Royal Tour: Wacheni Tuseme Ukweli

Royal Tour: Wacheni Tuseme Ukweli

voicer

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2020
Posts
5,545
Reaction score
11,943
Wazo lilikuwa zuri, lakini mleta wazo katuzidi ujanja.

Unapotengeneza filamu ambayo ni andishi la kitaaluma na kibiashara,tulipaswa kutanguliza taaluma zaidi kuliko siasa.

Mwanasiasa anaweza kukumbwa na kashfa au dosari za kiuongozi na kupelekea kupoteza soko kusudiwa baada ya kususiwa kote ilikotangawzwa na kuvuma. Huo ndio utamaduni wa wazungu.

Tulipaswa pia kuzilenga taasisi kubwa zilizobobea katika taaluma hiyo Duniani kama vile National Geographic au Animal Planet ambazo tayari zinajiendesha kupitia Vituo vyao binafsi vya kurushia Documentary zao Dunia nzima. Na zinaangaliwa na mamilioni ya watu Duniani kila siku.

Huyu Peter Greenbag hana Impact kubwa Duniani kama ambavyo ametuingiza mkenge kumdhania. Unaweza kutafakari hilo kwa kujiuliza aina ya watu ambao wamehudhuria uzinduzi wake huko Marekani.

Pia jiulizeni kwamba,inakuwaje utengeneze filamu ya kukutangangaza kibiashara,halafu unaiingiza Sokoni Amazon kuiuza.

Badala ya wewe Mtangazaji wa biashara yako ndio uwalipe wao ili wakutangaze.eti wewe ndio unaliuza tangazo lako kwa wateja.

Lengo likiwa kujulikana zaidi na hivyo kuvutia wateja kuja kuyaona yale uliyoyatangaza kupitia filamu yako.

Unapoanza kwa kuiuza bila kujua kama ita hit kwenye mauzo au la! Hii inaleta maswali mengi kuliko majibu.

Pia ingekuwa vema Rais angeambatana na wataalamu wa fani ya utalii pamoja na wabobezi wa African Wildlife Management.
Ambao tungewaona bega kwa bega na Rais wetu,wakimsaidia kujibu maswali na kukidhi kiu ya waulizaji. Kwa kujikita zaidi kitaaluma na kitakwimu sahihi. Hususan kwenye hafla za uzinduzi.

Ambapo majibu yao ya kitaaluma yangeongeza chachu ya watu kuitamani zaidi filamu ili wajionee uzuri wa Tanzania.

Tofauti na kilichofanyika kwa kwenda kumpambanisha Rais wetu,ambaye kitaaluma sio fani yake.

Hapo tayari umemchezesha Bahati Nasibu rais na watanzania bila kujua wala kupenda.

Hapo ni wazi kwamba waandaaji wameutumia muda wa Rais kwa manufaa yao zaidi.

Boston ndio mji ambao ni kitovu cha utalii na taasisi za utalii na wadau wake nchini Marekani.hasa kuhusu utalii wa nje ya Marekani kama Afrika na kwingineko.
Kuliko New York au Los Angeles

Hivyo ingekuwa vema uzinduzi ule ukafanywa katika mji huo,kuliko kwenye jiji la New York ambalo halina sifa ya utalii zaidi ya kujaa watoto wa mjini.

Kwa nini hata hawakupata wazo la kuingia mkataba na mmojawapo wa wasanii maarufu nchini Marekani,ili waweze kurekodi pamoja na Rais wetu ili kuiongezea chachu na umaarufu kimataifa?

Rais Samia ni Maarufu Tanzania ndiyo.
Lakini hajawa maarufu kimataifa kwa kiwango cha kuwashawishi watu kumiminika kuinunua filamu yake kwa sasa.
Kama waandaaji na wapiga debe mnavyotaka kuiaminisha Dunia.

Will Smith ametengeneza filamu ndogo tu ya jinsi alivyotembelea Afrika na Tanzania ikiwemo na inaweza kuipiku kwa mbali sana hii ya kwetu.kulingana na jinsi inavyoshambuliwa huko Marekani kwa mauzo.

Tujaribu kidogo kumuangalia Kagame wa Rwanda jinsi anavyoitangaza nchi yake bila kuingiza sura yake hata kidogo na Rwanda inapaa kimataifa.

Madhara ya kumtumia Rais moja kwa moja,
Na kuihusisha serikali yake kwenye masuala ya matangazo hasa haya ya kitalii. Ni kwamba soko lake pia litategemea rekodi yake pamoja na serikali yake kiutawala.
Wazungu huwa wanapiga chini kila kitu pindi mhusika anapokumbwa na kashfa yoyote ile.

Nimalizie kwa kuitaka serikali isikie maombi ya watanzania kutaka watuweke wazi kuhusu gharama na umiliki wa filamu ya Tanzania Royal Tour.

Nimemaliza kuutumia uhuru wangu kikatiba.
View attachment 2200347
 
Siku ya uzinduzi filam ilipata more than 3m viewers world wide.

Tuache ramli tusubiri matokeo.
At least, Mama Samia kajaribu kufanya kitu.

Kwa taarifa yako tu Wazungu wengi walijua Mlima Kilimanjaro uko Kenya hapo nyuma, Walijua Tanzanite inatoka Kenya na India n.k

Sasa tusipoitangaza Nchi tutaendelea kupigwa.

