Robert Heriel na Mshana Junior wapewe tuzo za heshima

monde arabe

JF-Expert Member
Oct 22, 2017
8,490
13,022
Habar za muda huu Mabibi na Mabwana

Kabla sijaanza kuandika kiini cha thread hii naomba ifahamike kuwa mimi Monde Arabe siyo Chawa wa mtu yeyote wala sitegemei kuuza utu wangu kwa kuwa Chawa wa mtu yeyote (natosheka na afadhali sihitaji zaidi) Pia,sijawahi kuwasiliana na wahusika niliowataja kwenye title ya thread hii

Ndugu zangu Wanajamii Forums pamoja na uongozi wa Jamii Forums naombeni sote kwa pamoja tuutambue mchango chanya wa watu hawa wawili (Robert Heriel a.k.a Taikon wa Fasihi na Mshana Junior).

Watu hawa wawili wameisaidia jamii ya wenye uhitaji na wasio na uhitaji,matajiri na masikini,waliosoma na ambao hawajasoma, watawala ma watawaliwa na makundi mengine kwenye jamii.Wameandika vitu vingi na muhimu kwenye ulimwengu wa roho, kwenye uchumi, kwenye siasa, kwenye elimu, kwenye mahusiano na ndoa na kwenye angle nyingine ambazo zinagusa maisha yetu ya kila siku wamefanya hivyo pia.

Waswahili tuliowengi hatuna ustatabu wa kutambua,kuthamini na ku-appreciate potentially iliyopo kwa wanadamu wenzetu pindi wanapokuwa hai. Robert Heriel na Mshana Junior maandiko yao na falsafa zao zimewasaidia watu wengi sana na bado zitaendelea kuwasaidia watu wengi kwa kizazi kinachoishi kwa hivi sasa na kwa vizazi vijavyo. Hawa ni manabii ambao hawapo kwenyw Qur'an tukufu wala Biblia takatifu lkn,fikra zao ni dira na ni mwanga pia

Naomba watu hawa wapewe heshima wanayostahili tangu sasa,naomba watu hawa ikiwezekana waanzishiwe jukwaa lao maalum au wapewe degree za heshima (Honorable Causa) ikiwa ni ishara ya kutambua michango yao kwenye Forum hii na kwenye jamii pia

Sisi wanadamu tukishindwa kuuzungumza ukweli basi hata mawe, mimea, Mbingu na nuru zitazungumza kwa niaba yetu.

Vilevile, hata ninyi serikali mnaweza kuwatumia watu hawa kwa maslahi mapana ya Taifa letu kwa kuwa wanavyo vitu vya ziada ambavyo vinaweza kuwanufaisha Watanzania wote endapo watapata platform ya kuweza ku-transform fikra zao into fiscal world releam kama vile U-DC, U-DED na nafasi nyingine nyeti ndani ya serikali

Asanteni na Mungu awabariki sana!
 
Habar za muda huu Mabibi na Mabwana

Kabla sijaanza kuandika kiini cha thread hii naomba ifahamike kuwa mimi Monde Arabe siyo Chawa wa mtu yeyote wala sitegemei kuuza utu wangu ....
Nakubaliana na wewe, tukiondoa mapungufu madogo ya kibinadamu hawa jamaa wanamchango mkubwa sana ktk maandiko yao hapa JF, wanastahili recognition fulani.

Maandiko yao mengi yana ile tunaita lishe ya ubongo ni watu wenye maarifa kwakweli, so tumuombe bwana Melo awaandalie udaktari wa heshima kutoka JF.
 
Robert na nyuz zake za kugandamiza wanawake hatutakii
Kwakweli boby yupo kama tapeli na tangu aanze kupata foleni kwenye nyuzi zake ni kama anajiona ana akili kuliko wengineo wote humu ndani, kuna mkaka flani alikuwa anajita lastborn wa jf, nae alipoanza kusifiwa akajaa bichwa ila wadau walivyomtupilia mbali akapotea,

Mshana huwezi kumfananisha na huyo tapeli
 
Kwakweli boby yupo kama tapeli na tangu aanze kupata foleni kwenye nyuzi zake ni kama anajiona ana akili kuliko wengineo wote humu ndani, kuna mkaka flani alikuwa anajita lastborn wa jf, nae alipoanza kusifiwa akajaa bichwa ila wadau walivyomtupilia mbali akapotea,

Mshana huwezi kumfananisha na huyo tapeli

Huyo last born ni nani 😂😂😂
 
Mshana yuko juu. Robert hapana kwa kweli. Kwanza ameathirika na mfumo dume, halafu anaamini mawazo yake yako sahihi kuliko mtu yeyote kitu ambacho sio cha kweli hata kidogo. Huyu sio wa kutambulia kwa namna mtoa mada anavyofikiri....Hapana
 
Back
Top Bottom