Rose Kamili amemsafisha Dr. Wilbrod Slaa. Hongera Rose Kamili na wenzako mliofanikisha hilo

Mwanahisa

JF-Expert Member
Jun 29, 2012
1,385
1,195
Unadai Rose Kamili kamsafisha Dr Slaa, lakini wewe kupitia tundiko lako hili umempaka matope Dr Slaa.

Wakati Dr Slaa yupo katika jopo la mapokezi ya Baba Mtakatifu Pope John Paul tayari ana mahusiano ya ndoa na watoto!.

Kwa taarifa yako hili likija julikana huko Vatican ni kashfa kubwa kwa Kanisa Katoliki Tanzania.

Mkuu usipake mavi kwa brush unazidi kusambaza tulia, huwezi kumsafisha Slaa kwenye hili hasafishiki!

Kweli tunatofautiana katika usawa wa fikra, inanipa mashaka kwamba kuna wanajamii hawajui wanachokisoma wala tafakari zao hazina mwendo.
 
maswitule

JF-Expert Member
Nov 5, 2010
1,392
1,500
Kusafishika kupi tena, Hata asiposafishika siku si nyingi Rose Kamili atasimama na kumsafisha Slaa, hapo wanakomaza dhahabu kwa kuipitisha kwenye moto.
 
Topical

JF-Expert Member
Dec 3, 2010
5,174
0
Dr. Slaa, badili dini uwe MWISLAMU........ Ongea na masheikh wew na huyo MUSHUMBUSI muwe waislamu.

Sisi tutakikaribisha vizuri sanaaaaaa......chonde, hukunhakuna shida hizo,ndoa tunakufungisha kiurahisi sanaaa!!!!""""""

Uliza mwenzako.JK ana.wake wangapi, anafaidi ile mbayaaaaaaa!!!!!!"""""

Kwakuwa Rose anampenda Slaa bado- anakuwa mke wa Kwanza

Kwakuwa Josephine anampenda Slaa bado -anakuwa mke wa Pili

Problem solved! Slaa welcome to Islam "solution for all mankind problems"
 
bdo

JF-Expert Member
Nov 20, 2006
5,812
2,000
haaa haa haaa,kweli kipenda roho jamani,yaani umetumia muda wote kuhangaika na maelezo yote haya kama vile wewe ni mdogo wake josephine mshumbusi ili kubarik ndoa sio?haa haaa ataolewa tu dada yako usiwe na wasiwasi

I congratulate, kwamba na wewe umetumia muda mrefu/mwingi sana kuisoma hii thread na kutafakari kilichowasilishwa, hebu ngoja tusibiri tuone, umewahi sana kusema, let's wait mwenzako kaja na theory hapo, i thought na wewe ungemwaga hata moja!
 
anney

Senior Member
Jul 9, 2010
155
0
Kabla ya July 2007 ni wachache sana walikuwa wakiithamini Habari ya sababu za Padri Wilbrod Slaa kuacha utumishi wake wa upadri. Binafsi hadi kufikia mwaka 2007 nilikuwa na theory kama tatu zote toka vyanzo Tofauti vikieleza ni sababu gani ilimfanya Dr. Slaa akaachana na shughuli za kanisa.

Theory ya kwanza niliyoisikia ilikuwa ni kwamba amempa mwanamke mimba na hivyo yeye mwenyewe akaamua kuachana na mambo ya misa akaomba kurudi uraiani ili akajenge familia yake. Theory hii mimi nilisikia katikati ya mwaka 2006

Theory ya pili niliambiwa kuwa alipokuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu (TEC) alifanya ufisadi wa hali ya juu. Ufisadi wenyewe ni ule wa kula hela za ujio wa Pope John Paul II hapa nchini September 1990 na hivyo Kanisa likamuondoa. Theory hii niliisikia mwishoni mwa mwaka 2007 baada ya yeye kutangaza list ya mafisadi pale Mwembeyanga.

Theory ya tatu niliyoisikia huwa siisikii ikisemwa hadharani ni kwamba Dr. Wilbrod Slaa alikorofishana na askofu mmoja ambaye ninalihifadhi jina lake. Ugomvi haukuanza na huyo askofu. Bali ni kwamba huyo askofu alikuwa na ndugu yake pale TEC na huyo ndugu alikuwa ni mmoja wa wakuu wa kitengo cha misaada kiitwacho CARITAS.
Tatizo likawa kwamba yule jamaa wa CARITAS akawa anatumia jina la Kanisa na misaada ile kupitisha maslahi yake kama vile makontena. Padri Wilbrod Slaa kama Katibu wa TEC akagundua hilo na akachukua hatua za nidhamu kwa huyo jamaa.

