Aiseee, pole sana, kuna siku na mimi nilienda kumuona mgonjwa(mchepuko) enzi hizo lakini, Nimefika pale tukapiga story akaniambia anataka akanunue maji ya kunywa, nilikua na kama elfu 37 hivi kwenye mfuko wa shati, sasa nazitoa ili nimpe hiyo hela ya maji si akazivuta zote!!!
Halafu sikua na usafiri na ilikua usiku ushaingia, na cm imezima chaji, nilichukia mno, nikamwambia basi nipe hiyo buku mbili nichukue bodaboda mpaka makumbusho then nipande daladala to home akawa anacheka ile kwa dharau.
Akatoka akaenda kununua vya kununua, na mimi nikatoka nikaanza mguu mosi mguu pili huku nikitafakari cha kufanya maana hata umeme ulikua umekatika kote. Ila mpaka leo sijawahi kurudi tena kwake. Alinifanya nimuwazie tofauti sana.