Rostam Aziz na Upatu wa Siasa!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rostam Aziz na Upatu wa Siasa!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sumba-Wanga, Jul 14, 2011.

 1. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #1
  Jul 14, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Hatimaye, yale yeliyosemwa sana, bila kujua mwisho wake, sasa yamefika. Mheshimiwa Aziz ametangaza rasmi kujiuzulu nafsi zake zote za kisiasa na kubaki kama mwana CCM wa kawaida!

  Probably it was a political timing.......! Retired presdent Mwinyo did the same in the 1970's!

  Nimesikiliza kwa makini sana hotuba yake. amejenga sekondari 27, ameleta maji, umeme na lami! Marehemu Kabeho hakuweza hayo yote. Anadai kuichukua wilaya hiyo ikiwa maskini kabisa, na sasa ameipandisha hadhi, hadi nchi za jirani wanafika kwake kujifunza jinsi ya kuendesha BIMA ya afya.

  Lalkini nimejiuliza, rekod hii kubwa ya mafanikio (kama ya Mheshimiwa Msuya) awezeje kuiweka?

  Kwa pesa za kwake mwenyewe? Yeye ni mfanya biashara mkubwa sana, hilo halina mjadala!

  Lakini, kutokana na rekodi yake ya nyuma, na kashfa lukuki alizonazo, ni rahisi mtu kuona kwamba aliweza kuchota pesa katika vyanzo mbali mbali (Richmond) na kiasi kiduchu kati ya hizo, akaleta maendeleo jimboni kwake!

  Kufa kufaana, wakati Watanzania wakimtuhumu kwa kashfa mbali mbali, upotevu wa mali za taifa na rekodi ya ufisadi, wana IGUNGA wanazimia ukumbini! Sio kosa lao, pesa hizo zimewasaidia, na Mbunge mzuri ni yule anaye DELIVER!

  Kufa kufaana!
   
Loading...