- Well, saa imefika sasa wameanza kama ilivyosemwa, sasa wakishatoka wote liangaliwe suala la Sheria!
Willie @ NYC, USA.
Rostam Aziz ajiuzulu nafasi za uongozi katika chama (Sehemu ya gamba imevuka)
Habari hii imepamba kurasa za mbele za magazeti ya leo pamoja na mazungumzo ya watanzania katika mikusanyiko mbalimbali. Ni ukweli usiopingika kwamba Rostam amechukua uamuzi huu katika mazingira yanayofahamika kwa watanzania wengi bila kujali ufafanuzi alioutoa Rostam katika hotuba yake kwa wapiga kura wake katika kutangaza hatua yake hiyo.
Kilichonifanya kuuliza swali hili ni hali iliyojitokeza katika baadhi ya makundi ya watu kutokana na jambo hili. Kuna baadhi ya watu wanashangilia na kufurahia hatua hii ya Rostam kwa kuonyesha kuwa . Pia kuna baadhi ya watu wanasikitika na wengine walifikia hatua ya kuzimia baada ya Rostam kutangaza hatua yake hiyo.
Kwa upande wa vyombo vya habari vipo ambavyo vimeelezea tukio hilo kwa ushabiki wa kufurahia na kuonyesha kuwa huu ni ushindi kwa chama fulani cha siasa katika hatua za kujisafisha.
Kwa jinsi ninavyoelewa hatua hii ya Rostam imetokana na juhudi ya baadhi ya wanasiasa na wanaharakati ambao kwa kipindi kirefu wamekuwa mstari wa mbele kufichua kashfa mbalimbali za rushwa na ufisadi ulioota mizizi tangu awamu ya pili ya uongozi wa nchi hii.
Swali langu hapa ni Je kujiuzulu kwa Rostam ni ushindi? na kama ni ushindi, ushindi huu ni wa nani?
SaaafiiiKama rostam anataka kulinda heshima yake ya kijamii na kibiashara sasa ni wakati wake wa kumwaga mboga kwakuwa wenzie walishamwaga ugali kwa kuelezea ushiriki wake katika kuchota hela za kagoda na jinsi zilivyotumika wakati wa uchaguzi wa 2005 kuwasaidia magamba kupata ushindi wa kimbunga vinginevyo heshima yake itashuka na atadharaulika machoni pa watanzania na nje hailipi kujiuzulu vyeo pia arejeshe sehemu ya fedha za epa kwakuwa kuna kiasi alichukua mwenyewe.verry sorry kwa heading
Hao akina baba na kina mama walio kuwa wanalia na kumwaga chozi huyu Rostam alikuwa anawalelea familia zao?
ni kweli mkuu, wa-TZ tuc jejisahau, mpira(wa miguu) ni dakika tisini, hapa tumefika dk kama ya kumi tu. kazi bado mbichi hii na kipute ndo kwanza kimetulizwa kunako dimba. Aluta continue mpaka mafisadi yote yafikishwe mahakamani na warudishe pesa zetu. Yaone kwanza haya mafisadi wahedi...!!! yanakula mavyakula yanayotuibia sisi mafukara, yanavimbiwa na yanajamba mpaka yanatapikia juu ya viatu vyetu sisi mafukara...pimbafu kweli haya!!!Mapambano bado yanaendelea mpaka mwisho wa mchezo maana bado kuna mafisadi wengi tu wamebaki huko CCM. Wakishaondoka kwenye chama hatua za kisheria inabidi zifuate. Lazima warudishe hela zote walizopata kwa njia za ujanja ujanja.
kaka yangu, unasema bravo nape kwaa kitu gani? tarumbeta na mpuliza tarumbeta nani apewe bravo? in my opinion, simply say bravo JK kwani nape kwa uwezo wake hawezi lolote!
Sasa wewe ulitaka aende msikitini kuombeleza? Topic uharoooooooJe wajua siku bwana Rostam Aziz anajivua gamba muheshimiwa JK alikua wapi? basi kwa sisi tulioko kanda ya kaskazini mkoa wa Arusha mimi nilikua niko kwenye mbuga za wanyama Serengeti niko na watalii wangu tunaangalia chui pamoja na simba ndipo kwenye kuangalia kundi la simba na chui tulikua pamoja na muheshimiwa JK tukijivinjari huku bwana Rostam akiwa Igunga na wananchi wake waliompigia kura siku anajivua gamba, nahisi kujivua gamba kwa bwana Rostam Aziz sio kwamba JK alikua hajui ni nini kinaendele hapana hawa watu walishapanga mpango mzima wa kuwahadaa wananchi kwa bwana Rostam kujivua ubunge pamoja na nyadhifa zote CCM lakini eti atabaki kama mwanachama tu! Mimi nasema haitoshi kama kweli hapendi siasa uchwara basi arudishe na kadi ya uanachama hapo tutamuelewa. Nawasilisha.