Zikomo Songea
JF-Expert Member
- May 15, 2016
- 670
- 580
Robert Mangaliso Sobukwe alizaliwa mjini Graaff-Reinet, Eastern Cape Province nchini Afrika ya Kusini mwaka 1924. Alijiunga na siasa za ANC mwaka 1948. Baada ya kuhitimu shahada ya kwanza katika Chuo Kikuu cha Fort Hare, Sobukwe aliajiriwa kama mwalimu wa sekondari na baadae kama mhadhiri wa Taaluma za Kiafrika (African Studies) katika Chuo Kikuu cha Witwatersrand.
Mwaka 1959, Sobukwe na wenzake kadhaa waliamua kuachana na ANC kutokana na kutoridhishwa na mambo kadhaa, kubwa likiwa ni siasa kiliberali za ANC ambazo zilikuwa zinaruhusu ushirikiano na Wazungu na watu wengine wasio Waafrika. Hawa walianzisha chama kipya cha siasa kilichoitwa Pan Africanist Congress (PAC), Sobukwe akiwa rais wake.
Itikadi kuu ya PAC ilikuwa ni kwamba Afrika ya Kusini ni nchi ya Waafrika (weusi) na kwamba Wazungu ni lazima wafukuzwe, tena ikibidi, kwa nguvu (si kwa kujadiliana). Inasemekana pia kuwa kilikuwa kinapokea msaada kutoka Marekani ili kuidhoofisha ANC ambayo Wamerekani hawakuipenda kutokana na mafungamano yake na chama cha Kikomunisti cha Africa ya Kusini (South African Communist Party).
Mara baada ya kuanzishwa kwake, PAC ilivutia wanachama wengi na kufanya chama hiki kuwa ndicho chama hasimu cha African National Congress. PAC, chini ya Sobukwe, ikatangaza kuanza maandamano ya nchi nzima kupinga sheria ya kubeba "pass". Maandamano haya yalipangwa kufanyika tarehe 21 Machi 1960. Ikumbubwe kuwa mwezi Disemba 1959, chama cha ANC kilipanga kufanya kampeni hiyo hiyo tarehe 31 Machi 1960. Kwa hiyo tunaweza kusema kuwa lengo la PAC lilikuwa ni "kuwazidi kete" ANC.
Siku ya tukio, wanachama wote wa PAC, popote walipokuwepo nchini, walitakiwa kukusanyika na kuandamana bila kubeba "pass" kujipeleka kituo cha polisi kilichokuwa jirani. Lengo lilikuwa kujaza vituo vya polisi kwa mahabusu. Viongozi wa chama walitakiwa kuwa mstari wa mbele katika maandamano (ilikuwa nimeikosa kwa kiongozi kuonyesha dalili za woga).
Katika eneo la Sharpeville, Johannesburg, Sobukwe na wenzake walianza maandamano kujipeleka Kituo cha Polisi cha Orlando. Kilichofuata baada ya hapo ni sintofahamu. Mashuhuda wanasema kuwa polisi waliwafyatulia risasi za moto wanachama waliokuwa wakiandamana kwa amani, bila salama. Kwamba polisi walipata hinu baada ya kuona kundi kubwa sana la watu. Duru za "kiintelijensia" za polisi zilidai kuwa polisi walikuwa wakijihami dhidi ya waandamanaji waliokuwa wameanza kuwashambulia kwa mawe.
Katika tukio hilo, watu 69 waliuawa kwa kupigwa risasi mgongoni walivyokuwa wakitawanyika. Hayo ndiyo yanayoitwa Mauaji ya Sharpeville au "Sharpeville Massacre." Wengine takribani 80 walijeruhiwa na 18,000 walikamatwa.
Matukio yaliyofuata baada hata hapo yalibadili kabisa uelekeo wa kisiasa nchini Afrika ya Kusini. Vyama vya PAC
na ANC vilipigwa marufuku na viongozi wake kukamatwa. Sobukwe akahukumiwa kiungo cha miaka mitatu (1960-63) jela. Baadae akaongezewa miaka sita mingine hadi 1969 chini ya kifungu cha sheria cha Sobukwe (Sobukwe Clause). Hata baada ya kutoka jela Sobukwe aliendelea kuwa kuzuiliwa Kimberley hadi alipofariki mwaka 1978.
Mapambano hayakukoma bali yalichukua sura mpya ya mapigano ya silaha. PAC ilitumia kikosi chake cha kijeshi kilichoitwa "Poqo" kama ambayo ANC walivyokuwa kikosi chake cha "Umkhonto we Sizwe" yaani Mkuki wa Taifa. Lakini kufikia 1964 serikali ilifanikiwa kuzima harakati za ukombozi walau kwa muda wa kama miaka kumi kabla ya harakati mpya za watu kama Steve Biko na wengine kuanza wazi wazi miaka ya 1970.
PAC (na ANC) iliruhusiwa tena kuendelea na siasa mwaka 1990 kama sharti mojawapo la kuanza majadiliano kati ya serikali na wapigania uhuru. Mwanzoni PAC ilikataa kushiriki katika mazungumzo ya amani chini ya "Convention for a Democratic South Africa" (CODESA). Lakini waijiunga nayo wakati mazungumzo hayo yanaelekea ukingoni mwaka 1994.