Roho inayotumwa kuharibu ndoa

Roho inayotumwa kuharibu ndoa

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
78,986
Reaction score
168,511
Nimepata neema ya kuanza kufundisha juu ya matatizo ya kiroho na mungu amenifunulia haya na kunionyesha uhitaji wa wengi juu ya hili na jana nilianza kufundisha juu ya ndoto nitaendelea kufundisha kwa kadri roho atakavyonifunulia endelea kuniombea ili tuwasaidie wengi huduma hizi za ukombozi zina vita sana hivyo maombi yako ni muhimu sana.

Aina hii ya roho ni aiba ya uchawi wa kutumwa na huwa na chaguzi mbili

1.Roho hii ikimwingia mwanamke humfanya mwanamke ghafla kutoridhika na muonekano wa mwanaume na kujawa na hasira anapokuwa naye

2.Asipoweza kumuingia mwanamke hutumia njia ya hisia kwa na kivuli hivyo kumfanywa mwanaume kumuona mwanamke ana sura mbaya na umbo baya kutokana na kivuri cha roho huyo wa kichawi aliyetumwa kuharibu.

Kwa matokeo ya roho huyu wa uchawi huu na kwa kivuli cha roho huyu hivyo basi ni rahisi sana mwanamke au mwanaume aliye vikwa nguvu hii kuchukiwa na mara nyingi pia roho hii inaweza kutumwa kwa mahusiano yanayoanza akitumwa roho huyu ngafla utashangaa upendo unakwisha au kupungua au hata mahusiano kufa kabisa

Aina hii ya roho ni mbaya sana kwani imetumika kuharibu ndoa nyingi sana kuna wakati roho hii ikiwa kubwa sana, kuna wakati mlengwa anapoingia nyumbani huhisi uchovu,haasira , mkali mgomvi na hali ya kutoridhika na kuamua kuondoka au kutoongea na kulala tu

Dalili za mtu na roho huyu

1.Maumivu ya kichwa yasiyosikia dawa za hospital au pindi anapokuwa na mwenza wake...

2.Maumivu ya kifua na mbavu kubana hasa muda wa al-asri na usiku

3.Mtu kuwa mkali,mwenye hasira , mgomvi, na maumivu ya mara kwa mara

4.Maumivu ya mgongo na kiuno hasa wakati wa kuelekea kwenye ndoa.

5.Vitu vya ajabu wakati wa kulala.

6.Kuhisi mwili mzito

7.Kuota unafanya tendo la ndoa mara kwa mara
Ninajaribu kuwaeleza mambo haya ili yawasaidie wengi kwani watu wengi mifumo ya dini tuliyojengewa ni kama mambo haya hayapo yalikuwa hayaongeliwi huku yakiwaacha wengi chini ya mateso na matatizo makubwa

Nitakuja kuelezea tena juu ya magonjwa ya kipepo na dalili za ndoto za mtu mwenye magonjwa ya kipepo

Share jumbe hizi na wengine wafunguliwe kwani najua wapo watu wengi wapo chini ya vifungo vya nguvu za giza na hawajui kama ni vifungo....
 
Mungu akutie nguvu mtumishi wa Mungu, natumai kupitia haya mafundisho ndoa nyingi zitapona.
 
Mm naomba niizungumze hii Kwa namna tofauti kidogo
Kizazi Cha Sasa NI kizazi ambacho hakina hofu ya Mungu Kwa hyo NI rahisi Sana ndiio kushindwa kusimama
Wazazi hatuna hofu ya Mungu tumezaa watoto wasio na hofu ya Mungu halafu tunataka wasimame kwenye ndoa imara
Pili malezi ya mzazi mmoja ambayo vijana wwngi wanapitia kwa Sasa yanachangia Sana kuharibu ndoa mume au mke anaona mbona anaweza kuzaliwa shi Kama mama yake au baba yake alivyoishi
Hili nalisema kwa sababu Nina ushahidi
Kukuta darasani la wanafunz 60 ambao 555 wanaisha na single parent n kitu Cha kawaida Sana
 
Ukweli mtupu

Kwann umchukie mtu ambaye moyo wako uliwaka kwa ajili yake miaka kadhaa kabla ya ndoa ??
 
Nimepata neema ya kuanza kufundisha juu ya matatizo ya kiroho na mungu amenifunulia haya na kunionyesha uhitaji wa wengi juu ya hili na jana nilianza kufundisha juu ya ndoto nitaendelea kufundisha kwa kadri roho atakavyonifunulia endelea kuniombea ili tuwasaidie wengi huduma hizi za ukombozi zina vita sana hivyo maombi yako ni muhimu sana.

Aina hii ya roho ni aiba ya uchawi wa kutumwa na huwa na chaguzi mbili

1.Roho hii ikimwingia mwanamke humfanya mwanamke ghafla kutoridhika na muonekano wa mwanaume na kujawa na hasira anapokuwa naye

2.Asipoweza kumuingia mwanamke hutumia njia ya hisia kwa na kivuli hivyo kumfanywa mwanaume kumuona mwanamke ana sura mbaya na umbo baya kutokana na kivuri cha roho huyo wa kichawi aliyetumwa kuharibu.

Kwa matokeo ya roho huyu wa uchawi huu na kwa kivuli cha roho huyu hivyo basi ni rahisi sana mwanamke au mwanaume aliye vikwa nguvu hii kuchukiwa na mara nyingi pia roho hii inaweza kutumwa kwa mahusiano yanayoanza akitumwa roho huyu ngafla utashangaa upendo unakwisha au kupungua au hata mahusiano kufa kabisa

Aina hii ya roho ni mbaya sana kwani imetumika kuharibu ndoa nyingi sana kuna wakati roho hii ikiwa kubwa sana, kuna wakati mlengwa anapoingia nyumbani huhisi uchovu,haasira , mkali mgomvi na hali ya kutoridhika na kuamua kuondoka au kutoongea na kulala tu

Dalili za mtu na roho huyu

1.Maumivu ya kichwa yasiyosikia dawa za hospital au pindi anapokuwa na mwenza wake...

2.Maumivu ya kifua na mbavu kubana hasa muda wa al-asri na usiku

3.Mtu kuwa mkali,mwenye hasira , mgomvi, na maumivu ya mara kwa mara

4.Maumivu ya mgongo na kiuno hasa wakati wa kuelekea kwenye ndoa.

5.Vitu vya ajabu wakati wa kulala.

6.Kuhisi mwili mzito

7.Kuota unafanya tendo la ndoa mara kwa mara
Ninajaribu kuwaeleza mambo haya ili yawasaidie wengi kwani watu wengi mifumo ya dini tuliyojengewa ni kama mambo haya hayapo yalikuwa hayaongeliwi huku yakiwaacha wengi chini ya mateso na matatizo makubwa

Nitakuja kuelezea tena juu ya magonjwa ya kipepo na dalili za ndoto za mtu mwenye magonjwa ya kipepo

Share jumbe hizi na wengine wafunguliwe kwani najua wapo watu wengi wapo chini ya vifungo vya nguvu za giza na hawajui kama ni vifungo....
Kheri umesema...mifumo ya imani..inatufanya kupokea sacramenti ndio mwisho wa matatizo..hatuna nguvi ya kupambana na mambo haya ya kiroho..matokeo yake tunaumizwa..ndoa hazina amani...watoto watukutu na ushoga bin usagaji...yaani ni shida...kumbe mengi ya haya yanatokea rohoni..mungu akubaliki kusema hili waziii
 
Amen
 
This is maturity. Kwenye mada za kibaba kama hizi huwezi ukakuta tule tuvulana twa kula tunda kimasihara tukichangia.
Well done uncle Bujee
 
Hapo, inahusika sana na roho za majini mahaba,na wao wana hulka hizo hizo.
 
Ukweli mtupu,ndoa bila ya kuwa karibu na Mungu lazima ipate misukosuko sana...
 
Back
Top Bottom