Roadmap 2026: Siasa za utakaso. Utu wa Kale

Roadmap 2026: Siasa za utakaso. Utu wa Kale

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
34,059
Reaction score
79,416
ROADMAP 2026: SIASA ZA UTAKASO. UTU WA KALE.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

1. Leo ni January Moja 2026.
2. Namshukuru MUNGU kwa kutupa nafasi hii. Wote mnajua jinsi mwaka uliopita 2025 ulivyokuwa mwaka mgumu na mbaya katika maisha yetu. Ulikuwa mwaka wa Damu.

3. Sasa mwaka 2026 umeaanza rasmi. Na hii kwetu iwe nafasi ya pekee kuimarisha mahusiano yetu ya kindugu, kijamii na kitaifa.

4. 2026, Mwaka wa Utakaso. Kujitakasa. UTU WA KALE.

5. Wale Power monger ambao wapo tayari kuua wengine kwaajili ya madaraka na vyeo vyao. Mwaka 2026 ni mwaka wa utakaso. Siasa za utakaso. Ili ule utu WA kale ambao tuliumbiwa nao urejee.

6. Yeyote ambaye hataki utakaso alaanike. Mimi kama mtibeli nailaani nafsi hiyo isiyotaka Utakaso. Isiyotaka utu WA kale.

7. 2026 Utakuwa Mwaka mtulivu. Na utulivu huo utaturejesha kwenye umoja na mshikamano.

8. Hatutaki Utekaji. Wala ukamataji WA polisi usiofuata Sheria. Utakaso kwenye vyombo vya usalama.

9. Tundu Lisu atolewe upesi kabla ya tarehe 15 January. Baada ya hapo hata akitolewa haina maana yoyote. Mimi kama Mtibeli kiona Mbali kwa nia safi, njema niliomba mwaka Jana. Aachiliwe. Lakini nilipuuzwa. Of course kama kiona mbali nilihusishwa kufahamu rohoni nin kinaweza kutokea. Na sasa tena Kwa Nia ileile safi na njema. Naomba Tundu Lisu aachiliwe kabla ya tarehe 15 mwezi huu January.

10. Huu ni mwaka wa utakaso, siasa za utakaso. Utu wa kale.

11. Naomba asitokee mtu yeyote kwa kiburi chake akapinga kutaka kuona nini kitatokea. Hata mimi sijui. Mambo ya rohoni hayaeleweki kwa akili za kawaida.

12. Tunataka mambo yakae Sawa. Kila MTU awe mnyenyekevu katika Haki na Utu.

13. Tunataka tujenge Nchi yetu kwa Amani. Bila hasira na chuki vifuani mwetu. Bila hofu na kuviziana.

14. Mwezi march iandaliwe tukio la kuwaenzi, kuomba Toba, kuwakumbuka mashujaa wote waliouwa MO29. Ni vijana wetu. Ni ndugu zetu. Makosa yalifanyika.

15. Walitaka ukombozi wa taifa Lao Kwa maandamano makubwa. Sasa tuwaenzi kwa kuwapa na kuwaonyesha tuliwasikia. Na ukombozi huo uonnyeshwe katika maeneo Makuu yafuatayo;
a) Utawala bora wa Sheria.
Hili lilikuwa lalamiko Lao kuu. Na mchakato wa katiba mpya utangazwe kuanza hata kama utaanza rasmi mwezi mwingine.

b) Uhuru wa kutoa maoni
Wapinzani na wanaharakati watoe maoni Yao Kwa kufuata Sheria za haki bila kufanyiwa matendo ya kihalifu na vyombo vya dola.

c) Watuhumiwa kutendewa haki kwa mujibu wa Sheria
Sio mtu unamkamata Leo unamshtaki wiki ijayo. Ukamataji usiofuata Sheria. Watuhumiwa kunyimwa haki zao za msingi baada ya kukamatwa.

d) Uwajibikaji kwa viongozi.
Kiongozi awajibike yeye binafsi kabla wengine hawajamuwajibisha. Kujiudhulu iwe utamaduni.

16. Maridhiano baina ya Wauaji na waliouliwa ndugu zao.
Yasiwe maridhiano ya kisiasa. Sijui yataandaliwa vipi lakini hayo maridhiano lazima yafanyike. Mtu Fulani atauliza yasipofanyika utafanya nini au itatokea nini? Jibu lake kitakachotokea ni kinyume cha Siasa za utakaso, na kinyume cha utu wa kale. Itatokeaje? Utaelewa tuu.

17. Nataka niwaambie bado tuna nafasi ya kuweka mambo sawa. Na nafasi hiyo inahitaji jitihada za makusudi kabisa kwa Kila mmoja wetu kuonyesha Nia na matendo ya kutuweka pamoja.

18. Tusifanye maridhiano huku watu wameficha bunduki na mawe.

19. Nawaambia mwaka huu ni mwaka wa utakaso. Siasa safi. Utu wa Kale.

20. Utakuwa mwaka mtulivu Sana.

21. Nafahamu kuna watu wanataka na kuombea kusiwe na siasa za utakaso. Na wanawaombea viongozi na vyombo vya Dola visifanye kazi kwa weledi. Vionee watu kwa kujifanya vinalinda nchi lakini nchi hailindwi kwa uonevu na dhulma.

22. Kuna watu wanataka na kutamani serikali iendelee kufanya matendo ya kihalifu, ukandamizaji na dhulma ili mambo yazidi kuwa mabaya.

23. Serikali na vyombo vya dola lazima wajue. Ndio sio hiyari. Lazima wajue kwamba kadiri wanavyotenda matendo ya kihalifu na dhulma wanatimiza malengo na mipango ya watu hao.

24. Serikali haiwezi kunufaika popote kwa Kuteka na kuua na kudhulumu baadhi ya watu. Serikali inanufaika kwa kufuata Sheria na utawala Bora.

25. Nakuhakikishia kuna watu watachukia watakapoona serikali inatakasika. Kwa sababu malengo yao hayatatimia.

26. Soma kisa cha mwanampotevu.

27. Adui zako hufurahia Sana unapokuwa mtu mbaya kuliko ukiwa mwema. Mfano kama wewe ni Mhalifu, muovu, watajifanya kukupinga na kuusema ubaya wako sio ili ubadilike. Bali wanafurahia kukusema kwa ubaya.

28. Mtoto wako akiwa mwizi. Adui zako watamsema kwa WIZI sio ili abadilike Bali ni kwa sababu wanajua hata yeye mwizi mwenyewe huumia kuitwa mwizi au kufanya wizi. Wazazi wake huona wamepata hasara na laana.

29. MTU mbaya akiacha mabaya watu wengine huchukia kwa sababu watakosa ubaya wa kumsema.

30. Unapoamua kuwa mwema, wabaya wako wataendelea kukutambua na kukuita kwa ubaya ulioutenda ili wajisikie vizuri lakini pia ili ukasirike urudi kwenye ubaya wako.

31. Kuungama na toba ya kweli ni muhimu. Na NIA ya dhati inahitajika.

32. Ungamo takatifu ni lile linalofanywa mtu akiwa na nafasi tena ya juu. Sio ungamo la MTU aliyefilisika au asiye kwenye nafasi.

Nawatakia mwaka mpya mwema. Nimefurahia kuwaona.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
 
Hakuwezi kuwa na maridhiano bila wauaji kujulikana na kuchukuliwa hatua za kisheria. Wenye mamlaka hawapo tayari huku wakitaka kukifanyia dressing kidonda kinacho hitaji mshono na antibiotics za kutosha.
 
Kwa hali iliyofikia saizi kwa watanzania na maumivu waliyonayo moyoni ni ngumu kukuelewa!, kuna kazi ya ziada kuwa rudisha na kuwaponya wakawa watanzania wa kabla ya tar 29/10.
 
Unalamba lolo kidogo halaf unakandia kidogo

Sifa kuu za wanafiki, ukiwa moto uwe moto na ukiwa barid uwe barid
 
Hakuwezi kuwa na maridhiano bila wauaji kujulikana na kuchukuliwa hatua za kisheria. Wenye mamlaka hawapo tayari huku wakitaka kukifanyia dressing kidonda kinacho hitaji mshono na antibiotics za kutosha.

Sahihi.
 
Back
Top Bottom