Msanii wa muziki wa hip hop, Roma Mkatoliki amefunguka na kutoa kilio chake kwa Basata ikiwa ni mwezi mmoja toka afungiwe kujihusisha na shughuli za sanaa kutokana na kudaiwa kutoa wimbo ‘Kibamia’ ambao hauna maadili.
Akiongea katika kipindi cha XXL cha Clouds FM Jumatato hii, Roma akiwa na mwanae, Ivan amesema anawaomba BASATA kumpungizia adhabu kwani hali yake ya kiuchumi siyo nzuri.
“Haya yote yanaongeleka, lengo ni Roma aendelee kufanya muziki wake kwa sababu muziki unamsaidia kama ajira.
Nyuma ya Roma kuna watu ambao anawasaidia.
Kwahiyo wakati mwingine naomba ieleweke kwamba tufanye tu Roma aendelee na muziki wake ili maisha yake yaendelee,” alisema Roma.
Basata wamesema walimfungia Roma baada ya kutakiwa na baraza hilo kubadili wimbo huo lakini hakufanya hivyo na kila alivyoita hakuweza kutokea.
Katika mahojiano hayo Roma alizidi kusema kuwa
”Tena nikitoka hapa nitawasiliana na Katibu mkuu wa Basata najua atanisikiliza, pia nimesikia Jumatatu kuna mkutano wa wasanii wote na BASATA utafanyikia pale BASATA, zote ni katika njia ya kwenda kuyaongelea haya mambo, lengo tuwe chombo kimoja."
Akiwa katika mahojiano hayo na mtoto wake, Ivan aliulizwa na matangazaji wakipindi hicho kwanini hakwenda shule, na mtoto alisema hajaenda shule kutokana na tatizo la ada.
“Sijakwenda shule leo baba hana ada,” alisema Ivan.
Source: Bongo 5