ROMA MKATOLIKI CV!!!! Sio tu Msanii??

Gwanda huyu jamaa ndio kama sare yake ya kazi.
Magwanda hata kabla hayajakuwa official Chadema wear yalikuwa ni mavazi ya wanaharakati wengi na wakombozi walopita. Baadhi Ya wankombozi waliotumia Au Kuvaa magwanda ni kama
1. Ernesto Che Guevara
2. Fidel Castro
3. J.K Nyerere (picha nyingi zipo)
4. Wapiganiaji uhuru wengi wa South Africa

Na wengine wengine wengi, so hii ni kama uniform ya wanaharakati nahisi ndio sababu ya huyu Kijana pia kuzitumia.

Pia Khaki Inaonekana kuwa ni kama vazi la Concious Artists wengi kama kina "Ice Cube", "Common", na wengine wengi.
Roma Mkatoliki Ni One The Most Realest MCs Kuonekana Tanzania Hii

UR right man!
Roma is an activist using his talent in music to deliver the message.
 
Namkubali sana roma hasa kwenye ngoma zake Tanzania,Mechi ya Ugenini na Tanzania Consiou rapper Consious MC
 
Anyway kuna kingine kinachonipa walakini hapa,..kuna tokea malalamiko siku za usoni kuhusu hawa clouds kuwatenda ndivyo sivyo wasanii wengi kwa kuwatumia katika matamasha yanayowaingizia millions of shs..kisha kuwatosa pasipo malipo sahihi yanayolingana na kazi yao...

1.Mara kadhaa sijaona clouds wakimsogelea,ni je wanamuogopa kutokana na msimamo wake?
2.Mara nyingi tunawasikia watangazaji wa clouds waliowasimulizi wa muziki wa hiphop wakiziongelea nyimbo zinazohit za hiphop,.mbona hawaisimulii hiphop iliyotukuka kutoka kwa huyu kijana?

Who are the "clouds? bro??
Tusiruhusu kutawaliwa kirahisi hivi jamani.... clouds ni redio kama redio zingine!
Tusipumbazike hivyo..... tumewapa kichwa vya kutosha hawa jamaa na hamna walichosimamia kwenye music yetu zaidi ya maslahi yao!
 
Roma amekubalika sana kutokana na kujua ni nini watanzania wanataka wasikie ..Akiendelea hivyo atakuwa ni moja ya mashujaa wa uziki wa Tanzania na atapata baraka za watanzania/washabiki kwa heshima kama Sugu.

Moja ya mambo ambayo wanamziki wengi wameshindwa kutabua ni uhalisia wa maisha yao wanakotoka na wanapokwenda .Wapo walioweza ku adress public issues kupitia muziki na wakapata heshima ila wamejisahau na kulewa sifa.Kwa wale wanaojua na kufuatilia muziki wa Tz kuna mtu ambaye kwa sasa graph yake ime stack (sijui ndio imefikia maximum) kwamba haipandi hala hashuki.Ila kama mambo yatakuwa hivyo yalivyo inaweza anza kushuka na kubaki jina kama moja ya wahasisi huyu sio mwingine ni Prof Jay.

Prof alikuja kwa nguvu kama Roma sasa ,ila kwenye album zake za hivi karibuni amekuwa anatoa mashairi mazuri kwani yeye bado ni bingwa wa kuandika ,ila mashairi ya kiuwanaharakati kama kuongelea uhalisia wa maisha ya kibongo imekuwa finyu sana.Hii ni ukilinganisha na nyimbo zake za mwanzoni mwa miaka ya 2000 Ndio Mzee,Sio zee,Chemsha bongo,Bongo Dar es Salamu.

Wasanii kama fid q na Jo Makini wanauwezo mkubwa ila wanakosa ujasiri wa ku adress issues bila woga kama alivyofanya Roma ama Sugu na Prof Jay enzi hizo,pia huwa wanatumia mafumbo na tafsida kali sana kiasi kwamba inahitaji umakini na utulivu kuweza kuwaelewa wanachozungumzia.Roma yupo straight hivyo kila rika wanaweza elewa anachoongelea kwa urahisi.

Roma ni mwanahip hop wa kweli na anaweza kuwepo kwenye chati kwa muda mrefu kama ataheshimu na kuyaenzi mafanikio aliyoyapata kwa muda mfupi.Wanamuziki wa Tz wanachoshindwa kuelewa nini mafanikio ya muziki kama kazi yao.Wengi wameweka akilini mafanikio ni kununua gari la kutembelea na vitu vya namna hiyo.Muziki kama bidhaa inatakiwa ikubalike na wateja/wasikilizaji ,hayo ndio mafanikio vingine vinakuja baada ya bidhaa ikishakubalika.Ukisikiliza interview za wanamuziki wakubwa Afrika kama Angelique kidjo,Youssou N'dour ,Yvonne Chaka Chaka,Koffi Olomide,Josee Chamilion na hata wa marekani wengi wa hawa wanapoulizwa swali kuhusu mafanikio yao hawataji mali walizonazo bali kitendo cha wao/kazi zao kukubalika ndio mafanikio.
 
kwa kulinganisha na roma kisanii,fid bado anamwacha mbali uyu mtoto..fid kidogo anafikilisha unapomsikiliza,roma amekaa ki-fm fm sana

Hahahahahah eti amekaa ki fm fm!
Ni kweli fid ni mkali.
Ila kuna kitu kimekuwa ni tatizo kidogo kwa sisi wapenzi wa music yetu, tuna kule kulewa na kitu tunachopangiwa na hizi redio.
Kama suala la kukaa ki fm fm hata Fid amekaa kifm tena inaweza ikawa zaidi kuliko Roma. Sababu fid huyu ambaye leo wabongo wanamshobokea sio fid yule wa getto, sio fid yule wa "vita baridi" kipindi hcho yupo na "hurtful dodgers"....
Usingesema suala la u-fm fm labda tungemchek kwa vigezo vingine vya
"5 mic"....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom