RPC Mwanza : Nilisema ' Kidumu Chama Cha Mapinduzi, sikusema CCM Oyee…'

Salamu ya “kidumu Chama cha Mapinduzi” aliyotoa kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jonathan Shana Butiama mkoani Mara wakati wa hafla ya kumbukizi ya miaka 19 ya kifo cha Baba wa Taifa, imeibua mjadala kwenye mitandao ya kijamii, huku mwenyewe akisisitiza angependa vyama vingine vife.

Akiwa katika mashindano ya Mwalimu Nyerere Historical Marathon yaliyohusisha mbio za riadha, baiskeli na matembezi ya kilomita mbili yaliyofanyika wilayani Butiama, Oktoba 13, Kamanda Shana alisema salamu hiyo ni maalumu kwa sababu ni ya chama kilichoasisiwa na kuongozwa na Mwalimu Nyerere.

Kabla ya kutoa salamu hiyo, kamanda huyo aliyemwakilisha Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Sirro, katika hafla hiyo aliwaeleza waliohudhuria kuwa ana salamu maalumu ambayo angependa kuwafundisha na kuwataka waitikie kama ishara ya kumuenzi Mwalimu.

Huku akipunga ngumi ya mkono wa kulia hewani na kuwahimiza wahudhuriaji nao kufanya hivyo, Kamanda Shanna alisikika akisema, “Leo naomba niwafundishe salamu mpya, nikisema kidumu Chama cha Mapinduzi mnatakiwa kuitikia kidumu milele.”

Akizungumzia suala hilo jana baada ya kuulizwa na Mwananchi iwapo ofisa wa polisi anaweza kuwa shabiki wa siasa, msemaji wa Jeshi la Polisi, Barnabas Mwakalukwa alisema limetokea mkoani Mara hivyo atafutwe kamanda wa polisi wa mkoa huo kulizungumzia.

“Mpigie kamanda wa Mara, huko ndiko alikofanya hilo tukio, msikilize yeye ndiye ana nafasi nzuri ya kulizungumzia,” alisema Mwakalukwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Juma Ndaki alisema Shanna alipotoka kwa sababu jeshi hilo halishabikii chama chochote cha kisiasa.

Ndaki alisema hivyo huku akihoji kwa kufanya hivyo wanachama wa vyama vingine watamfikiriaje na kumuangaliaje.

Kamanda huyo alisema watu hao wataona kama hayupo upande wao.
“Kijeshi hakufanya sawa, ila ungemuuliza mwenyewe nadhani angekuwa na majibu mazuri. Sipo kwenye nafasi nzuri ya kuzungumzia, (ila) ninachojua jeshi halifungamani na chama chochote, ni la watu wote,” alisema kamanda huyo.

Hata hivyo katika mahojiano na Mwananchi, kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Shanna kuhusiana na ‘clip’ hiyo, alisema kama ifuatavyo;

Mwandishi: Kamanda habari yako, umeonekana kwenye video inayosambaa mitandaoni ukikisifiwa Chama cha Mapinduzi, taratibu za Jeshi la Polisi zinaruhusu hilo?

Shana: Wewe dini gani?
Mwandishi: Mkristo kamanda
Shana: Umewahi kuwasalimia Waislamu kwa salamu yao.

Mwandishi: Kamanda ungenipa jibu tu kuwa ulikuwa unawasalimia CCM kwa salamu yao au vipi kwa muktadha wa swali lako la dini?

Shana: Ninasema hivi, ile haikuwa sherehe ya CCM yalikuwa maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 19 tangu kufariki Baba wa Taifa. Nikawaambia njia pekee ya kumuenzi Baba wa Taifa ni kutaka chama alichokiasisi kidumu, ambacho ni CCM.

Mwandishi: Pamoja na hivyo kamanda maadili ya polisi yanaruhusu hilo?
Shana: Nenda kasikilize ile video vizuri urudi kwangu, salamu niliyotoa mimi hata CCM wenyewe hawasalimiani hivyo, nilisema kidumu Chama cha Mapinduzi, sijasema CCM oyee.

