Riwaya: Upepo wa usiku-1

Riwaya: Upepo wa usiku-1

UPEPO WA USIKU-15
BONIFACE BIRAGE

Ilikuwa damu ya nini?Mama mkwe bado hakujua.Kuona damu katika mazingira kama yale yalimpa mawazo mengi.Kimuhemuhe kilichomgusa moyo kikamfanya aufungue mlango wa chumbani akaingia.Alianza kukagua kile chumba akifuata pale alipohisi alikanyaga damu.Moyo ulimuenda kmbio kwa hofu!Alipotizama akaufuata mchirizi huo wa damu ambao bado ulikuwa mbichi kabisa.Ilielekea chini ya mvungu.Mama mkwe akasita kidogo nakurudi hadi ukumbini kwa haraka hata kabla hajaangalia chini ya mvungu kuna nini?

Huku maswali yakizidi kupanda.

“Damu za nini?”alijiuliza.

“Tena zinaelekea chini ya mvungu!Au ndo kwasababu anaonekana wa ajabu ajabu kama mtu anayelia?”alijiuliza asipate jibu.Alipokuwa pale alisikia kama simu inayounguruma kwa mtetemeko.Ukimya uliokuwepo ulimpa fursa ya kusikia chochote kinachoendelea mule ndani.Akasogea nakuichukua ile simu.Alikuwa mama wa kisasa hivyo vitu vya kiteknolojia havikumsumbua jambo lolote.Akaikagua aliona namba ngeni lakini hakupokea.Simu ilikata na bila shaka kulikuwa na msururu wa ujumbe mwingi uliokuwa umetumwa kwenye simu pamoja na simu nyingi ambazo zilipigwa bila kujibiwa.Kwenye kioo cha simu aliona picha ya Hamza pamoja na Laredo wakiwa katika pozi la busu ambalo usingesema shemeji atakaa na shemeji mtu!Mama mkwe alikuwa mdadisi alipekua kwenye simu jumbe nyingi alizoona zilikuwa za kawaida hasa lawama kwamba Hamza anapigiwa simu lakini hapokei.Mama akapekua tena kwenye picha za simu.Alifanya hivyo baada ya kuona picha ikiwa imehifadhiwa kwenye kioo cha simu kati ya Laredo na Hamza alitaka kujua kuna picha ngapi nyingine zina utata!Halafu kama Hamza kasafiri kwanini simu ipo hapa tena imewashwa na kuna simu nyingi zimeingia bila kupokelewa?

Alipofika kwenye faili la picha mama mkwe alichanganyikiwa.Alikuta picha nyingi lakini asilimia kubwa za picha zilikuwa kati ya Laredo na Hamza.Mara wakiwa katika maeneo ya faragha.Picha za selfie na nyingine zikionesha Laredo akiwa mtupu bila shaka picha hizi zilichukuliwa wakiwa pamoja maeneo yenye hatari sana.Hilo halikukwepeshs wazo kwamba kuna kitu kati ya Laredo na shemeji yake!Mama mtu akameza jambo hilo akingoja wasaa wakulitapika vilivyo.Aliendelea kukagua picha hilo moja baada ya nyingine.Mazingira ya picha zile yalipigwa ndani ya nyumba ile!Chochote kilichofanyika lazima kilikuwa kwa uwazi mpaka hatua ya kupiga picha ilimpa uhakika kwamba hakuna mzaha kati ya Hamza na mke wa kaka yake!

Mama mkwe akatoka hadi nje ya chumba kile.Alipokuwa anatizama huku na kule alisikia tena simu nyingine ikiita!Moyo ukapiga paa!Alifuata mlio ulitokea dirishani kwenye chumba cha Masua!Kwa kuwa alimjua mpangaji huyo aliamua kwenda hadi dirishani hapo akachungulia lakini hakuona mtu zaid simu ilikuwa kwa dirishani ni kiasi cha kupenyeza mkono nakuitoa!Akaichukua!Alipotizama kwenye kioo akashtuka!Ilibidi akimbie ndani.

Kwenye kioo cha simu kulikuwa na picha ya Laredo na Masua wakiwa katika pozi la mahaba!Katika kukagua picha ile aligundua fika kwamba halikuwa pozi la jirani kwa jirani lilikuwa zaid ya kawaida!Bila kufikiri sana alienda kwenye faili la picha huko nako alikuta vituko!Picha zilikuwepo kibao kati ya Laredo na Masua wakiwa katika pozi zenye kutilia mashaka wala usingewaza mara mbili kwamba watu hawa ni wapenzi!Mama mkwe aliduwaa!Alienda hadi chumbani tena huku akiwa na maswali lukuki.

“Inakuwaje anapiga picha za ajabu na shemeji yake hadi na jirani yake huku sikuutukanisha uke jamani?Huyu msichana si bure anatabia ya ajabu!”

Akiwa pale chumbani alipeleka upekuzi kwenye chumba kile moja ya picha akiwa na Hamza ilikuwa palepale chumbani mashuka na blanketi lilelile bila kubisha.Wasiwasi wa maswali hayo ukamfanya mama apeleke macho kitandani.Lakini ghafla akaona mchirizi wa damu kwenye shuka la pale kitandani ukiwa kwenye kingo za kitanda!Akafuata ni kama alama za mikono ya mtu aliyekuwa ameshika damu na tena ni kama aligusa kitanda bila kutarajia!.Ilibidi aende hadi uvunguni lakini kabla haja gusa kitu alisikia mtu kumsimamia kwa nyuma!

“Mama! “aliita Laredo hali iliyofanya mama mkwe kuinuka ghafla!

“Kuna nini umenishtua!”alisema akiwa kwenye mshtuko wa kukutwa.Laredo nusura moyo umpasuke maana kamkuta mama amechutama anataka kuchungulia uvunguni.Je,kama amesha chungulia?

“Nilikuwa na kwambia uje…eh!...Uje…”kigugumizi kikamshika!Lakini palepale mama akarudi kuchutama akaelekeza macho uvunguni.Akapeleka mkono nakugusa kitu!Moyo ulipigaa paa!Aligusa mguu ulianza kupoa!Ilikuwa ngozi ya mtu!Ilibidi auvute tena kwa nguvu akaona ni mgumu!Akavuta!Alijua bila shaka kuna mwanaume kafichwa huku nini?Hilo lilikuja baada ya kuona picha za ajabu ajabu kwenye simu mbili alizookota!Halafu likaja wazo lakuona damu!Vyote hivi vilikuja kichwani kwa haraka.Akauvuta mguu wote!Akakutana na maiti!Ni jinamizi bay asana kuwahi kumtokea.Lilimtisha na kumfedhehesha maisha yake yote!Mama huyu aliyekuwa na taaluma ya uuguzi ambaye kwa sasa ni mstaafu alijikuta akiinuka kwa haraka!Ulikuwa mwili usio na fahamu maana aliuvuta ukatokeza kutoka miguuni hadi kiunoni!

Laredo katumbua macho!Ilikuwa sadfa!Haikupangwa japo ipo siku mtu angezigundua maiti zile lakini sio kwa haraka vile!Palepale Laredo alijua fika kaumbuka!Atasema nini!

Hakuna mama asiyejua mwili wa mwanaye!Mama mkwe palepale aliutambua mwili ule!Ni wa mwanaye!Hamza!

“Mwananguuu!”alipika kite!Nywele za malaika zikamsimama!Ilibidi bimkubwa huyo ajishike kichwa kwa sekunde kama tano!Halafu akarudi chini nakuuvuta miguu!Akauburuza wote kutoka uvunguni!Alikutana na mwili wa Hamza!Ulikuwa kimya macho kayafumba!Mama aliduwaa!Ilikuwaje?Alienda hadi pale chini akamshika mkono kuhisi kama kulikuwa na mapigo ya mshipa!Balaa!Jambo likazuka palepale.Tumbo la uchungu alilolisikia miaka mingi iliyopita aliukumbuka uchungu huo katika fikra ya saikolojia nakuanza kuyahisi yale maumivu kwenye tumbo lake kwa kasi ya ajabu!Hapa kuna maiti ya mwana wake!Alipigwa na bumbuazi la uhakika!Akadata!Hiki ni kizaazaa!

“Mwanangu maiti!Uuuwii!...Hamza wangu wamekutendaje!..Nipeni shuka jamanii…nipeni shukaaa!...Nipeni shuka niliee uwii!”

Hakika ilikuwa huzuni kubwa sana!Mama alikuwa akilia kwa uchungu wa hali ya juu!Lakini katika kuuangalia mwili wa Hamza kulikuwa hakuna damu zaidi ya kama povu lililoganda kinywani nakuteleza kwenye kuta za shavu!Ile damu ilimfanya mama wa watu akiwa analia aingie chini ya uvungu tena!Akaona miili imerundikwa!Laredo alikuwa amekwisha!

Nguvu za kuvuta ile miili zikaisha pyuu!Alimgeukia Laredo aliyekuwa anatetemeka zaidi ya kifaranga kilicho mwagiwa maji!Alikuwa amefumwa!Hakuweza hata kumtizama mama mkwe wake vizuri!Alikuwa akigusanisha viganja vya mikono kana kwamba ananawa!Hakueleweka!

Mama mkwe alimshika kwa kumkunjanguo ya juu!Lakini mikono ya mama ilikuwa dhaifu sana alijikuta akimwachia huku kilio kikimshinda!Laredo naye alianza kulia ni kama bomba la machozi lilifunguliwa kati yao!Huyu analia kapoteza mwana,huyu analia kapoteza mume!

“Mwanangu kafa na nini?”aliuliza mama mkwe! Lakini ghafla kitu kika mwambia Laredo akimbie na atokomee!Mama kakuta maiti takribani nne katika chumba chake!Hilo tayari ni kosa!Inatakiwa polisi wa aitwe!Asingesema eti hajui miili hiyo kaitoa wapi?Tayari alishajikoroga kwenye majibu kuwa watu hawa wamesafiri wakati wameshauliziwa takribani mara kadhaa!Kwanza na mama mkwe!Pili mama Shully!Hii ni hatari kwa usalama wake!

“Niambiee…niambieeeee!...Wananguu wamekuwaje!...Mjukuu wangu mmefanyajeee!”alipiga kelele mama mkwe.Wote hawakuwa na pumzi.Laredo alitikisa kichwa kana kwamba hajui lolote!Alikumbuka vyema alivyofyetua risasi kwa kujihami lakini ikawa kosa akajikuta kampiga mwanaye!Alijikuta akilia tena!Alikumbuka pia usiku uliopita aliwaacha wanaume hao salama,kuja kuamka asubuhi anakutana na maiti.Bila shaka alishajua chakula kilikuwa na sumu lakini mpishi ni yeye!Wakati akiwaza hayo akakumbuka kauli ya Hamza alivyojaribu kumshawishi amuue Bario iliwabaki wote.Hilo lilimpa njia mpya kwamba aliyeua si yeye bali kuna mkono wa Hamza maana alionesha dalili!

Lakini akiwa hajajipanga alijikuta akisikia hodi ikibishwa!Kutoka mlango wa sebuleni.Bila hata kuwaza alimrukia mama mkwe na kumkwida shingo akaanguka naye hadi chini!Alikuwa anamnyonga!
 

Attachments

  • UPEPO USIKU.jpg
    UPEPO USIKU.jpg
    51.5 KB · Views: 109
UPEPO WA USIKU-16
BONIFACE BIRAGE
Alimkamata kwa nguvu zote alizohisi anazo!Alikuwa amedhamiria!

‘’U…Uuuh!”mama alikoroma.Laredo alimkwida kisawasawa nakung’ang’ania shingo.Walizungushana huku mama akitafuta kitu cha kujishikiza lakini akawa anababaika kwa haraka!Walipelekana puta hadi wakaanguka kitandani!Mara waende sakafuni!Mara wainuke kidogo alimradi Laredo apate nafasi ya kumkwida shingo vizuri aweze kumdhibiti!Mama alifanikiwa kushika kitu kilikuwa kioo akipindisha mkono kwa nguvu zote akitafuta shabaha ya kumpiga mkabaji wake aliye kaza mikono yake vizuri!Ghafla binvuu!Mama alipata mwanya mzuri ambao aliutumia kiuhalali!Alirusha mkono kwa nguvu akampiga na kioo kwenye paji la usoo.Vilikuwa vile vioo vyenye kishikizo.

Laredo alipepesuka nakuanguka chini.Alikuwa amechanika kwenye paji la uso!Akajikusanya kukabiliana na mama mkwe ambaye muda huo alikuwa akikohoa akitafuta hewa baada ya kukabwa kwa nguvu!Mpepesuko wake ulimpa Laredo nafasi ya kujiandaa upya kumkabili ambapo Laredo alimrukia mama huyo kwa fujo ya hatari akamvaa shingoni!

Purukushani zikaendelea.Mama alikuwa amemuona mvamizi wake hivyo akaachia kombora nakumtwanga mtu Yule!Laredo alikinga kwa mkono hivyo kupata kipigo kwenye mkono!Wakati wanaendelea vile bado mlango ulizidi kugongwa!Laredo aliruka nakukimbilia upande wa pili aliona taulo akaliokota nakurudi kufanya shambulizi.Alikuwa akiiwinda shingo ya mama mkwe.Mama naye alijua shabaha ya mshambuliaji wake.Hivyo alidhibiti kwa kushika kwa mikono taulo lililokuwa limesokotwa shingoni kwa mtindo wa kunyonga!Alinyongwa kwa nguvu zote huku akitapatapa kutafuta pumzi.Mkandamizo wa kunyongwa ulisababisha misuli na mishipa iliyopita shingoni kukaza nakuvimba huku ikijitokeza kwenye ngozi kutafuta usalama!Lilikuwa tukio baya sana.Hata muuaji mwenyewe hakujua alifanya vile kwa dhumuni gani?Alikuwa anaua!

“Ee…eh…aaa…aeh!”mkwamo wa sauti ulijitokeza kwenye koromeo ambalo tayari lilikuwa mashakani kwenye mbano wa kutisha!Mama alianza kuhesabiwa sekunde zake za kuishiHuku uhai ikititia!Laredo akakaza mikono kwa nguvu zote!Alijikuta anakuwa muuaji!

Aliyebisah mlango alikuwa amezidiwa na subra za majibu aliamua kufungua!

“Wenyewe?...Wenyewe?...Laredo?”ilikuwa sauti ya mama Shully!Huko chumbani ulisikika mkoromo wa mwisho na mama mkwe hakuwepo tena!Laredo akili ilimrudi tena upya!Alihisi mikono kuloa hatia!Alikuwa ameondoa uhai wa mama mkwe!Siku ileile alikuwa amekuta maiti tatu za waume zake,akakosea akamuua mwanae bahati mbaya akidhani kavamiwa!Sasa kamuu mama mkwe wake akimhisi angemsaliti kwa kutoa siri kwamba ndani ya nyumba ile kuna maiti takribani nne!Na Laredo ameshinda na maiti hizo tangu asubuhi!

Sauti ile ilikata halafu mtu mwenyewe akaja hadi chumbani!Aliufungua mlango nakuingia ndani!Mama mwke yupo pale chini macho yamemtoka pima!Mama Shully moyo ulimpiga mkambi!Alitumbua macho kwa mshangao!Pale chini anaona mwili umelala.Akiangalia vizuri anaona takribani miili mine!Mama Shully akaishiwa usemi!Ukimuangalia Laredo anavuja jasho la uhakika halafu anathema sana.Pia alikuwa na uso wa kilio!

“Kuna nini shoo?”aliuliza.

Kimya!Laredo alikosa cha kujibu kwa muda!Akili ilisimama kwa muda Fulani!

“Mbona hawa wamelala chini?”aliuliza?Kuona ukimya wa Laredo alijua fika hakuna usalama eneo lile.Ilibidi ajitwike jukumu la kupekua miili ile ajue kunani?Alijaribu kumtingisha mwili lakini mama alikuwa kimya!Aliufuata miili mingine akijaribu kuitingisha!Ilimchukua takribani dakika tatu bila kuuuanza kuhisi eneo lile halina usalama wa aina yoyote.Mlikuwa na miili isiyoonesha dalili za kuamka kwa wakati ule.Ilibidi mwanamke huyo ajitungie sentensi kichwani kwamba watu hawa watakuwa wagonjwa?Wamepatwa na nini?Mbona Laredo alisema wamesafiri hasa Bario!Hamza huyu hapaz!Masua jirani wa Laredo naye yu hapa.Isitoshe kuna mwili wa mtoto.Vyote vilitosha kumthibitishia kwamba watu hawa hawapo kawaida!Tena kuna jambo zito la kushtusha ambalo Laredo mwenyewe analijua!

“Laredo hawa wamefanyaje?”aliuliza kwa sauti ya ukali kidogo!

“Wamekufa!”ilimtoka kwa kitetemeshi!

Mama Shully alihisi nywele kumsimama!Alikumbuka hadi uoga wake wa utotoni uliomtesa kwa miongo hiyo ya utoto!Alijikuta kinywa kikichezacheza bila mpangilio kwa hofu inayotafuna nakummeza!

“Ma…ma..ma..iti?”aliuliza kwa kitetemeshi!Kinywa kikamkauka!
“Ndiyo!...”alijibu Laredo huku akijishika mikono kichwani!Aliumbuka!Amwambie nini?Kulikuwa na wakati mgumu kumwelewesha jirani yake huyo.Japo wana usuhuba wa dhati hiyo isingehalalisha kwa jambo kama hili.

Mama Shully alianza kurudi kinyumenyume kana kwamba anataka kukimbia.Hofu ilimpata aliijua mwenyewe!Kuoneshwa takribani maiti tano za watu anaowajua vizuri sana halikuwa jambo la mzaha kabisa!Hizi sio tu maiti bali ni watu wa karibu wa rafiki yake.Kuna mwili wa Bario mume wa Laredo.Kuna mwili wa Hamza shemeji yake Laredo.Kuna mwili wa Masua ambaye ni jirani namba moja wa Laredo.Halafu kuna mwili wa mtoto wa Laredo!Pia kuna mwili wa mama mkwe wa Laredo ambaye walizungumza naye dakika chache zilizopita!Kukuta hizi maiti hapa lilikuwa jambo lisiloingia akilini kirahisi!

Laredo aliwahi kumshika shoga yake mkono akimzuia kukimbia!

“Tafadhali usiende.”alimzuia kwa nguvu!

“Nimesema niache?”ilimtoka kwa nguvu!Laredo alipania kutumia mwanya huo pengine angeweza kusawazisha.Ilikuwa muhali.Mama Shully hakutaka kuelewa lolote sichochote!

“Tafadhali mama Shully usiondoke!”

“Nimesema niachee!Sitaki ushahidi!”alijitetea.

“Ungeniuliza kwanza kabla hujaamua kuondoka!”

“Niulize kitu gani wakati humu ndani kuna maiti!Shoo sina utani na uhai kwanza naogopa sana!”

“Ukiondoka nani atanisaidia.”alijitetea mtu huyo akiwa na hofu dhidi ya siri yake kugundulika.

Mlikuwa na maiti tano nani angekuwa tayari kukaa eneo lile?Hata kama ni mwendawazimu bila shaka angetakiwa akimbie.!Mama Shully alizidi kuvutwa akizuiwa asiondoke.Mvutano ulidumu kwa muda kidogo maana Laredo hakuwa tayari kumuachia.

“Naogopa shoga!Hebu niachieee!”alipiga ukulele.Ilikuwa kazi kweli kumshawishi akae pale.Timbwili la mvutano likawa limewadia.

“Ngoja shoo!”

“Hapana.”

“Ungenisikiliza kwanza wewe ndo mtu wa kunisitiri.Chondechonde mama Shully nihurumie mwenzio.”

Mama Shully alitulia nakuacha kujivuta kuondoka!

“Nikusitiri wakati hii ni ishu ya polisi!”

Kusikia polisi Laredo alishtuka sana hilo sio jambo dogo.Angetumbukia kwenye tandabelua kubwa.Polisi hawana dogo mbele ya sheria!Tena kwa mauaji haya wasingemletea utani wowote!

“Polisi?”
“Ehh!Waite polisi.”

“Hili sila polisi hapa nitafungwa bure!”

“Kwani ilikuwaje?”aliuliza mama Shully akiwa makini na swali lake lililohitaji ufafanuzi.

“Ndo nataka nikwambie iliujue masaibu yaliyonifika.”

“Lakini tusiongelee hapa.Naogopa sana.”

“Twende nyumbani kwangu.”alishauri mama Shully.Ilibidi watoke waelekee kwa mama shully.Hali ilikuwa imechafuka si tena shwari kama alivyotegemea.Ni siku hiyohiyo na tayari siri imegundulika.Hata angetaka kukimbia angekimbilia wapi?

Ndani ya dakika chache walikuwa nyumbani kwa mama Shully.Laredo alieleza kisa chote kilivyotokea na mpaka hapo alipofikia.

