thebogo055
Member
- Jun 22, 2020
- 19
- 176
Kuna watu tunatofautiana sana kimawazo, fikra, weledi nk.
Wapo binadamu hata umfanyie nini bado hatokuheshimu wala ku appreciate yote uliyomfanyia.. yupo radhi akuue achukue nafasi yako. Sishangai hii ni human nature (ubinafsi) tuna ubinafsi sana ingawa ni ngumu sana kuuonesha lakn deep inside kuna roho ile ya kwanini, sio wote lakini.
Nawapa mfano mmoja kwenye maisha yangu. Binafsi nina roho ya huruma kiasi kwamba kuna baadhi ya ubaya huwa nachukulia poa ukinifanyia. Nina uwezo wa ku- control hasira zangu na maswaiba yanayonipata.. najua hichi ni kipawa pia kwasababu kuna watu hawawezi kuvumilia.
Sasa kwa ufupi ni hivi. nimekutana na mtu mwenye roho mbaya sijawah kuona duniani. dah! Nimebahatika kumsaidia mtu kupata kazi, nikamuamini sana na kumpa nafasi kubwa katika maisha yangu, lakin nimekuja kugundua huyu mtu ni muongo, mnafik, mzandiki, black mailer yaan kila sifa anayo.
Hivi inawezekana vipi nakutuma ufuatilie pesa yangu mahali halafu umeipokea na kwangu huileti. Na bahati mbaya yule mtu alietoa hiyo pesa alipoteza simu so akawa hapatikani. Sasa kila nikimuuliza yule mtu vipi umepewa ile pesa anasema hamuoni na hawajaonana kumbe kashapokea na kula.
Sasa leo natoka safarini kwenye misele yangu ghafla nakutana na yule ambae alikuwa na pesa yangu... tukapeana hi.. then nikakumbushia deni!
Cha ajabu jamaa anasema hela alimpa yule mtu niliemtuma zaidi ya week mbili sasa, ikabidi nipge simu niweke loud speaker, yule mpumbavu akakana hajapokea. Sasa ili kujua nani muongo nikamchukua yule mtu nikaenda kwa jamaa.
Dah ni aibu tupu..kumbe hela kapewa na katumia yote na bado anafanya kazi kwenye sehem ambayo mimi ndio nilimuweka kwa sababu ya kumuonea huruma.
Na mbaya zaidi nimepata taarifa anatangaza ile sehemu ya kazi ni yake. Jamani kuna binadamu wanafanya tusisaidiane.
Nimeamua nimtupe kila mtu ashinde mechi zake. Leo kaja Home kamkuta wife anamwambia ana maongezi naye. Ila kwa kuwa nilimpa maagizo wife kwamba akija amfukuze ikabidi jamaa asepe tu.
Sasa nasikia ananitafuta huko anataka suluhisho.