Kilichotokea Afrika Kusini ni Kama Uchaguzi wa Tanzania Mwaka 1995 na 2015

Kimalingano

JF-Expert Member
Mar 27, 2023
479
629
Nimefuatilia kidogo kilichotokea Afrika Kusini nikakumbuka hoja ya Baba wa Taifa kuwa mpinzani wa kweli wa kisiasa Tanzania, atatoka ndani ya CCM.

Mwaka 1995 Lyatonga Mrema (RIP) alipojitoa CCM alitoa upinzani mkubwa sana dhidi ya CCM. Pia Lowasa mwaka 2015 alipunguza ushindi wa CCM alipogombea dhidi ya CCM.

Na ndicho kilichofanyika Afrika Kusini kwenye uchaguzi wa safari hii. Uchaguzi wa mwaka 2019, ANC kilipata 57.5%, DA 21% (chama cha wazungu), na cha Malema kilipata 11%.

Uchaguzi wa mwaka ANC kimepata 40%, DA 22%, na cha Malema kilipa 9%. Chama kipya cha Zuma (MK) kimepata zaidi ya 14%. Hii ni sawa na upungufu wa wastani wa 17.5% kwa upande wa ANC. Maana yake vyama pinzani na ANC vilivyokuwepo havijaonesha kuongeza upinzani wa maana; Chama cha wazungu kimeongeza 1% tu na chama cha Malema kimepungua kwa 2%. Ni Zuma ndiye aliyesababisha ANC kushuka.

Maana yake bila Zuma kuhamia upinzani, ANC ingeendelea kutamba.

Pia soma Kuelekea 2025 - Huko Afrika Kusini ANC imepigwa kipigo cha mbwa mwitu kwenye Uchaguzi. Je, huku kwetu CCM watakubali Uchaguzi Huru na wa Haki?
 
Nimefuatilia kidogo kilichotokea Afrika Kusini nikakumbuka hoja ya Baba wa Taifa kuwa mpinzani wa kweli wa kisiasa Tanzania,atatoka ndani ya CCM.

Mwaka 1995 Lyatonga Mrema (RIP) alipojitoa CCM alitoa upinzani mkubwa sana dhidi ya CCM.Pia Lowasa mwaka 2015 alipunguza ushindi wa CCM alipogombea dhidi ya CCM.

Na ndicho kilichofanyika Afrika Kusini kwenye uchaguzi wa safari hii.Uchaguzi wa mwaka 2019,ANC kilipata 57.5%, DA 21% (chama cha wazungu), na cha Malema kilipata 11%.

Uchaguzi wa mwaka ANC kimepata 40%, DA 22%, na cha Malema kilipa 9%.Chama kipya cha Zuma (MK) kimepata zaidi ya 14%. Hii ni sawa na upungufu wa wastani wa 17.5% kwa upande wa ANC. Maana yake vyama pinzani na ANC vilivyokuwepo havijaonesha kuongeza upinzani wa maana; Chama cha wazungu kimeongeza 1% tu na chama cha Malema kimepungua kwa 2%. Ni Zuma ndiye aliyesababisha ANC kushuka.

Maana yake bila Zuma kuhamia upinzani, ANC ingeendelea kutamba.

Pia soma Kuelekea 2025 - Huko Afrika Kusini ANC imepigwa kipigo cha mbwa mwitu kwenye Uchaguzi. Je, huku kwetu CCM watakubali Uchaguzi Huru na wa Haki?
Punguza uongo wa kijinga. ANC ingetambaje ?. Zuma amepata ngekewa kwa sera yake ya kutaifisha Migodi na kuwapa weusi. Kule wanafuata sera na sio Mkumbo Kama bongo.
 
Malema ameshuka kutokana na sera yake ya open borders ambayo haikupokelelwa vizuri na wapiga kura.
 
SA na Tz hazilingani kabisa. Ni porojo kulinganisha mambo ya ANC na CCM.

ANC ushindi wake kuongezeka au kupungua ni uhalisia wa kura inazopata. Mfumo wa uchaguzi wa SA ni free and fair. Kuna tume huru ya uchaguzi na mfumo wa mahakama ulio huru kabisa. Chaguzi zao zinachambulika kikamilifu na wadau wote kwa facts and figures to the fine details katika mchakato mzima wa uchaguzi.

CCM ni chama dola. Ushindi ni lazima. Hautegemei kura wala haupimiki. Hauna uhalisia kwa matokeo ya kura. Rais na dola yake ndio wanaoamua CCM ishinde kwa kiwango gani (kura ngapi) na majimbo gani/mangapi ya uchaguzi. Hakuna mdau yoyote mwenye access na mwenendo wa mchakato wa uchaguzi. Taarifa zake ni zile zinazotolewa na tume ya uchaguzi kwa nyakati wanazooamua na hazihojiwi popote. Ni uhaini kuhoji.
 
ANC 🇿🇦 & CCM 🇹🇿 vyama vikongwe barani Africa, utofauti wa vyama Hivyo ni style ya kubaki madarakani. Mmoja amechagua njia ya kidemokrasia kubaki madarakani mwingine nguvu ya Dola ndiyo turufu Pekee aliyonayo ya kumbakiza madarakani.
 
Kwanini umtazame zuma badala yakutazama wapiga kura kama wao ndio wamesababisha hilo baada yakuona kuna haja yakutafuta mabadiliko nje ya ANC.Kwakifupi nikwamba huo ni mwanzo wa mwisho wa ANC.kiu na chachu ya mabadiliko inakua kwa kasi sana.Ata kwa Ccm ni swala la muda tu.
 
Back
Top Bottom