.Mbona hata sasa hatuna uhuru wa kuchagua kurudi nyuma katika muda? Ningetaka kurudi 1982 nikae na wapendwa fulani waliofariki, lakini siwezi.
Utasemaje tumepewa uhuru wa kuchagua wakati hatuwezi kurudi nyuma katika muda?
Ukisema kunyimwa uhuru wa kuchagua ni kuwa ma robot, mbona sasa hatuwezi kurudi nyuma katika muda, kwa hiyo kwa kushindwa kurudi nyuma katika muda tunakuwa ma robot?
Mungu kwa nini hakuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani kama isivyowezekana kurudi nyuma katika muda?
4 amefanyika bora kupita malaika, kwa kadiri jina alilolirithi lilivyo tukufu kuliko lao.Mwana ni Mkuu kuliko Malaika
5 Kwa maana alimwambia malaika yupi wakati wo wote,Ndiwe mwanangu,Mimi leo nimekuzaa?Na tenaMimi nitakuwa kwake baba,Na yeye atakuwa kwangu mwana?
6 Hata tena, amletapo mzaliwa wa kwanza ulimwenguni, asema,Na wamsujudu malaika wote wa Mungu.
7 Na kwa habari za malaika asema,Afanyaye malaika wake kuwa pepo,Na watumishi wake kuwa miali ya moto.
8 Lakini kwa habari za Mwana asema,Kiti chako cha enzi, Mungu, ni cha milele na milele;Na fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya adili.
9 Umependa haki, umechukia maasi;Kwa hiyo Mungu, Mungu wako, amekutia mafuta,Mafuta ya shangwe kupita wenzio.
10 Na tena,Wewe, Bwana, hapo mwanzo uliitia misingi ya nchi,Na mbingu ni kazi za mikono yako;
11 Hizo zitaharibika, bali wewe unadumu;Nazo zote zitachakaa kama nguo,
12 Na kama mavazi utazizinga, nazo zitabadilika;Lakini wewe u yeye yule,Na miaka yako haitakoma.
13 Je! Yuko malaika aliyemwambia wakati wo wote,Uketi mkono wangu wa kuumeHata nitakapoweka adui zako chini ya nyayo zako?
14 Je! Hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?
Waebrania1:5-14. Ukielewa utamwelewa Yesu.
Ha ha ha ...wewe hufuati maandiko ya kitabu u achokiamini, unafuata dhehebu!!!??? kanisa!!! ulishawahi kushika biblia ukasoma mwenyewe?samahani! Wewe mkristo wa dhehebu gani ambao wanafundisha kuwa Yesu ni binadamu?
.
Mimi naamini kuna Mungu, wewe unaamini hakuna mungu.
Nihakikishie wewe kwanza kwamba mungu hayupo ili iwe chachu ya mimi kukuhakikishia kinyume chake.
Kwanza mimi nasema Mungu ninaeamini yupo ndie hupanga yale yote yanayoendelea katika maumbile na kwamba sisi hatuna hiyari ya kuyafanya vinginevyo mf wa makuzi, kuzeeka na hatimae kufa.
Sasa wewe kama huamini yupo ambaye ndiye hupanga hayo tungetamni kuona kutokuwepo kwake kufanye hayo yaliyoamriwa kuwa kinyume chake.
Laa kama hutaweza basi uliisha kusalimishwa kwake hata kama hukutaka kujisalimisha maana hili halipo katika hiari yako. Yeye ndie mmiliki wako.
Huyo hataki kuelewa swali lake limejibiwa vizur na clip niliyompa ...hajaisikiliza na kuielewa anarudia swali lilelile thread nzima!!!Mkuu Alwatan habari yako, mkuu huwezi jifunza jambo kwa watu wasio na ujuzi na jambo hilo zaidi itakuwa ni mabishano yasiyo na tija,michango itolewayo humu kuhusiana na swali lako haikidhi kiu yako ya jibu.
Nilikushauri na pia narudia tena kama unataka elimu kuhusu majambo haya haswa kwa upande wa uislam basi wako wanachuoni wenye elimu juu ya haya mambo, kinyume cha hapo ni mabishano yasiyo na tija na ukomo pia
Hatuwezi kuthibitisha kuwa jua litachomoza kesho au halitachomoza,hivyo hatuna jinsi ila ni kuisubiri tu kesho.Na jua linaweza kupiga supernovae leo lisichomoze kesho.
Kushindwa kuthibitisha kitu kama kipo au hakipo hakuoneshi lolote kuhusu kuwapo au kutokuwapo hicho kitu.
Unaweza kushindwa kuthibitisha kitu kipo, kwa kitu ambacho hakipo.
Unaweza kushindwa kuthibitisha kitu kipo, kwa kitu ambacho kipo.
Kwa hiyo kushindwa kuthibitisha kitu hakuna maana yoyote.
Ukitaka kujua kitu kipo, njai pekee ya kujua kwa hakika, ni kuthibitisha kwamba kipo.
Ndiyo maana nakuuliza, unaweza kuthibitisha Mungu yupo?
Kamaunaweza, thibitisha.
Na ukishindwa, unajuaje kwamba yupo, umeshindwa kuthibitisha tu kwamba yupo, na si kwamba hayupo na umeshindwa kuthibitisha yupo kwa sababu hayupo?
Kwa hiyo unakubali kwamba kwa sasa huna uhakika?Hatuwezi kuthibitisha kuwa jua litachomoza kesho au halitachomoza,hivyo hatuna jinsi ila ni kuisubiri tu kesho.
Na suala la uwepo wa mungu nalo pia mwisho wa siku tutaweza kujua kiuhakika kuwa ni kweli yupo au hayupo.
Kwanza tusaidiane hapa Mungu ninanYesu Si Mungu. Na hawezi kuwa Mungu.
Mungu haonekani hivyo hana mfano.
Hizo nyingine ni simulizi.
Hakuna sababu inayofanya Yesu Awe Mungu Mkuu
Kwanza la suala Chid Benz sio la imani na hata mwishoni alisema ni ulikuwa utani.Sawa, sinatatizo na imani, nina tatizo na imani potofu.
Hata ukipanga mkutano wa kesho, unapanga kwa imani.Unaamini kesho itakuwepo, jua litachomoza,hutafariki usiku wa leo. Hiyo yote ni imani. Bila imani hatuwezi hata kupanga mambo ya kesho.
Sina tatizo na imani, nina tatizo na imani potofu.
Kama imani, Chidi Benz ana imani kwamba ametoa nyimbo na wasanii wakubwa kina Rihanna na 2Pac.
Hiyo ni imani pia.
Na anaweza kukwambia u prove kwamba hajatoa hizo nyimbo, ukashindwa ku prove.
Lakini kumbe imani hiyo ni potofu, Chidi Benz hajatoa nyimbo hizo.
Sasa, utajuaje kwamba imani yako wewe ni sahihi, Mungu yupo, na si imani potofu kama ya Chidi Benz, kwamba unaamini Mungu yupo wakati hayupo?
Ulimwengu unakufanyaje uamini Mungu?Kwanza la suala Chid Benz sio la imani na hata mwishoni alisema ni ulikuwa utani.
Hata hivyo tulipofika ni pazuri,kwanza moja ya jambo linalonifanya niamini mungu ni huu ulimwengu(hili linaelezwa sana) hivyo ukiliangalia hilo suala ni wazi imani yangu ya kuwepo mungu naona ni sahihi kabisa.
AsanteYesu alipozaliwa na mwanamke lengo lilikuwa kuuvaa mwili wa duniani kwa sababu yeye ni roho..Na ili uweze kukaa na kumudu mazingira ya dunia lazima uwe na mwili wa mnyama,,binadamu,,ndege,,mdudu au bacteria nk.The same baharini lazima pia uwe na mwili wa samaki au viumbe wa baharini...Kwa kuwa Yesu ni Roho na anaeishi katika mbingu ambayo ndiko makao na makazi ya roho,,,hapa duniani ilim,,bidi kuvaa mwili ili awe na ufananio na viumbe wa realm hii ya dunia,,,chek (Waebrania 10:5)) Ukisoma vizuri utaona anauongelea mwili akiwa nje ya mwili
"""Kwa hio ajapo ulimwenguni asema,Dhabihu na toleo hukutaka,,lakini mwili uliniwekea tayari."""" Kwa kufikiria deeply utaelewa kwamba Yesu angelikuwa ndani ya mwili asingeongea maneno hayo.Alikuwa kwenye realm ya uhalisia wake nje ya mwili.
Unajichanganya.
Kwa nini Mungu hakuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani kuwepo kama alivyoumba ulimwengu ambao time travel haiwezekani?
Hujajibu swali hili.
Ukisema habari za uhuru aliopewa mtu,hilo si jibu.
Baba hampi mtoto wake mchanga asiye na akili pevu maziwa na sumu, ili tu mtoto awe na uhuru wa kuchagua kunywa maziwa aishi au sumu afe.
Huyo baba akifanya hivyo, kisha mtoto akachagua sumu na kufa, atashitakiwa na kufungwa.
Sasa kwa nini Mungu ambaye alikuwa na uwezo wa kutupa viumbe vyake maziwa tu, asitupe sumu kabisa, kwa nini katupa maziwa na sumu?
Kwa nini tumuhukumu huyu baba mwenye uwezo wenye mwisho, upendo wenye mwisho na ujuzi wenye mwisho hukumu mbaya, wakati mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote tunamsifu kwa kufanya kitu kile kile?
Naona tumefika kwenye point ambayo tunaanza kuelewana na ninaomba niende na wewe hatua kwa hatua kwanza swali ulilolileta la kwanza nishalijibu
lakini naona bado hatujaelewana basi narudia tena Mungu aliuumba ulimwengu mkamilifu usio na taabu, kifo wala njaa na Alipanga mwanadamu autawale huu ulimwengu hayo mabaya unayoyasema yaani Mungu Aliuumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana ili swali linajibiwa kwa muktadha huu kwamba Mungu alitaka mwanadamu amtii na amheshimu na amuabudu
na haya yote yangewezekana kama mwanadamu angelichagua kwa moyo wake mwenyewe kumtii kumheshimu na kumuabudu na tofauti na hapo yaani Mungu angemuumba mwanadamu ambaye anayohulka ya kumtii Mungu ya asili ambayo ni tofauti na moyo wa mwanadamu unavyochagua basi tungemuabudu Mungu kwa shuruti yaani sio kwa mapenzi yetu wenyewe bali kwa sababu ametufanya tumuabudu.
Hapo ndipo Mungu akaamua kumpa mwanadamu free will
ambayo ilimpa mwanadamu uwezo wa kuamua sasa ilibidi hii free will ipimwe kuwa je mwanadamu kweli atachagua kumtii Mungu kwa hiari yake mwenyewe na kumbuka hii hiari tayari alikuwa ameshapewa na Mungu ndipo basi mti wa mema na mabaya unapoingia ambapo uliwekwa ili kutathimini kama mwanadamu atatii maagizo ya Mungu kwa kuwa hiari au free will tayari anayo.
Hapa tunaona baada ya Mungu kumpa onyo mwanadamu kuwa usile lile tunda na akampa na sababu kuwa ukila hilo tunda basi Hakika utakufa ndipo mtihani sasa wa kutathimini kama mwanadamu atamtii Mungu au atatii maagizo aliopewa na Mungu ukaanza na tunaona kuwa mwisho wa siku mwanadamu akakaidi maagizo ya Mungu na ndipo sasa dhambi inaingia ulimwenguni na kifo kinaingia ulimwenguni na hapo ndipo sasa mabaya yanaingia ulimwenguni.
Na swala la mabaya kuwezekana ni conditional kwa sababu mwanadamu angelichagua kumtii Mungu na kutii maagizo yake basi mabaya yasingekuwepo na huu ndio uliokuwa mpango wa Mungu kuwa mwanadamu amtii bila shuruti bila kulazimisha bali kwa maamuzi yake mwenyewe na tunaona kumbe baada ya ukaidi wa mwanadamu dhidi ya sheria ya Mungu ndipo mabaya yakawezekana ndio maana haya yote yalikuwa yameshikiliwa na free will kama tungelichagua kumtii Mungu basi hadi sasa tungelikuwa na ulimwengu ambao mabaya yasingelikuwepo lakini kisa ukaidi wetu ndio maana ulimwenguni mabaya yanawezekana na sio mpango wa Mungu mkuu.
Na pia inabidi ujue kuwa Adamu hakuwa mtoto bali aliuumbwa bali aliuumbwa mtu mzima kamili mwenye uelewa ndio maana alikuwa ana uhuru wa kuchagua na wa kuamua kwa hiari yake mwenyewe na mtoto hana hicho kitu hana hiari au uwezo wa kuchagua ndio maana Adamu na Hawa wote walikuwa wanaujua mti ule wa mema na mabaya uko wapi na ukoje unafanana vipi ili watakapokula wasije wakaleta kisingizio kuwa tuliufananisha. Kwa hiyo mfano wako hauna mhimili na kama ungetaka uwe na mhimili ungeuweka hivi kama Baba yako na nna litumia hili jina kwa heshima zote angelikuwa anataka kupima kama unamheshimu na unamtii angechukua glasi mbili za maziwa moja ikiwa ina maziwa tu na nyingine ikiwa ina maziwa na sumu ndani yake na akakuonyesha wewe (na nnasema wewe nikiwa namaanisha kuwa una uwezo wa kujua kuwa haya ni maziwa na pili una uwezo wa kuchagua kunywa au kutokunywa yaani hiari au free will) na kukuambia kuwa maziwa kwenye glasi hii ya kwanza (tuiite glasi A) unaweza kunywa lakini maziwa kwenye glasi hii ya pili yaani glasi B usinywe maana siku utakapokunywa haya maziwa Hakika utakufa.
Je wewe ukienda kunywa maziwa kutoka kwenye glasi B huoni kuwa utakuwa hujamtii na cha pili kuwa utakufa maana ina sumu ndani yake na isitoshe ulikuwa na uhuru wa kuchagua yaani hiari au free will ya kunywa au kutokunywa na juu ya hilo kulikuwa na glasi A ya maziwa ambayo uliruhusiwa kunywa wewe huoni kama utakuwa umedharau maagizo ya Baba yako na umekaidi alichokuambia na pia inaonyesha humtii wala humheshimu.
Sijui tunaelewana mkuu.
.Imani haina shurutiwala nguvu,unaruhusiwa kuamini chochote,kuna "Universal Declarationof Human Rights"inatetea haki yako ya kuamini, mradi usivunje sheria tu. Katiba ya Tanzania inatoa Uhuru wa kuamini, sina nia ya kujadili imani.
Nina nia ya kujadili ukweli.
Vitu viwili tofauti.
Kisichopo hakiwezi kuthibitishwa kwa uhakika, kwa sababu hakipo.
Kama umeibiwa, mwizi kavunja dirisha lako kaingia ndani mwako, kashika kitasa kwa ndani, kafungua mlango, kaiba, wakija wataalamwa polisi wataweza kuona alama za vidole za mwizi.
Lakini, kama hakuna mwizi aliyeingia utathibitishaje kwamba hakuna mwizi aliyeingia?
Utasema hizi hapa alamaza vidole za mwizi ambaye hajaingia ndani humu?
Ukichunguza utaona,nje ya logical analysis, kuthibitisha kisichopo kwamba hakipo hakuwezekani.
Kwa sababu hakipo ili kithibitishwe kwamba hakipo.
Uthibitisho wa logicalanalysis nimeutoa hapojuu,proof by contradiction. Soma.
Kufa hakuthibitishi Mungu yupo, kufa kunathibitisha Mungu hayupo.
Kwa nini?
Mnasema Mungu anauwezo wote, ujuzi wote na upendo wote.
Mwenye ujuzi wote,uwezo wote na upendo wote, anatakiwa kuwa na nature ya kutotaka kuwatenganisha viumbe wake wanaopendana.
Kifo kinatenganisha vumbe wanaopendana.
Hivyo, kifo ni ushahidi kwamba Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote hayupo.
Angekuwepo asingeruhusu kifo kiwezekane katikaulimwengu wake.
Suala si kuamini, suala ni kuthibitisha.
Unaweza kuthibitisha Mungu yupo?
Kabla ya kufika kote huko, unaweza kuthibitisha Mungu yupo?
Kwa mimi ninavyoelewa hapa ni kwamba yule mwanamke mpunga pepo alitumia pepo la utambuzi kumpasha mfalme Sauli habari ya mambo yatakayo tokea. Japo shetani anao uwezo wa kumpatia mtu maono.Masahihisho kidogo. Sio nabii Nathan, bali ni nabii Samuel. Na maandiko hayasemi kuwa roho iliyoongea na Sauli ilukuwa ya shetani. Alikuwa ni Samweli mwenyewe. Fuata maandiko yanavyosema, sio mawazo ya watu wa theolojia. Kama shetani alimpandisha Bw. Yesu juu ya mnara wakati alipojaribiwa na shetani unaonaje isiwezekane mchawi wa Endori kupandisha kivuli cha nabii Samweli?.
Kwanza kabisa, kamanilivyoeleza hapo juu, kisichopo,hakina proof nje ya logical construct,kwa sababu hakipo..
Hakuna anaeshurutisha imani na ndio maana hata wewe umebaki huru katika imani yako ya kutokuwepo mungu.
Basi kama unakiri kwamba huna shaka na swala la imani ila ku proof imani iliyo kweli ndipo nikakutaka wewe unipe proof ya imani yako ya kutokuwepo mungu.
Kama huna uwezo wa ku proof kwa nini wewe umtake anaeamini uwepo wake ku proof?
Yesu alipokimbilia kwenye Mlima wa Zaituni na huku akisakwa na Mayahudi alijitenga na wanafunzi wake. Huko faraghani aliomba hivi:
Ee Baba, ikiwa ni mapenzi yako, uniondolee kikombe hiki; walakini si mapenzi yangu, bali yako yatendeke. Malaika kutoka mbinguni akamtokea akamtia nguvu.
Luka 22.42-43
Hapa tunaona mambo matatu muhimu:
1. Yesu anamwomba Mungu. Yesu anamwabudu Mungu. Wawili hao ni mbali mbali, na vyeo vyao ni mbali mbali. Yesu ni mtumwa mnyonge mwenye kuomba na kuabudu. Na Mungu ni Mwenyezi Mungu mwenye uwezo wote na mwenye kustahiki kuabudiwa pekee, hata na Yesu, mwenye kutakiwa msaada pekee, hata na Yesu.
2. Mapenzi ya Mungu ni mbali na yale ya Yesu. Yesu hataki kuuliwa, ananyenyekea na kuomba kwa Bwana wake: "uniondolee kikombe hiki" cha mauti. Yesu hana azma hata chembe ya kufa msalabani, kifo cha mhalifu, kifo cha laana kama maadui zake Mayahudi walivyoazimia kumpatilisha nacho. Lakini anakiri kuwa ni mapenzi ya Mungu sio yake yeye yatendeke. Yeye hana hila wala nguvu za kuzuia kudra ya Mwenyezi Mungu.
3. Yesu, Mwana wa Adamu, anakata tamaa. Imani inampunguka. Kavunjika moyo. Ikabidi "Malaika kutoka mbinguni akamtokea akamtia nguvu."
Jee, yaelekea kuwa Yesu ndiye Mungu? Yaelekea kuwa yeye na Mungu kuwa ni sawa? Kama upo wasiwasi wo wote wa kujibu hayo, mwenyewe Yesu anajibu kama anavyo hadithiwa na Yohana kuwa kasema:
Baba ni mkuu kuliko mimi.
Yohana 14.28
Na mwishoni naye yupo mslabani:
Na kama saa tisa, Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akisema, Eloi, Eloi, lama sabakthani? yaani, Mungu wangu, Mungu wangu, Mbona umeniacha?
Mathayo 27.46
Yafaa hapa tujiulize: Yesu akimlilia Mungu gani hapo msalabani ikiwa naye mwenyewe ni Mungu? Au nini alikusudia aliposema: "Mungu wangu naye ni Mungu wenu"?Maneno hayo kama yanaonyesha cho chote basi yanaonyesha unyenyekevu wa Yesu mbele ya Mungu wake. La kustaajabisha ni kule kukata tamaa kwake na kuvunjika moyo.
Huwaje mtu wa imani, licha ya nabii na mwana pekee wa Mungu, akate tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu. Ama kuwa Mungu akate tamaa na Mungu, na kumyayatikia: "Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha", ni jambo ambalo halimkiniki kuwa.
Kwa uthibitisho ulio wazi Biblia inatwambia kuwa Yesu si Mungu, wala Mungu si Yesu.