Raisi kaanza kwa kadri aliweza. Badae wataboresha zaidi. Sio Jambo la kubeza hata kidogo. Labda una lako Jambo.
 
Wewe na mimi ndio tunaomjua Samia na siyo kila mtu Duniani kama unavyodhani mkuu.
 
Siku ya uzinduzi filam ilipata more than 3m viewers world wide.
Tuache ramli tusubiri matokeo.
At least, Mama Samia kajaribu kufanya kitu.

Kwa taarifa yako tu Wazungu wengi walijua Mlima Kilimanjaro uko Kenya hapo nyuma, Walijua Tanzanite inatoka Kenya na India n.k
Sasa tusipoitangaza Nchi tutaendelea kupigwa.

Raisi kaanza kwa kadri aliweza. Badae wataboresha zaidi. Sio Jambo la kubeza hata kidogo. Labda una lako Jambo.
Wewe unazo taarifa kiasi gani kwamba hii imewazindua leo?

Je unaweza kutupatia chanzo cha takwimu zako mkuu?
 
Ni wa kawaida sana ukiangalia guests/clients wake wa the royal tour.

He also produces and hosts a television series called The Royal Tour which airs on PBS. The series features various heads of state giving Greenberg and viewers a personal tour of their country. It has featured a number of world leaders including New Zealand's Helen Clark, Israel's Benjamin Netanyahu, Abdullah II of Jordan, Peru's Alejandro Toledo, Mexico's Felipe Calderón, Rwanda's Paul Kagame, Poland's Mateusz Morawiecki and Tanzania's Samia Suluhu Hassan. Greenberg was previously the Travel Channel's chief correspondent.
 
Hivi mleta mada ushawahi kuiangalia Royal Tour film ya Rwanda? Je Kagame hakuwepo kwenye filamu? Tatizo lenu dada zetu wa siku hizi kila kitu mnakichukua kimipasho mipasho ilimradi na nyie muonekane kuwa mnajua kusuta.

Unaweza kukuta mleta mada ni raia wa nchi nyingine hivyo maendeleo yoyote kwa Tanzania ni sawa na msumali wa moto katikati ya makalio yake. Shem on you poor girl. JF imeingiliwa na mabinti wa mipasho na wanaharakati koko.

images (64).jpeg

39876622880_75ab92ae28_b.jpg
 
Hongera kwa andiko lako

Chawa watakuja kusema kuwa humpendi Samia!!! Lazima mjifunze kufanya utafiti kabla ya kukurupuka na kufanya mambo ya kujitafutia umaarufu!! Hapo kuna watu wamepiga hela yao safi na kuipitisha kwenye foundation ya Mjomba wa Msoga!!! Ndio maana nae alitangulia kwenda kwenye uzinduzi ingawa walimficha kwenye picha zao!
 
Siku ya uzinduzi filam ilipata more than 3m viewers world wide.
Tuache ramli tusubiri matokeo.
At least, Mama Samia kajaribu kufanya kitu.

Kwa taarifa yako tu Wazungu wengi walijua Mlima Kilimanjaro uko Kenya hapo nyuma, Walijua Tanzanite inatoka Kenya na India n.k
Sasa tusipoitangaza Nchi tutaendelea kupigwa.

Raisi kaanza kwa kadri aliweza. Badae wataboresha zaidi. Sio Jambo la kubeza hata kidogo. Labda una lako Jambo.
Achana nalo hilo chawa. Halina hoja yoyote zaidi ya kuonekana ni kihoja tu hapa JF.
 
Umejieleza, ingawa inaweza kuwa ngumu kueleweka kwa baadhi ya wasomaji. Umetumia uwasiliaji mgumu kidogo, hasa kwa wasomaji wako ambao hawapo kwenye hiyo fani yako.
Kwa mfano, unapochanganua hapa haya maeneo matatu: Kitaaluma, Kibiashara, Kisiasa...
Unapotengeneza filamu ambayo ni andishi la kitaaluma na kibiashara,tulipaswa kutanguliza taaluma zaidi kuliko siasa.
Inakuwa vigumu kuelewa hasa ni maeneo yapi ya 'movie' hiyo yamelenga biashara, siasa au taaluma.

Lakini kiujumla, ninakubaliana nawe kwamba kilichofanyika hapa ni mwendelezo ule ule wa "kiujanja ujanja" unaotumiwa na serikali hii na hasa huyo kiongozi wake mkuu. Nadhani anaamini kwamba maneno matamu matamu na sauti nyororo ndio nyenzo muhimu zaidi kwake katika kuwahadaa watu, huku matendo yakiwa yanalenga manufaa binafsi zaidi kuliko manufaa ya nchi.

'Movie' hii ni sehemu ya Kampeni ya kujijenga kuelekea 2025. Hawa watu wanaookotezwa kama hawa akina Rostam na hao akina Greenberg, ni mpango ule ule wa kujijenga wao na huyo anayewapa ulaji wa 'free range'.

Tanzania itapigwa sana kupitia kwenye siasa hizi za janja janja za kuwalaza watu akili zinazotumika wakati huu. Hakuna tena kuburuzana na polisi, au vyombo vingine vya mabavu, kama kuulizwa uraia, lakini kuburuzwa kunabaki palepale kwa kutumia njia mbadala.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom