Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 75,159
- 157,211
Roho ya korosho ni msemo wa Siku nyingi wa lugha ya Kiswahili.
Msemo huu unamaanisha roho mbaya aliyonayo MTU.
MTU mwenye roho ya korosho ana chuki, ana husda, ana wivu, ana hinda, ana gubu, ana fitna, ni mchoyo, na ni mbinafsi, ni mzandiki na ana Kila sifa mbaya.
Kwa namna rahisi tunasema ana ROHO DUKNA.
Korosho ya Tanzania iimetuonyesha roho yake kwamba yenyewe haiogopi wanajeshi wala magari yao.
Haiuziki kwa mabavu wala maguvu ya watawala.
Hii korosho ilikusanywa kwa mbwembwe na kejeli nyingi kwa wafanyabiashara, kuwa sisi hela ya kununua tunayo, tena pesa taslimu.
Tukashindwa kuinunua kwa pesa taslimu, tukawakopa wakulima, tukaanzisha zengwe na figisu, Mara mashamba yenu tuonyeaheni yalipo, Mara korosho hazina ubora na mwisho tukazirudisha kwa wakulima.
Katikati walipatikana Wakenya, ambao nao hata sijui wamepotelea wapi, tuliambiwa wana mijidola ya kufa MTU. Korosho haiwaogopi wakenya wala mabeberu, korosho INA roho yake bwana.
Matokeo ya roho ya korosho tumwpoteza mapato halmashauri za wiliya na hata serikali kuu pia imekosa mapato.
Tumepoteza fedha za kigeni kwa ajili ya biashara nzima ya korosho mwaka huu.
Korosho INA roho yake jamani, tusiingie kichwakichwa kisa tu una mbichwa mkubwaaaaaa hadi huna saizi ya helmet I.
Tukutane kijiweni.