Mwandishi: Kwa hiyo kamanda unataka kusema nini, naona kama sielewi.
Shana: Huelewi nini, hata leo ukiniuliza unamzungumziaje Mwalimu Nyerere, nitajibu kidumu Chama cha Mapinduzi ambacho alikiasisi.

Mwandishi: Sawa kamanda mimi nimeelewa nitajitahidi kuwaelewesha wasiokuelewa.
Shana: Kawaeleweshe shauri yao wasiponielewa.

Akifafanua, kwa nini amerekebisha kiitikio kuwa “kidumu milele” badala ya mwitikio uliozoeleka wa “kidumu chama tawala”, kamanda huyo alisema angependa kuona CCM inadumu milele na vyama vingine (shindani na CCM) vife kwa sababu hicho ndicho chama cha ukombozi na kilichoasisiwa na waasisi wa Taifa.

“Kama kikifa (CCM) hatutakuwa tunamuenzi (Mwalimu Nyerere), kinatakiwa kudumu milele na hivyo vingine (vyama vya upinzani) vifie mbali huko,” alisema Kamanda Shanna huku akishangiliwa katika mashindano hayo.

Wakati akisema na kutamka maneno hayo, kiongozi huyo wa ngazi ya juu wa polisi mkoani Mwanza alikuwa katika sare rasmi za jeshi hilo, huku nyuma yake akiwa amesimama askari ambaye ni mpambe wake aliyevalia sare za polisi Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU).

Akiwa katika hali ya hamasa na bashasha, Shanna aliyehamishiwa mkoani Mwanza Agosti 15 akitokea Mkoa wa Pwani alitumia hafla hiyo kummwagia sifa Rais John Magufuli kwa kuishi na kutekeleza kwa vitendo ndoto na maono ya Mwalimu Nyerere ikiwemo sera ya elimu bure kwa kila mtoto.

“Mwalimu Nyerere alipigania haki sawa kwa Watanzania ikiwemo elimu bure kwa wote. Baadaye tulianza kulipia na hata mimi nililipa kidogo, lakini sasa Serikali inayafanya yale aliyopigania Mwalimu Nyerere kwa kutoa (elimu) bure. Lazima tumpongeze Rais Dk John Magufuli,” alisema Shanna.

Alisema hata maisha ya Watanzania hivi sasa ni mazuri hadi askari wa majeshi nchini ambao masilahi na mishahara yao imeboreshwa.

“Hata sare zetu siku hizi ni mpya, safi na nadhifu, lazima tumpongeze (Rais Magufuli). Ninyi Abyatyama (Watu wa Butiama) tunatakiwa kumuenzi Mwalimu Nyerere kuanzia hapa kiwilaya, kimkoa na hatimaye kitaifa maana nyumbani kumenoga,” alisisitiza.

Wakati viongozi wa Serikali na CCM waliohudhuria hafla hiyo ambayo mgeni rasmi alikuwa Spika wa Bunge mstaafu, Pius Msekwa walionekana kufurahia maneno hayo, mmoja wa wastaafu serikalini aliyezungumza kwa sharti la kutotajwa jina gazetini alikosoa akisema ni kinyume cha maadili ya utumishi wa umma kwa kiongozi wa polisi kuonyesha mapenzi na itikadi za kisiasa hadharani.

“Kwa maneno yake ni dhahiri huyu (Kamanda Shanna) hawezi kuwatendea haki wanachama wa vyama vingine vya siasa. Nimesikia amemwakilisha IGP Sirro sijui kama ndiye aliyempa maneno haya aliyoyasema au haya ni yake binafsi. Itoshe tu kusema amepotoka na kukiuka maadili,” alisema mstaafu huyo.

“Mfumo wa vyama vingi vya siasa uko kikatiba na kisheria, hata kama RPC ni muumini na mwanachama wa CCM hakupaswa kuonyesha hilo hadharani kwa sababu kwa nafasi yake anawahudumia Watanzania wa vyama vyote na sheria inamkataza kuwa na itikadi kisiasa.”

Katibu wa Chadema Mkoa wa Mara, Chacha Heche alisema alichokifanya Kamanda Shanna ndio uhalisia anauona miongoni mwa viongozi na watendaji wa jeshi hilo.

“Tofauti yake na wenzake ni kwamba yeye (Shanna) katoka hadharani kuthibitisha kinachofanyika kwa kificho,” alisema Heche.

Mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Serengeti, Rhobi Magoiga alisema alichokisema Shanna ndicho kinachotekelezwa na watendaji serikalini nyakati za chaguzi mbalimbali kwa kuhakikisha mgombea wa CCM anatangazwa kuwa msindi kwa gharama yoyote.

“Kama RPC anataka CCM idumu milele unategemea mpinzani atatangazwa mshindi kwenye uchaguzi ili CCM isidumu milele?” alihoji Magoiga.

View attachment 900761
Nadhani tulishakosea tangu 1992,tulishindwa kuseparate public servants na chama,pia hawa wazee ningumu Kuwaweka pembeni na CCM,ningumu kwa mfumo uliopo kwa public servants kuwa mbali na chama hata sectors nyingijne
 
Hawa wazee wanafikiri ni kama enzi zile wao tu ndo walikuwa wasomi wanaweza kujifanyia tu watakavyo.
Zama zimebadilika. Teknolojia imekua. Bora watumie busara tu. Hapa kinachoendelea ni kizazi kinawasikilizia. Msipojiandaa mtadhalilishwa sana.
 
Kwani Mtu akiwa CCM na kiongozi hawezi kuwatendea Haki watu wa vyama vingine? Sio kila jambo muandike ni upuuzi na ujinga ni sawa na kusema ukiwa mkristu huwezi kuwatendea haki Waislamu.. Ili gazeti lilitakiwa kufungiwa
Ukiwa ccm na wakati huo huo ccm hiyo hiyo ikashindana na vyama vingine lazima usimame upande wa ccm! Maana wanateuliwa kwa sababu hiyo,umeshamuona Rpc gani anayeshabikia vyama pinzani kama wana haki hiyo?
 
Swali ni je kiongozi wa kijeshi anapoamua kinyume cha sheria na katiba kukipigania chama fulani cha siasa atakuwa tayari kuwatendea haki wa vyama vingine hata pale wanapostahili haki hiyo? Je angesema Chadema idumu milele ungemchukulia kama unavyomchukulia sasa?punguza takataka kichwani mkuu!
avevunja katiba gani wakati anaheshim kipengele cha uhuru wa mawazo na kujieleza, yeye amesema angependa vitu alivoanzisha mwl vidumu ikiwemo sisiem... ina maana anganzsha NCCR au CUF nayo angesema idumu... emu mueleweni huyu kamanda. msingi wake n kwa kua tu hiki chana kimeanzshwa na mwl ndio maana anasema kidumu
 
Polisi pamoja na majeshi mengine hayana haki hiyo ya kushabikia chama fulani cha siasa hadharani,labda tu akubali kuwa yeye ni polisi wa ccm tu,
 
Ukweli unajua huwa unauma... hivi unadhani kwa siasa hizi nyepesi nyepesi za kutegemea matukio na kauli za viongozi kuongoea ndio CDM waseme au kuongea sisiemu itaacha kudum na kutawala milele??? kwahiyo achene kuumwa na ukweli huo.
Mwingine huyu hapa ,
 
Bwana, Mfalme wa Israeli, Mkombozi wako, Bwana wa majeshi, asema hivi; Mimi ni wa kwanza, na mimi ni wa mwisho; zaidi yangu mimi hapana Mungu.

Isaya 44:6
 
Kamanda wangu kapotoka anastahili kushushwa cheo mara moja awe sergeant, natamani kuona mabaya juu ya nafasi yake yakimpata
 
Kwani Mtu akiwa CCM na kiongozi hawezi kuwatendea Haki watu wa vyama vingine? Sio kila jambo muandike ni upuuzi na ujinga ni sawa na kusema ukiwa mkristu huwezi kuwatendea haki Waislamu.. Ili gazeti lilitakiwa kufungiwa
Acha ujinga, ufala na unoko mpuuzi wewe ambae umelelewa jalalani, Una akili timamu kwanza? Toka lini muislam amtendee mazuri mkristo au mkristo amtendee mazuri muislam.
.
Hujui lolote nenda msikitini ukasikilize mawaidha uje na majibu hapa kwanini mtu ambae si muislam anaitwa kafiri na kwanini mtu ambae si muislam si ndugu wa muislam?
.
UMENIUDHI SANA MPUMBAVU WEWE
 
Kwani Mtu akiwa CCM na kiongozi hawezi kuwatendea Haki watu wa vyama vingine? Sio kila jambo muandike ni upuuzi na ujinga ni sawa na kusema ukiwa mkristu huwezi kuwatendea haki Waislamu.. Ili gazeti lilitakiwa kufungiwa
We jamaa mpuuzi kweli, unashindwa kuelewa sentesi kamili kabla ya kuandika upuuzi wako!!!? Mtu kataka na kutamani hivyo vyama pinzani vife kibaki milele ccm...kwa akili ya kawaida na nafasi yake serikalini huoni kama inatoa mwanya kumfikiria tofauti ktk utendaji wake, kama mtekelezaji wa kusimamia haki na sheria hii inaleta ukakasi.....kimaadili kamanda Shana kwa kauli yake ni Ziro bila kumung'unya maneno.[emoji34][emoji34][emoji34]
 
Polisi pamoja na majeshi mengine hayana haki hiyo ya kushabikia chama fulani cha siasa hadharani,labda tu akubali kuwa yeye ni polisi wa ccm tu,
huyu hajashabikiaispokua kaunga mkono jambo alilofanya mwl.... kwa hiyo angesema anaunga mkono jambo la alilofanya mwl la kukomesha ukabila akasema liendelee na kudum ungelalamika pia?
 
Kujipendekeza kukizidi lazima uumbuke tu..watu wakujipendekeza kama hawa mwisho wa siku wanalawitiwa
 
Salamu ya “kidumu Chama cha Mapinduzi” aliyotoa kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jonathan Shana Butiama mkoani Mara wakati wa hafla ya kumbukizi ya miaka 19 ya kifo cha Baba wa Taifa, imeibua mjadala kwenye mitandao ya kijamii, huku mwenyewe akisisitiza angependa vyama vingine vife.

Akiwa katika mashindano ya Mwalimu Nyerere Historical Marathon yaliyohusisha mbio za riadha, baiskeli na matembezi ya kilomita mbili yaliyofanyika wilayani Butiama, Oktoba 13, Kamanda Shana alisema salamu hiyo ni maalumu kwa sababu ni ya chama kilichoasisiwa na kuongozwa na Mwalimu Nyerere.

Kabla ya kutoa salamu hiyo, kamanda huyo aliyemwakilisha Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Sirro, katika hafla hiyo aliwaeleza waliohudhuria kuwa ana salamu maalumu ambayo angependa kuwafundisha na kuwataka waitikie kama ishara ya kumuenzi Mwalimu.

Huku akipunga ngumi ya mkono wa kulia hewani na kuwahimiza wahudhuriaji nao kufanya hivyo, Kamanda Shanna alisikika akisema, “Leo naomba niwafundishe salamu mpya, nikisema kidumu Chama cha Mapinduzi mnatakiwa kuitikia kidumu milele.”

Akizungumzia suala hilo jana baada ya kuulizwa na Mwananchi iwapo ofisa wa polisi anaweza kuwa shabiki wa siasa, msemaji wa Jeshi la Polisi, Barnabas Mwakalukwa alisema limetokea mkoani Mara hivyo atafutwe kamanda wa polisi wa mkoa huo kulizungumzia.

“Mpigie kamanda wa Mara, huko ndiko alikofanya hilo tukio, msikilize yeye ndiye ana nafasi nzuri ya kulizungumzia,” alisema Mwakalukwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Juma Ndaki alisema Shanna alipotoka kwa sababu jeshi hilo halishabikii chama chochote cha kisiasa.

Ndaki alisema hivyo huku akihoji kwa kufanya hivyo wanachama wa vyama vingine watamfikiriaje na kumuangaliaje.

Kamanda huyo alisema watu hao wataona kama hayupo upande wao.
“Kijeshi hakufanya sawa, ila ungemuuliza mwenyewe nadhani angekuwa na majibu mazuri. Sipo kwenye nafasi nzuri ya kuzungumzia, (ila) ninachojua jeshi halifungamani na chama chochote, ni la watu wote,” alisema kamanda huyo.

Hata hivyo katika mahojiano na Mwananchi, kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Shanna kuhusiana na ‘clip’ hiyo, alisema kama ifuatavyo;

Mwandishi: Kamanda habari yako, umeonekana kwenye video inayosambaa mitandaoni ukikisifiwa Chama cha Mapinduzi, taratibu za Jeshi la Polisi zinaruhusu hilo?

Shana: Wewe dini gani?
Mwandishi: Mkristo kamanda
Shana: Umewahi kuwasalimia Waislamu kwa salamu yao.

Mwandishi: Kamanda ungenipa jibu tu kuwa ulikuwa unawasalimia CCM kwa salamu yao au vipi kwa muktadha wa swali lako la dini?

Shana: Ninasema hivi, ile haikuwa sherehe ya CCM yalikuwa maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 19 tangu kufariki Baba wa Taifa. Nikawaambia njia pekee ya kumuenzi Baba wa Taifa ni kutaka chama alichokiasisi kidumu, ambacho ni CCM.

Mwandishi: Pamoja na hivyo kamanda maadili ya polisi yanaruhusu hilo?
Shana: Nenda kasikilize ile video vizuri urudi kwangu, salamu niliyotoa mimi hata CCM wenyewe hawasalimiani hivyo, nilisema kidumu Chama cha Mapinduzi, sijasema CCM oyee.

Mwandishi: Kwa hiyo kamanda unataka kusema nini, naona kama sielewi.
Shana: Huelewi nini, hata leo ukiniuliza unamzungumziaje Mwalimu Nyerere, nitajibu kidumu Chama cha Mapinduzi ambacho alikiasisi.

Mwandishi: Sawa kamanda mimi nimeelewa nitajitahidi kuwaelewesha wasiokuelewa.
Shana: Kawaeleweshe shauri yao wasiponielewa.

Akifafanua, kwa nini amerekebisha kiitikio kuwa “kidumu milele” badala ya mwitikio uliozoeleka wa “kidumu chama tawala”, kamanda huyo alisema angependa kuona CCM inadumu milele na vyama vingine (shindani na CCM) vife kwa sababu hicho ndicho chama cha ukombozi na kilichoasisiwa na waasisi wa Taifa.

“Kama kikifa (CCM) hatutakuwa tunamuenzi (Mwalimu Nyerere), kinatakiwa kudumu milele na hivyo vingine (vyama vya upinzani) vifie mbali huko,” alisema Kamanda Shanna huku akishangiliwa katika mashindano hayo.

Wakati akisema na kutamka maneno hayo, kiongozi huyo wa ngazi ya juu wa polisi mkoani Mwanza alikuwa katika sare rasmi za jeshi hilo, huku nyuma yake akiwa amesimama askari ambaye ni mpambe wake aliyevalia sare za polisi Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU).

Akiwa katika hali ya hamasa na bashasha, Shanna aliyehamishiwa mkoani Mwanza Agosti 15 akitokea Mkoa wa Pwani alitumia hafla hiyo kummwagia sifa Rais John Magufuli kwa kuishi na kutekeleza kwa vitendo ndoto na maono ya Mwalimu Nyerere ikiwemo sera ya elimu bure kwa kila mtoto.

“Mwalimu Nyerere alipigania haki sawa kwa Watanzania ikiwemo elimu bure kwa wote. Baadaye tulianza kulipia na hata mimi nililipa kidogo, lakini sasa Serikali inayafanya yale aliyopigania Mwalimu Nyerere kwa kutoa (elimu) bure. Lazima tumpongeze Rais Dk John Magufuli,” alisema Shanna.

Alisema hata maisha ya Watanzania hivi sasa ni mazuri hadi askari wa majeshi nchini ambao masilahi na mishahara yao imeboreshwa.

“Hata sare zetu siku hizi ni mpya, safi na nadhifu, lazima tumpongeze (Rais Magufuli). Ninyi Abyatyama (Watu wa Butiama) tunatakiwa kumuenzi Mwalimu Nyerere kuanzia hapa kiwilaya, kimkoa na hatimaye kitaifa maana nyumbani kumenoga,” alisisitiza.

Wakati viongozi wa Serikali na CCM waliohudhuria hafla hiyo ambayo mgeni rasmi alikuwa Spika wa Bunge mstaafu, Pius Msekwa walionekana kufurahia maneno hayo, mmoja wa wastaafu serikalini aliyezungumza kwa sharti la kutotajwa jina gazetini alikosoa akisema ni kinyume cha maadili ya utumishi wa umma kwa kiongozi wa polisi kuonyesha mapenzi na itikadi za kisiasa hadharani.

“Kwa maneno yake ni dhahiri huyu (Kamanda Shanna) hawezi kuwatendea haki wanachama wa vyama vingine vya siasa. Nimesikia amemwakilisha IGP Sirro sijui kama ndiye aliyempa maneno haya aliyoyasema au haya ni yake binafsi. Itoshe tu kusema amepotoka na kukiuka maadili,” alisema mstaafu huyo.

“Mfumo wa vyama vingi vya siasa uko kikatiba na kisheria, hata kama RPC ni muumini na mwanachama wa CCM hakupaswa kuonyesha hilo hadharani kwa sababu kwa nafasi yake anawahudumia Watanzania wa vyama vyote na sheria inamkataza kuwa na itikadi kisiasa.”

Katibu wa Chadema Mkoa wa Mara, Chacha Heche alisema alichokifanya Kamanda Shanna ndio uhalisia anauona miongoni mwa viongozi na watendaji wa jeshi hilo.

“Tofauti yake na wenzake ni kwamba yeye (Shanna) katoka hadharani kuthibitisha kinachofanyika kwa kificho,” alisema Heche.

Mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Serengeti, Rhobi Magoiga alisema alichokisema Shanna ndicho kinachotekelezwa na watendaji serikalini nyakati za chaguzi mbalimbali kwa kuhakikisha mgombea wa CCM anatangazwa kuwa msindi kwa gharama yoyote.

“Kama RPC anataka CCM idumu milele unategemea mpinzani atatangazwa mshindi kwenye uchaguzi ili CCM isidumu milele?” alihoji Magoiga.

View attachment 900761
Haya mambo ndio yaliyomfanya Igp Mahita enzi zake akatoka na vijiko na umma kama majambia [emoji16][emoji16][emoji16]...yaani akili kichwani zinasimama unawaza kichama chama tu.......na hapo inategemea chama chenyewe na wanachama wake wanafikiria kwa kutumia kiungo gani ktk mwili, na bahati mbaya iwe kichwa wanatumia kufugia nywele.NI BALAA
 
Hahahhhhhhhh atiiiii alisema nini sio nini.. ndezi kweli anafanya WaTz hamnazo!
 
huyu hajashabikiaispokua kaunga mkono jambo alilofanya mwl.... kwa hiyo angesema anaunga mkono jambo la alilofanya mwl la kukomesha ukabila akasema liendelee na kudum ungelalamika pia?
Nyerere aliombea vyama vingine vife na ibaki ccm milele!??? unaelewa maana ya mfumo wa vyama vingi!? Unafikiri ni kwa nini Nyerere aliukubali utumike ingali wengi walikuwa hawajaukubali!!? Msimsingizie Nyerere kwa sababu ya mapungufu yenu ya kushindwa kuwaza vizuri au ubashitelisim kwa lugha ya kigeni[emoji41][emoji41][emoji41]
 
Back
Top Bottom