“Sasa kama ni hivyo kwanini hukuwa taarifu polisi?”aliuliza mama Shully.

“Ningeanzaje na wakati chakula mimi ndo nimepika nan do mpakuaji?Kibaya zaidi usiku sikula chochote.Watasema mimi mpishi ndo nimefanya ndumba ile.”

“Kwa hiyo na mama mkwe ulimfutilia mbali?Yaani Laredo umekuwa muuaji?”

Laredo aliangua kilio tena.Hungedhani kama anajuta au anatnia kuficha makucha yake.

“Sikutaka iwe hivyo alinioweka kwenye wakati mgumu nasikuwa na budi bali kumfutilia mbali.”

Mama Shully hakuvumilia aliona bora apige simu polisi!Lakini apige kwa namna ambayo shoga yake hata jua lolote.

“Sasa umepanga ufanye nini?”
“Hapana siju hata nianzie wapi?”alisema akijishika kichwa huku akiendelea kulia.

“Kumbuka watu hao wataanza kutafutwa!”

Hapo Laredo akishiwa pumzi ya ujasiri!Moyo ukazidi kumdunda kwa nguvu!

Laredo aliamka,”Nimesahau kurudishia mlango.”

Mama Shully alimuelewa akampa ruhusa aondoke.Lilikuwa kosa kubwa sana kumwachia aende.Laredo alitoka nje ya nyumba ili ili arudi kwake.Anakumbuka aliacha mlango wazi kwa kutofunga na ufunguo bali aliurudishia tu.Kumaanisha atakayeingia anaweza kuufungua kwa wepesi.Wakati ameondoka,mama Shully alichukua simu yake nakutafuta namba ya polisi aliyemjua!

Laredo alipofika getini alishtuka kwa alichokiona!
 

Attachments

  • UPEPO USIKU.jpg
    UPEPO USIKU.jpg
    51.5 KB · Views: 87
UPEPO WA USIKU-17
BONIFACE BIRAGE

Geti lilikuwa wazi!Hii bila shaka ilimpa ripoti iliyokinzana kama kweli aliuacha mlango au aliufunga!Alitembea kwa hatua zilizotilia shaka kuingia kwake.Kucheki kweli geti lilikuwa wazi!Akasogea karibu nakuingia ndani moja kwa moja.Hakutaka kuamini.Lakini ukweli mlango umefunguliwa na kuna mtu kaingia ndani.Palepale mtu mzima aliwaka tumbo joto!Akaenda hivyo akijiuliza atakuwa nani.Jibu litapatikana akijua.Nywele zilikuwa zinsisimka.Siku ilikuwa ngeni kwa upande wake na mashaka mengi yalikuwa yanamuandama ini na moyo!

Kufika ndani ya uwanja wa nyumba akatupa macho hadi mlangoni kwake.Kulikuwa na kitu kilichomtisha tena!Mlango wa kuingilia nyumbani ulikuwa wazi!Laredo akaishiwa pumzi!Alikuwa nani?Ujio wa watu hawa kama unazidi kuifyonza siri ya mtu mmoja nakuwa ya wengi.

Akaingia ndani potelea mbali bora ajue ni nani kaingia kwake.Ile kutokea ukumbini tu akakutana na mtu ambaye hakumtegemea maisha yake yote!Alikuwa ni baba mkwe!

“Mwanangu nimekutahakuna mtu lakini mlango upo wazi.Nisinge subiri hapo nje muda mrefu iimbidi niingie siunajua miguu yangu ni mibovu!”alisema baba mkwe akiachia tabasamu la uhakika.

Laredo alimwangalia mzee kwa umakini mkubwa bila kusema chochote.Ni wazi butwaa lilikuwa limempa kisogo.Mdomo ni kama ulipigiliwa msumari.

“Hujambo mwanangu.”mzee alijimwaga kama jamvi kwenye shughuli.Aliamua kuwa mwenye bashasha hasa akija kuwaona watoto wake.Tabasamu lake lilibeba furaha ya kiutu uzima akijianda kujimimina kwa wanawe pamoja na hoja zilizomleta katika nyumba hii.Utuuzima wake wenye busara ulimpa wasaa wa kupokea heshma kuu kama mzee.Alikuwa kimbilio la wenzake kwenye ukoo.Mjuaji mzuri wa kutatua matattizo.Hata yak wake yanapomfika alitumia busara kuyatatua.

“Mwanangu narudia tena hujambo?”

“Oh!...Shkamoo mzee wangu.”aliamkia.

“Marhabaa.Samahani nimekuja ghafla bila taarifa niikaingia ndani.”

Mzee alianza kujiongeza ilikuondoa hali ya huzuni.Kwa kumsoma Laredo saikolojia ni wazi alishtushwa na ujio wa mzee hapa kwake.Ule ukimya wa kuchelewesha majibu ni tuhuma tosha za kwamba karibu ilikuwa yakusuasua.Mzee alijitahidi kumtengenezea binti huyu sura ya tabasamu ilikuondoa hofu.

“Bila samahani mzee wangu hapa ni kwako.”

Laredo alijishtua aweze kutoa mazungumzo mazuri.Alikuwa na mawao mengi na tayari matukio ya siku ile yalikuwa magumu sana kiasi kujitete lilikuwa swali gumu kuliko yote!Ujio wa huyu mzee ni tishio kubwa kwake na hakujua hatma yake kama atamuacha akiwa salama au la!Atakuwa amejua siri ya uwepo wa maiti?Au kajua lakini anajifanya ili huyu msichana asihis jambo lolote?Alijaza hilo fumbo mwenyewe!

“Asante mwanangu.Nimekaribia.Nimewakumbuka sana.Naomba maji ya kunywa.”Alisema mzee akigusa koo lake kuashiria kwamba ana kiu.Laredo aliizembea kwa dakika kama moja hadi mzee alipoonesha ishara kwamba anahitaji maji.Hilo likamzindua kwa kumchipua kutoka lindi zito la mawazo.Uwazi wa mchana ulikuwa umemkuma na siku haikuwa imeisha.Alikuwa amekutwa na siri imegundulika tayari kwa watu wawili.Mama mkwe ambaye tayari amefariki na maiti ipo huko ndani.Huyo amekwenda na siri ile ya mauaji ndani ya boma lile.Mtu mwingine ni mama Shully ambaye baada ya kuongea naye ingawa hajajua msimamo wake ataweza kumpanga.Lakini pia lazima awe makini maana hakuna siri.Kwa namna zote Laredo hakutaka kuhusishwa na mauaji yale.Bario,Masua na Hamza walikufa kimaajabu kwa chakula ambaco alikipika yeye lakini hakula.Ila kilikuwa na sumu hii ni baada ya kumpa mbwa wake ambaye alikula nakufa!Hiyo ilimpa tahadhari kwamba chakula hicho kilikuwa na dosari.Pia alikumbuka maneno ya Hamza kuhusu kumuua Bario.Pengine Hamza ndo aliye weka sumu kwenye chakula.Alikumbuka alipokuja mezani chakula kilikuwa kimeshapakuliwa lakini akakirudisha kwenye bakuli kuu akachanganya kisha akakigawa mwenyewe.Bila shaka aliyekigawa mwanzo kabla ya yeye kufanya ugavi alijua anachofanya.Anaamka asubuhi anakuta watu watatu wamekufa.Wanaume ambao kwa upande wake ni waume zake.Mtoto alipokuja aklifyatua risasi akidhani kavamiwa.Akamuua.Aliua watu wawili akiwemo mama mkwe.Mazingira ya mauaji hayo yalitosha kumwingiza hatiani kama polisi wangejua historia nzima ya tukio lote.Hakutaka kufika huko kabisa.

Alimletea baba mkwe jagi lenye maji pamoja na kikombe akammiminia kimiminiko hicho cha na maji nakumpa anywe!

Baba alikata glasi tatu zilizoondoa kiu yake.Halafu akapumua kwa kuunguruma kwa raha hasa mtu anapokata kiu,”Asante sana mkwe wangu.”alisema akitoa miwani yake ya macho akaipumulia mvuke kisha akaivuta kwa kitambaa nakuikagua kama imekuwa safi.Alirudia zoezi hilo mara tatu kisha akiivaa tena miwani yake.

“Hapa hamjambo lakini?”

Lilikuwa swali lenye mushkeli kidogo kulipatia ufumbuzi wa majibu.

“Ni muda tangu tuonane.”

“Hatu jambo mzee wangu.Sijui wewe huko nyumbani.”

“Sisi ni kwema.Ila kuna matatizo madogo ambayo nita yatatua mwenyewe.”

Kutaja matatizo kwa baba mmkwe kulimrudidha Laredo kwenye kero zake.

“Kuna nini tena mzee?”aliuliza kwa adabu.

“Naomba niitie mama mkwe wako.Mwambie nipo hapa.”ilikuwa kauli ambayo ni tata kuielewa kwa haraka.Kauli yenye kumtishia Laredo.Amwite mtu huyo kutoka wapi?Kuzimu!

“Alikwambia anakuja hapa?’’alikwepesha.Hilo likamfanya mzee atikise kichwa halafu akacheka kicheko cha udhaifu kana kwamba anaficha kitu.

“Ha!Ha!Ha!”akacheka tena mzee wa watu hadi akgusanisha viganja vya mikono.Halafu akasema,”Ndo kakwambia uniambie hivyo?”

Jibu hilo likamfanya ajue kwamba mzee anajua nyendo zote za mama na anajua mama kaja hapa!Kukwepa nikuleta hoja isiyo na msingi.Ni kama alimwambia wacha kunidanganya najua unajua alipo mke wangu!

“Mbona unacheka mzee wangu?”aliuliza katikati ya huzuni na mshtuko.

“Najua mama mkwe wako kaja hapa.Ni hivi tuna ugomvi nyumbani.Tulikorofishana kidogo nay eye akakimbilia kuja hapa.Nimeamua kumfuata mwenzangu tuyamalize.Sipendelei ayalete kwa watoto.Hivyo naomba umwambie nipo hapa nataka kuonana naye.Najua hapa atanisikiliza.”alizungumza kwa utulivu tena busara iliyohsiba.Aletewe maiti?

Hakujua amjibu kitu gani mzee wake.Kama ilivyo kwa mama mkwe ndivyo kwa mzee ilikuwa ngumu kusema jambo lolote.

“Baba mama hajaja hapa.”

“Mwanangu namjua mke wa ngu vizuri sana.Aliondoka kwa hasira na huwa akiwa hivyo kama tuna mzozo basi hukimbilia walipo watoto wake.Nimeishi naye miaka mingi.Wewe muite umwambie nipo hapa!”

