Don san tan
JF-Expert Member
- May 23, 2015
- 575
- 443
- Thread starter
- #21
RIWAYA: HUJUMA 06
MTUNZI: richard R. MWAMBE
SHALABAH alitulia kitini akinywa taratibu kahawa yake. Gari moja nyeusi aina ya Toyota Nadia ilisimama mita chache kutoka pale alipokuwa ameketi. Mwanamke mrefu akateremka, aliyevaa kininja, akavuta hatua ndefundefu mpaka pale alipoketi, akavuta kiti na kukaa.
“Sina maneno mengi, ila unajua kuwa nimekwsihamaliza kazi uliyotaka nifanye, nimefata hundi yangu,” Fasendy akamwambia Shalabah.
“Usijali, niliketi hapa kukusubiri wewe, ili kukukamilishia malipo yako lakini pia kuna kazi nyingine ya kufanya,” Shalaba akamwambia Fasendy huku akimpatia bahasha nyeupe ambayo ndani yake kulikuwa na hundi hiyo. Akaifungua na kutazama akaiona ni sawa, akaifutika ndani ya nguo yake.
“haya, ongea linguine,” Fasendy akamwambia Shalabah.
“Nifuate,” Shalabah akamwambia Fasendy kisha akanyanyuka na kuingia ndani ya jengo hilo lililoonekana kama gofu, lililotelekezwa kwa muda mrefu sana, wakapita koridoni mpaka kwenye moja ya chumba, wakaingia na kukatiza milango kama mitatu hivi, mlango wan ne ulikuwa mlango wa kioo safi uliozungukwa na kamera za cctv ili kulinda usalama wa eneo hilo. Shalabah akabonya kitufe na mara mlango ule ukafunguka, wakaingia ndani.
Kilikuwa ni chumba kidogo lakini chenya kila kitu kinachohitajika katika ofisi yoyote duniani. Shalabah akamkaribisha Fasendy na wote wawili wakaketi katika viti vyenye vono safi. Katika meza iliyokuwa mbele yao kulikaliwa na mtu mmoja mnene mwenye mwili mkubwa aliyejaa katika suti kali nyeusi, kichwa chake kilionekana kuungana na kiwiliwili, hakuonekana shingo yake kama ilikuwepo au ilimezwa na unene huo.
“Karibu sana mwanamke,” akamkaribisha Fasendy, akajikohoza na kuendelea, “ kwanza nikupongeze kwa kazi ngumu nay a hatari uliyoifanya ya kutuletea wale watu wawili wanaojifanya kufuatilia nyayo za samba. Nafikiri malipo yako umeshayapata, lililobaki huku mbeleni tuachie sisi tunajua cha kuwafanya, lakini nina jambo moja, hawa Watanzania wakishaona wenzao hawapatikani kwa mawasiliano kwa vyovyote watatuma mtu mwingine au watu wengine kuja kuwatafuta, sasa nataka nikupe kazi nyingine ya mkataba wa miezi mitatu, ya kuhakikisha kila anayeingia hapa ni kumpoteza moja kwa moja kama tulivyofanya kwa wale Waamerika waliojifanya waandishi wa habari, upo tayari?” yule mtu akauliza.
“Wewe unajuaje kama watatuma watu wengine?” Fasendy akauliza.
“Mimi najua, ninalokwambia ndilo hilo, kumbuka tuna wanajeshi wao ishirini na tano, na hawa wawili, unafikiri watavumilia? Tunataka kuhakikisha biashara yetu inakwenda safi kabisa,” yule Bwana akamaliza.
Fasendy, akatulia kimya akiitafakari uzito wa kazi hiyo.
“Sawa, hamna tabu,” akajibu Fasendy. Yule mtu mnene akasimama na kumpoa mkono Fasendy kisha akamruhusu aende. Shalabah akamsindikiza hadi nje na kuagana naye.
“Sharon,” yule mtu mnene akaita. Sharon akajitokeza kutoka katika mlango Fulani pembenzoni mwa chumba kile, akasimama akisikiliza, “Boss ansema uhakikishe wale mateka wawili wanajutia walichokifanya na upeleke onyo kali kwa waliowatuma, kisha simamia biashara nzima, wateja wetu wamesema watakuja baada ya siku tatu kuangali makombora yaliyobaki, kama kuna shida yoyote wasiliana na Shalabah, yeye ndiye mwenye uwezo wa kuwasiliana na mimi na Mr Lonely kwa utatuzi wa mwisho,” yule Bwana akamaliza na kuagana na watu wake, kisha akabaki yeye na Shalabah tu.
§§§§§
MOQDISHO TEXTILE
Jamil alikuwa amefungwa kamba na kuning’inizwa kichwa chini miguu juu, hakuweza kufanya lolote kwani pembeni yake alikuwa akilindwa na vijana wawili wadogo waliokuwa na silaha za maana zilizodungwa mkanda mrefu wa risasi, hawakuona taabu kummiminia yeyote atakayeleta shida katika himaya hiyo. Walikuwa ni vijana wawili wenye kukadiriwa umri wa miaka kumi na tano na kumi nane. Vinywani mwao waote walikuwa wanakula mirungi. Jamil aliwatazama kwa zamu ili aone kama kuna jinsi ya kujiokoa lakini hali ilikuwa siyo, kwa kuwa mlango wa chumba hicho ulikuwa ni wa chuma madhubuti kabisa. Jamil alitulia palepale huku akiwaza ni wapi Gwamaka atakuwapo kwani alimuacha hotelini.
Mara mlango ukafunguliwa, Sharon akaingia ndani na vijana wengine wawili waliovaa kiraia lakini wakiwa na silaha nzito. Jamil aliona wazi hawa jamaa hawajui matumizi ya silaha kwamba silaha hii nitumia vitani na sio kutembea nayo nah ii nitumie wapi, ilikuwa haishangazi kumkuta mjini au sokoni begani mwake amejitwika RPG huku akitalii akitazama hili na lile.
“Mfungue, umtoe hapa,” Sharon aliamuru, kijana mmoja akaja na kisu na kukata kamba iliyofunga miguu ya Jamila, akaanguka na kutanguliza kichwa, akajipiga kwenye sakafu na kubwagika chini kama mzigo. Jamil akatoa mguno hafifu wa maumivu, kisha akatulia kimya. Wakamfungua kamba za miguu na kumuinua, akasimama wima lakini akiegemea ukuta maana alikuwa akisikia kizunguzungu cha hali ya juu.
Sharon akamsogelea Jamil.
“Komandoo, koamndoo utakuwa wewe? Hiyo serikali yenu bora iombe msaada niwape hawa watoto wawili tu ni sawa na vikosi vyenu kumi vya kijeshi, na sasa utajuta, kukamatwa na sisi, sisi hatuna serikali kwa taarifa yako, na sasa utaenda kushuhudia ndugu yako anavyouawa na hiyo ndiyo salamu kwa serikali yako, mataifa ya magahribi yameshindwa itakuwa ninyi, ninyi ni nani hata mjifanye mna uchungu?” Sharon alimwambia Jamil, alipomaliza tu kusema akageuka na kuwaamuru watu wake kumuongoza Jamil upande wa pili wa jengo. Wakamto ilhali akiwa na kamba mkononi mwake.
Ulikuwa ni ua mkubwa sana wenye malori kadhaa yaliyokuwa yameegeshwa. Watu wenye silaha walikuwa wengi, vijana, watu wazima, walikuwa na silaha nzito nzito.
“Simama hapa” Jamila aliambiwa na wale waliokuwa wakimlinda, akasimama pamoja na watu wengine wawili, wazungu walioonekana kuchoka sana. Mara akachukuliwa mmoja wao na kupelekwa katikati ya ule uwanja, kelele zikaanza kusikika, kelele za mashangilio, huku wakipiga risasi hewani, yule aliyempeleka pale akachomoa jambia na kumkata shingo, akamchinja na kutenganisha kabisa kichwa na kiwiliwili. Kwa kitendo hicho wenzake wakashangilia sana, ilikuwa ni kama tafrija kwao. Jamil alishindwa kutazama kitendo hicho, aliinama na kufumba macho.
“Watu makatili sana hawa, sidhani kama ni binadamu wa kawaida,” Jamil aliongea kwa sauti ya chini. Kisha yule jamaa aliyemchinja yule mtu akaja kwa Jamil na yule mwingine, akasimama mbele yao.
“Burudani yetu ni kuwachinja watu kama ninyi, siku yenu bado,” akamaliza na kuondoka. Jamil na yule mwenzake wakachukuliwa na kufungiwa ndani ya chumba kisicho hata na dirisha isipokuwa tundu dogo kama shimo la panya lililoweza kuingiza hewa kwa tabu na mwanga kidogo sana.
Kufungiwa ndani ya chumba hicho kwa Jamil haikuwa mateso, bali kukaa bila kujua Gwamaka yuko wapi hilo ndilo lilikua teso kubwa kuliko yote, alibaki hivyo akitafakari bila jibu, hakuwa na jinsi ilimpasa kutulia.
