Mkuu wanawake hawasifiwagi kijingajinga hivyo.
Kumpenda haukatazwi, lakini usijichanganye kumuungamia kama ulivyojaribu kufanya hapa Jf! Mpende kimoyomoyo, ukimdhihirishia kwa maneno, umekwisha! Mdhihirishie kwa matendo yatosha.
Tena huo ujinga unafanywa sana na vijana makamo yenu, hasa wakati wa kilele cha kukwea mlima kitonga, ukifika kwenye kilele ubongo unazubaa na kisha kusinyaa na kuwa mdogo kama wa jogoo, bila ridhaa ya kujitambua, unaanza kuweweseka na udenda mdomoni kama taahira! Ndiyo uungameje?
......Ooh... akiyaMungu ninakupenda sana na ukiniacha najiua....
Hapo mkuu utakuwa umejikaanga kwa mafuta yako mwenyewe.
Lakini nisikupelekeshe sana, aweza kuwa hana mood ya kuwasiliana na wewe kwa ajili ya uchovu na kiubinadamu tu na si vinginevyo.
Mpe nafasi ya falagha zake ili penzi liendelee kustawi.
Kumfuatafuata kisogoni muda wote akakosa hata pa kutemea mate atakuchoka mapema na penzi kupauka.