Laredo akaduwaa.Amdanganye vipi mwanaume huyu.

Baba mkwe hakuwa mtu wa kumdanganya.Alitakiwa ajitete kwa haraka.

“Una uhakika gani kama mama yupo hapa?Sikudanganyi baba.”

“Namjua mamako hapo ameshakulisha sumu ya ulimi kwamba nikija usiniambie.Na tena sitoki hapa hadi aje!”
 

Attachments

  • UPEPO USIKU.jpg
    UPEPO USIKU.jpg
    51.5 KB · Views: 95
UPEPO WA USIKU-19
BONIFACE BIRAGE

Mlio huo ulimshtua mzee wa watu ambaye alianguka chini kama gogo!Laredo alikuwa amepiga risasi juu!Ilikuwa kumuonya mzee dhidi ya kuingia chumba chake.Lakini mzee alikuwqa akikagua vyumba vyote bila kuonea chochote.Muanguko wa mzee ulimfanya Laredo kutumbua macho akiwa hajui kama kweli mzee anaweza kushtuka hadi aanguke kwa mtindo huo.Alichofanya alisogea pale,”Baba samahani ilijifyatua kwa bahati mbaya amka mzee wangu.”alipindisha maelezo ili mzee Yule asishtuke kitu chochote.Lakini mzee wa watu alikuwa hajitingishi kwa lolote.

Laredo akahisi kufadhaika kwa kiasi kikubwa kwamba kamchezea mzee wake rafu mbaya.Alipiga risasi juu maksudi ila akataka ionekane kana kwamba ni bahati mbaya.Kibaya zaidi kaifyetua nyuma yam zee.Uzito wa ule mlio ulimwogopesha baba mkwe kwa kiasi kikubwa.

Kabla hajamfikia akasikia vishindo huko ukumbini.

“Sauti imetokea chumbani.Kuweni makini.”alisikia sauti ya mtu kutoka nje.Laredo akaduwaa.Mwili ukasisimka.Miguu ilimtetemeka kwa nguvu zote akajikuta akaishindwa aanzie wapi kabla hajapiga hatua yoyote alishtukia watu wamevamia kwenye korido ile.Akaonekana!

“Weka silaha chini mikono juu!”sauti ilitoka nyuma yake.Laredo akajikuta akipandwa na woga uliomtafuna hadi kwenye mapafu.Homa ilipanda bila kujua imetokea wapi na hatma yake ni nini?Aliweka mikono kichwani kabla ya kushusha silaha chini.

“Nimesema weka silaha chini taratibu kisha uweke mikono kichwani.”sauti iliamrisha muda huo mzee baba Bario alikuwa kimya hajitambui pale chini.Laredo aliipeleka silaha yak echini.

“Taratibu…iweke!”sauti iliamrisha kwa uimara.
Bila shaka walioingia ndani walikuwa na uhakika kwamba msichana huyu alikuwa ni hatari sana na wao walikuwa na silaha./Laredo akaiweka ile bastola yak echini kisha akaweka mikono kichwani.

“Haya piga magoti mikono ikiwa kichwani!”

Laredo akatii amri akapiga magoti mikono ikiwa kichwani akashuka chini nakukunja mifupa ya goti hadi akawa amepika magoti.Wale polisi wakiongozwa na afande Rajabu waliwahi wakamshika binti Yule wakamtia pingu kwenye mikono.Ilisikika mlio wa pingu ukifunga mikono yake!Tayari amekamatwa eneo la tukio.Laredo alihisi jasho jembamba likipita hadi kwenye mifereji ya sehemu za siri!

“Haya kagueni.”

Polisi waliingia kazini wakaanza kukagua nyumba nzima nakufanikiwa kukuta maiti tano katika chumba cha Laredo ambaye alikuwa amekwisha!Huku wengine walibaki pale wakimkagua Yule mzee.

“Kuna miili mitano humu chumbani.”alisema moja ya wale polisi.Huku akijaribu kuhisi mapigo ya mioyo ya watu wale.Hakuambilia kitu zaidi ya ukimya ulioashiria uhai hakuna.

“Wazima?”

“Hapana afande wote sio wazima.Hata huyu mzee amefariki tayari!”
“Kwa hivyo jumla ni maiti ngapi?
“Ni maiti sita sasa.”

Laredo aliposikia na mzee hayupo alijikuta akiangua kilio kingine kizito.Hakutegemea kabisa jambo hilo kama lingejiri.Ina maana mzee kafariki kwa ule mshtuko?Alijiuliza na huo ndo ukawa ukweli kwa upande wake.Tayari kesha sababisha mauaji ya watu sita.Watatu ni yeye chanzo cha kuwashurutisha waume watatu wamuoe nao wakakubali na akawa anaishi nao nyumba moja.Kutokuridhika kwa wivu wa mapenzi kukamfanya mmoja wao awawekee sumu wenzake ili awauwe kwa bahati mbaya chakula kilichanganywa na Laredo bila kujua kama kina sumu kisha akawapakulia wote hivyo kuwapa wote sumu bila kujua.Yeye hakuwa na hamu ya kula siku ile ndo maana akaepuka kifo kile.Maiti nyingine tatu zilikuja kwa mkono wake.Mtoto wake alimuua kwa risasi akidhani ni mtu kavamia pale ndani.Kifo cha mama mkwe alikifanya kwa mkono wake pia baada ya kumnyonga ilikuficha siri ya vifo kule ndani.Hayo yalitosha kumtia hatiani.Kifo cha sita alifyetua risasi juu akiwa na nia ya kumtishia baba mkwe asiingie chumbani mwake ambamo kuna miili sita!IKumbe kufyetua ile risasi alikuwa amemshtua baba nakusababisha kifo palepale!

Kilio kilikuwa kina vuja kutoka moyoni mwake.

Polisi wakaendelea kufanya uchunguzi katika ile nyumba.Mwili wa mtoto ulikuwa na jeraha la kupigwa risasi.Alikuwa mwanafunzi akiwa na sare zake.Ilikuwa ni silaha iliyopigwa kwa minajili yakuua.Risasi ilikuwa imepasua kichwa nakuharibu yaani hata hakutamanika kuangaliwa!Bimkubwa alijipata akitetemeka mwili mzima.

“Kijana amepasuliwa kichwa kwa risasi.”

“Nini kilitokea hapa?”

“Kwanza kabla ya yote aitwe mwenye nyumba binti wewe si mpangaji hapa ndani?”

Laredo akaitikia kwa kutingisha kichwa!Kuonesha yeye ni mpangaji kwenye nyumba ile.Polisi wakaendelea kufanya upekuzi wao kujiridhisha mazingira yote.Alikuwa amekamatwa.Kukimbia asingeweza tena.Ni nani aliyefanikiwa kumuuza?Bila shaka ni mtu pekee aliyekuwa anajua mauaji yale naye si mwingine ni mama Shully!

“That bitch betrayed me!”alijisemea kimoyomoyo na kung’ata meno kwa hasira huku akiendelea kulia kimoymoyo!

Ndani ya muda mfupi baba mwenye nyumba akiambatana na balozi pamoja na viongozi wengine wa mtaa waliwasili eneo lile.Ujio wa kikosi kikubwa cha polisi kuliamsha mtaa mzima wakiwa na sinto fahamu zao.Ndani ya muda mfupi tayari ikaeleweka kwamba kuna mauaji makubwa yamejiri katika nyumba ile.Waandishi wa habari wakapenyezewa habari.Watu wakiwa na simu zao za mkononi walichukua picha za nyumba ile na waliofanikiwa kuingia ndani waliweza kuchukua picha za mazingira nakuanza kuzisambaza kwenye simu na mitandaoni.

Ilibidi polisi watoe maiti zile wakafunga nyumba ile kwa utepe wa njano iliwafanye uchunguzi zaidi.Wakati maiti takribani sita zinatolewa kulizuka vilio kutoka kwa majirani pamoja na Laredo mwenyewe!Hali ilikuwa tete!Lilikuwa lenye fedheha sana likiwaliza wengi.Kila mtu alitaka kujua kilichotokea siku hiyo.Japo Laredo alikuwa na ushirikiano mzuri na majirani zake lakini ushirikiano huo sio wamazoea kivile useme alikuwa mtu wa kujichanganya nao sana.Alijitokeza kwa shughuli maalum tu nasio mara kwa mara!Ilikuwa vigumu kumsema vibaya.

Polisi ilibidi waite waandishi wa habari nakuteta nao,”Naombeni utulivu.Tukio lililotokea ni kubwa sana.Kuna takribani maiti sita humu ndani.Moja ikiwa imepigwa risasi ya kichwa na kuharibiwa vibaya.Hizi nyingine bado tunasubiri zichunguzwe kisha tupewe ripoti.Hadi sasa tuna mshikilia mwanamke anayeishi hapa bi Laredo Bario hadi hapo uchunguzi utakapokamilika.Najua tumepata msiba mkubwa maana hawa ni majirani zetu ndugu jamaa na rafiki.”alikuwa akitoa maneno kidogo afande Rajabu.Japo waandishi wa habari walitaka kuja na maswali lakini mengi yaliepukwa na afande Rajabu ilikuruhusu uchunguzi ukamilike kwanza.

Ndani ya muda kidigo waliondoka na mtuhumiwa kuelekea kituoni kwa mahojiano zaid.!
 

Attachments

  • UPEPO USIKU.jpg
    UPEPO USIKU.jpg
    51.5 KB · Views: 78
UPEPO WA USIKU-20
BONIFACE BIRAGE

Waliwasili kituoni baada ya dakika 30.Laredo alipelekwa moja kwa moja ndani kwanza akisubiri utaratibu uendelee.Huko kituoni bado kuna rundo la waandishi wa habari walijikusanya wakisubiri maelezo zaidi.Afande Rajabu alishughulikia miili ikapelekwa hospitali kwaajili ya uchunguiz na kuhifadhiwa kwa miili ile kwenye chumba cha kuhifadhia maiti.Hali ilikuwa nzito na kila mtu ndani ya taifa zima alikuwa akisikilizia tukio hilo.

Safari ya kwenda hospitali ya mkoa kupeleka miili ya watu sita waliokufa kwenye mazingira tatanishi iliwadia.Kikosi maalum kikiongozwa na afande Rajabu kilienda hospitali.Miili ilifikishwa na kupokelewa na matabibu.Afande Rajabu aliandika maelezo kuhusu miili hiyo na kile anachokitaka katika uchunguzi huo.Dokta wa uchunguzi wa maiti alitolewa kutoka kitengo cha Forensic Science maalum kwa kesi hiyo.Maana afandee Rajabu alitaka majibu sahihi kuhusiana vna vifo vya watu wale.

