Rostam, Lowassa wakatwa miguu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rostam, Lowassa wakatwa miguu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Byendangwero, Apr 14, 2011.

 1. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #1
  Apr 14, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kitendo cha kamati na halmashauri kuu ya CCM kuamua kuwachukulia hatua E.L; R.A; na E.C bila ya kutoa kwao kwanza orodha ya mambo wanayotuhumiwa nayo na kuwataka kuwasirisha utetezi wao kwenye vyombo hivyo vya juu vya chama hicho ni ukihukwaji mkubwa wa haki za msingi za watumiwa hao kwa mujibu wa kifungu cha 13(6)(a) cha katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania. Ukiukwaji huo unatoa mwanya kwa watuhumiwa hao, kubatirisha maamuzi yaliyochukuliwa dhidi yao katika siku zijazo.
   
 2. m

  mambombotela New Member

  #2
  Apr 14, 2011
  Joined: Feb 9, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hap umesema kweli! Kwanza kabisa napenda kujitambulsha kwamba mimi ni mwancaham hai wa CCM lakini ninayo yaona mimi ni kwamba chama chetu hakiwezi kuendeshwa kama familia ya mtu mmoja.

  Eti zidumu fikra za mtu mmoja hata kama hana vision, ila fitina, majungu and lack of confidence to address serious issues!.

  Chama changu igeni nchi zingine za hapa Africa kuepuka migongano zaidi ya kichama such as South Africa, Kenya etc. Mnakalia majungu tupu.. eti mtu anasimama na kusema, tunahitaji ushahidi wa namna gani kuhusu hawa mafisadi, ..wakati mnaona mimi nilikomea asilimia 61% wakati wa uchaguzi mkuu..stupid!

  Refer to Mwl JK.Nyerere speech..Chama cha upinzani wa ukweli lazima kitameguka toka CCM. This is the right moment. New Political Party, strong one and very pursuasive party is coming.

  Let us learn from William Ruto (Kenya), Charity Ngiru (Kenya), Jacoob Zhuma (SA) etc, huwezi kumzuia mtu kuwa kiongozi kwa kumwanzishia majungu na fitina. Time will tell.. lazima CCM tusome alama za nyakati. CCM yote tutahamia chama kingine. Trust my words brothers and sisters!

  Amandlla!

  We are saying 'No' to old CCM, tunaomba wote munaotuhumiwa ufisadi bila ushahidi wowote kutolewa mbele ya NEC mhame sasa na kuanzisha chama chenu kipya, tutakuwa tayari kuwaachia CCM yao ya Kikwete na Mzee Mwinyi.
   
 3. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #3
  Apr 14, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mambotela anaonekana kupotosha maudhui ya thread yangu; nilichosema mimi, ni kwamba hatua zilichukuliwa dhidi ya hao wanaoitwa vinara wa ufisadi hazikufanyika kwa umakini, kwakuwa mchakato uliofuatwa katika kufikia maamuzi hayo umeacha mwanya wa kupingwa kwa hatua hizo hapo baadaye. Kwa mfano hivi sasa kuna utata ya nini kilicho azimiwa hasa na NEC kuhusiana na watuhumiwa wa ufisadi. Kuna wanaosema wamepewa siku 90 wajihengue wenyewe vinginevyo chama kiwahengue, wengine wanasema hapakuwepo azimio la aina hiyo; katika mkanganyiko huo kuna kila uwezekano watuhumiwa kuponyoka
   
 4. Chapa Nalo Jr

  Chapa Nalo Jr JF-Expert Member

  #4
  Apr 14, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 6,375
  Likes Received: 3,210
  Trophy Points: 280
  Wewe umetumwa na mafisadi nini! Elewa hukumu za kisiasa sio hukumu za mahakamani za ku-prove beyond resonable doubt, ukituhumiwa na wanajamii yako unayoongoza na wakawa hawana imani nawe ndio basi jiuzuru, hawakutaki tena.
   
 5. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #5
  Apr 14, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Nafikiri haukumwelewa Byendagwero, Ni kweli Halmashauri Kuu ya CCM imekiuka hata Katiba ya CCM watuhumiwa hawakusomewa mashataka yao na kupatiwa nafasi ya kujitetea, mambo yalizungumzwa kujuujuu tu kwa nia ya Kuwalinda baadhi ya washiriki katika Ufisadi huo hususan ushiriki wa Kikwete. Laiti kama kila mtuhumiwa angesomewa mashataka yake kama Katiba ya CCM inavyoelekeza ni lazima wangetajana nani alimtuma nini na nani alituma nini.
   
 6. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #6
  Apr 14, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Fisadi utamjua tu kwa maneno yake! Sasa na wewe unataka kuwatetetea mafisadi wenzako? Anzisheni chama kama mtapata hata mbuzi tu awe wanachama
   
 7. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #7
  Apr 14, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Nimemaliza kuyapitia maazimio ya kikao kilichopita cha NEC, ambapo nimebaini ya kwamba kuna upotoshwaji wa nini hasa kimeazimiwa kuhusiana na wakina Lowasa.

  Azimio namba 5(d) ambalo ndilo linahusiana na suala hilo linasomeka ifuatavyo:

  "Chama cha mapinduzi na serikali zake kiongeze kasi ya mapambano dhidi ya viongozi na wanachama wanaojihusisha na rushwa. Aidha viongozi na wanachama wanaotuhumiwa kwa vitendo vya rushwa wajenge tabia ya kuwajibika wenyewe kwa maslahi ya chama. Wasipofanya hivyo chama kiwajibishe kwa maslahi ya chama na nchi."

  Kutokana na azimio hili, madai kwamba akina Lowasa wamepewa siku 90 wajihengue ni ya uwongo. Maazimio haya yanapatikana katika tavuti ya CCM.
   
 8. fangfangjt

  fangfangjt JF-Expert Member

  #8
  Apr 14, 2011
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 571
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33
  sijui Bangi. Ule usiku JK, Chiligati na Nape wote waliongelea swala la mafisadi kujiwajibisha , wakichelewa basi chama kita wawajibisha
   
 9. m

  mambombotela New Member

  #9
  Apr 14, 2011
  Joined: Feb 9, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naomba nieleweke kwamba mimi siko biased kama wan JF wengine. I'm neutral and very obejctive to each every person.

  Kama members mlivyocahngia kwamba, CCM inayo katiba na kanuni zinazosimamia shughuli za kila siku za chama. Chama kinatoa haki kwa kila mwanachama kujieleza na kusikilizwa. Founders of the party knew this from the beginning ya kwamba atakuja tokea mhuni mmoja kagombana na Msaidizi wake bar na kesho an dictate maauzi ya kumchukulia.

  Sitetei mtu hapa lakini EL, RA, EC and others were suposed to be informed in writing on their allegations na wakasiklizwa. Kama yangetokea hayo sote tungepigwa bumbuwazi kwa maana ungesikia kokolo likinasa na wale mnaowaita Saints.

  Hizi ni njama tu kwa EL kwa sababu anaungwa mkono na wanachama wengi wa CCM kama next President. Kwa vile JK na wapambe wake tayari wana mtu wao kama UVCCM walivyosema pale awali, basi kila wakiona kivuli cha EL na RA wanachachawa.

  This is so clear, kwamba hoja hapa si UFISADI bali urais wa 2015.

  Tuache ushabiki wa mambo na chuki kwa watanzania wenzetu bila sababu kwa vile inaweza kupelekea kule Bhengazi ha sehemu zingine kama hizo.

  Please Mr. President, dont divide the party and make it one. Dont work on majungu na fitina za kisiasa, they are very harmful to the nation. Look on what has happened on the past two days in Ivory Coast and Egypt.

  Mr. Chairman (CCM) soma alama za nyakati, 2015 siyo mbali chama kitakufia mkononi mwako na itakuwa aibu ya karne kama yaliyompata mzee Moi kule Kenya (KANU).