Kumbe ambalo Padri Slaa hakujua ni kwamba yule jamaa hakuwa peke yake, alikuwa anashirikiana na askofu huyo ambaye jimbo lake liko kanda ya ziwa Victoria. Askofu yule akapata habari ya kusimamishwa yule staff wa CARITAS. Akamjia juu Padri Slaa.

Padri Slaa akakataa shinikizo la kumrudisha yule fisadi wa CARITAS na hivyo majibizano yakawa makali kati ya Slaa na yule askofu. Ikaonekana wazi kwamba kumbe yule askofu yuko team moja na yule jamaa wa CARITAS.

Kwa sababu mali za CARITAS ni zinasimamiwa na TEC basi hapa katibu wa TEC yaani Padri Slaa akaona huyu naye ni mtuhumiwa mwingine anayepaswa kuwajibika tena kwa ubishi wake. Hivyo, Padri Slaa akaamua Polisi wamweke ndani askofu yule kwa kushiriki ule ufisadi na yule jamaa wa CARITAS.

Kitendo cha askofu kuwekwa ndani kikawashtua na wakawasiliana haraka japo enzi hizo simu za mkononi hazikuwapo lakini Kanisa lina mawasiliano mengi tu wakati huo. Ndipo maaskofu wakati huo wakaingilia na askofu mwenzao akatoka rumande. Hivyo, askofu wa Kanisa Katoliki Tanzania akawa ameonja adha ya kuwekwa ndani kwa muda wa masaa! Rais wa TEC wakati huo akiwa Mrehemu Askofu Samba wa Musoma akaingilia kati na ikaamuriwa kwamba Padri Wilbrod Slaa amefanya utovu wa nidhamu kumweka askofu ndani. Na hili likamuudhi Dr. Slaa akaamua kuachana na utumishi ambako wengi kimakosa huita kuachana na upadri.

Hizi ndizo theory tatu nilizowahi kusikia kuhusiana na sababu za Dr. Slaa kuacha upadri. Narudia kueleza, theory zote hizi ninazijua tangu mwaka 2007.

Sasa tuje kuzichambua theory hizi. Theory ya kwanza imenichukua miaka mingi kuiamini kwani sikuwa namjua Rose Kamili kwani niliambiwa kwamba mwanamke mwenyewe ni mzungu wala si Rose Kamili. Sasa niliposikia kuwa Rose Kamili ni mke wa Dr. Slaa basi nikaanza kutoipa nafasi hiyo theory.

Theory ya pili ya kufisadi hela za Pope sikuwa na vigezo vya kuipinga. Lakini sikushangaa ilipoanza kutumiwa na wanasiasa mfano ni Stephen Wasira alivyoitumia kwenye kampeni ya uchaguzi mdogo huko Arumeru. Lakini hatimaye aliyekuwa Rais wa TEC hadi mwezi uliopita yaani Askofu Jude Thaddaeus wa Mwanza alikana hadharani kwamba Dr. Slaa hajawahi kutuhumiwa wizi wa hela za ujio wa Papa.

Theory ya tatu kwamba Dr. Slaa alimweka ndani askofu nimekuwa nikibishana na wenzangu wengi. Ukweli wanaoijua huwa tunatofautiana na handling ya issue hiyo lakini siyo event. Mtu mwingine kabisa ambaye nilidhani haijuia aliwahi kunieleza kwamba baada ya Dr. Slaa kumweka ndani yule askofu akalalamika kwa Askofu Anthony Mayala wa Mwanza. Mimi nimekuwa nikipinga na kuuliza iweje Dr. Slaa ashitakiwe kwa Askofu wa Mwanz wakati yeye hakuwa Padri wa Jimbo la Mwanza na alikuwa wa Jimbo la Mbulu?

Ninapowauliza hivyo wanakosa majibu. Lakini kukosa majibu maana yake ni kwamba tunakubaliana kwamba Dr. Slaa alimweka ndani yule askofu lakini tunatofautiana kujua hatua zilizofuata.

Utaona kwamba kama kulikuwa na juhudi ya wanasiasa kupeleleza habari za Dr. Slaa kule TEC basi hakika hii theory ya tatu hata kama wakiijua hawataweza kamwe kuitangaza. Kwa nini hawataweza? Kwa sababu Padri kumweka ndani askofu ni kweli unaweza kujenga hoja kwamba ni utovu wa nidhamu. Lakini kizazi cha sasa hakiishii hapo. Watu watauliza sababu ya kujua kwa nini askofu awekwe ndani.

Umati ukipogundua kwamba kumbe Dr. Slaa alimweka askofu kwa sababu ya ufisadi wa CARITAS basi maana yake ni kumpandisha chati zaidi kwamba kumbe Dr. Wilbrod Slaa alianza vita ya ufisadi tangu akiwa kanisani na mafisadi wa huko walimkoma.

Nimesema zote hizi tatu ni theory. Narudia tena kusema hii ya tatu sijawahi kuisikia kwenye vyombo vya habari ila ninaisikia tu kwa wachache sana wanaopenda kujishughulisha na mambo ya Kanisa Katoliki. Tunaijadili kwenye meseji zetu, kwenye vigenge vyetu na inaishia huko.

Lakini zile thoery mbili zimashamwagwa magazetini na wote mnajua.

Nilioongea hapo juu ni history sasa tuje kwenye hoja ya leo. Juzi, Rose Kamili anakuja na hoja mahakamani akisema kuwa alifunga ndoa na Dr. Wilbor Slaa June 18, 1987. Hapa maana yake ni nini? Maana yake ni kwamba haijulikani kama iko siku Pope John Paul II atakuja kuitembelea Tanzania.

Sanasana kila nchi na kila jimbo mwaka huo walikuwa na mikikimikiki ya kuadhimisha mwaka wa Mama wa Yesu uliotangazwa na Papa huyu January ya mwaka huo.

Mnaopenda nyimbo za Bikira Maria mnakumbusha kipindi hiki ndipo zilitoka kwa wingi na zinavuma hadi leo. Ndiyo ilikuwa kazi kuu ya Kanisa wakati huo.

Sasa, kama Dr. Slaa alifunga ndoa ya kiserikali tarehe hiyo kwanza hapa unapaswa kujiuliza maswali mengi. Je, idara iliyofungisha ndoa hiyo haikujulishwa kwamba huyo mfunga ndoa ni padri wa Kanisa Katoliki? Binafsi ninajua kuwepo kwa mahusiano ya siri kwa mapadri na maaskofu dunian na wanawake lakini ndoa ya siri tena imesajiliwa hii ni habari niliyojifunza.

Tuendelee kuchambua. Pope John Paul II alipokelewa na Rais Ali Hassan Mwinyi pale airport September 01, 1990. Airport iko D'Salaam basi kikanisa askofu aliyemkaribisha alikuwa ni wa Jimbo la D'Salaam yaani Laurian Cardinal Rugambwa akiwa na Msaidizi wake (Coadjutor) aitwaye askofu Polycarp Pengo.
Katibu wa Baraza la Maaskofu aliyekuwaepo ni Padri Wilbrod Slaa.

Hii maana yake ni nini? Maana yake ni kwamba Pope alikuja nchini ikiwa ni zaidi ya miaka mitatu huku Padri Wilbrod Slaa akiwa kweny endoa na Rose Kamili. Kumbe, wakati sisi tunajua kwamba Katibu wa TEC yuko kwenye jopo la kumkaribisha Pope mwenzetu Rose Kamili anaona kwamba mumewe wa ndoa anamkaribisha Pope tena ndoa yenye watoto wawili tayari.

Rose Kamili amewasilisha mahakamani maelezo kwamba kitendo cha Dr. Slaa kuzaa naye na kufunga ndoa June 18, 1987, kilimfanya aanze taratibu za kuondoka kwenye nafasi za upadri. Hapa Rose Kamili anatufunulia ukweli ambao hatukuujua. Ukweli uliotufanya tuogelee katika kila mtu na theory yake. Wasira alikuwa na theory moja wakati mimi nilikuwa na theory tatu nimezitaja hapo juu.

Kumbe wakati tunaona Padri Slaa anachacharika nchi nzima kuandaa ziara ya Pope basi leo ndiyo tumefunuliwa na kujulishwa kwamba hapohapo alikuwa na process nyingine ya kuanza kuachana na upadri.

