Roho za mauti: Ni kitu gani hiki?

Asili ya kina baba zangu ni malaya malaya hv!wanazaa watoto na kutelekeza !kwangu mimi ni tofauti kidogo!japo napenda niwe na wake wengi !naona mmoja hanitoshi najali sana wanangu!lakini Dogo ana watatu,wawili katelekeza!!!Alikua hataki kuondoka kwangu eti akae alinde mali zangu!!nikaona uchawi huu nikamtimua akakafanye kazi alee familia yake!yeye hataki!!!kivumbi ndio hapo sasa!!!
Hili tatizo ni kubwa na komavu na litaenda mpaka kizazi cha tatu au cha nne... Wewe ndio umeinuliwa kuikomboa familia na damu chafu kazi kwako
 
Kusamehe hakujawahi kuleta furaha ewe mshana tusidanganyane!!!Hivi mtu anakusnichi kwa bosi wako!unafikiri ukisha msamehe ataacha tabia yake???!!!unajidanganya!!unahitajika umakini na hata kupunguza maneno kabisa!!!
Mshana kuna mahali aliandika, ukishindwa kusamehe lipiza kisasi, hapa anamaanisha kusamehe ni kujisaidia mwenyewe kwa maana ya kuwa huru , na kuondoa visivyo vya rohoni:
Still kusamehe na msamaha ni bora zaidi kuliko kisasi
 
giphy.gif
 
-Siri/secret operating
Ulimwengu wa roho unaendesha mambo yake kwa SIRI NA MAFUMBO sana.Mwenye uwezo wa kutambua hayo ndiye anayeshinda kabisa kwenye ulimwengu wa damu na nyama.Ni muhimu kujua siri ya baraka zako au matatizo unayokumbana nayo.Wakati mwingine unaweza kujiona upo sahihi ukichunguza mwenendo wako;la hasha kumbe matatizo au tatizo lako limeletwa na mtu au watu waliopita katika maisha yako.Kuwa makini sana na mwenza(mume au mke),marafiki,majirani na ndugu.Wanaweza kuwa anguko au inuko lako kutokana na roho walizobeba.CHUMA HUNOA CHUMA.
Mfano Soma 2Samweli 21:1-9 n Yoshua 9 yote kuna funzo utalipata.
Madhara yanaweza kukupata hata kama wewe hukutenda mabaya kama wazazi wako walikuwa kama Sauli.Kuna nguvu katika maagano.Maagano yana viapo,matamko na madhara yanayoendana na kukiuka maagano_Ole wako unayechukulia poa maagano unayofanya na wengine hakika utalipa kwa njia moja ama nyingine.Iwe katika ndoa au kazini tunza kiapo chako.Ukikiuka tu kuna madhara utayapata mwenyewe au uzao wako.Jitahidi kujua siri ya tatizo lako na si kukimbilia kwa wasaidizi wa kiroho wa uongo watakuokuengezea mzigo wa matatizo.Mwombe Mungu wa kweli akujulishe siri ya matatizo yako.Lakini kwa wale wenye kumbukumbu za kifamilia fatilia ujue umepataje hayo mema isije kuwa umeyapata kwa kuwatenda wengine mabaya ikawa chanzo cha shida kwa uzao wako baadaye
 
-Ni ulimwengu wa mbadilishano/Trade oeiented.
Maisha ya mwanadamu katika kila kitu kina mbadilishano.Naamanisha utatenda hili upate lile.Hakuna kinachokuja bure.Na kila upande mwema au mbaya huvutia kwake kwa sera nzuri lakini zenye masharti ya mficho ndani yake.Tumeumbiwa free will katika kufanya maamuzi,amua leo unataka mema au mabaya?Amua nani unayetaka kumtumikia?Mungu ama shetani maana wote ni roho.Maamuzi yako ndiyo yatakayoainisha ni nini kikupate baadaye.Na usije ukajidanganya huko utakapochagua kuenenda ndipo utapata malipo yake.Umeamua kupata vitu kwa uhalali pasipo dhuluma wala manung'uniko hakika utapata mema yadumuyo.Lakini unatafuta kwa dhuluma,ushirikina,kutumia mwili wako isivyo halali au kwa ushawishi wa pesa ama zawadi ndiyo yapo mafanikio ya muda mfupi yenye kilio kwako au kwa wengine.Unatoa nini upate nini?Kama ulivyosema kaka unaburudisha mwili leo lkn unazoa roho au mapepo yanaweza kukudhuru mwenyewe afya ya mwili na akili pia na uchumi.
Je unatumia nyezo gani katika mbadilishano?
(Moyo wako,pesa,kuiba nyota za watu,uchawi,kumwaga dammu za watu nk).
Jiulize mwisho wa hayo yote unayoyafanya yanakupa amani ya moyo na ungependa utendewe hivyo kupata mafanikio au kutatua shida zako?
Ninachoamini dhambi husameheka lakini madhara yake je?Vipi kwa wengine wasiojua baba au mama alitoa nini apate nini?
 
La msingi ni kusimama katika haki na kujichunguza mara kwa mara kwa mara tunavyoenenda ili tusiache vilio kwa vizazi vyetu.UTAVUNA ULICHOPANDA HAKIKA.Kama sio wmewe basi uzao wako.Lakini MAVUNO mabaya ya wazazi wetu yasizuie kuotesha fikira,mawazo na mitazamo mipya kama mbegu bora zinayoweza kuzaa matunda mema katika jamii zetu.
Credit: Chimodoi
 
Back
Top Bottom