  Dont marginalise the group called MAFISADI.
  i LOVE MY COUNTRY TANZANIA
   
 10. MawazoMatatu

  MawazoMatatu JF-Expert Member

  #10
  Apr 14, 2011
  Joined: Sep 6, 2008
  Messages: 505
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  UNAWEZA kusema kwamba huu ni mwisho wa zama kwa Edward Lowassa, Rostam Aziz na Andrew Chenge ambao, juzi Jumatatu, chama chao kiliwatosa kwa kuwapa siku 90 kujiondoa katika nafasi walizonazo kwa vile wamekuwa wakichafua haiba ya chama hicho.
  Taarifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), iliyotolewa juzi usiku kwa vyombo vya habari, mjini Dodoma, imeeleza kwamba vikao vya juu vya chama hicho vinataka wanasiasa hao watatu wajiuzulu nafasi zao zote za uongozi katika Chama.
  Vikao hivyo vya Sekretariati, Kamati Kuu na Halmashauri Kuu (NEC), vilivyokuwa vimeanza Jumatano ya wiki iliyopita na kukamilika juzi usiku, vililenga kutekeleza dhamira ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete ya chama hicho ‘kujivua gamba’.
  Dhana ya CCM kujivua gamba inahusishwa na matokeo mabaya ya chama hicho katika uchaguzi wa 2010 ambapo kilipata upinzani mkali kutoka Chadema.
  Chenge, Rostam, Lowassa wapime wenyewe
  “Kama mlivyomsikia Mwenyekiti (Jakaya Kkwete) wale wote ambao wamekuwa wakituhumiwa kukichafua Chama, NEC imeamua watupishe.
  “Uamuzi ni kwamba katika miezi mitatu wapime wenyewe, wajiondoe katika nafasi zao. Kama watakuwa hawajafanya hivyo katika miezi mitatu ijayo, hadi tutakapokutana hapa, basi chama kitawaondoa,” alisema John Chiligati, Katibu wa uenezi katika sekretariati iliyopita ambaye mabadiliko yaliyotangazwa juzi yamempa nafasi ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara).
  Kuanguka kwa Lowassa, Waziri Mkuu aliyejiuzulu mwaka 2008 ambaye pia ni Mbunge wa Monduli na mjumbe wa NEC, Rostam Aziz ambaye ni mfanyabiashara, Mbunge wa Igunga na mjumbe wa NEC na Chenge, mwanasheria aliyechafuka baada ya kutumikia nafasi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kipindi chote cha awamu ya Benjamin Mkapa, Mbunge wa Bariadi Magharibi na mjumbe wa NEC, ni jambo lililotarajiwa.
  Wanasiasa hao watatu wamekuwa wakitajwa katika tuhuma mbalimbali za ufisadi lakini uongozi wa CCM umekuwa ukitetea ukidai kutokuwapo kwa ushahidi wa kisheria dhidi yao.
  Mwanasheria Mkuu achochea ‘moto’
  Pengine aliyeharakisha kuanguka kwao ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema ambaye alikuwa ameitwa mwishoni mwa wiki iliyopita na Mwenyekiti Kikwete, kutoa ufafanuzi kwa Kamati Kuu juu ya mambo kadhaa, likiwamo suala la mchakato wa Katiba mpya.
  “Kifo cha kina Lowassa, Rostam na Chenge kimeharakishwa na Werema. Aliletwa na Mwenyekiti kuja kufafanua mambo kadhaa kama mchakato wa Katiba mpya.
  “Katika mchango wake kama mtu aliyeko nje ya Chama, alizungumzia mambo ambayo yeye alisema hayaendi sawa ndani ya CCM. Kwanza alianza kwa kusema yeye si mwana CCM; japo huko nyuma, kama walivyokuwa wengi, alipata kuwa mwanachama.
  “Akasema kwao anakotoka (Jaji Werema anatoka Mkoa wa Mara) mwanamume anapaswa kusema ukweli hata kama ukweli huo unauma kiasi gani.
  “ Akasema kwamba alikuwa anaona tatizo kwamba taarifa nyingi za vikao kama hicho alichokuwa ameitwa kuzungumza, zilikuwa zinavuja sana.
  “ Akasema hata hayo ambayo angeyasema, jioni yangekuwa yamewafikia watu wa nje, na wahusika wakubwa wa kuvujisha taarifa hizo walikuwa ndani ya Kamati Kuu hiyo hiyo.
  “ Akiachana na hilo, akahoji kwa nini, chama hicho kinalialia kuwa haiba yake imeshuka na wakati huo huo kikikumbatia vitu kama Richmond na Dowans ambavyo vinaichefua jamii na ambavyo wahusika wake wakuu wamo katika uongozi wa juu wa chama,” anasema mjumbe mmoja wa Kamati Kuu aliyezungumza na Raia Mwema.

  Chiligati, Malecela wapigilia msumari

  Ni kana kwamba moto aliokuwa ameuwasha Jaji Werema jana yake ulirejewa na Chiligati ambaye akiwasilisha ripoti ya Sekretariati kuhusu tathmini ya hali ya siasa nchini na uchaguzi uliopita kwa Kamati Kuu, aliendeleza mwanzo wa mwisho wa safari ya Lowassa, Rostam na Chenge.
  Akizungumza katika kikao cha Kamati Kuu cha kuandaa ajenda za NEC, Chiligati alieleza kwamba haiba ya chama hicho ilikuwa imechafuliwa kwa kiasi kikubwa na viongozi waliokuwa wakitajwa katika tuhuma za ufisadi.
  Bila kutaja majina, Chiligati alisema kwamba tuhuma za kampuni ya kufua umeme ya Richmond ambayo baadaye ilizaa kampuni nyingine tata ya Dowans na kashfa ya ununuzi wa rada, wizi katika Benki Kuu wa kampuni hewa ya Kagoda ni kati ya mambo yaliyochangia sana katika kukinyima kura chama chao katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka jana na hivyo Sekretariati inapendekeza wahusika na tuhuma hizo wawajibike.
  Taarifa zinasema wajumbe kadhaa walichangia katika ripoti hiyo. Waziri Mkuu wa zamani John Malecela akisema kwa maoni yake isingekuwa muafaka watoswe Lowassa, Rostam na Chenge tu huku ikijulikana kuwa Sekretariti, na hasa Katibu Mkuu, Yusuf Makamba, akiwa anahusika kwa matendo na kauli zake kukinyima chama kura.
  Mwingine ambaye alipigilia msumari katika ‘jeneza’ la wanasiasa hao, ni Zakhia Meghji ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Fedha na yeye alimrushia makombora waziwazi Rostam akimtaja kuwa ni mhusika wa kampuni ya Kagoda na kwamba amekuwa akimchafua katika vyombo vya habari; huku akijua kufanya hivyo anaichafua CCM.
  Meghji, ambaye ameingia tena katika Kamati Kuu, anaelezwa kueleza wazi kwamba Rostam anastahili kuchukuliwa hatua bila kuchelewa.

  Sofia Simba awatetea, Kikwete amkejeli

  Na kama kawaida, Lowassa, Rostam na Chenge safari hii pia hawakukosa watetezi. Alisimama Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) Sophia Simba ambaye akiungwa mkono na mjumbe mmoja kutoka Zanzibar, walitaka uletwe ushahidi wa tuhuma hizo, vinginevyo hayo yalikuwa ni maneno ambayo yasingeweza kufanyiwa kazi.
  Hatua hiyo ya kina Sophia Simba kwa namna ilikejeliwa na Mwenyekiti Kikwete aliyechomekea ya kuwa ushahidi ulikuwa ni ushindi wake wa asilimia 61 mwaka 2010 badala ya asilimia 82 za mwaka 2005.

  Msekwa, Kinana waongeza nguvu hoja

  Hatua hiyo ya Mwenyekiti Kikwete ilimsimamisha Makamu Mwenyekiti Pius Msekwa, ambaye pamoja na Abdulrahman Kinana walishiriki katika tume ya usuluhishi wa wabunge na viongozi wa CCM mwaka jana ambao kwa kiasi kikubwa ulikuwa umechangiwa na tuhuma za vigogo katika masuala kama Richmond, Dowans, Kagoda na ununuzi wa rada.
  Bila kutafuna maneno, Msekwa alisema katika maoni yote waliyokusanya wakati wa usuluhishi, majina matatu yalikuwa yakipata maksi za juu. Na hayo ni ya Lowassa, Rostam na Chenge.
  Wakati akitaja majina hayo, Chenge na Rostam ambao walikuwa wajumbe wa Kamati Kuu, walikuwa katika kikao hicho na walionekana kuduwaa.
  Msekwa akasema hapakuhitajika ushahidi wa kipolisi kubaini kwamba watatu hao sasa walikuwa ni mzigo kwa chama na hoja za kila mara kwa Upinzani na wakosoaji wa CCM, na kwa ajili hiyo wakitakiwa kuwajibika.
  Taarifa zinasema kwamba huku upepo ukivuma vibaya kwa Lowassa, Rostam, Chenge na Makamba ndani ya Kamati Kuu, alisimama Kinana.
  Akasema kwamba matendo yote yaliyokuwa yakihusishwa na tuhuma za ufisadi yalifanyika mbele ya macho ya wajumbe wa Kamati Kuu.
  Naye, kama Msekwa, akasema hakukuwa na haja ya kutafuta ushahidi kwa vile tayari nguvu ya umma ilikuwa inataka CCM ichukue hatua dhidi ya ufisadi na watuhumiwa wa ufisadi.
  Akasema, kwa maoni yake, Mwenyekiti wa CCM ambaye pia ni Rais wa Jamhuri, ana vyombo vikuu vya kumshauri viwili, Baraza la Mawaziri na Kamati Kuu.
  Taarifa zinasema ni Kinana aliyependekeza Kamati Kuu ijiuzulu kwa kushindwa kumshauri vyema Mwenyekiti, uamuzi ambao kwa muda, ulionekana kuwa ulikuwa unawapunguzia joto na kuwalindia heshima Rostam na Chenge, lakini ambao ungewasilishwa kwenye NEC kupata baraka.

  Makongoro Nyerere mwiba mkali

  Lakini la kuvunda halina ubani, juzi ikiwa tayari Sekretariati na Kamati Kuu za zamani zikiwa zimejiuzulu, akichangia katika tathmini na mapendekezo ya Kamati Kuu ya kutaka Lowassa, Rostam na Chenge wawajibike, Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa Mara, Makongoro Nyerere, alizungumza kwa hisia za mguso mkubwa akisema isingewezekana Lowassa, Rostam na Chenge kuendelea kuwa na nafasi za uongozi ndani ya chama.
  Anasema mtoa habari wetu: “Kwanza alianza kwa kumwambia Mwenyekiti kwamba japo yeye ni Mwenyekiti wa Taifa, yeye (Makongoro) naye ni Mwenyekiti wa Mara na kwamba NEC ndio waajiri wa Mwenyekiti Taifa.
  “Akasema anapokaa Mwenyekiti wa Taifa ni mahala patakatifu, na kwa ajili hiyo pasingeweza kusogelewa na shetani, hata kama siku moja Mungu alipata kukutana na shetani barabarani.
  “Akasema kule site (kwenye eneo la ujenzi ambako yeye ndiko anakoshinda akichanganya zege na kupiga bati) wanasema na wanataka watuhumiwa wote wa ufisadi watoke kwenye nafasi zao.
  “Lowassa ni ndugu yangu. Sina matatizo naye. Najua ananipenda, nami nampenda. Lakini kule site wanasema hapana. Atoke. Tena nawe Mweyekiti ulipokwenda Monduli, ukainua mkono wake juu, ukasema hujapata kuona kama yeye (Lowassa), kule site wakauliza, sasa hii ndiyo nini?
  “Rostam simfahamu vizuri. Ninakotembelea yeye hawezi kuja na mimi siwezi kwenda anakotembelea. Sina ugomvi naye. Lakini kule site wanasema naye hapana. Ulipokwenda Igunga ukamuamsha mkono ukasema ni kama timu ya mpira iliyokamilika watu kwenye site wakauliza sasa hii ndiyo nini?
  “Nasikia Chenge wanamwita Mzee wa Vijisenti. Ni ndugu yangu. Sina hakika kama anavyo vijisenti kiasi hicho. Lakini kwenye site, si mimi, watu wanasema naye hapana.
  “Ulikwenda pia Rombo, ukamuamsha mkono Mramba, kule kwenye site watu wakatuuliza hii ni nini?, “ alikaririwa akisema Makongoro.
  Mifano aliyoitaja Makongoro kwa kumhusisha Kikwete ilijitokeza wakati akiwa katika kampeni za Uchaguzi Mkuu wa 2010, katika majimbo ya Igunga alikokuwa akigombea ubunge Rostam, Rombo alikokuwa akigombea ubunge Basili Mramba na Monduli alikogombea ubunge Lowassa.
  Akiwa katika majimbo hayo, Kikwete aliwanadi viongozi hao waliokuwa wamepitishwa na chama chake kuwania ubunge, licha ya tuhuma za ufisadi zilizokuwa zikielekezwa kwao.
  Kutokana na hatua hiyo ya Kikwete, makundi mbalimbali ya kijamii nchini yalikosoa hatua hiyo ya Rais kuwanadi watuhumiwa wa ufisadi, akitumia lugha ya “watu hao ni safi” huku Mramba akijinadi kuwa yeye ni panga la zamani lisiloisha makali.
  Habari zinaeleza kwamba wajumbe kutoka Zanzibar walizidi kuwakandamiza Rostam, Lowassa na Chenge, wakisema Visiwani hakuna watuhumiwa wa ufisadi na kwamba hawawezi kuwa chama kimoja na watuhumiwa wa ufisadi wanaokichafua chama, huku wakionyesha kuwa ni kauli ya pamoja kutoka CCM Zanzibar.
  Wajumbe wengi wa NEC-CCM wamelieleza gazeti hili kwamba, mbele ya macho yao, kwa mara ya kwanza Kikwete ameonyesha ni Mwenyekiti wa Chama tangu achukue madaraka hayo.
  Wanaeleza kuwa ameongoza vikao vyote kwa ujasiri mkubwa bila ubabaishaji pengine kama walivyokuwa wamemzoea na wameanza kujenga matumaini juu yake.
  Hata hivyo, wameeleza kuwa uamuzi mgumu uliochukuliwa na chama hicho ni lazima uambatane na juhudi za kubadili hali za uchumi kwa wananchi wa kawaida, vinginevyo itakuwa kazi bure.
  Katika uamuzi wake huo ambao unapaswa sasa kwenda sambamba na juhudi za kubadili hali za uchumi za wananchi, mabadiliko mengine yaliyofanywa yanalazimu Katiba ya chama hicho kubadilishwa.

  Pendekezo Baraza la Wazee liundwe

  Mabadiliko yanayolazimu Katiba kubadilishwa na mkutano mkuu wa CCM ni pamoja na kuanzishwa kwa Baraza la Wazee litakalokuwa na vikao na uamuzi huru na wakati wowote watakuwa na uwezo wa kutaka kuwasilisha mawazo yao katika vikao vikuu vya chama hicho.
  Mbali na baraza hilo, katiba pia itabadilishwa kuruhusu wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama hicho kuchaguliwa kutoka ngazi ya wilaya badala ya ngazi ya mkoa ya sasa.
  Inaelezwa pia kuwa itabidi chama hicho kifanye mabadiliko makubwa ya uongozi katika ngazi nyingine za mikoa na wilaya, ikitajwa bayana kuwa Makamba alikuwa amepachika watu wake wasiokitetea chama hicho kwa mujibu wa katiba yake na badala yake wamekuwa wakitumia madaraka yao kujifaidisha.

  Kejeli za Yusuf Makamba

  Wakati akitoa hotuba ya kuaga mbele ya wajumbe wa NEC, katika hali inayoweza kutafsiriwa kuwa amefurahia kung’oka kwa baadhi ya viongozi wenzake, Makamba alisema ameondoka lakini hakuondoka peke yake.

  Hata hivyo, kati ya watu ambao wameondoka wakiacha alama ya kutafsiriwa kuwa ni viongozi waliokigharimu chama hicho ni pamoja na yeye.
  Mara baada ya Makamba kung’oka watumishi mbalimbali wa CCM, Makao Makuu walishangiliwa, wengine wakijumuika katika tafrija ndogo ikiwa dhahiri kuwa hawakuwa katika utumishi wenye utulivu wakati wa kiongozi huyo.
  Raia Mwema ilimshuhudia mmoja wa wafanyakazi hao akiwa amevalia fulana ya njano, ikionekana imepauka kwa umri, yenye picha ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na maandishi yaliyoanza kufifia yaliyosomeka: “Bila CCM madhubuti nchi yetu itayumba”.
  Raia Mwema ilimuuliza mfanyakazi huyo, kwa nini umevaa fulana hii leo? (siku ambayo habari zilikuwa zinavuma za Sekretariati na Kamati Kuu kujiuzulu).
  Alijibu: “ Tena tangu asubuhi nimevaa hivihivi, na nilikaa kwenye lango kubwa ili kila mjumbe wa NEC anayepita hapa asome ujumbe huu,” alisema mfanyakazi huyo wa siku nyingi wa CCM. Maneno hayo ya Mwalimu, ya Agosti 1990, yameandikwa pia kwa herufi za mkolezo ndani ya ukumbi wa NEC Dodoma.
  Makamba pia amewahi kutoa kauli mbalimbali zilizopata kutajwa kuudhi baadhi ya viongozi waandamizi wa chama hicho, hasa wastaafu.
  Katika kongamo la miaka 10 baada ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, baadhi ya viongozi na wadau wengine nchini walijadili na kupendekeza Rais Jakaya Kikwete kuchukua uamuzi mgumu kwa kuwafukuza baadhi ya viongozi wa chama na serikali waliokuwa wakituhumiwa kwa ufisadi, na akishindwa ang’olewe yeye.
  Makamba alijitokeza na kujibu kuwa wanaofikiri hivyo ni wendawazimu na kwamba Kikwete hawezi kutoswa kwa sababu ndiye mtaji wa chama hicho.