Miili iliandaliwa kwaajili ya uchunguzi.Afande Rajabu alizungumza na dokta atakayesimamia zoezi hilo.

“Unadhani itachukua muda gani?”

“Kwa matokeo ya mwaanzo mwanzo tutatumia masaa manne kwa mwili mmoja hii nikulingana na uzoefu wangu wa kazi.Na kukamilisha ripoti kwa saa 24 ila ripoti kamili huchukua hadi wiki 6.”

“Nataka ripoti ifanywe kwa umakini wa hali ya juu.Hili situkio la kawaida kwa kweli.”

“Usijali tutapata majibu.”
“Hata kama nikuongeza masaa ya kazi tafadhali fanya jambo hili.”

“Sawa mkuu.”aliitikia dokta akiwa anaweka maandalizi kwa aajili ya uchunguzi wa miili ile.Afande Rajabu aliporidhika na taratibu zile aliamua kuondoka akarudi kituoni kwaajili ya mahojiano maalum na Laredo mtuhumiwa namba moja.Tayari kwenye kichwa anakumbuka maelezo ya mama Shully hivyo alitegemea Laredo atatoa maeleoz kama yale.Japo katika uzoefu wake wa kazi sio wote wanaokubali kutoa maelezo sawa na vile hali halisi ilivyo lakini kwa huyu kidogo aliujua ukweli nyuma ya pazia.Aliomba Mungu aweze kumaliza fumbo la vifo vya watu hawa sita!Ni moja ya matukio ya kutisha sana kwa mwaka huo.Mara nyingi hukuta ni mtu mmoja ndo kauawa lakini sio watu sita.Imani ya kwamba watu hawa wameuawa nikufuatia ripoti ya mama Shully pamoja na kukuta maiti ya mtoto imepasuliwa kichwa halafu walisikia mlio wa bastola punde walipofika eneo la tukio.Vyote hivi vilimpa taarifa kwamba hawa sio bure.Japo miili hii mingine haikuwa na jeraha kivile lakini hungejua tukio lote lipoje hadi mtuhumiwa namba moja aeleze kilichojiri.

Alijiambia kama Laredo hata mueleza habari inayoeleweka bila shaka atamtumia mama Shully kama shahidi kwa namna yoyote ile.Kulivalia njuga swala hili ilikuja baada ya IGP wa polisi kuwalaumu watendaji kazi wake kuzembea kwa kudhibiti matukio ya vifo kwa njia ya mauaji hasa kwenye makazi ya watu.Hilo alitaka ulidhibiti kwa kushughulikia swala hili kwa umakini mkubwa.

Aliondoka hospitali nakurudi makao makuu.Mwendo mfupi alikuwa amefika kituoni.Utaratibu wa kuandaa faili la tukio lile ulianza mara moja.Afande Rajabu alienda kwa RPC wake aliitwa.

Aliingia ofisini nakupiga saluti kisha akaketi chini.Meza ya RPC ilisheheni mafaili yaliyopangwa kwa ustadi mkubwa.Huku mengine akiwa ameyafungua.Alikuwa akiongea na simu kisha alimaliza akaiweka chini nakumgeukia kijana huyu.

“Keti.’alikaribishwa kiti na RPC.Rajabu aliketi chini.

“Nimepata maelezo ya juujuu kuhusu tukio jhili.Hapa nimeshapokea simu kutoka makao makuu pamoja na ikulu wanataka majibu haraka kwa swala hili.Hili sio tukio dogo ni kubwa sana!Vipi unaonaje kuhusu tukio hili?”

“Mkuu kwa sasa sina cha kukuambia maana ndo miili tumeifikisha hospitali nasubiri ripoti husika.Ila nataka nimuhoji huyo binti anipe ufahamu wake kwenye tukio hili nione anajua kitu gani?”

“Yaani nimeshtushwa sana kwa tukio hili.Watu sita.”
“Huyo mtoto aliuawa kwa risasi lakini hawa wengine bado sijaona alama.Mwili wa Bario,Hamza na Masua hakuna alama yoyote ya kupigwa kwa kitu chochote.Pengine ni sumu.Lakini majibu tutapewa na huyu binti.”

“Mmmh?”aliguna RPC,halafu akasema,”Basi mfuatilie kwa umakini.”

Rajabu alitoka ofisini kwa RPC akaenda moja kwa moja hadi chumba cha mahojiano.Akiwa kule Laredo alitolewa mahabusu kisha akaletwa kwa afande Rajabu ambaye mpaka sasa jukumu la upelelezi limemuangukia yeye.

Meza kubwa mbele alikuwemo Laredo kaketi halafu kaweka mikono juu ya meza akiwa katiwa pingu.

Afande Rajabu aliandaa kiredio cha mahojiano huku akimwanagalia Laredo,” Sitaki tupoteze muda unaweza kuniambia kilichotokea hapo kwako?”

Laredo alikuwa akitetemeka hadi kichwa.Kinywa kilimchezaheza asijue anaanzia wapi?Amefika eneo ambalo hakutaka kabisa lije limtokee alikuwa mikononi mwa polisi na lazima atoe majibu ya kuridhisha.Ukweli wote ulipita kichwani mwake kama daftari vile lilifunguka ili asome majibu yote moja baada ya Lingine.

“Nahitaji kupata maelezo kutoka kwako.Au una mwanasheria wako ambaye unamsubiri?:”

Laredo alitikisa kichwa.Kama angekuwa na mwanasheria basi angekwepa jambo hilo.Lakini akili ya kutafuta mwanasheria wake haikuwepo kabisa kwenye kichwa chake.

“Binti ni bora unieleze vizuri kabisa kilichotokea kuwa kimya hakuna utakachofaidika ni bora uniambie kilichotokea.Tambua nchi nzima inataka majibu ya tukio hili.Simu kutoka juu zimeshapigwa nakutuamrisha tutumie namna yoyote ili utupe majibu ya tukio hili?”
Laredo bado hakuwa na sauti ya kusema kitu chochote.Kimya chake kilizidi kumkera afande Rajabu ambaye alitamani kumfunua kinywa binti Yule hata kama nikwakumpiga makofi ilimradi aweze kupata majibu ya maswali yake.Lakini alichoambulia sanasana ni uoga uliojichora kwenye uso wa msichana huyo.Alikuwa akitetemeka.

“Najua unaogopa sana lakini tafadhali niambie kilichojiri.Una uhusiano gani na hawa marehemu?”

Laredo akajikaza kisha akasema,”Ni…ni…”kigugumizi kikamshika tena kilimkba hadi kooni akajikuta akiangua kilio.

“Bario ni mumeo?”

Kimya msichana wetu hakujibu kitu alibaki kutumbua macho tu.Rajabu akashindwa kuvumilia.

Akainuka kwenye kiti nakumzaba kofi la uso msichana Yule ambalo lilimfanya ahisi kuona vimulimuli.Kidogo hilo likamzindua,”Usinipotezee muda stupid!:”akafoka afande Rajabu.

Laredo alishindwa hata kujisugua shavu lake.

“Niambie kitu gani kilitokea hapo kwako?Una maiti sita ndani ya nyumba halafu tunakuuliza unajidai kukaa kimya.Huo ukimywa wako ndo tunaoupinga hautakusaidia kitu chochote zaidi ya kuweka mambo magumu.

“Kwa taarifa yako una miaka mingi inakungoja jela nakuhakikishia kama hutanyongwa basi kifungo cha maisha hakiepukiki.Ni bora utuambie kilichotokea angalau tujue shutuma zinaenda kwa nani?”

Laredo bado hakujibu kitu chochote kile zaidi ya kuwa kimya muda wote huku machozi yakifaladi kilio kwa kayamba za huzuni.Chumba kilitawaliwa na sauti ya afande Rajabu peke yake.Kukiwa na mahojiano ambayo bado mabichi na hayajatoa neno lolote mlango wa kile chumba ulifunguliwa wakaingia watu.

“Afande Rajabu tunamuhitaji huyu binti.”

“Lakini bado mahojiano hayajaisha?”alisema Rajabu kwa hasira mana hakutaka kukatishwa na yeyote isitoshe huyu binti ni kama kamdharau kwa kitendo cha kumpa ukimya uliomkosesha majibu ya maswali yake!Kuingia kwa hawa watu nikuondoa uwepo wa mahojiano na pengine aende na siri nyingi sana bila wao kufikia hitimisho la upelelezi.

“Tunajua lakini tunamhitaji sasa hivi.”

“No!”alisema nakupiga ngumi kwenye meza tayari jazba ilishampnda.Akainuka kukabiliana na hawa wanaotka kumnyang’anya mtuhumiwa aliyemkamata.

“Afande hii ni amri sio ombi!Tunamtaka Laredo sasa hivi!”alisema moja ya afande zake.

“Saba nakwambia hakuna mtu anatoka hapa.”

“Rajabu anahitajika huyu mwanamke na usalama wa taifa!”
“What?”ikawa zamu ya Rajabu kushangaa.Hii kesi inazidi kuiva.Laredo kusikia ni usalama wa taifa alijikuta akizimia palepale mezani.

“Nimekwisha Laredo mie.”alijisemea akipoteza fahamu hakujua kilichoendelea.
 

Attachments

  • UPEPO USIKU.jpg
    UPEPO USIKU.jpg
    51.5 KB · Views: 73
UPEPO WA USIKU-21

BONIFACE BIRAGE

Fahamu zilikuja kurejea baada ya muda Fulani wakati huo alihisi kichwa kuwa kizito kutokana na matukio yote ikiwamo kukamatna vyombo vya dola.Laredo alijaribu kukupesa macho ajue amefikishwa wapi?Alisikia muungurumo wa gari ukirindima.Bila shaka alikuwa kwenye chombo hicho.Cha msingi kwa wakati kama ule nikujifikiria yeye mwenyewe anajiondoaje kwenye kitanzi kile ambacho kimeonesha kwa dhati kumdhibiti yeye mwenyewe.Laredo akafungua macho nakujikuta amewekwa kwenye kiti kafungwa pingu!Kwa kuwa alikuwa mikononi mwa wanausalama wa taifa alijuafika hana mwanya wa kuepuka.Alitamani kusema jambo lakini ulimi ukawa mzito.Eneo kama lile ni hatari kwake.Tena kubwa sana na alitakiwa ajipange kiakili kwa kujiandaa kisaikolojia.