Leo nimeona picha za wabunge wa CCM yaani Esther Bulaya, Sofia Simba wakimkubatia Rose Kamili bungeni leo. Siwezi kusema ni kumpongeza au kumfariji au ilikuwa ni issue nyingine. Lakini kama kuna watu nyuma ya Rose Kamili binafsi ninaona kwamba ni walewale ambao hawajui kwamba unapopambana na jambo linalohusisha Kanisa Katoliki basi inabidi ama tukuhurumie au tuone ulivyo na akili nyingi sana hapa duniani.

Kwani wengi hapa duniani ambao hujikuta wamegusa mambo yanayoguswa na Kanisa Katoliki wameishia kuumbuka kwa sababu ya ujinga wao kutojua mengi yanayohusiana nalo. Na wasipojirekebisha wataendelea kuumbuka tu.

Hili la Rose Kamili tayari ninauona ni ushindi kwa Dr. Slaa na kilio kwa wote waliomtafuta kwa scandal za tangu akiwa Kanisani.

Kwa sababu hadi dakika hii kuna wanaocheka wakidhani Dr. Slaa kaumbuka, lakini kwa kweli Rose Kamili katurahisishia kazi kubwa kutujulisha kwamba ni nini kilimfanya Padri Wilbrod Slaa aache upadri na aingine mtaani. Bahati nzuri Rose Kamili haongei bila ushahidi.

Sisi wengine wote na yote tuliyosema hayana ushahidi. Binafsi hadi sasa, niliamini zaidi theory ya kumweka ndani yule askofu kuliko theory zote. Lakini ukiniuliza ushahidi nitakwama, hadi siku yule askofu akisema au Dr. Slaa akisema au hata askofu yeyote akisema, kitu ninachoamini haitatokea.

Niliwahi kumsikia Dr. Slaa kwamba afadhali wamsingizie kwamba alikosana na baadhi ya maaskofu hapo angetetemeshwa kidogo na tuhuma hizo. Pia mlioangalia mdahalo kwenye TV siku mbili kabla ya uchaguzi wa 2010, Dr. Slaa alieleza wazi kwamba alipokuwa TEC, contena lilikuwa likija kwa kutumia jina la kanisa alikwua anaingilia na kwa kusaidian na Usalama wa Taifa walikuwa wanalipiga mnada.

Kwa mimi muumini wa theory ile niliona kana kwamba anautaja mgogoro ule lakini kwa jinsi ambavyo si rahisi kwa mtu baki kuulewa.

Hivyo, nahitimisha kwa kusema kwamba Rose Kamili amemsafisha Dr. Wilbrod Slaa hata kama kuna watu akili yao leo inashangilia kitendo cha Rose wakati akili zao hizohizo zilishangilia tuhuma za Stephen Wasira kule Arumeru kwamba Dr. Slaa alitimuliwa upadri kwa sababu ya kufisadi hela kwa ziara ya Pope John Paul II.

Hongera sana Rose Kamili. Kama kuna wenzio nyuma ya hili naomba uwafikishie hongera zangu kwao hata kama kila mtu katika Jamii Forum atanipinga kwa hili.

By the way what is theory? this are just streat narration!
 
Kimbunga

Platinum Member
Oct 4, 2007
14,467
2,000
Hivi yule askofu Migingo aliyekuwa Vatican hakuoa wakati ni askofu ma baadaye akaaachana na mke wake na kurudi kundini kwa ridhaa ya Papa? Aliwezaje kuoa wakati vyombo vyote vinajua kwamba ni Askofu tena mwenye joho, kofia na pete ya Uaskofu? Tusiwe wasemaji wa Rose Kamili ama Dr. Slaa. Wako kwa pilato basi pilato atawahukumu kwa haki. Unaweza kuanguka ukiwa mtumishi kisha ukaomba msamaha na kurudi kundini.
 
Rejao

JF-Expert Member
May 4, 2010
9,237

Hongera sana kwa kujitahidi kuandika maneno meengi. Hatumjaji Slaa kutokana na yanayosemwa au according to those theories ulizozisema. Analysis yetu inabase kwenye hali halisi, kwa tunachokiona sasa kutoka kwa Slaa.
Kwa kifupi Slaa ni mchafu!
 
segwanga

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
2,788
2,000
Hongera sana kwa kujitahidi kuandika maneno meengi. Hatumjaji Slaa kutokana na yanayosemwa au according to those theories ulizozisema. Analysis yetu inabase kwenye hali halisi, kwa tunachokiona sasa kutoka kwa Slaa.
Kwa kifupi Slaa ni mchafu!