  Mgawo wa fedha kwa watetezi

  Taarifa zaidi za kiuchunguzi zinabainisha kuwa baada ya upepo kwenda mrama dhidi ya watuhumiwa wa ufisadi, baadhi ya wajumbe inaodaiwa walipewa fedha kwa ajili ya kuwatetea watuhumiwa hao, walibaki kimya.
  “Kuna wajumbe fulani walipewa fedha kwa ajili ya kuwatetea kama ilivyo kawaida yao na hawa wanajulikana, lakini safari hii walikwama. Walisoma upepo wa kikao na ukali wa Mwenyekiti Kikwete, ilibidi wakae kimya wasije wakahatarisha nafasi zao pia,” anaeleza mjumbe mmoja.
  Mbali na hali hiyo, inaelezwa kuwa baadhi ya wajumbe sasa wamekuwa na wasiwasi juu ya hatima yao kisiasa na hasa wale ambao walikuwa wakitumia madaraka yao ndani ya chama hicho kukomoa wanachama wenzao; hasa waliokuwa wakiomba nafasi za uongozi ukiwamo ubunge.
  Imeelezwa kwamba baada ya uamuzi wa ‘kujivua gamba’ ngazi ya taifa, CCM sasa itahamishia kazi hiyo katika ngazi ya mikoa na kwamba tayari kuna taarifa za kuchukuliwa hatua kwa viongozi kadhaa wa mikoa wakiwamo Wenyeviti na Makatibu kadhaa.

  My Take: Ujasiri huu wa hawa watu umetoka wapi? kwanini wameamua kusema sasa? Je huu ndio mwisho wa mtandao ndani ya CCM? Je kuna kundi jipya limeibuka ndani ya CCM?
   
 11. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #11
  Apr 14, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,422
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  Mhhhhhhhh thanks, good food for thought!!!!!!!!!!!!!

  Pipozzzzzzzzzzzzzzzzz!!!!!!!!!!!!!!
   
 12. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #12
  Apr 14, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Tuwekee hapa
   
 13. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #13
  Apr 14, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Ni suala la kusubiri ila maisha yasipobadilka haitasaidia it means kwa raia maana wanapeana majukumu wao kwa wao,
  makundi hayatoisha na yataongezeka zaid,TUSUBIR
   
 14. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #14
  Apr 14, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Maamuzi ya NEC ya Tarehe 10.04.2011
  Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) imekutana tarehe 10 Aprili 2011 mjini Dodoma chini ya Mwenyekiti wa CCM, Mhe. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete. Katika kikao hicho, imejadili mambo mbali mbali na imetoa maamuzi yafuatayo:-

  UTEUZI WA WAGOMBEA UJUMBE WA NEC.

  Halmashauri Kuu ya Taifa imepitisha majina ya Wabunge na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa CCM walioomba wawe Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa. Kwa mujibu wa Katiba ya CCM, Wabunge wa CCM kumi (10) kutoka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Kamati ya Wabunge Wote wa CCM watakuwa Wajumbe wa NEC.

  Aidha Wawakilishi wa CCM watano (5) kutoka Kamati ya Wajumbe wote wa CCM wa Baraza la Wawakilishi watakuwa pia Wajumbe wa NEC.

  Nafasi 10 za Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa.

  Katika kugombea nafasi 10 za ujumbe wa NEC wamejitokeza Wabunge 40 wakiwamo Wanawake 13 na Wanaume 27. Katika kuwania nafasi hizi yametengwa makundi mawili kama ifuatavyo:-

  (a) Nafasi nane (8) zitagombewa na Wabunge kutoka Tanzania Bara.

  (b) Nafasi mbili (2) zitagombewa na Wabunge kutoka Zanzibar.

  Aidha kati ya nafasi nane zinazogombewa na Wabunge kutoka Tanzania Bara, nafasi tatu (3) zitagombewa na Wabunge Wanawake, na nafasi tano (5) zitagombewa na Wabunge Wanaume.

  Halmashauri Kuu ya Taifa imeamua kupitisha wagombea wote waliojitokeza ili waweze kipigiwa kura na Wabunge wenzao.
  Waliopitishwa kugombea nafasi hizo ni hawa wafuatao:-

  Kundi la Wanawake nafasi tatu (3):
  1. Mhe. Munde Tambwe ABDALLAH
  2. Mhe. Lolesia Maselle BUKWIMBA
  3. Mhe. Felister Aloyce BURA
  4. Mhe. Hawa Abdullrahaman GHASIA
  5. Mhe. Angella Jasmine KAIRUKI
  6. Mhe. Rosweeter Faustine KASIKILA
  7. Mhe. Betty Eliezer MACHANGU
  8. Mhe. Lita Louse MLAKI
  9. Mhe. Martha Moses MLATA
  10. Mhe. Ledian Mafuru MNG'ONG'O
  11. Mhe. Prof. Anna Kajumulo TIBAIJUKA
  12. Mhe. Martha Jachi UMBULLA
  13. Mhe. Anastazia James WAMBURA

  Kundi la Wanaume nafasi tano (5):

  1. Mhe. Said Ramadhan BWANAMDOGO
  2. Mhe. Mendrad Lutengano KIGOLA
  3. Mhe. Livingstone Joseph LUSINDE
  4. Mhe. Eng. Athuman Rashid MFUTAKAMBA
  5. Mhe. Nimrod Elirehemah MKONO
  6. Mhe. Abbas Zuberi MTEMVU
  7. Mhe. Mtutura Abdallah MTUTURA
  8. Mhe. Dr. Harrison George MWAKYEMBE
  9. Mhe. Mwigulu Lameck NCHEMBA
  10. Mhe. Job Yustino NDUGAI
  11. Mhe. Dr. Faustine Engelbert NDUGULILE
  12. Mhe. Hassan Athuman NGWILIZI
  13. Mhe. Ismail Aden RAGE
  14. Mhe. Christopher Donyokile Ole SENDEKA
  15. Mhe. Peter Joseph SERUKAMBA
  16. Mhe. Samwel John SITTA
  17. Mhe. Dr. Charles John TIZEBA
  18. Mhe. Murtaza Ally MANGUNGU
  19. Mhe. Ahmed Ally SALUMU
  20. Mhe. Dr. Hamis Andrea KINGWANGALLA

  Aidha, Halmashauri Kuu ya Taifa imepitisha majina ya wagombea wanaotokana na Baraza la Wawakilishi Zanzibar ili wote wapigiwe kura na Wawakilishi wenzao.

  Waliopitishwa kugombea ni hawa wafuatao:-

  Kundi la Wanawake Zanzibar nafasi moja (1):

  1. Mhe. Faida Mohamed BAKARI
  2. Mhe. Mwanakhamis Kassim SAID

  Kundi la Wanaume Zanzbar nafasi moja (1):

  1. Mhe. Yahya Kassim ISSA
  2. Mhe. Mahadhi Juma MAALIM
  3. Mhe. Dkt. Abdallah JUma SAADALA
  4. Mhe. Salum Hassan TURKY
  5. Mhe. Mohamed Amour CHOMBO
  6. Mhe. Said Mussa ZUBEIR

  Halmashauri Kuu ya Taifa pia imeplitisha majina ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi watakaogombea nafasi tano (5) za Ujumbe wa NEC. Kati ya nafasi hizo, mbili ni kwa Wawakilishi wanawake na tatu kwa Wawakilishi Wanaume.

  Kundi la Wanawake nafasi mbili (2):

  1. Mhe. Viwe Khamis ABDALLAH
  2. Mhe. Wanu Hafidh AMEIR
  3. Mhe. Salma Mussa BILAL
  4. Mhe. Raya Suleiman HAMAD
  5. Mhe. Sira Ubwa MAMBOYA
  6. Mhe. Fatma Mbarouk SAID
  7. Mhe. Shadya Mohamed SULEIMAN

  Kundi la Wanaume nafasi tatu (3):

  1. Mhe. Hamza Hassan JUMA
  2. Mhe. Mlinda Mbarouk JUMA
  3. Mhe. Mohamed Said MOHAMED
  4. Mhe. Dkt. Mwinyihaji Makame MWADINI
  5. Mhe. Mohamed Mohamed MUSSA
  6. Mhe. Suleiman Othman NYANGA
  7. Mhe. Haroun Ali SULEIMAN
  8. Mhe. Issa Haji USSI (Gavu)

  2. WAGOMBEA NAFASI YA KATIBU WA KAMATI YA WABUNGE WOTE WA CCM

  Halmashauri Kuu ya Taifa imepitisha majina ya Wabunge wote wawili walioomba nafasi hiyo ambao ni:-

  (1) Mhe. Mohamed Seif KHATIB - Mbunge wa Uzini (Zanzibar)
  (2) Mhe. Jenista J. MHAGAMA - Mbunge wa Peramiho

  Wagombea Nafasi ya Katibu wa Kamati ya Wajumbe wote wa CCM wa Baraza la Wawakilishi.