Baada ya mwendo Fulani walifika mahali ambapo gari lilikata kona kona kadhaa hadi wakaingia jingo Fulani.Huko Laredo alishushwa kutoka kwenye gari nakukimbizwa kwenye jingo hilo.Asingepatambua kwa haraka maana sio eneo alilolijua.Alipelekwa kama kondoo machinjioni.Wote walliokuwa pale walimwangalia kiaina.Kwa muonekano waliokuwa pale walikuwa watu makini sana wasio na mchezo na yeyote..Laredo alipitishwa vyumba kadhaa hadi alipoingizwa sehemu husika waliyomtaka awepo.

Kilikuwa chumba Fulani akaingizwa na kuketi kwenye kiti kusubiri maagizo.Ndani ya muda mfupi aliingia mtu aliyevalia suti yake safi.

“Habari yako msichana?”alianza mtu Yule kwa sauti yenye utulivu.Wajihi wake ulibeba umakini wa kistaarabu kiasi asingeweza kutambua kinachofuata.Laredo akavuta pumzi ndefu nakuzishusha ambapo mfumo wake wa upumuaji ulijipanga vyema.Hakujibu salamu ile.

“Ukimya wako hautasaidia kitu.Nilitaka twende kistaarabu lakini inaonekana wewe hujui ninachokitaka kutoka kwako?”

Bado binti Laredo aliamua kukaa kimya kuhusiana na mahojiano kati yake na yule mtu.Ukimya huu ulitafsirika tofauti na mtu Yule kuona kwamba binti huyu anakiburi na hayupo tayari kutoa ushirikiano wanaoutazamia.Ukimya huu ni hatari kwa lengo lao.Pengine utachelewesha majibu husika.

“Nimepata taarifa kwamba hata mikononi mwa polisi uliwapa ukimya.Nataka kukuhakikishia kwamba mikononi mwetu utaongea tu!Penda usipende!”

Kauli kavu yenye vitisho wala haikuyumba!Hilo lilitosha kuitikisa mifupa ya Laredo moja kwa moja nakumpa fikra nyingine.Hata ukimya wake haikujulikana umechangiwa na sababu gani.

“Hebu amka.”alisema bwana Yule kisha wakatoka naye nje nakwenda chumba Fulani.Huko Laredo alikuta kuna binti yumo akiwa makini kwenye tarakilishi yake.

“Utapimwa alama za vidole.”alisema Yule bwana.Laredo alichukuliwa alama za vidole vyake.Alioneshwa mashine yakuchukulia alama akaweka mikono yake kisha mashine ikapitia alama zake za vidole.

“Ukimya wako unatutia shaka sana.”alisema bwana Yule wakati zoezi la kuchukua alama za vidole likiendelea.Kisha akaendelea,”Sijapendezwa na ukimya huu kabisa.Kati ya watu wote waliofia nyumbani mwako kuna mmoja ni muhimu sana kwetu na wewe pekee ndo unajua mauti yake yalikuwaje?”

Laredo akameza hilo.Bila shaka anachomaanisha bwana huyu nikuwa kuna mmoja ni mtumishi wa usalama wa taifa!Laredo akajikuta anatetemeka ini na moyo!Inamaana kamuua wakala wa usalama wa taifa!Kwa kweli kwa wote hakujua kabisa ni nani alikuwa mtumishi wa idara hiyo!Hajui jambo hilo?Ni Bario?Hamza?Au Masua?Hilo lilikuwa geni kwake na hana uthibitisho wowote.Bario alikuwa mfamasia muuuza dawa,Hamza alikuwa dereva na Masua alikuwa mfanyakazi na mwenza wa mama Shully.Kampuni aliyofanyakazi Masua ilihusika na ukataji bima,sasa bima wapi na wapi na usalama wa taifa?Udereva wa Hamza haukuendana kabisa na shughuli hiyo ya usalama wa taifa.Bario mfamasia au dokta kama waliomjua walivyopenda kumwita hakuwa na dalili zozote za usalama wa taifa.Hata mama mkwe wake na baba mkwe taaluma zao hazikumpa ushawishi kwamba wanaweza kuwa wanausalama wa taifa.Japo kazi hiyo huwa na usiri sana lakini sio kwa viwango vile kwa jinsi alivyoijua yeye.

“Tutapima alama za vidole vyako kuhusiana na ile bastola uliyokutwa nayo.Kisha tutapima risasi iliyomzibua mwanao ubongo kama inaendana na bastola hii.Pia lazima tuangalie usajili wa bastola hii.Nategemea tumalize zoezi hili haraka na niamini utaongea tu.”alihakikisha bwana Yule.
Laredo alikuwa bado kimya asijibu kitu chochote..Alijihesabia za kwake tu.Baada ya vipimo kuchukuliwa Laredo alirudishwa tena kwenye kile chumba cha mahojiano.Kule nako alitembelewa na watu wachache wakimuuliza kistaarabu kama anaweza kuwaambia lolote kuhusiana na mauaji yale.Lakini hakuwajibu lolote zaidi ya kuushona mdomo wake kwa nyuzi za tairi ya gari akihakikisha hakuna maelezo yoyote yatatoka kwake.Kila mara meza zilisikika zikigongwa na watu wale wakitoka kwa hasira bila kuambulia jambo lolote kwa binti huyu.Alishikiliwa pale kwa muda wa siku saba.Kila kitu alipewa vizuri hasa malazi na chakula.Vyote alipata isipokuwa ni uhuru tu.Muda wote huo hakuweza kupata mawasiliano na nduguze wa uraiani nakujua hatma ya misiba ya watu wake.Hilo lilikuwa pigo kubwa kuliko yote.

Alimeza pigo laukiwa asijue hatma yake ni nini mikononi mwa watu hawa wasio na mchezo nay eye.Wasingempa uhuru wake kirahisi namna hiyo.Hatimaye baada ya takribani siku saba watu wale walimleta tena kwenye mahojiano yaleyale.

***

“Binti tunaomba utuambie ni nini kilitokea katika nyumba ile?”huyu alikuwa bwana Sospeter alikuwa na cheo kikubwa katika idara hiyo ya siri ya taifa.

Ukimya ulirejea kama awali.

“Uchunguzi umeonesha kwamba Bario,Hamza na Masua wamekufa kwa sumu iliyowekwa kwenye chakula.Mwanao alikufa kwa kupigwa risasi ya kichwa.Bastola iliyotumika imesajiliwa na mumeo bwana Bario na hata risasi zimetumika kutoka bastola hiyohiyo!Mamake Bario aliuawa kwa kunyongwa.Mwili wake tulipata alama za vidole ambazo zimefanana na zako.Baba mkwe alikufa kwa mshtuko nadhani ni ule mlio wa risasi uliopiga wewe maana ulikutwa na bastola huku baba mkwe wako akiwa amelala chini!Tunachotaka kujua je,hiyo sumu iliwekwa na nani?Alama za mwisho za vidole zilikutwa kwenye bastola uliyokuwa nayo niza kwako!”Sospeter aliendelea kueleza upelelezi wake.

Laredo alikuwa makini kumsikiliza huku akijua kila lililosemwa ni la kweli.Lakini ataepukaje viunzi vile?Haiwezekani hata kidogo kabisa!

“Wewe ndo uliyetumia bastola ile kumfyatua mwanao!Wewe ndo uliyemnyonga mkweo.Hata ushahidi wa rafiki yako unaonesha wazi kwamba ni wewe uliyeamua kutekelza jambo hilo na ulitaka kudhibiti siri hiyio isijulikane na hata mama mkwe alipogundua siri yakuwepo kwa maiti za wanawe ulifikia uamuzi wa kumuua mkweo kwa kumnyonga ukiwa umekusudia!Baba mkwe vilevile wewe ulichangia kukatisha uhai wake kwa kufyetua risasi hatujui lengo kama ulikuwa unamtisha au ulidhamiria kumuua!Ulipiga risasi ambayo haikumpta maana ulipiga kwenda juu.Mshtuko wa mlipuko huo ukamzidi mzee hadi kusababisha presha yake kupanda nay eye kufa!Huyo naye aliikuwa amejua siri yako maana mwili wake tuliukuta ukiambatana na maiti za wanawe!”

“Kuna maiti sita nyumbani mwako!Pia tulimkagua mbwa wako aliyekuwa amekufa naye tulikuta kauawa kwa kula sumu kwenye chakula.!Uliweka sumu kwenye chakula?”
 

Attachments

  • UPEPO USIKU.jpg
    UPEPO USIKU.jpg
    51.5 KB · Views: 76
UPEPO WA USIKU-22

BONIFACE BIRAGE


“Sijaweka sumu mimi!”alizidiwa!Saikolojia yake ilikuwa imeiva kupokea maelezo ya Sospeter.

“Wewe ni mke wa Bario bila shaka wewe ni mpishi wa nyumba ile sasa lazima utuambie aliyepika ni nani?”

Laredo alifikiri kidogo huku mikono ikitetemeka kwa tishio za habari ile.Kweli hakujua hatma yake inaenda wapi maana alizidiwa kabisa kwa maelezo ya bwana Yule.

“Ni mimi nilipika lakini sikuweka sumu!”
“Na ilikuwaje Masua akakutwa kwako?’’hilo likawa gumu kujibu.

“Si..si”kigugumizi kikamshikamshika.

“Maelezo tuliyopata ni kuwa ulisema watu hawa wapo safarini sasa iweje wawepo kwako wakiwa tayari ni maiti?”

Ulimi usitasita lakini alijikusanya nakuanza kuachia ngeli zake,”Sikuwawekea sumu na wala sikuwa na lengo la kumuua yoyote?”

“Ulikuwa na mahusiano gani zaid na hawa watu?”aliulizwa swali la msingi sana.Hapo alijikuta akiinamisha kichwa chini akikosa majibu murua ya kurdhisha hata aseme aeleweke.

“Tumekuta simu kadhaa.Napenda kuku fahamisha kwamba tunapofanya uchunguzi huwa tuna pitia kila sekta.Jambo lolote dogo hutusaidia kujua kwanini kitu flani kilifanyika hivi na vile.Tumekagua simu zako zote pamoja na za marehemu na kukuta mazungumzo pamoja na picha za mnato zenye kutia shaka.Usipoanza kuongea itakuwa ngumu sana kwa wewe kuepuka kesi hii.”alisema bwana Sospeter.

“Lakini mimi sina ninalojua.”

“Hata stori ya kilichotokea siku ile hujatuambia mambo mengi tunajijazia wenyewe.”sasa alizungumza kwa utulivu sana kiasi akaeleweka.Halafu akaweka mikono mezani nakuifumbata yote miwili.Kisha kwa utulivu tena akamwambi msichana Yule,”What happened that day?”

