Rostam Aziz bilionea no. 1 Tanzania

Rostam Aziz bilionea no. 1 Tanzania

Tunachohitaji kufahamu, ni namna gani aliupata utajiri huo akiwa Mtanzania na kiongozi. Tunachohitaji si yeye kuwa maskini kama sisi lakin ni usafi na uhalali wa ukubwa wa utajiri wake.

Tunataka kufahamu biashara ama kazi iliyomfikisha hapo na kama alilipa kodi zetu ipasavyo na kufuata taratibu za kisheria.

Wivu hapana. Lakini tunahitaji kuhoji na kujirhidhisha kama si fedha haramu zilizopatikana kwa kutuibia ama kwa uharamia wowote. Ccm hawaaminiki.


UJUMBE RASMI. YEYOTE ALIYETUIBIA, KWA WAKATI WOWOTE, ATAWAJIBIKA. NA MALI YETU YOTE ILIYO KWIBWA, AMA ILIYOPATIKANA KWA HUJUMA, TUNAITAKA KUTOKA KATIKA PEMBE YOYOTE YA DUNIA.

Waambieni Rostam, Lowasa, Ridhiwani, na wezi wengineo.
 
Juzi tu gazeti la Ventures Africa lilimtaja MO kuwa ndio bilionea namba moja Tanzania akifuatiwa na Rostam, hawa jamaa wanachanganya!
 
Tunachohitaji kufahamu, ni namna gani aliupata utajiri huo akiwa Mtanzania na kiongozi. Tunachohitaji si yeye kuwa maskini kama sisi lakin ni usafi na uhalali wa ukubwa wa utajiri wake.

Tunataka kufahamu biashara ama kazi iliyomfikisha hapo na kama alilipa kodi zetu ipasavyo na kufuata taratibu za kisheria.

Wivu hapana. Lakini tunahitaji kuhoji na kujirhidhisha kama si fedha haramu zilizopatikana kwa kutuibia ama kwa uharamia wowote. Ccm hawaaminiki.


UJUMBE RASMI. YEYOTE ALIYETUIBIA, KWA WAKATI WOWOTE, ATAWAJIBIKA. NA MALI YETU YOTE ILIYO KWIBWA, AMA ILIYOPATIKANA KWA HUJUMA, TUNAITAKA KUTOKA KATIKA PEMBE YOYOTE YA DUNIA.

Waambieni Rostam, Lowasa, Ridhiwani, na wezi wengineo.
msg sent!!!!!!!!!!!!
 
...na NUKUU Dar es Salaam, anasema katika andishi lake kuwa alishuhudia mikataba hiyo ndani ya ofisi za kampuni ya Caspian Construction Limited ambayo inamilikiwa na mfanyabiashara na mbunge wa Igunga, Rostam Aziz.

Aidha, kwa ushahidi wa Sanze, mbunge Rostam Aziz, ndiye kinara wa mpango mzima uliofanikisha wizi wa zaidi ya Sh. 40 bilioni kutoka BoT.

“Niliitwa na Bw. Malegesi ofisini kwa Bw. Rostam Aziz, 50 Milambo, Ofisi za Caspian Construction Limited. Nilipofika…niliwakuta Bw. Rostam Aziz, Peter Noni na Bw. Malegesi, wakaniambia fedha hizo zinahitajika
 
...na NUKUU ! MBUNGE wa Igunga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rostam Aziz, ni miongoni mwa wafanyabiashara kadhaa wanaotajwa kufilisi Mfuko wa Chakula (FACF) baada ya kuchotewa na serikali zaidi ya Sh. 200 bilioni.

Taarifa za ukakika zilizothibitishwa na Serikali, zinasema Rostam alichotewa mabilioni hayo ya shilingi kupitia kampuni yake ya African Trade Development.

Mfuko huo unaoendeshwa kwa pamoja kati ya Serikali ya Tanzania na Japan.

----------- imeelezwa kwamba Rostam, pamoja na wafanyabiashara wenzake kadhaa wameshindwa kurejesha fedha hizo kama walivyotakiwa na serikali.

Kampuni ya Rostam ilichotewa zaidi ya Sh. 2.012 bilioni Novemba 1999, lakini hadi mwishoni mwa mwaka jana, fedha hizo hazikufanya kazi iliyokusudiwa.

Aliyekuwa Waziri wa Kilimo na Chakula katika serikali ya rais mstaafu Benjamin Mkapa, Charles Keenja, ameithibitishia gazeti hili kutolewa fedha hizo.

Alisema, "ni kweli wapo wafanyabiashara ambao walipewa fedha kutoka katika mifuko hiyo. Na hadi naondoka ofisini (mwaka 2005), nyingi ya fedha hizo zilikuwa hazirudishwa."

Hata hivyo, Keenja aliongeza kwamba "fedha za Mfuko wa Chakula huwa hazikopeshwi, bali mhitaji hutakiwa aandae mradi wa maendeleo wenye manufaa kwa jamii. Akishindwa kuendesha mradi, anatakiwa kurudisha fedha mara moja."

Mbali na Rostam, wakurugenzi wengine wa African Trade Development, ni Gulam A. Chakaar na Bahram A. Chakaar.

Makampuni mengine yaliyochotewa fedha, ni Tanganyika Farmers Association Limited (TFA) ambayo wakurugenzi wake ni Ndesario K. Shangali, Elia R.K. Mshiu, C.J Bannister, Elisamia I. Swai, Eric Jorgensen na Charles D.J. Mungai.