  Wagombea wote walioomba nafasi hiyo wamepitishwa na Halmashauri Kuu ya Taifa nao ni hawa wafuatao:-

  1. Mhe. Mgeni Hassan JUMA
  2. Mhe. Salmin Awadh SALMIN
  3. Mhe. Mussa Khamis SILIMA
  4. Mhe. Mbarouk Mussa WADI (Mtando)

  3. KUJAZA NAFASI WAZI YA MWENYEKITI WA UMOJA WA VIJANA WA CCM TAIFA

  Kutokana na kujiuzulu kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Taifa, Ndugu Hamad Yussuf Masauni (MNEC) tarehe 18 Mei, 2010, nafasi hiyo imekuwa wazi kwa muda wote huo. Kwa mujibu wa Kanuni za Umoja wa Vijana wa CCM, Mwenyekiti anapokuwa hayupo Makamu Mwenyekiti ndiye anayekaimu nafasi yake. Kwa sasa Ndugu Beno Malisa, Makamu Mwenyekiti wa UVCCM ndiye anayekaimu nafasi hiyo.

  Baada ya Kanuni za Uchaguzi wa UVCCM Toleo la Saba la mwaka 2008, kuzingatiwa, Halmashauri Kuu ya Taifa imetoa idhini ya nafasi ya Mwenyekiti wa UVCCM Taifa iliyoachwa wazi itangazwe.

  Aidha, Halmashauri Kuu ya Taifa imetoa ratiba ya mchakato wa kujaza nafasi hiyo kama ifuatavyo:-

  Tarehe 11-20 Mei, 2011
  -
  Kuchukua na kurudisha fomu.

  Tarehe 01-30 Juni, 2011
  -
  Vikao vya mchujo kuanzia Sekretarieti, Kamati ya Utekelezaji na Baraza Kuu.

  Tarehe 01-30 Julai, 2011
  -
  Vikao vya Uteuzi vya Chama Cha Mapinduzi

  Agosti/Septemba, 2011
  -
  Agosti/Septemba, 2011

  4. KUHUSU MUSWADA WA SHERIA YA KUREKEBISHA KATIBA

  Halmashauri Kuu ya Taifa, katika kikao chake ilipata fursa ya kupewa maelezo juu ya yaliyomo ndani ya Muswada wa Sheria ya Kuanzisha Tume ya Kuratibu Mchakato wa Mabadiliko ya Katiba na kuazimia yafuatayo:-

  (i) Wananchi waelimishwe kuhusu madhumuni halisi ya muswada huu, kwamba madhumuni yake ni kuweka taratibu zitakazotumika katika kukusanya maoni ya wananchi juu Katiba wanayoitaka. Huu si Muswada wa Katiba yenyewe.

  Muswada huo utafsiriwe kwa lugha ya Kiswahili ili kuwawezesha wananchi wengi kuuelewa na hivyo kuwa katika nafasi nzuri ya kutoa maoni.

  5. KUHUSU TATHMINI YA UCHAGUZI MKUU 2010

  Halmashauri Kuu ya Taifa baada ya kujadili taarifa ya Tathmini ya Uchaguzi Mkuu wa 2010, imeagiza mambo yafuatayo:-
  (a) Halmashauri Kuu ya Taifa imetoa Shukurani kwa wana CCM na wananchi kwa jumla kwa kukiunga mkono Chama Cha Mapinduzi wakati wa uchaguzi kwa kukipigia kura nyingi zilizokipa ushindi na hatimaye kuunda Serikali ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Wananchi wanaombwa kuendelea kukiunga mkono Chama Cha Mapinduzi katika chaguzi zingine zijazo.
  (b) Serikali zote mbili, ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, zimetakiwa zitekeleze ipasavyo Ilani ya CCM ya 2010-2015 kwa kadri Chama kilivyoahidi wakati wa kampeni; kama zilivyo tekeleze kwa ufanisi mkubwa Ilani iliyopita iliyopita ya Uchaguzi ya 2005-2010.
  (c) Serikali zote mbili ziongeze kasi ya kushughulikia matatizo ya wananchi ili kuwaondolea kero zinazowakabili, hasa tatizo la kupanda kwa gharama za maisha.

  (d) Chama Cha Mapinduzi na Serikali zake kiongeze kasi ya mapambano dhidi ya viongozi na wanachama wanaojihusisha na rushwa. Aidha viongozi na wanachama wanaotuhumiwa kwa vitendo vya rushwa wajenge tabia ya kuwajibika wenyewe kwa maslahi ya Chama wasipofanya hivyo Chama kiwawajibishe kwa maslahi ya Chama na nchi.

  6. KUHUSU MAGEUZI NDANI YA CHAMA

  Halmashauri Kuu ya Taifa imejadili kwa makini agenda ya hoja na haja ya kufanya mageuzi ndani ya Chama, na imetoa maamuzi yafuatayo:-

  (a) Imewapongeza Wajumbe wa Kamati Kuu iliyopita, na Wajumbe wa Sekretarieti, kwa uamuzi wao wa kijasiri na hekima wa kujiuzulu ili kutoa nafasi kwa Mwenyekiti na Halmashauri Kuu ya Taifa kuunda upya Kamati Kuu na Sekretarieti, kama hatua ya mwanzo ya kuleta mageuzi ndani ya Chama kwa lengo la kukijenga upya Chama Cha Mapinduzi.

  (b) Kama hatua ya kujipanga upya, NEC imewateua Wajumbe wa Kamati Kuu wafuatao:-

  (1) Dr. Hussein Ali MWINYI
  (2) Dr. Maua Abeid DAFTARI
  (3) Ndugu Samia Suluhu HASSAN
  (4) Ndugu Omar Yussuf MZEE
  (5) Prof. Makame Mnyaa MBARAWA
  (6) Ndugu Mohammed Seif KHATIB
  (7) Ndugu Shamsi Vuai NAHODHA
  (8) Ndugu Abdulrahaman KINANA
  (9) Ndugu Zakiah Hamdani MEGHJI
  (10) Ndugu Abdallah Omar KIGODA
  (11) Ndugu Pindi Hazara CHANA
  (12) Ndugu Steven Masatu WASSIRA
  (13) Ndugu Constansia BUHIE
  (14) Ndugu William LUKUVI

  (c) Vile vile NEC imeteua wafuatao kuwa Wajumbe wa Sekretarieti:-

  (1)
  Katibu Mkuu
  -
  Ndugu Wilson MUKAMA
  (2)
  Naibu Katibu Mkuu (Bara)
  -
  Capt. (Mst) John Z. CHILIGATI
  (3)
  Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar)
  -
  Ndugu Vuai Ali VUAI

  Wakuu wa Idara

  (1)
  Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi

  -
  Ndugu Nape Mosses NNAUYE
  (2)
  Katibu wa NEC, Organaizesheni

  -
  Ndugu Asha Abdallah JUMA
  (3)
  Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha

  -
  Ndugu Mwigulu MCHEMBA
  (4)
  Katibu wa NEC, Siasa na Ushirikiano wa Kimataifa
  -
  Ndugu Januari Yussuf MAKAMBA
  (d) Halmashauri Kuu ya Taifa imeagiza kwamba katika mageuzi yatakayofanywa yazingatie maeneo yafuatayo:-
  a. Muundo wa Chama utazamwe upya ili kuona kama unakidhi mahitaji na mazingira ya kisiasa yaliyopo hivi sasa.

  b. Mfumo wa uchaguzi ndani ya Chama, na hasa kura za maoni nao utazamwe kwa lengo la kuboresha.

  (e) Halmashauri Kuu ya Taifa imeamua kurejeshwa kwa Tume ya Udhibiti na Nidhamu ili kukabiliana na tatizo lililozuka kwa kasi la ukiukwaji wa maadili na utovu wa nidhamu ndani ya Chama.

  (f) NEC imehimiza uimarishwe utaratibu wa mafunzo kwa viongozi na makada, na kwamba ujenzi wa vyuo vya Chama vya Ihemi (Iringa) na Tunguu (Zanzibar) uharakishwe ili kutekeleza azma hii, kama sehemu ya mageuzi ndani ya Chama.

  (g) NEC imeagiza kwamba Chama kirudi kwa wanachama; katika kukirudisha Chama kwa wanachama, Katiba ya Chama itoe madaraka ngazi za chini, kwa kufanya mambo yafuatayo:-

  (i) Ngazi za Matawi na Shina ziimarishwe kwa raslimali na mafunzo ili kuboresha utendaji wake, na hasa kuimarisha kufanyika kwa vikao vya Shina na Matawi.