Ok slaa mchafu jk dhaifu
 
chitambikwa

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
3,940
2,000
Hiyo ya kumtia ndani askofu kwa tuhuma za ufisadi kupitia mgongo wa kanisa ni kweli ila halikumtoa kwenye upadri bali lilimtoa kwenye cheo cha ukatibu wa tec.
Kilichomtoa upadri ni baada ya kuandika barua ya petition kwa pope kwasababu tayari alikuwa ana familia na kuijulisha hivyo rome.
Dr.Amesoma sheria za kanisa kwa ufasaha sana na anazijua vizuri
 
bdo

JF-Expert Member
Nov 20, 2006
5,812
2,000
Ushabiki wa imani ya kidini ukiambatna na chuki dhidi ya ukatoliki ni mbaya sana. Lakini mwisho wa siku, kama mtoa hoja alivyosema, hushia kwa mpinga u-RC kuumbuka. Labda ni vyema kujiuliza why failure? Ni wazi kanisa Katoliki lina watu wanaotumia akili zaidi ktk kukabiliana na maisha duniani! Na hili ndilo linalowatofautisha na imani nyingine zote duniani!

Mkuu napingana na wewe kidogo - usihitimishe hoja kwa kusema katoliki are the best kuliko imani zingine....nadhani Ukatoliki na siasa katika mazingira ya Tanzania, imetokea baada ya wapumbavu fulani kuhusisha mchakato wa uchaguzi wa 2010 kuwa - Dr.Slaa alikuwa backed/katumwa na Wakatoliki - especially ndg wa imani ingine na hasa baada ya kutolewa kwa the so called "waraka wa maaskofu/kanisa katoliki". Na baada ya CCM -JK kum-underestimate Dr. Slaa na kuona muziki wake ni Mkubwa akaanza kusema nchi ina udini! Na sidhani before kulikuwa na issue za Dini na watu wengi wajinga/wavivu wa kufikiri wakisikia Slaa wahusisha direct na Ukatoliki - yaani Slaa=Ukatoliki, ninachotaka kusema hapa ni kuwa kila imani ndani yake kuna watu vichwa (wanaotumia akili sana na wabovu) na usije na wewe ukawa umeingia mtego wa kuamini kuwa kwa kuwa Dr.Slaa kwa kuwa was Askofu (ni Mkatoliki) ukaamini katika mfano uliyotolewa wa Maaskofu waliyostaafu na kuwa presidents (kuwa ni vichwa) wakati is a matter of chance,maana nina aamini kila mtu ana akili zake na zinachemka kulingana na Mazingira yake, ila labda kama utakuja na ushawishi mwingine.
 
bdo

JF-Expert Member
Nov 20, 2006
5,812
2,000
Hii stori wala hamsafishi badala yake inaleta maswali mengi, ikimsimulia hii stori mtu fresh na huru ambaye hakuwahi kusikia mambo haya, kichwani mwake atasema pointi moja na pointi mbili ni sahihi.

1.Atajiuliza hivi alikuwa Padre akawa na watoto wakati huo huo, hivyo mama watoto akawa anashinikiza lete fwedha bila hivyo nakusemea vatican, jamaa hana pakutoa pesa anaenda kuchota pesa za zaka. Kila mara mama anashinikiza leta pesa watoto watakufa njaa ukikataa na toboa siri jamaa anachota pesa. Hivyo

2. Baada ya kuchota pesa za kutosha na kabla ya kugundulika ikabidi aachie ngazi. ama ilishagudulika akaachia ngazi kwa shinikizo.
3. mama Lete pesa, na jamaa pesa kigangoni zimeisha, zimeisha kama unataka nisikusemee sahizi aacha u-padre uje ulee watoto wako, maana kwa mwendo huo kulikuwa hakuna jinsi lazima upadree uachie.
4. Aliachia ngazi ili aje kulea wanawake, lakini hii ni hataenda pekee bila kuhusisha na kuchota pesa za kanisa kwa ajili ya kuikimu familia yake wakati kiwa ktk utawa.

Tafadhali jibu theory za jamaa, tofauti na hapo MkamaP naona kama unaleta majungu ya ziwani
 
bdo

JF-Expert Member
Nov 20, 2006
5,812
2,000
Hongera sana kwa kujitahidi kuandika maneno meengi. Hatumjaji Slaa kutokana na yanayosemwa au according to those theories ulizozisema. Analysis yetu inabase kwenye hali halisi, kwa tunachokiona sasa kutoka kwa Slaa.
Kwa kifupi Slaa ni mchafu!

Uchafu gani
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom