Rocket Science: Vikinga Radi kwenye launch pad

Mzawa_G

JF-Expert Member
Feb 27, 2014
667
1,467
Launch Pad ni eneo maalumu ambapo vifaa vya kupaa anga za mbali hupaki kabla ya kurushwa.
Katika Launch Pad ndipo ufanyiwa assembling ya vifaa vyote vitakavyotakiwa kupaa kwenye mission husika.

Kama inatakiwa kupaisha payload kutumia, kwa mfano, Rocket ya Falcon Heavy, itatakiwa Rocket hiyo ipangwe ikiwa kwenye Launch Pad, kuanzia engine base, Tank la Oxygen, juu yake itaongezewa tank la Hydrogen, kisha itafungwa Boaster mbili moja baada ya nyingine, itajazwa mafuta na kukaguliwa ikiwa kwenye Launch Pad.
Kazi hizo zote zinaweza kuchuka zaidi ya mwezi mzima.

Wakati huo yote yakiendelea kunakuwa na uangalizi mkubwa wa vifaa maana wanatumia teknolojia za hali ya juu na za gharama kubwa, hivyo inatakiwa kulinda vifaa vyote kwenye pad visiharibike kirahisi.

Katika kuweza kupaa angani, vifaa vinahitaji kuwa na mafuta ya kutosha, mafuta yanayotumika kwa wingi ni vimiminika vya Hydrogen na Oxygen au Nitrogen, kwenye booster kunakuwepo na mafuta yabisi (Solid Fuel) ambayo ni Mchanganyiko wa kemikali kuunda kitu kama unga wa risasi amabao utalipuka kupaisha chombo juu.

Kwa malighafi zinazotumika kwenye kuunda vyombo vyenyewe, na mafuta yanayokuwa yakipakiwa kwenye ma-tank ya Rocket itakuwa ni rahisi vyombo hivyo kuwa na
"active charges" za umeme mda wote.
Na hata hivyo kwa sababu ya mahitaji ya nguvu ya kupaa juu sana, vyombo hivyo vinatakiwa kuwa virefu kwa ajili ya kutunza mafuta ya kutosha.

Urefu, Charge, Material, Mafuta ya kemikali na Muda vinavyokaa kwenye uwanja wa kurushia husababisha kitu kikubwa ambacho ni rahisi kuviharibu vyombo hivyo kiwe ni Radi.
Hapo ndipo inapokuja kazi ya minara: kukinga Radi.

Ukifatilia kwenye vituo vya kurushia vyombo vya anga hasa mission ambazo zinatumia Liquid Fuel utaona minara kadhaa kuanzia mitatu hadi minne inayokuwa mirefu kuliko Space shuttle,
Uliwahi kujiuliza hiyo minara ni ka kazi gani.!?

Ukiachana na minara hiyo minne, Launching mission nyingine kunakuwa mnara mmoja mkubwa, huo unakuwa ni "Assembling Tower" lakini unakuwa na peak iliyopanda juu kuliko Space Craft ilipoishia, nao huwa na kazi mbili zaidi.

Ile minara huwa ni "Lighting Tower" ni vikinga radi au wengine wanaita "mtego wa Radi" inakuwa imeunganishwa na waya mpaka ardhini (Earthing) kwa ajili ya kukusanya umeme wa Radi hadi "underground".

Tofauti na waya wa Earthing na Earth-rod majumbani unakuwa wa Copper, kwenye minara hii waya huwa Silver, lengo lake ni kubeba umeme mkubwa sana wa Radi utakaoweza kunaswa na "golden plates" zinazokuwa kwenye ncha za minara hiyo.

Huwa pia kuna muunganiko wa minara hiyo kwa kutumia nyaya kwenye ncha zake, lengo ni ikiwa umeme utakuwa mkubwa kwenye mnara mmoja basi utasambazwa kwenye minara yote na kushushwa kwa urahisi ardhini.

Kama isingefanyika hivyo umeme ukiwa mwingi kwenye mnara mmoja, vyuma vya mnara huo vingeweza kushika umeme na kupiga 'shoti' mazingira yake ya karibu, ikiwemo vyombo vya anga.

Kwa ajili ya Radi kufikia minara kabla ya kupiga chombo cha anga, inatakiwa minara iwe mirefu kuliko kitu chochote pale kwenye Kituo cha kurusha vifaa vya angani.
Ikitokea mission inahitaji chombo kirefu na kikubwa kikakaribiana na urefu wa ile minara, basi minara huwa inaunganishwa na umeme 'mwembamba' ili mda wote iwe na charge za kuvuta radi.

Eneo la Launch Pad linakuwa na vyuma vingi, kemikali nyingi zinazoyeyuka na kupaa (volatile chemicals), kemikali nyingi zinakuwa kwenye mgandamizo (pressure) kubwa, gesi zikiwa kama vimiminika (Liquid oxygen, liquid hydrogen, Nitrogen nk), vinu vya umeme mkubwa, Winch, Loader, Motor na nyaya zinazobeba umeme mkubwa,

Kwa ufupi Launch Pad inakuwa ni eneo lenye umeme mkubwa, na Charge nyingi sana za umeme, kupigwa 'shoti' eneo lile ni kitu cha kawaida sana, hivyo ebwo hilo lina hatari kubwa sana ya kupigwa Radi tena radi yenye nguvu kubwa sana.

Kwa sababu hiyo, minara ya kukinga au kudaka radi inakuwa ni mikubwa sana, yenye vyuma na nyaya za Steel ama hata Aluminium kwa ajili ya kuhimili mikiki ya umeme wa Radi, kuhimili karibu Volt Laki 3 za umeme wa angani.
Unazifahamu 300,000 Volts wewe.!?

Siku nyingine tutaongelea Radi.
Usikose kumualika mwingine kwenye ukurasa huu, tugawane madini pamoja.

Gerald
Source: ELIMU YA ANGA By Cekay 🪐
FB_IMG_1666191314464.jpg

View attachment 2392115
 
Nilisikia kwenu bukoba Kuna mganga anauza radi, Hadi ya elfu 5 unapata
 
Chombo cha anga kikisharushwa, je, kuna operator atakayekiendesha kikiwa huko angani kama ilivyo kwa ndege, au kikirushwa kinajioperate chenyewe huku abiria wake wakiendelea na shughuli zingine kama vile kuchukua picha nk? Na je kikishamaliza kazi yake huko angani, kinashuka chini kikitanguliza kichwa au kinarudi kinyumenyume?
 
Back
Top Bottom