Mengine ni Ramwigema General Suppl ambayo inamilikiwa na G. Mwinuka na wenzake na Sales Point Company Limited, inayomilikiwa na Matunda Abdulrahman na Abdallah S. Hassan.

Makampuni mengine yaliyochotewa fedha ni VIP Engineering inayomilikiwa na James B. Rugemalira, Mathias Mutabirwa, Suleiman A. Abubakar, Gwalugano Mwamukonda na Mohamed B. Somji.

Mengine ni TANTI Co. Ltd., inayomilikiwa na Nuru A. Kihiyo na Twaha Y. Kaujanja; BCS Limited ikimilikiwa na Jackson V. Kaale, Kandaga J. Muhangwa, Edmund Mkwawa, Flavian I. Gowele, Judith M. Juma, Abdul Nuru Suleiman, Fatuma B. Mikidadi na Salome J. Mbatia.

Ipo pia Agro – Impex inayomilikiwa na Parvez Vira na Azmina Vira.

Wakurugenzi wengine ni makampuni yao kwenye mabano, ni Juma Ngalema na wenzake (Kiswele Salt Works Ltd); Bupen S. Tank na wenzake (Shivlal Tank & Co) na W.C. Marwa na wenzake (Tanzania Fertilizer Company).

Mbali na Mfuko wa Chakula, pia fedha hizo zilitolewa katika Mfuko wa Pembejeo.

Mifuko hiyo ilianzishwa kwa lengo la kuiwezesha Serikali kupata uhakika wa chakula kwa wananchi wake pamoja na kusukuma mbele miradi ya maendeleo katika sekta ya afya, elimu na maji.

Mfuko wa Chakula ulikuwa ukitoa ruzuku kwa wafanyabiashara wakati Mfuko wa Pembejeo ulitoa mikopo ya pembejeo za kilimo ambayo ililazimu mkopaji kurejesha.

Taarifa kutoka Ubalozi wa Japan nchini, zimesema kwamba hatua ya serikali kutoa fedha hizo bila ya kufanyiwa kazi iliyokusudiwa, imechangia kuzorotesha madhumuni ya mifuko hiyo.

----------- lilipowasiliana na Afisa Mtendaji Mkuu wa mifuko hiyo, Dk. Lorri Willibald, alithibitisha kuwapo kwa wafanyabiashara waliochotewa fedha hizo lakini wakashindwa kuzitumia kama ilivyotarajiwa.

Hata hivyo, Dk. Lorri alisema kwa sasa hayuko katika nafasi nzuri ya kuzungumzia suala hilo kwa vile yuko nje ya ofisi.

Juhudi za kumpata Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Profesa Peter Msolla, hazikuzaa matunda kwani simu yake haikupatikana kwa muda mrefu.

Aliyekuwa Naibu Waziri wa Kilimo na Chakula ambaye sasa ni Naibu wa Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Christopher Chiza, alisema ingawa walifanya jitihada kubwa kuhakikisha fedha hizo zinarudishwa, hadi anaondoka, kiasi kikubwa kilikuwa bado hakijapatikana.

Tukio hilo linaendelea kuthibitisha namna fedha za umma, zikiwemo zile zinazotolewa na washirika wa maendeleo, zinavyotafunwa na wajanja wachache kwa maslahi yao binafsi.

Aidha, taarifa hizi zinakuja wakati Watanzania wakisubiri hatma ya wakwapuaji wengine waliotafuna mabilioni ya shilingi katika Akaunti ya Malipo ya Nje (EPA).

Wajanja wametafuna zaidi ya Sh. 133 bilioni za fedha hizo zilizochotewa makampuni kadhaa kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na Wizara ya Fedha katika kipindi cha mwaka 2005/06.

Wizi wa fedha hizo uligunduliwa na maodita, kampuni ya Ernst & Young walioelekezwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali nchini (CAG) baada ya kubainika upotevu wa fedha katika akaunti hiyo.

Vilevile, sakata hili linaibuka sasa wakati ambapo haijajulikana hatma ya watendaji serikalini waliongiza nchi katika mkataba wa kinyonyaji wa Richmond.

Katika mkataba huo, shirika la umeme Tanesco linailipa kampuni hiyo kupitia dada yake Dowans, Sh. 152 milioni kwa siku.
 
nawashanga aga matajiri hawa mihela kibao ata kusaidia mtu mwenye shida ata milioni wana shindwa kila siku tunaona kwenye ma tv yao watu wanalia wagonjwa wana waomba msada walalahoi wenzao wananchi wanatuma buku buku watu ndio wanaenda kutibiwa. lakini hiyo mitajiri ndo kwanza kuongeza wigo wakuiba hela kiulaini mmmh hapa duniani kulivyo jamani. kweli pesa mwanaharamu. kuna hela ina tamkwa apa sijui milioni mia ngapi au bilioni ngapi ki kawaida kawaida wabongo wengi hawaja wahi ata kuziona kwanacho zilivyo.. li mtu lina hujuma hela zote izo lina ka kimya kweli tajiri ndo muwaji duniani na hanaga mana yakuwa na mihela yake yote haina ata misada wana roho mbaya sana. bora ata mengi kidogo ana kaubinadamu mitajiri mingine yote roho mbayaa.
 
Juzi tu gazeti la Ventures Africa lilimtaja MO kuwa ndio bilionea namba moja Tanzania akifuatiwa na Rostam, hawa jamaa wanachanganya!
Walisema bilionea kijana. Soma vzr katikati ya mistari vinginevyo utajichanganya mwenyewe
 
Forbes mbona hawaeleweki? Juzi si walisema Mo ndio namba moja kwa 2.2m $?
 
Back
Top Bottom