“Mimi sina chakusema maana sijui lolote.”alijibu purazai kama vile hayakumuhusu ndewe wala sikio.Kujiamini kwa binti huyu kuliwapa tishio hao waliofanya uchunguzi.Wakati anafikiria chakumfanya huyu mschana aliinuka ghafla bwana Sospeter nakuipiga meza teke akiisukumia kwa Laredo jambo ambalo lilifanya meza ijipigize tumboni nakumsukumia kwenye ukuta huku akileta maumivu makali sana.Sura mpya ya mahojianio ilikuwa imewadia.

Sospeter akachapuka haraka nakumuwahi kwa ngumi ya uso kama tatu za mshindo mzito kisha akamkwida shati nakumvuta kwa haraka.Ghafla akampiga makofi mfululizo.Laredo kabla hajajikusanya alikutana na kipigo cha uhakika!Ngumi zikarindima.Ndani ya sekunde kadhaa alikuwa natiririka damu kwenye papi za midomo huku mashavu yakiiva kwa wekundu!Alishambuliwa vibaya!Tayari hatari imeonekana.Hakuna tena mahojiano ya kubembelezana.

“Ninapotaka majibu ya uhakika lazima niyapate pumbavu wewe!”aliropoka bwana Sospeter.Zile kelele mule ndani zilifika hadi nje na ghafla mlango ukafunguliwa akaimngia mwanamke.Alikuwa ameshika bastola uso umeiva!”

“Linda umefuata nini huku?”Sospeter akauliza kwa kushangaa.Hakuwa amemtegemea.

“Huyu muuaji kaniuliaa mchumba wangu niache nimmalize!”alitamka Linda akielekeza bastola kwa Laredo!

“Linda hatufanyi kazi hivyo tuna sheria za kufuata.”
“Hapana kaniharibia ndoto zangu!”
“Tafadhali weka bastola chini!”

“No!”Linda alikuwa ameidhibiti bastola mikononi mwake akiwa ameielekeza kwa Laredo aliyekuwa ametoa macho huku akiwa anavuja damu!

“I am giving you a direct order put the gun down!”sauti kali ya Sospeter ilirindima!Linda alikubali yaishe akaishusha ile silaha nakuiweka mezani! Kesha salimu amri ya mkuu wake!

“Samahani mkuu ila naomba nimuhoji maswali kadhaa kabla ya yote!”aliomba Linda muda ule pengine bosi angemwelewa kwa lolote.

“Nitakuachia lakini ukiwa umetulia.”bosi alimuelekeza kidogo bihasira alimuelewa kidogo.Alitoka nje Linda nakuenda hadi kwenye ofisi yake akachukua bahasha akarudi nazo ndani alimo Laredo.Kisha akafungua bahasha ile saizi ya A4,akatoa picha kadhaa ambazo zilimuonesha Laredo akiwa katika pozi tofauti za kimahaba na Hamza,Masua,na Bario.Picha zile nikama zilimvua nguo kwa pamoja.Akajikuta akiduwaa.Asingesema zimetengenezwa maana hata mazingira aliyajua na wakati picha hizo za mnato zinachukuliwa alikuwepo nay eye ndo muhusika mkuu.Zilimuonesha vizuri wala hakuweza kusema zimehaririwa.

Mwili ulipiga paa!

“Picha hizi uliichukua ukiwa na akili timamu hapa naona umepiga na mumeo,lakini pozi ulizoweka na Hamza na Masua zinatia shaka kama zilikuwa picha za kawaida!Kama hii simnapeana pambaja na busu za kweli?”alisema Linda.Angeuliza maswali hayo kwa maana mmoja wao alikuwa mchumba wake.

“Kwa uchunguzi wangu naona ulikuwa na uhusiano na hawa marehemu.Sisi huwa tunafuatilia lolote ilikujenga hoja ya tukio zima la mauti.Theory ya kwanza inanijia japop naikataa.Ila nataka uniambie ni nani aliweka sumu Hamza,Masua na Bario wakainywa?”

Laredo alibaki na karata ya ukimya.

“Isitoshe hakukuwa na uadui kati yako na hawa watu.Tumejaribu kuuliza majirani zako wote wanasema mna uhusiano mzuri na hawa marehemu.Hakuna uadui tuliouhisi ni hadi tulipopekuwa simu yako ndo kuona picha zenye kuleta utata.Picha hizi zilipatikana kwa simu ya Masua na Hamza.Jumbe mlizotumiana zote tulifanikiwa kuzidukua nakugundua kulikuwa na uhusiano zaidi wa kishemeji kati yako na Hamza na pia kati yako na ujirani mwema wa Masua!Kulikuwa jumbe za kutilia shaka.Hata maongezi ya simu yalionesha wazi kuna mapenzi kati yenu!Ndo maana theory ya kwanza inayonituma nikuwa mauaji haya yalichangiwa na mapenzi!”alisema Linda akiwa makini!Laredo aliona huyu mwanamke anakaribia ukweli ambao hata yeye alikuwa anaujua.Lakini angeonekana vipi?
“Kwa taarifa yako Masua alikuwa mchumba wangu!Masua huyuhuyu alikuwa wakala wa usalama wa taifa!”
 

Attachments

  • UPEPO USIKU.jpg
    UPEPO USIKU.jpg
    51.5 KB · Views: 90
UPEPO WA USIKU-23

BONIFACE BIRAGE

“Masua alikuwa ni wakala wetu tena imara.Serikali ilitumia gharama nyingi kumpa mafunzo aje alisaidie taifa lake.Alikuwa imara mwenye mafunzo ya hali ya juu.Shushushu gredi 1.Wewe umekuja na ukahaba wako ukamlevya nakusababisha mauti yake.”
“sijamuua mimi!”
“Alikuwa mchumba wangu namjua vizuri.Angefeli sehemu moja tu nako ni mapenzi!”alisema Linda kwa ukali.Macho yake mazuri yalikuwa yamekasirika sana.

“Lazima uhusiano huu unahusika na kifo chake.Niambie ukweli wewe mwanamke!”

Laredo alifikiri akaona isiwe taabu bora ajifiche wala asijulikane simulizi ya Linda hakutaka aikubali maana ingemtia mashakani.

“Tumefundishwa kufanya upelelezi.And am good at that!Kila nililo kwambia ni ukweli mtupu!Wewe umechangia pakubwa kusababisha kifo chao.Nimetumia masaa sabini na mbili kukagua nyumba yako detail kwa detail nakujaribu kutengeneza picha ya tukio.”

Wakati wanasema yale waliona huyu binti anakiburi sana!

“One more thing nitajua tu ulichokifanya.”hilo alihakikishiwa.Linda alitoka mule chumba cha mahojiano.Alienda pamoja na Sospeter kisha walirudi nakumchukua Laredo wakampeleka chumba kingine.Wakamwambia avue nguo zote.Laredo alitii nakuvua mavazi yale kisha Linda akaanza kumkagua.Kwenye shingo ya Laredo aliona tattoo imechorwa aliutilia shaka ule mchoro.Kisha akatoa simu nakuupiga picha.

“Kifo cha wakala wa usalama wa taifa gredi 1 kimetokea nyumbani mwako tena kauawa kirahisi sana kwa sumu nataka kujua maelezo kwa kirefu!Kwanini simu yako nay a wakala huyu wa usalama wa taifa zikutwe na picha za mnato za mahaba.Isitoshe hizi nyingine mpo uchi kabisa mazingira ya nyumbani mwako.Wewe ni mke wa mtu!Hilo linatosha kutilia shaka uhusika wako na vifo vya wakala wetu!Kama unafikiri ni tukio dogo madam umenoa jipange!”Linda alizidi kutia mkazo mashtaka yake kwa binti huyu.

Wakiwa pale likaletwa bomba kubwa la maji.Linda alikunja mikono ya shati lake kisha akashika lile bomba saizi ya zimamoto.Alimuelekeza nalo msichana wetu Laredo nakufungulia maji ya baridi akaanza kumnyeshea!Ubaridi ulikuwa mkali sana usiovumilika!Alitumia takribani dakika tano hadi Laredo akahisi mwili wote ukizizima!Lilikuwa teso kubwa sana kwake.Alitetemeka toka mifupani!Hakuutamani mwili wake wakati msururu wa mateso unaendelea!Laredo alidata kwa kweli!

“Hakufa mtu wa kawaida nyumbani mwake na lazima ukiri yote yaliyojiri ndani ya nyumba yako!”

Linda aliropoka wakati akizidi kumpa mateso binti Laredo aliyeishiwa ujanja kwa wakati ule.Mara ileile Yule mtesaji alifunga lile bomba kisha akachukua fimbo Fulani ya plastiki nakumfuata anayemtesa.Alianza kumcharaza kwa kishindo.Alifyetua viboko vya uhakika huku akisababisha mwili wa Laredo kuvimba sana!Laredo hakulia kwa kutoa sauti bali alikuwa kimya huku machozi yakimtoka tu.Hilo liliwaonesha ishara kwamba huyu wanayemtesa ni mgumu kupita maelezo!

“Nitakutesa hadi ujue mimi ni nani?”alizidi kufoka sana.Mateso yalizidi hadi Laredo akapoteza fahamu!Linda pamoja na wenzake walimchukua nakumrudisha kwenye chumba kingine kisha walimtupa sakafuni kwenye baridi.Wakaleta shuka chafuchafu maalum kwa mateso wakamtupia juu ya mwili wake uliokuwa kimya!

Bado walikuwa hawajapata majibu.Maelezo yao hayajathibitishwa!Masua alikuwa wakala wa idara hiyo ya usalama mwenye mafunzo ya hali ya juu.Kufa kwa sumu ya panya ilikuwa kama tusi kwao.Tena kafia nyumbani kwa Laredo alipofia kwa sumu kulitangaza vita kati ya Laredo na idara hiyo!Kimafunzo alifundishwa kuwa makini sana sio kila chakula ale hovyo.Sasa siku ile anakutwa kafia kwenye nyumba ya mtu kirahisi lilikuwa jambo la kushtusha sana kwa upande wao!

Laredo pekee ndo mwenye majibu ya kifo chake ilikuwaje wakala huyo akauawa kwa sumu wakati ni mtu imara!Isitoshe alikuwa na kazi kapewa muhimu na alitakiwa kupeleka taarifa sasa kufa kwake ghafla kulileta mushkili katika kazi aliyopewa ikiwa alikatishwa uhai na hao aliotumwa kuwachunguza au?Hapo mkono wa Laredo ulitiliwa shaka sana!