  (ii) Katiba ya CCM itazamwe upya ili iwezeshe viongozi wa Matawi wawe Wajumbe katika Vikao vya Halmashauri Kuu ya Wilaya.

  (iii) Wajumbe wa NEC sasa wachaguliwe kutoka ngazi ya Wilaya badala ya ngazi ya Mkoa, isipokuwa Wawakilishi wa makundi maalumu ya Vijana na Wanawake hawa wataendelea kuchaguliwa kutoka ngazi ya Taifa.

  (iv) Halmashauri Kuu ya Taifa imeamua kuugawa Mkoa wa Mjini Magharibi kuwa mikoa miwili ya kichama: Mkoa wa Magharibi na Mkoa wa Mjini ili kuleta ufanisi wa shughuli za Chama.

  (h) Halmashauri Kuu ya Taifa imeagiza kwamba huu ni mwanzo wa mchakato wa mageuzi ndani ya Chama, na kwamba mageuzi haya ni muhimu yafanyike hivi sasa ili CCM iende na wakati kwa lengo la kujijenga upya tayari kwa chaguzi zijazo.

  7. UTEUZI WA WAJUMBE WA NEC
  Kwa mujibu wa Katiba ya CCM, Mwenyekiti amepewa mamlaka ya kuteua Wajumbe 10 wa Halmashauri Kuu ya Taifa. Awali Mwenyekiti aliwateua Wajumbe wawili ambao ni Ndugu Cleopa Msuya na Ndugu Salim Ahmed Salim.

  Mwenyekiti wa CCM amewateua Wajumbe wengine ambao ni:-

  1. Ndugu Anna Abdallah
  2. Ndugu Peter Kisumo
  3. Ndugu Mwigulu Nchemba
  4. Ndugu Januari Makamba
  5. Ndugu Ali Juma Shamhuna
  6. Ndugu Wilson Mukama
  7. Dr. Emmanuel Nchimbi  Imetayarishwa...
  10:27:38 11.04.2011
   
 15. Tina

  Tina JF-Expert Member

  #15
  Apr 14, 2011
  Joined: Jul 9, 2007
  Messages: 571
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 45
  Na Lowassa, Chenge na Rostam si mafisadi kwa mujibu wa tafsiri yako? Je, azimio hilo lilitokana na nini? Je, waliochangia hawakuwataja? Soma Mtanzania ya jana utaona wamewataja mafisadi na hilo ni gazeti lenu, ila mulichosema ni kwamba mumeiba na JK sasa anawaacha munakamatwa wenyewe lakni hamsemi kuwa nyie si wezi.. Jamani nyie ni wezi, suala la kutaka kupamba ppamba maneno haitawasaidia kitu
   
 16. S

  Safre JF-Expert Member

  #16
  Apr 14, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 240
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Msaada kidogo kubadilisha uongozi ndan ya chama ni kosa kwan ni lazima wataarifiwe kama mwenyekiti hawez fanya mabadiliko(hata kama mabaya au mazuri)
   
 17. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #17
  Apr 14, 2011
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,499
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Wanaoichafua ccm sio hao peke yao. Wako wengi sana na wengine badi wamebaki katika kamati kuu. Kuna magamba mengi yanayotakiwa kuvuliwa;
  Kilichofanyika ni mwenyekiti kuweka timu yake kwa malengo anayoyajua mwenyewe; bado nyoka anabaki nyoka tu!
   
 18. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #18
  Apr 14, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,760
  Likes Received: 83,064
  Trophy Points: 280
  Rostam, Lowassa wakatwa miguu

  Waandishi Wetu, Dodoma
  RAIA MWEMA
  Aprili 13, 2011

  [​IMG]Yumo pia Chenge, sasa watakiwa kujiuzulu

  [​IMG]Werema, Malecela, Meghji wawamaliza

  [​IMG]Richmond, Kagoda na Rada zawaponza

  UNAWEZA kusema kwamba huu ni mwisho wa zama kwa Edward Lowassa, Rostam Aziz na Andrew Chenge ambao, juzi Jumatatu, chama chao kiliwatosa kwa kuwapa siku 90 kujiondoa katika nafasi walizonazo kwa vile wamekuwa wakichafua haiba ya chama hicho.

  Taarifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), iliyotolewa juzi usiku kwa vyombo vya habari, mjini Dodoma, imeeleza kwamba vikao vya juu vya chama hicho vinataka wanasiasa hao watatu wajiuzulu nafasi zao zote za uongozi katika Chama.
  Vikao hivyo vya Sekretariati, Kamati Kuu na Halmashauri Kuu (NEC), vilivyokuwa vimeanza Jumatano ya wiki iliyopita na kukamilika juzi usiku, vililenga kutekeleza dhamira ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete ya chama hicho ‘kujivua gamba'.
  Dhana ya CCM kujivua gamba inahusishwa na matokeo mabaya ya chama hicho katika uchaguzi wa 2010 ambapo kilipata upinzani mkali kutoka Chadema.
  Chenge, Rostam, Lowassa wapime wenyewe
  "Kama mlivyomsikia Mwenyekiti (Jakaya Kkwete) wale wote ambao wamekuwa wakituhumiwa kukichafua Chama, NEC imeamua watupishe.

  "Uamuzi ni kwamba katika miezi mitatu wapime wenyewe, wajiondoe katika nafasi zao. Kama watakuwa hawajafanya hivyo katika miezi mitatu ijayo, hadi tutakapokutana hapa, basi chama kitawaondoa," alisema John Chiligati, Katibu wa uenezi katika sekretariati iliyopita ambaye mabadiliko yaliyotangazwa juzi yamempa nafasi ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara).

  Kuanguka kwa Lowassa, Waziri Mkuu aliyejiuzulu mwaka 2008 ambaye pia ni Mbunge wa Monduli na mjumbe wa NEC, Rostam Aziz ambaye ni mfanyabiashara, Mbunge wa Igunga na mjumbe wa NEC na Chenge, mwanasheria aliyechafuka baada ya kutumikia nafasi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kipindi chote cha awamu ya Benjamin Mkapa, Mbunge wa Bariadi Magharibi na mjumbe wa NEC, ni jambo lililotarajiwa.

  Wanasiasa hao watatu wamekuwa wakitajwa katika tuhuma mbalimbali za ufisadi lakini uongozi wa CCM umekuwa ukitetea ukidai kutokuwapo kwa ushahidi wa kisheria dhidi yao.

  Mwanasheria Mkuu achochea ‘moto'
  Pengine aliyeharakisha kuanguka kwao ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema ambaye alikuwa ameitwa mwishoni mwa wiki iliyopita na Mwenyekiti Kikwete, kutoa ufafanuzi kwa Kamati Kuu juu ya mambo kadhaa, likiwamo suala la mchakato wa Katiba mpya.

  "Kifo cha kina Lowassa, Rostam na Chenge kimeharakishwa na Werema. Aliletwa na Mwenyekiti kuja kufafanua mambo kadhaa kama mchakato wa Katiba mpya.

  "Katika mchango wake kama mtu aliyeko nje ya Chama, alizungumzia mambo ambayo yeye alisema hayaendi sawa ndani ya CCM. Kwanza alianza kwa kusema yeye si mwana CCM; japo huko nyuma, kama walivyokuwa wengi, alipata kuwa mwanachama.

  "Akasema kwao anakotoka (Jaji Werema anatoka Mkoa wa Mara) mwanamume anapaswa kusema ukweli hata kama ukweli huo unauma kiasi gani.

  " Akasema kwamba alikuwa anaona tatizo kwamba taarifa nyingi za vikao kama hicho alichokuwa ameitwa kuzungumza, zilikuwa zinavuja sana.
  " Akasema hata hayo ambayo angeyasema, jioni yangekuwa yamewafikia watu wa nje, na wahusika wakubwa wa kuvujisha taarifa hizo walikuwa ndani ya Kamati Kuu hiyo hiyo.

  " Akiachana na hilo, akahoji kwa nini, chama hicho kinalialia kuwa haiba yake imeshuka na wakati huo huo kikikumbatia vitu kama Richmond na Dowans ambavyo vinaichefua jamii na ambavyo wahusika wake wakuu wamo katika uongozi wa juu wa chama," anasema mjumbe mmoja wa Kamati Kuu aliyezungumza na Raia Mwema.

