GE2025 Rosemary Kirigini ahamia ACT-Wazalendo Kutoka CHADEMA na CCM

GE2025 Rosemary Kirigini ahamia ACT-Wazalendo Kutoka CHADEMA na CCM

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,437
Reaction score
5,235
Mwanasiasa mwandamizi aliyewahi kuwa Mbunge wa Viti Maalumu CCM mkoa wa Simiyu, Mkuu wa Wilaya ya Meatu na pia Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWACHA) Kanda ya Serengeti, Rosemary Kirigini amejiunga na chama cha ACT Wazalendo.

Kirigini amejiunga na Chama hicho na kutangazwa mbele ya wananchi wa Mwandoya Jimbo la Kisesa, Mkoani Simiyu siku ya Jumamosi Agosti 16, 2025.

Akizungumza baada ya kutangazwa kujiunga, Kirigini amesema wananchi watarajie mambo makubwa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 kwani chama hicho kimejipambanua vya kutosha.

 
Back
Top Bottom