitokea hivyo ichi kifaa kinapeleka taarifa kwa ndege zote mbili na kinashauri ndege moja ishuke na nyingine ipande..

Sasa sheria za ndege kwa nchi husika zinatofautiana.. kuna nchi nyingine maelezo ya ATC (controller) ndio yanapewa kipaumbele na sio "Instruments" za ndege hapo ndipo paliposababisha iyo ajali maana ATC aliiambia ishuke ndege iliyopaswa ipande juu na ndipo ajali ikatokea..
 
Huyo rubani ana roho nzuri sana inaonyesha hana mtimanyongo kwa huyo mwanafunzi ndo maana kamuambia dogo komaa
 
Hapana, hujanielewa au ni mimi sijakuelewesha vyema, naamini kuna nguvu ya ASILI ipitayo nguvu zote na ndio asili ya yote, tunamuita Mungu.

Nisichoamini mimi na ambacho ndo ukweli wenyewe, kwamba Mungu anapanga kila kitu kinachomtokea au kumzunguka mwanadamu au viumbe, big no. Ametoa kanuni, ni jukumu letu kunifuata na zipo tangible.

Usipozifuata zitakufikisha mahali na akizifuata pia zitakufikisha mahali pake. Ni kanuni tu, kila idara kuna kanuni zake, pasi kanuni hakuna litakalompa kuwa kuwepo.

Sasa sisi tunavunja kanuni ukilipata linalokupata lawama kwa ASILI kuu, ni kosa. Mfano, gari umeambiwa lipakie watu 30 na tumepewa kanuni za jinsi ya kulimiliki na kuliendesha, menu book, hufanyi, yakikutukia eti Mungu kapanga, hapana.
 
Huu usafiri natumia kwa sababu tu nakuwa sina namna, ila mimi sijawahi kabisa kuizoea ndege, ningekuwa mimi humo nafikiri hali yangu ingekuwa mbaya mno
Ni wasiwasi wako tu ila ujue usafiri wa ndege ndio usafiri salama zaidi kulinganisha na vyombo vyote vingine vya usafiri..
 
sio ishu sanaa ndege za siku hizi ni full auto piloting... marubani tumekuwa kama backup tu.. incase auto pilot ya kiwanja husika haipigi mzigo vizuri!!
 
Kuna kesi moja ilikua ndege ya warusi ilikua inaenda Japan i think basi kuna pilot alikua likizo akawa anasafili na watoto wake sasa ile kupenda sifa akawapeleka watoto wake kwenye cockpit akawaomba wale ma pilot wenzie coz walikua wanafahamiana kuwa mwanangu anataka ku experience ku endesha ndege jamaa wakakubali da wakaweka auto pilot ngoma iko hewani na abiria wa kutosha kama 200 hivi dogo si akauchezesha usukani dege likayumba akauludisha ikakaa sawa wote wakafurai badae wazee wakawa wanapiga story wamejisahau dogo akauchezesha usukani akapiliza limit ya ile auto pilot ku handle ndege ikageuka kilichowapata mungu anajua hakutoka hata mtu mmoja tangu kipindi hicho ikapitishwa sheria watoto hawaluhusiwi kwenye cockpit so nilichoka kusema sometimes auto pilot huwa zina fail
 
ni kitu cha kawaida hicho rubani anaweza kuset ndege ikaenda yenyewe sema huwa wanaogopa abiria wanaweza pata wasiwasi km hivyo
Kweli kabisa, ndege nyingi zina auto pilot facility, una feed root baada ya kufika kwenye cruising altitude, hapo hata ukiuchapa usingizi hamna noma, usafiri wa ndege siyo kama wa aboud ana Mohamed trans.
 
ni kweli Mungu ameweka kanuni na ndio maana kuna watu wataenda peponi na watu wataenda motoni

Kama ingekua binaadamu ni viumbe tunao ishi kwa "script" then mtu angeona kuwa sio fair kwa Mungu kuwa adhibu wale watao muasi maana yeye ndio kawapangia wamuasi, right?

je nabii Adam asingekula lile tunda kule peponi sisi leo tusingekuwepo hapa? je tuna exist accidentally just because walikula (Adam {a.s}) hilo tunda?

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…