Mzito Kabwela
Platinum Member
- Nov 28, 2009
- 18,904
- 7,746
Rosemary Mayemba ni mjumbe wa kamati kuu ya Chadema. Alikuwa Mwenyekiti wa Mkoa wa Njombe kabla uchaguzi haujafutwa ambapo yeye Rose anadai uchaguzi ulikuwa na figisu. Sio lengo langu kujadili hizo figisu isipokuwa nataka watu wajue hali halisi ilivyo hapa Njombe.
Rosemary Mayemba kama mjumbe wa kamati kuu aliyeshiriki vikao vya retreat kule Bagamoyo ambako walikalishwa na kuonywa juu ya mgawanyiko mkubwa uliopo Chadema na kuombwa wafikapo kwenye maeneo yao wakaunganishe chama, Rose amekuwa kama aliyeota mapembe. Anawakejeli wote ambao hawakumuunga mkono Lissu, anawatukana na kuwabagua.
Rose ameshakuwa mjumbe wa kamati kuu. Kwa kutumwa au kujituma mwenyewe, bado anataka kugombea tena uenyekiti wa mkoa. Katika hali ya sasa ambapo Chama hakiko katika utengamano, Rose alitakiwa kuwaachia watu wengine wagombee nafasi hiyo huku msisitizo wake uwe ni mapendano ndani ya chama.
Rose anaongoza genge la watu wachache kushughulikia wenzake. Tangu ameteuliwa kuwa mjumbe wa kamati kuu amegeuka kuwa "first lady" wa Chadema hapa Njombe.
Hashauriki, mbishi, mjuaji na kuona kama chama mkoa wa Njombe ni mali yake binafsi.
Natoa angalizo na wito kwa viongozi wa chadema. Hiki chama mnakiua. Na hamna uwezo wowote wa kukihuisha kuwa cha moto kama kilivyokuwa.