Imani nyingine ni matatizo matupu! Kwa maoni yangu kijana huyu alikuwa na matatizo ya kisaikolojia. Wahusika mtanisamehe kama nakosea kwa kusema hivi, lakini kuna kila dalili kuwa Godwin alikuwa na tatizo zaidi ya imani kali. Hakuna sehemu Mungu ameagiza tukafie porini kwa kusali, hata Yesu mwenyewe alipanda mlimani na kushuka kuendelea na shughuli nyingine.