RPC Liberatus Sabas na Kashfa ya Leopard Tours

lubajaro

JF-Expert Member
Mar 29, 2015
1,256
364
WanaJamiiForums,

DCP Liberatus Sabath kamanda wa Polisi Jijini Arusha, amekuwa ni kamanda mwenye marafiki wengi ambao ni wafanyibiashara wakubwa jijini Arusha mmoja wao ni Mr Fazal wa Leopard Tours na Boss mwingine wa Kibo peak Tours, Kamanda huyu amekuwa anafumbia macho maovu yanayofanywa na mr fazal kiasi kwamba hata magari ya Leopard Tours hapa jijini Arusha, Traffic wanayaogopa kuyakamata hii inatokana na ulevi wa kupindukia wa uchukuaji wa Rushwa kutoka kwa kamanda huyu.

Amekuwa akizizima chini kwa chini, kesi nyingi za jinai na uhalifu kutoka kwa,wafanyibiashara wakubwa wa hapa jijini Arusha kwa sababu ya Rushwa. TUNAOMBA JPM atumbue jipu la kamanda huyu anayemiliki nyumba zaidi ya 20 za kupangisha alizojengewa na wafanyibiashara wa jijini Arusha.

Nawasilisha
 
Last edited by a moderator:
Jeshi la Polisi Arusha ni majanga plus traffic kila kona mpaka vichochoroni kukamata magari ili wajipatie rushwa.

Traffic anakuja na private car yake anapaki mahali anaanza kukamata magari.

Hivi mshahara laki 2 wanaolipwa polisi unaweza nunua gari na kujenga nyumba yako plus nyumba za wapangaji.

Rushwa Arusha ni zaidi ya kipindupindu.
 
Last edited by a moderator:
Huu ni uvimbe unahitaji operation kubwa.
 
Last edited by a moderator:
Kwa Arusha si jambo la siri kuzungumzia rushwa ya polisi maana hawako kazini wako kushindana nani atakuwa na pesa nyingi jioni. Trafic ndo usiseme kabisa wamefanya magari ya watu kama vitega uchumi vyao. Kila ukisimamishwa lazima wakuombe pesa. Ifike wakati sasa makao makuu ya polisi wasikilize vilio vya watu wa Arusha na hatua zichukuliwe. Haya yote yanatokea kwa kuwaacha hawa maaskari kituo kimoja muda mrefu bila uhamisho eitha wa kimkoa au kumbadilishia idara. Maana niaminivyo mimi askari wana mafunzo yote hakuana anae soma ulinzi na mwingine trafic etc
 
Polisi TRA Mikoa yote wahamishwe maana tumewachoka sasa hivi TRA wanalazimisha wafanyabiashara wadogo wa madini wakate leseni 250000.

Unakuta broker mdogo mtaji wake 1m isitoshe cnc sep hajawahi ona hata point ya jiwe sasa atalipaje mapato
 
Last edited by a moderator:
Arusha ni kichaka cha polisi wala rushwa, malaya na wagomvi bar! IGP need to overhaul the whole cabinet kuanzia kamanda wao hadi mpokea simu ya upepo mwizi mkubwa. Nimemaliza
 
Huyu Mkuu wa Jeshi la Polisi Mr Mangu yupo kimya Sana.

Matukio yanatokea yeye yupo kimya.

Tunamtaka yeye Kama big boss atwambie nini kinaendelea.

Maana matukio ya hovyo yanayohusisha Polisi yamekuwa mengi mno.
 
Last edited by a moderator:
jeshi la police arusha ni majanga plus traffic kila kona mpka vichochoroni kukamata magari ili wajipatie rushwa......traffic anakuja n private car yke anapaki mahali anaanza kukamata magari.....hivi mshahara laki 2 wanaoliopwa police unaweza nunua gari n kujenga nyumba yko plus nyumba za wapangaji........rushwa arusha ni zaidi y kipindupindu
Swala la kuwa na gari sio ishu maana wengine wasomi mishahara yao iko juu na kuna mikopo, tatizo labda ni hiyo rushwa.
 
Kuna harufu isiyo sahihi waleta hoja naona wanakata kulitumia Jukwaa kwa vita ya kimasilahi hii ni thread sijui ya pili kuhusu Leopard Tours na mahusiano na Watumishi wa Umma.
 
Majuzi nilikuwa naenda Nairobi nikiwa speed ya kawaida kabisa hiyo hawa traffic wakanitia mikononi wakachukua lipesa langu..
 

Attachments

  • 1452670717186.jpg
    1452670717186.jpg
    40.5 KB · Views: 75
Swala la kuwa na gari sio ishu maana wengine wasomi mishahara yao iko juu na kuna mikopo, tatizo labda ni hiyo rushwa.

Mkuu mshahara wa traffic hata kama ana V tatu hawezi kuwa na gari 2 plus nyumba.

Hata kama analipwa laki 4 mkopo ni 400,000×10 ya mshahara wake.

Hayo maendeleo yote atafanya kwa mshahara wake kweli, rushwa ndio inaendesha 99% ya maisha ya trafiki na polisi.
 
Last edited by a moderator:
pamoja na yote hayo hivi nyinyi watu wa arusha kila mara mnaugomvi na polisi? simtetei kamanda lakini
 
Back
Top Bottom