  Chiligati, Malecela wapigilia msumari
  Ni kana kwamba moto aliokuwa ameuwasha Jaji Werema jana yake ulirejewa na Chiligati ambaye akiwasilisha ripoti ya Sekretariati kuhusu tathmini ya hali ya siasa nchini na uchaguzi uliopita kwa Kamati Kuu, aliendeleza mwanzo wa mwisho wa safari ya Lowassa, Rostam na Chenge.

  Akizungumza katika kikao cha Kamati Kuu cha kuandaa ajenda za NEC, Chiligati alieleza kwamba haiba ya chama hicho ilikuwa imechafuliwa kwa kiasi kikubwa na viongozi waliokuwa wakitajwa katika tuhuma za ufisadi.

  Bila kutaja majina, Chiligati alisema kwamba tuhuma za kampuni ya kufua umeme ya Richmond ambayo baadaye ilizaa kampuni nyingine tata ya Dowans na kashfa ya ununuzi wa rada, wizi katika Benki Kuu wa kampuni hewa ya Kagoda ni kati ya mambo yaliyochangia sana katika kukinyima kura chama chao katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka jana na hivyo Sekretariati inapendekeza wahusika na tuhuma hizo wawajibike.

  Taarifa zinasema wajumbe kadhaa walichangia katika ripoti hiyo. Waziri Mkuu wa zamani John Malecela akisema kwa maoni yake isingekuwa muafaka watoswe Lowassa, Rostam na Chenge tu huku ikijulikana kuwa Sekretariti, na hasa Katibu Mkuu, Yusuf Makamba, akiwa anahusika kwa matendo na kauli zake kukinyima chama kura.

  Mwingine ambaye alipigilia msumari katika ‘jeneza' la wanasiasa hao, ni Zakhia Meghji ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Fedha na yeye alimrushia makombora waziwazi Rostam akimtaja kuwa ni mhusika wa kampuni ya Kagoda na kwamba amekuwa akimchafua katika vyombo vya habari; huku akijua kufanya hivyo anaichafua CCM.

  Meghji, ambaye ameingia tena katika Kamati Kuu, anaelezwa kueleza wazi kwamba Rostam anastahili kuchukuliwa hatua bila kuchelewa.

  Sofia Simba awatetea, Kikwete amkejeli
  Na kama kawaida, Lowassa, Rostam na Chenge safari hii pia hawakukosa watetezi. Alisimama Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) Sophia Simba ambaye akiungwa mkono na mjumbe mmoja kutoka Zanzibar, walitaka uletwe ushahidi wa tuhuma hizo, vinginevyo hayo yalikuwa ni maneno ambayo yasingeweza kufanyiwa kazi.

  Hatua hiyo ya kina Sophia Simba kwa namna ilikejeliwa na Mwenyekiti Kikwete aliyechomekea ya kuwa ushahidi ulikuwa ni ushindi wake wa asilimia 61 mwaka 2010 badala ya asilimia 82 za mwaka 2005.

  Msekwa, Kinana waongeza nguvu hoja
  Hatua hiyo ya Mwenyekiti Kikwete ilimsimamisha Makamu Mwenyekiti Pius Msekwa, ambaye pamoja na Abdulrahman Kinana walishiriki katika tume ya usuluhishi wa wabunge na viongozi wa CCM mwaka jana ambao kwa kiasi kikubwa ulikuwa umechangiwa na tuhuma za vigogo katika masuala kama Richmond, Dowans, Kagoda na ununuzi wa rada.

  Bila kutafuna maneno, Msekwa alisema katika maoni yote waliyokusanya wakati wa usuluhishi, majina matatu yalikuwa yakipata maksi za juu. Na hayo ni ya Lowassa, Rostam na Chenge.

  Wakati akitaja majina hayo, Chenge na Rostam ambao walikuwa wajumbe wa Kamati Kuu, walikuwa katika kikao hicho na walionekana kuduwaa.

  Msekwa akasema hapakuhitajika ushahidi wa kipolisi kubaini kwamba watatu hao sasa walikuwa ni mzigo kwa chama na hoja za kila mara kwa Upinzani na wakosoaji wa CCM, na kwa ajili hiyo wakitakiwa kuwajibika.

  Taarifa zinasema kwamba huku upepo ukivuma vibaya kwa Lowassa, Rostam, Chenge na Makamba ndani ya Kamati Kuu, alisimama Kinana.
  Akasema kwamba matendo yote yaliyokuwa yakihusishwa na tuhuma za ufisadi yalifanyika mbele ya macho ya wajumbe wa Kamati Kuu.

  Naye, kama Msekwa, akasema hakukuwa na haja ya kutafuta ushahidi kwa vile tayari nguvu ya umma ilikuwa inataka CCM ichukue hatua dhidi ya ufisadi na watuhumiwa wa ufisadi.

  Akasema, kwa maoni yake, Mwenyekiti wa CCM ambaye pia ni Rais wa Jamhuri, ana vyombo vikuu vya kumshauri viwili, Baraza la Mawaziri na Kamati Kuu.

  Taarifa zinasema ni Kinana aliyependekeza Kamati Kuu ijiuzulu kwa kushindwa kumshauri vyema Mwenyekiti, uamuzi ambao kwa muda, ulionekana kuwa ulikuwa unawapunguzia joto na kuwalindia heshima Rostam na Chenge, lakini ambao ungewasilishwa kwenye NEC kupata baraka.

  Makongoro Nyerere mwiba mkali
  Lakini la kuvunda halina ubani, juzi ikiwa tayari Sekretariati na Kamati Kuu za zamani zikiwa zimejiuzulu, akichangia katika tathmini na mapendekezo ya Kamati Kuu ya kutaka Lowassa, Rostam na Chenge wawajibike, Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa Mara, Makongoro Nyerere, alizungumza kwa hisia za mguso mkubwa akisema isingewezekana Lowassa, Rostam na Chenge kuendelea kuwa na nafasi za uongozi ndani ya chama.
  Anasema mtoa habari wetu: "Kwanza alianza kwa kumwambia Mwenyekiti kwamba japo yeye ni Mwenyekiti wa Taifa, yeye (Makongoro) naye ni Mwenyekiti wa Mara na kwamba NEC ndio waajiri wa Mwenyekiti Taifa.

  "Akasema anapokaa Mwenyekiti wa Taifa ni mahala patakatifu, na kwa ajili hiyo pasingeweza kusogelewa na shetani, hata kama siku moja Mungu alipata kukutana na shetani barabarani.

  "Akasema kule site (kwenye eneo la ujenzi ambako yeye ndiko anakoshinda akichanganya zege na kupiga bati) wanasema na wanataka watuhumiwa wote wa ufisadi watoke kwenye nafasi zao.

  "Lowassa ni ndugu yangu. Sina matatizo naye. Najua ananipenda, nami nampenda. Lakini kule site wanasema hapana. Atoke. Tena nawe Mweyekiti ulipokwenda Monduli, ukainua mkono wake juu, ukasema hujapata kuona kama yeye (Lowassa), kule site wakauliza, sasa hii ndiyo nini?

  "Rostam simfahamu vizuri. Ninakotembelea yeye hawezi kuja na mimi siwezi kwenda anakotembelea. Sina ugomvi naye. Lakini kule site wanasema naye hapana. Ulipokwenda Igunga ukamuamsha mkono ukasema ni kama timu ya mpira iliyokamilika watu kwenye site wakauliza sasa hii ndiyo nini?

  "Nasikia Chenge wanamwita Mzee wa Vijisenti. Ni ndugu yangu. Sina hakika kama anavyo vijisenti kiasi hicho. Lakini kwenye site, si mimi, watu wanasema naye hapana.

  "Ulikwenda pia Rombo, ukamuamsha mkono Mramba, kule kwenye site watu wakatuuliza hii ni nini?, " alikaririwa akisema Makongoro.

  Mifano aliyoitaja Makongoro kwa kumhusisha Kikwete ilijitokeza wakati akiwa katika kampeni za Uchaguzi Mkuu wa 2010, katika majimbo ya Igunga alikokuwa akigombea ubunge Rostam, Rombo alikokuwa akigombea ubunge Basili Mramba na Monduli alikogombea ubunge Lowassa.
  Akiwa katika majimbo hayo, Kikwete aliwanadi viongozi hao waliokuwa wamepitishwa na chama chake kuwania ubunge, licha ya tuhuma za ufisadi zilizokuwa zikielekezwa kwao.

  Kutokana na hatua hiyo ya Kikwete, makundi mbalimbali ya kijamii nchini yalikosoa hatua hiyo ya Rais kuwanadi watuhumiwa wa ufisadi, akitumia lugha ya "watu hao ni safi" huku Mramba akijinadi kuwa yeye ni panga la zamani lisiloisha makali.

  Habari zinaeleza kwamba wajumbe kutoka Zanzibar walizidi kuwakandamiza Rostam, Lowassa na Chenge, wakisema Visiwani hakuna watuhumiwa wa ufisadi na kwamba hawawezi kuwa chama kimoja na watuhumiwa wa ufisadi wanaokichafua chama, huku wakionyesha kuwa ni kauli ya pamoja kutoka CCM Zanzibar.

  Wajumbe wengi wa NEC-CCM wamelieleza gazeti hili kwamba, mbele ya macho yao, kwa mara ya kwanza Kikwete ameonyesha ni Mwenyekiti wa Chama tangu achukue madaraka hayo.

  Wanaeleza kuwa ameongoza vikao vyote kwa ujasiri mkubwa bila ubabaishaji pengine kama walivyokuwa wamemzoea na wameanza kujenga matumaini juu yake.

  Hata hivyo, wameeleza kuwa uamuzi mgumu uliochukuliwa na chama hicho ni lazima uambatane na juhudi za kubadili hali za uchumi kwa wananchi wa kawaida, vinginevyo itakuwa kazi bure.
  Katika uamuzi wake huo ambao unapaswa sasa kwenda sambamba na juhudi za kubadili hali za uchumi za wananchi, mabadiliko mengine yaliyofanywa yanalazimu Katiba ya chama hicho kubadilishwa.
  Pendekezo Baraza la Wazee liundwe
  Mabadiliko yanayolazimu Katiba kubadilishwa na mkutano mkuu wa CCM ni pamoja na kuanzishwa kwa Baraza la Wazee litakalokuwa na vikao na uamuzi huru na wakati wowote watakuwa na uwezo wa kutaka kuwasilisha mawazo yao katika vikao vikuu vya chama hicho.

  Mbali na baraza hilo, katiba pia itabadilishwa kuruhusu wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama hicho kuchaguliwa kutoka ngazi ya wilaya badala ya ngazi ya mkoa ya sasa.

  Inaelezwa pia kuwa itabidi chama hicho kifanye mabadiliko makubwa ya uongozi katika ngazi nyingine za mikoa na wilaya, ikitajwa bayana kuwa Makamba alikuwa amepachika watu wake wasiokitetea chama hicho kwa mujibu wa katiba yake na badala yake wamekuwa wakitumia madaraka yao kujifaidisha.

  Kejeli za Yusuf Makamba
  Wakati akitoa hotuba ya kuaga mbele ya wajumbe wa NEC, katika hali inayoweza kutafsiriwa kuwa amefurahia kung'oka kwa baadhi ya viongozi wenzake, Makamba alisema ameondoka lakini hakuondoka peke yake.

  Hata hivyo, kati ya watu ambao wameondoka wakiacha alama ya kutafsiriwa kuwa ni viongozi waliokigharimu chama hicho ni pamoja na yeye.
  Mara baada ya Makamba kung'oka watumishi mbalimbali wa CCM, Makao Makuu walishangiliwa, wengine wakijumuika katika tafrija ndogo ikiwa dhahiri kuwa hawakuwa katika utumishi wenye utulivu wakati wa kiongozi huyo.
  Raia Mwema ilimshuhudia mmoja wa wafanyakazi hao akiwa amevalia fulana ya njano, ikionekana imepauka kwa umri, yenye picha ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na maandishi yaliyoanza kufifia yaliyosomeka: "Bila CCM madhubuti nchi yetu itayumba".
  Raia Mwema ilimuuliza mfanyakazi huyo, kwa nini umevaa fulana hii leo? (siku ambayo habari zilikuwa zinavuma za Sekretariati na Kamati Kuu kujiuzulu).

  Alijibu: " Tena tangu asubuhi nimevaa hivihivi, na nilikaa kwenye lango kubwa ili kila mjumbe wa NEC anayepita hapa asome ujumbe huu," alisema mfanyakazi huyo wa siku nyingi wa CCM. Maneno hayo ya Mwalimu, ya Agosti 1990, yameandikwa pia kwa herufi za mkolezo ndani ya ukumbi wa NEC Dodoma.
  Makamba pia amewahi kutoa kauli mbalimbali zilizopata kutajwa kuudhi baadhi ya viongozi waandamizi wa chama hicho, hasa wastaafu.

  Katika kongamo la miaka 10 baada ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, baadhi ya viongozi na wadau wengine nchini walijadili na kupendekeza Rais Jakaya Kikwete kuchukua uamuzi mgumu kwa kuwafukuza baadhi ya viongozi wa chama na serikali waliokuwa wakituhumiwa kwa ufisadi, na akishindwa ang'olewe yeye.
  Makamba alijitokeza na kujibu kuwa wanaofikiri hivyo ni wendawazimu na kwamba Kikwete hawezi kutoswa kwa sababu ndiye mtaji wa chama hicho.

  Mgawo wa fedha kwa watetezi
  Taarifa zaidi za kiuchunguzi zinabainisha kuwa baada ya upepo kwenda mrama dhidi ya watuhumiwa wa ufisadi, baadhi ya wajumbe inaodaiwa walipewa fedha kwa ajili ya kuwatetea watuhumiwa hao, walibaki kimya.

  "Kuna wajumbe fulani walipewa fedha kwa ajili ya kuwatetea kama ilivyo kawaida yao na hawa wanajulikana, lakini safari hii walikwama. Walisoma upepo wa kikao na ukali wa Mwenyekiti Kikwete, ilibidi wakae kimya wasije wakahatarisha nafasi zao pia," anaeleza mjumbe mmoja.

  Mbali na hali hiyo, inaelezwa kuwa baadhi ya wajumbe sasa wamekuwa na wasiwasi juu ya hatima yao kisiasa na hasa wale ambao walikuwa wakitumia madaraka yao ndani ya chama hicho kukomoa wanachama wenzao; hasa waliokuwa wakiomba nafasi za uongozi ukiwamo ubunge.

  Imeelezwa kwamba baada ya uamuzi wa ‘kujivua gamba' ngazi ya taifa, CCM sasa itahamishia kazi hiyo katika ngazi ya mikoa na kwamba tayari kuna taarifa za kuchukuliwa hatua kwa viongozi kadhaa wa mikoa wakiwamo Wenyeviti na Makatibu kadhaa.
  Uongozi Mpya

  Katika uamuzi huo, CCM iliunda upya Kamati Kuu yake na Sekretarieti ya chama hicho kwa kumuingiza, Wilson Mkama kuwa Katibu Mkuu wa CCM kuchukua nafasi ya Yusuf Makamba.

  Mkama amekuwa kiongozi kwa muda mrefu Serikalini , na kwa sasa ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Magazeti ya Serikali ya Tanzania Standard Newspapers (TSN).

  Aliyekuwa Katibu wa Uenezi na Itikadi CCM, John Chiligati sasa anakuwa Naibu Katibu Mkuu CCM Tanzania Bara kuchukua nafasi ya George Mkuchika.

  Naibu Katibu Mkuu mpya wa CCM Zanzibar ni Vuai Ali Vuai, kuchukua nafasi ya Ramadhani Feruzi na Januari Makamba anakuwa Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa badala ya Bernard Membe.

  Mwigulu Mchemba anakuwa Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha, akichukua nafasi ya Amos Makala, wakati Aisha Abdallah Juma anakuwa Katibu wa NEC Oganaizeshi, akichukua nafasu ya Kidawa Saleh na Nape Nnauye anakuwa Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi.

  Kamati Kuu mpya ya CCM ina wajumbe 14; Wajumbe kutoka Tanzania Bara ni Abdulrahman Kinana, Zakia Megji, Abdallah Kigoda, Pindi Chana, Stephen Wassira, Costansia Bugie na William Lukuvi.

  Wajumbe kutoka Zanzibar ni Dk. Hussein Mwinyi, Dk. Maua Daftari, Samia Suluh Hassan, Shamsi Vuai Nahodha, Omary Yusuf Mzee, Profesa Mnyaa Mbarawa, na Mohamed Seif Khatib.

  Katika kujiimarisha, Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete, kwa mujibu wa Katiba ya chama hicho, amewateua wajumbe saba wa NEC ili kukamilisha idadi ya wajumbe 10 anaoruhusiwa kuwateua.

  Walioteuliwa ni Anna Abdallah, Peter Kisumo, Mwigulu Mchemba, Januari Makamba, Wilson Mkama, Ali Juma Shamhuna, na Dk. Emmanuel Nchimbi.
   
 19. k

  kayumba JF-Expert Member

  #19
  Apr 14, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 654
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ni mapema kusema kwa usahihi nini kitawafika....!

  Ikumbukwe walioondoka wameacha wameotesha mbegu kibao!!!
   
 20. T

  Tz Asilia Member

  #20
  Apr 14, 2011
  Joined: Oct 30, 2009
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ndugu wakigombana............................................!
   
Loading...