Roboti anayesafisha nyumba

Roboti anayesafisha nyumba

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2020
Posts
1,283
Reaction score
2,590
Kampuni ya roborock inayounda roboti mbalimbali za Teknolojia kwa shughuli za kibinadamu, hatimaye imeleta toleo jipya la Roboti aina ya Q5 pro na Q8 max yenye nguvu na Teknolojia kubwa kuliko zilizopita.

Q5 pro
Ni Roboti ambaye anajishughulisha na masuala ya Usafi unaweza kumtumia kwenye mazingira yoyote Yale Kwenye ardhi ngumu au nyepesi Kwenye (carpet au hard flooring).

Roborock-Q5-Pro.jpg


Yenyewe Ina mifumo miwili ya silicone kwa ndani ambayo inakupa nafasi ya kusafisha hata maeneo magumu uchafu hatq kama ikiwa mdogo kama mchangq inaondoa na kusafisha eneo lote.

Q5 pro inakuja na mop zake inakupa uwezo wa kuweka maji kidogo ndani ya huyo roboti yenyewe automatic inafanyq usafi bila hata kumgusa.

Utofauti wa Q5 pro na Q5 pro + Kwenye kusafisha na kubakishq eneo safi jinsi inavyokusanyq takataka na kuweza kuzifadhi ndani yake kwani Q5 pro + yenyewe inaweza kufanya Kazi wiki nzimq bila kuchoka wala kupungua chaji.

Nilichokipends zaidi wanafanya usafi kwa haraka sana ndani ya muda mfupi.
Gharama zake
• Q5 pro ni dollar 399
• Q5 pro plus (+) dollar yake ni 536 mpaka 599
 
Mbona zipo siku nyingi sana hizi robot na bei zake za kawaida sana, kampuni nyingi tu wanazo Xiaomi, Google etc.
 
Vp Kuhusu matumizi ya umeme
Za kawaida hizi kama watts 60 hadi 100, assume kinatumia masaa 3 kwa siku kusafisha kwa mwezi hata 3000 inaweza isifike ya umeme.

Na vinasafisha na kujichaji vyenyewe.

Kifupi mkuu kifaa kinacho tumia battery hakili umeme sana.
 
Back
Top Bottom