RTO Kinondoni: Matumizi sahihi ya barabara katika makutano ya barabara ya Morogoro hasa Magomeni

Inkoskaz

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
6,372
2,375
FROM RTO KINONDONI

KUHUSU MATUMIZI SAHIHI YA BARABARA KATIKA MAKUTANO YA NJIA KTK MOROGORO ROAD HASA MAGOMENI

Naomba nieleze kwa ufupi kuhusu matumizi ya barabara ktk makutano ya barabara ya morogoro/kawawa eneo la magomeni traffic lights. Nimeona nitoe ufafanuzi ili kusaidia uelewa kwa madereva na watumiaji wengine wa barabara hiyo.

Kwanza kabisa napenda ieleweke kuwa unapofika magomeni traffic lights hauruhusiwi kupinda kulia(No right turn).Hivyo basi utaratibu upo kama ifuatavyo:

1. Kwa madereva wanaotokea Jangwani kuelekea Kinondoni, atapaswa apitilize kama anaelekea ubungo hadi kwa shekhe yahaya atapinda kulia na kurudi hadi magomeni tragfic light na ndipo atapinda kushoto kuelekea kinondoni(Kuna kibao cha maelekezo upande wa kushoto karibu na msikiti mkubwa kabla ya kufika traffic lights).

Ama unapofika Magomeni Mapipa ukitokea jangwani utapinda kulia na na kwenda kutokea eneo la moroko hotel karibu na kanisa la RC utapinda kulia kuelekea kinondoni(kuna alama ya mchoro brbrn eneo hilo la mapipa inaelekeza kwenda kulia kwa wanaelekea upande huo).

2. Ukitokea kinondoni kuelekea ubungo(kuna kibao cha maelekezo kupande wa kushoto karibu na kanisa la KKKT kabla ya kufika traffic lights) dereva atakapofika mataa atapaswa apinde kushoto kama anaelekea jangwani na atakapofika Bondeni hotel (kuna alama chini barabarani na kibao cha maelekezo) atapinda kulia kuingia barabara ya kawaida kurudi mataa ndipo aendelee na safari yake ya kuelekea upande wa Ubungo.

3. Ukitoka Kigogo round about kuelekea jangwani (kuna kibao cha maelekezo upande wa kushoto karibu na petrol station kabla ya kufika mataa) dereva atapaswa apinde kushoto kama anaelekea ubungo hadi kwa shekhe yahaya atapinda kulia kurudi traffic lights na kuendelea na safari yake kuelekea jangwani/mjini.

4. Pia eneo la njia panda mabibo /morogoro rd na junction ya mikumi kwa shekhe yahaya hairuhusiwi kupinda kulia kwa wale wanaotokea Ubungo. Vibao vipo vinaelekeza namna ya kupita kwenda mabibo au mikumi.

NB: Mabadiliko hayo yanatokana na uwepo wa barabara za BRT. Madereva walio wengi wanaendesha kwa mazoea na siyo kufuata sheria za barabarani kwa maana alama na michoro iliyopo barabarani. Naamini kila dereva akizingatia na kuheshim utaratibu na alama zilizopo, hakutakuwa na tatizo lolote wala hakuna dereva atakayekamatwa.

Baadhi wanaposimamishwa na askari ili waelimishwe matokeo yake wanakuwa wakali.Haki na wajibu lazima viende pamoja.

Naomba kuwasilisha.

RSA TANZANIA.
USALAMA BARABARANI NI JUKUMU LETU SOTE..
 
Yaani hawa jamaa ndo bure kabisa, sijawahi ona mradi pumba kama huu just give it time mtaona kitakachotokea. . . wanaleta design za ulaya hapa. . . pumba kabisa. . .
 
Mm nilichemka jana

Mkuu ni ngumu sana, kwa walichofanya kwa siku za jumapili itakuwa powa sana lakini siku za foleni kama j3 ni mtifuano. . . . assume unatoka jangwani unaenda moroco na ile foleni ya jioni kwa huo utaratibu wao. . . wamebugi sana
 
Mkuu ni ngumu sana, kwa walichofanya kwa siku za jumapili itakuwa powa sana lakini siku za foleni kama j3 ni mtifuano. . . . assume unatoka jangwani unaenda moroco na ile foleni ya jioni kwa huo utaratibu wao. . . wamebugi sana
Huyo aliyekubali huo mpango atakuwa sio mtanzania anayepita njia ile...kwanza mradi wenyewe wanaita wa kwenda kasi wameweka mataa kibao
 
FROM RTO KINONDONI

KUHUSU MATUMIZI SAHIHI YA BARABARA KATIKA MAKUTANO YA NJIA KTK MOROGORO ROAD HASA MAGOMENI

Naomba nieleze kwa ufupi kuhusu matumizi ya barabara katika makutano ya barabara ya Morogoro/kawawa eneo la Magomeni traffic lights. Nimeona nitoe ufafanuzi ili kusaidia uelewa kwa madereva na watumiaji wengine wa barabara hiyo.
Kwanza kabisa napenda ieleweke kuwa unapofika magomeni traffic lights hauruhusiwi kupinda kulia (No right turn). Hivyo basi utaratibu upo kama ifuatavyo:

1. Kwa madereva wanaotokea Jangwani kuelekea Kinondoni, atapaswa apitilize kama anaelekea ubungo hadi kwa shekhe yahaya atapinda kulia na kurudi hadi magomeni tragfic light na ndipo atapinda kushoto kuelekea kinondoni (Kuna kibao cha maelekezo upande wa kushoto karibu na msikiti mkubwa kabla ya kufika traffic lights). Ama unapofika magomeni mapipa ukitokea Jangwani utapinda kulia na na kwenda kutokea eneo la moroko hotel karibu na kanisa la RC utapinda kulia kuelekea kinondoni (kuna alama ya mchoro brbrn eneo hilo la mapipa inaelekeza kwenda kulia kwa wanaelekea upande huo).

2. Ukitokea kinondoni kuelekea Ubungo(kuna kibao cha maelekezo kupande wa kushoto karibu na kanisa la KKKT kabla ya kufika traffic lights) dereva atakapofika mataa atapaswa apinde kushoto kama anaelekea jangwani na atakapofika Bondeni hotel (kuna alama chini barabara na kibao cha maelekezo) atapinda kulia kuingia barabara ya kawaida kurudi mataa ndipo aendelee na safari yake ya kuelekea upande wa Ubungo.

3. Ukitoka Kigogo round about kuelekea Jangwani (kuna kibao cha maelekezo upande wa kushoto karibu na petrol station kabla ya kufika mataa) dereva atapaswa apinde kushoto kama anaelekea Ubungo hadi kwa shekhe yahaya atapinda kulia kurudi traffic lights na kuendelea na safari yake kuelekea jangwani/mjini.

4. Pia eneo la njia panda mabibo /morogoro rd na junction ya Mikumi kwa shekhe Yahaya hairuhusiwi kupinda kulia kwa wale wanaotokea Ubungo. Vibao vipo vinaelekeza namna ya kupita kwenda mabibo au Mikumi.

NB.
Mabadiliko hayo yanatokana na uwepo wa barabara za BRT. Madeva waliowengi wanaendesha kwa mazoea na siyo kufuata sheria za barabarani kwa maana alama na michoro iliyopo barabarani. Naamini kila dereva akizingatia na kuheshimu utaratibu na alama zilizopo, hakutakuwa na tatizo lolote wala hakuna dereva atakayekamatwa. Baadhi wanaposimamishwa na askari ili waelimishwe matokeo yake wanakuwa wakali. Haki na wajibu lazima viende pamoja.
Naomba kuwasilisha.

RSA TANZANIA.

USALAMA BARABARANI NI JUKUMU LETU SOTE.
 
Tungeomba mchoro kama mlivyofanya wakati ule wa matengenezo ya pale Ubungo mataa, hii ingesaidia kwani mtu anaprint copy anakuwa nayo kwenye gari lake, thanks for the updates though
 
Yaani hawa jamaa ndo bure kabisa, sijawahi ona mradi pumba kama huu just give it time mtaona kitakachotokea. . . wanaleta design za ulaya hapa. . . pumba kabisa. . .
Muhimu kufuata alana za barabaran kazi inakuwa raisi sasa hivii nchi za afrika zote hakuna sehemu hakuna msongamano kama south tu barabara zakutosha na trafic jam kama kawaida asb na jion
 
Tungeomba mchoro kama mlivyofanya wakati ule wa matengenezo ya pale Ubungo mataa, hii ingesaidia kwani mtu anaprint copy anakuwa nayo kwenye gari lake, thanks for the updates though
shida madereva wengi hawajasoma kama nchi za wenzetu kisa wanajuwa automatic anaweka D ananuna lesen yupo road
 
RTO Kinondoni si kuna alama za barabarani tena za Kimataifa kabisa? Endeleeni kukaza taratibu za Usalama barabarani. Hiki kitakuwa kiama kwa madereva makanjanja wasiojua kusoma alama za barabarani.. Tuiandae DAR kuwa 'Metropolitan City'..
 
Muhimu kufuata alana za barabaran kazi inakuwa raisi sasa hivii nchi za afrika zote hakuna sehemu hakuna msongamano kama south tu barabara zakutosha na trafic jam kama kawaida asb na jion

Mkuu its a joke kufananisha road za south na bongo . . . . we chek hyo barabara wembamba wake tu hata costa mbili kwenda parallel ni kaz. . . . kama nilivyosema just give it a time utashuhudia mtifuano . .
 
Mkuu its a joke kufananisha road za south na bongo . . . . we chek hyo barabara wembamba wake tu hata costa mbili kwenda parallel ni kaz. . . . kama nilivyosema just give it a time utashuhudia mtifuano . .
Hapana mkuuu c fananishi road za SA na hapa na zungumzia folen hata kwa kaburu tukiamka kwenda job tunakutana na folen tukirudi tunakuatana na fole mvua ikinyesha folen
 
Back
Top Bottom