pesa maua
Member
- Jun 13, 2016
- 35
- 17
Kwa jina naitwa Mr.beca ni mzaliwa wa mkoani Dodoma...!!!mnamo mwaka 2001nikiwa darasa la tano nilitokea kuvutiwa na binti mmoja ambae kiukweli nilimpenda sana...tena sana!!katika kipindi hiko yeye pia alitokea kunipenda ila hakuna ambae alipata ujasiri wa kufunua mdomo na kumtamkia mwenzie neno hili"NAKUPENDA''
Tuliendelea na masomo yetu tena tukiwa darasa moja...!!
Katika shule ile ambayo tulikua tunasoma tulikua wanafunzi wengi mno hivyo kuna eneo la jirani ambalo lilikua wazi iliamriwa ijengwe shule nyingine ili kukidhi idadi hii ya wanafunzi...hivyo kukawa na shule mbili katika eneo moja...!!na zikapewa majina ya A na B.....!!!!!!!!!!!!!!!
Mimi nilibahatika kupelekwa B,ina maana binti yule aliachwa hapa hapa A...!nikiwa katika shule hii B nilijikita mawazo yangu yotee katika elimu kwa kuangalia hali ngumu ya maisha ya nyumbani....!!!!hatimae siku zikasonga mithiri ya upepo kilimani na mawazo juu ya binti yule yakiwa kwenye mgando wa friji ya moyo wangu...!!
Kwakua shule zilikua karibu sana kuna muda niliweza kumuona japo kwa uchache ila ilitosha kunifariji mie...!!
GHAFLAAAA.....
Nikawa simuoni kabisa ndani ya macho yangu...nilijiuliza sana ila sikupata jibu na pia sikuthubutu kumuuliza MTU yeyote maana nilikua na aibu sana pia sikutaka mtu yoyote atambue hili jambo...!!!
Hatimae muda ulifika ambapo niliweza kuhitimu darasa la saba,nikiwa na upungufu machoni na moyoni kwa kutomuona mrembo yule..!!
Nikiwa nyumbani muda ambao nimemaliza la saba,nikawa najaribu kuulizia kwa chinichini habari za binti yule ila sikuweza ambulia japo hata kidogo...!!hatimae muda ulisonga ukafika muda ambapo matokeo ya la saba yalitoka na nikafanikiwa kufaulu na kuchaguliwa kujiunga katika shule flani pale Dodoma...!!kipindi chote hiki sikuwahi kufikiria wala kujiingiza katika kundi lolote la mapenzi...maana niliamini yule binti alikua chaguo la nafsi na moyo wangu.....!!!!!
Siku zikasonga,hatimae kidato cha pili,hatimae kidato cha tatu Mungu mkubwa hatimae nikaingia kidato cha NNE....!!!nikiwa kidato cha NNE nilikua na rafiki wa karibu sana,ambae nikisoma nae darasa la kwanza mpaka la saba...huyu kuna siku nilipata kumuuliza habari za binti yule...!!naam alinipa jibu ambalo nilihisi ndoto zangu za kumuona tena binti yule zinetimia...!!
Yule rafiki aliniambia maneno haya ''mbona huwa namuona sana maeneo ya chamwino...!!tena hata Jana nilimuona...''nilifurahi sana kusikia maneno Yale...akaongeza "tena huwa na muona na....ITAENDELEA