3… Dar es salaam – Tanzania… saa 7:05 mchana
JUA kali la saa saba lilikuwa likichoma kwelikweli, mji wa Dar es salaam uligubikwa na joto kali, kila umuonaye kama hana kitambaa mkononi cha kufuta jasho basi alikuwa kifua nusu wazi ilimradi apate kaupepo hako kadogo. Lakini wote waliokuwa wakiteseka na joto hilo ni wale watu wa KCC yaani Kima Cha Chini, lakini kwa mwenye nazo daima jiji la Dar es salaam ni jiji lenye baridi sana kiasi kwamba kila muda anatembea na suti ya vipande vitatu.
Jiji linalosifika kwa uzuri na linalovutia watalii kwa historia yake ya utulivu na amani. Kila kijana wa Tanzania anaamini kuwa katikan jiji hilo ndiko maisha yanakoanzi hivyo huwafanya wengi kukimbilia huko ili kuanza maisha mapya wakiamini watatajirika. Lakini hali huwa tofauti sana wakifika katika jiji hilo, mwisho wake ndio vibaka, wabwia unga, makahaba kuongezeka katikati ya jiji na kwenye viunga vyake. Ijapokuwa kila mara wanasomba na polisi na kuwekwa mahabusu lakini wakitolewa tub ado huendelea na shughuli zao hizo hizo wanaacha kwenda vijijini wakawekeze katika kilimo na ufugaji, lakini siwalaumu wao, ila nailaumu serikali inayoshindwa kuwawekea mafunzo thabiti ya ujasiriamali tangu wakiwa shule ya msingi, hata somo la sayansi kilimo lililokuwapo shuleni siku hizi hata haliko katika mitaala, basi waache vijana wajikimbilie mjini na taifa kuwa taifa la vibaka.
Katika ofisi ya wizara ya ulinzi na jeshi lakujenga taifa, Mwenge, Mlalakuwa hali ya utulivu ilikuwa imetawala, ni bendera tu ya Taifa iliyokuwa ikipepea huku na huko kadiri ya upepo ulivokuwa ukiitaka. Geti lilifunguliwa taratibu na mwanajeshi aliyekuwa lindoni siku hiyo.
“Kuna mzigo wenu hapa,” kijana mmoja aliyekuwa juu ya pikipiki aina ya Yamaha alikuwa akiwaambia walinzi hao.
“Ok, nenda mlango ule pale kuna mwanadada pale mkabidhi,” yule MP akampa maelekezo baada ya kusoma anwani na kukuta imeelekezwa katika ofisi ya waziri mwenyewe.
Katibu muhtasi wa wizara, Miranda, alisaini kitabu cha dispatch cha kijana huyo kamba ameupokea mzigo huo katika hali ya usalama. Kisha wakaagana.
Kilikuwa ni kikasha cha mbao, kilicho tengenezwa vizuri na kupigwa vanish safi, pembeni anwani yake ilikuwa imeandikwa kwa maandishi ya chuma yaliyokuwa yaking’aa sana, na kwa sababu kilikuwa na anwani ya ofisi haikuwa tabu kwa Miranda kukifungua kujua ndani kuna nini kwa kuwa ni mzigo wa kiofisi, akachukua kijinyundo kidogo na kubabazua mfuniko wa kikasha hicho nao ukafunguka, ndani yake akakuta kitu kama box hivi, alipoligusa lilikuwa la baridi kama lina barafu ndani yake, akaondoa gundi iliyofunga box hilo na kulifungua ndani, huko akakuta kasha maalum sililoruhusu barafu kuyeyuka akaondoa mfuniko wake.
“Aaaaaaaaaaaaaaaiiiiiiiiiggghhhhhhhhh!!!!!!!” ilikuwa ni kelele moja kali kutoka kwa Miranda, mara ikakatika ghafla na kishindo cha kikasikika, Miranda akaanguka na kupoteza fahamu.
Mp aliyekuwa getini alisikia kelele ile na ukinya uliofuata akamwachia mwenzake lindo akakimbia kutazama kuna nini, alipoingi alimkuta Miranda chini hana fahamau, akaomba msaada haraka na wengine wakatoka maofisini kuja kumsaidia kwa huduma ya kwanza, hakuna aliyejua ni nini kimeamfanya aanguke. Ni pale mwanajeshi mmoja aliposogelea lile box akabaki kaduwaa, kinywa wazi. Hakutaka kuyaamini macho yake kwa kile yanachokiona. Kichwa cha binadamu, kichwa cha Gwamaka kilikuwa kimetulia ndani ya box lile, hakuongea kitu alitoka nje na kulia sana. Kila aliyeingia ndani ya ofisi hiyo alitoka akilia kwa uchungu…