Laredo alipopata fahamu alijikuta aking’atwa na kunguni waliokuwa kwenye lile shuka!Hilo lilizidisha hasira na maumivu kwa sana.Njaa ilimkereza tumbo!

Alitupa lile shuka pembeni kwa hasira!Alibaki anajikunyata kwa uchungu mwili wake ukiwa na baridi la uhakika!Meno yalichezacheza utadhani mtu anachapisha barua kwa mlio yaliotoa!

Kwa baridi lile pamoja na maumivu yakuadhibiwa hakuweza kabisa kufikiria jambo lolote zaidi ya kulia kwa shake!Akili ikaganda tena kama siku ile ya tukio!Picha za mwanaye zilipita kichwani akikumbuka jinsia alivyokuwa anamfyatulia bastola hapo alijikuta akisononeka sana!Alikosa tumaini la kuishi!Ikapita tena picha ya waume zake na maisha yaliyojaa mahaba tele.Alikumbuka alivyoweza kuwashawishi waume wote waweze kushiriki naye mapenzi kwa kumuoa!Yalikuwa maisha matamu yenye kumridhisha yeye mwenyewe!Kweli mambo yamebadilika sana na leo imekuwa kwake!

Kumbukumbu pekee ndo kitu akili iliweza kukileta.Katika kumbukumbu zile alijaribu kupotezea baridi lile lakini hakufanikiwa bado lilimgandisha.Mtetemo wake ni kama mtu mwenye uraibu wa kutumia madawa ya kulevya!Alijikuta akiweweseka!Ukasikika ukelele,”AAAH!” mkali kama mtu kukanyaga kaa la moto au nguruwe kupigwa na mkuki wa ubavu!Alijikuta akiangalia chumba kizima asijue sauti ile inatokea wapi!Alihisi manyezi yakimfuatilia japo alikuwa peke yake!Chumba kikamuogopesha sana asijue anaanzia wapi na anaishia wapi?

Hakuna mtu alikuwa mwenyewe!Halafu akaisikia sauti ya mwanaye,”Mamaa nimeleta ripotii!”sauti ilikuja kwa mwangwi na chumba chote kumsisimua maradufu hadi akahisi anaishiwa na nguvu nakujikuta akapwaya mikono yake kwa mshtuko!

“Mamaaaa!”sauti ilizidi kuita katika saikolojia yake!Utulivu uliokuwepo pale ndani haukuwa wakawaida!Katika tukio lile la kuogofya akashangazwa zaidi kwa kusikia sauti nyingine ikija katika mawimbi yale,”Bebii!...Njoo mpenzi wangu…Nimekuletea lolpop!”zote zilikuwa tatu zilizokuja kiutofauti.Aliweza kuzitambua vizuri sana!Zilikuwa za kina Hamza,Masua na Bario baba lao!Uoga uliingia hadi kwenye mishipa ya fahamu nakujikuta akiwa na presha ya kupanda ya uoga!

Pumzi ikawa nzito nakifua kuanza kumbana!Alihisi kushindwa kupumua!Mambo yalikuwa yamebadilika na mateso kuwa mazito sana kwa upande wake!.Uoga hauna urafiki!Ukiukumbatia unakumaliza!Alikumbuka matisho hayo!Akiwa pale na kitetemeshi alihisi mtu kumsimamia!Kulikuwa na harufu kali ya marashi ikinukia!Utuli uliosheheni chumba chote kama dhoruba!Alijikuta akigeuza shingo nakuona mwanamke kasimama mbele zake!Ni mwanamke yuleyule aliyemtokea Bario akiwa kazini kwake!

(REJEA UPEPO WA USIKU 4 kujua kisa cha mwanamke huyo atamfanyaje Laredo!)
 

Attachments

  • UPEPO USIKU.jpg
    UPEPO USIKU.jpg
    51.5 KB · Views: 96
UPEPO WA USIKU-24

BONIFACE BIRAGE

Laredo nywele zilisisimka kwenye mizizi yake ubongoni!Mwanamke mbele yake alikuwa kama shombeshombe.Harufu kali ya manukato ilizidi kuchanja mashimo ya pua zake nakumfikia hadi kwenye mlango wa ufahamu wa harufu!Laredo hakujua mwanamke huyu ameingiaje humu ndani kwani hakuwa amesikia mlango ukifunguliwa.Japo hali yake haikuwa kawaida napengine asingesikia ujio wa mtu kuingia hapo lakini hilo lisinge kuwa suluhu kwamba hajasikia mtu kuingia katika chumba kile.

Mwili wake ukachemka kwa woga wa hali ya juu!Mwanamke Yule alimsogelea karibu huku akimwangalia Laredo kwa makini kana kwamba anataka kitu.

Pengine akili yake ilikuwa imezama sana kiasi cha kuanza kuona ambavyo hatakiwi kuviona.Lakini cha kushangaza picha ya mwanamke Yule ilianza kama kufifia kiasi cha kuona upande wa pili.Yaani alimuona kama karatasi la nailoni au kioo unachoona upande wa pili.Hilo likamuogopesha sana!

Kizuu si kizuu kwa tafsiri ya haraka iliyokuja ubongoni mwake.Lakini katika lile bumbuazi alishtukia Yule mwanamke akimkazia macho bila kumwambia lolote!Halafu akafunua baibui lililokuwa limeufunika hadi mdomoni kiasi cha kuach macho tu.Alifunua kiasi cha kuacha mdomo uonekane!Hapo akajikuta akitetemeka sana kuliko alivyodhani yeye mwenyewe!Aliona kitu cha kuogofya kwamba mwanamke Yule alikuwa na kinywa kama cha paka sip aka lakini manyoya yalionekana dhahiri usoni!Hilo likamleta kwenye kitetemeshi kikubwa sana hadi akajikuta akiamka nakusimama akakimbilia mlangoni!Alitaka kuufungua mlango atoke nje lakini akashindwa hajui afanze jambo gani!

Mara akaona mguu ukichomoza kutoka nyuma ya Yule mwanamke kana kwamba kuna mtu alikuwa amesimama nyuma yake.Mguu ule ukatokea kwa mbele yake halafu huyo aliyechomoza mguu akatokea!Alikuwa ni Hamza!Mwili wake ulioneka vilevile alivyokuwa mara ya mwisho na uso wenye kuonesha maumivu makali sana huku kwenye kingo za mdomo kukiwa na michirizi ya kitu kama povu!Bila shaka ni tapiko la kudhuriwa na sumu!Kizaazaa kikaibuka!

Laredo alipigapiga ule mlango akitaka ufunguke lakini wapi mlango haukufunguka hata kidogo!Halafu akahisi kama miguu yake imeshikiliwa na kitu kizito kwa kichini nailikuwa kama inamvuta!Ilikuwa mikono yenye ubaridi kuliko vile alivyokuwa na baridi!Kifua kilichombana kilizidi maradufu huku pumzi ikiwa janga la upumuaji!Ni kama uimara wa mikono iliyomshika miguuni ilikuwa imemiminwa zege ya kutosha!Bimkubwa alipoteza data za kichwa chake!Huyu hapa mwanamke wa ajabu mwenye wajihi wa kutisha halafu nyuma yake katokea Hamza ambaye ni marehemu!Mzuka si mzuka hakuelewa!

Walianza kumsogelea karibu!Laredo alitapatapa akipiga mlango ufunguliwe!

Mara mlango ulifunguliwa Laredo alimparamia aliyeufungua akitaka kutoka lakini akawa amesukumwa kurudi ndani!

“Niacheeniii!”alipiga kelele.

“Unataka kwenda wapI?”ilikuwa sauti ya Linda yenye ukali!
“Sikai humu ndani!”alizungumza kwa shida sana maana kifua kilikuwa kimembana vya kutosha!

“Hutoki humu ndani nimesema!”ilikuwa sauti ya Linda ikifoka.

Laredo alipogeuza macho kuangalia wale watu wawili waliomtisha akakuta hakuna mtu!Na ile mikono iliyomshika miguuni ikawa kama imeyeyuka!Alistaajabu sana!Alibaki akitetemeka kama kifaranga cha kuku!Hata kubishana na Linda hakuendelea tena!

“Nataka uniambie ukweli ulitumwa na nani kumuua Masua?”Linda aliuliza huku akiwa amekunja uso.Alitoa bastola kwenye kiuno chake kisha akamshikia bibi huyu usoni!

“Nitasema ukweli!”alijitetea Laredo!Huku akizidi kuwa na hofu kuu,”Masua alikuwa mume wangu!”

“What?’’ akashtuka mwana Linda huku wivu ukichepuka kutoka uvungu wa moyo wake.Anakumbuka vizuri kwamba huyu mwanamke alikuwa mke wa mtu sasa iweje aseme Masua alikuwa mume wake!Lakini kabla Laredo hajaendelea chochote alijikuta akipoteza fahamu nakuanguka chini!Linda aliimuwahi pale chini nakuhisi mapigo ya moyo wake yalikuwa chini sana!Aliinua bastola yake nakuwa tayari kumuua palepale!Lakini akairudisha kiunoni kisha akaona bora nitumie mikono kummaliza huyu fis!Aliikamata shingo ya Laredo ambayo kwa sasa ilikuwa dhaifu sana!Akawa anapiga mahesabu yake alijua akimkwida vizuri palepale anamuua kabisa!Huyu ndoa aliharibu kabisa penzi lake kwa Masua!Kumbe wakati Masua ameanza kumpotezea huyu hayawani alikuwa anamfaidi!Kilichomuuma zaidi nikuwa mke wa mtu ndo kaja kumuibia mchumba wake akidai ni mume wake!Hapo akakumbuka kuna nyaraka nyingi zilichukuliwa kutoka nyumbani kwa Laredo na bado alikuwa hajazikagua baadhi!

Alichofanya nikuishika tena shingo akajikaza kwa nguvu zote nakuanza kuiminya shingo ya Laredo kwa nguvu zote!Ilikuwa ni ndani ya sekunde thelathini tu angekuwa amemaliza kazi lakini alikomea sekunde ya kumi natano!AKaghairi.

“We mbwa una maswali mengi ya kunijibu!”alisema akimuachia klsha akaita timu ya wataalamu wa afya ambo alimchukua Laredo kwa haraka nakuondoka naye kwenda kwenye chumba cha matibabu.Ilibidi ashughulikiwe palepale maana hawakutaka aende hospitali ijulikane alifanyiwa mateso ya hali ya juu jambo lisiloendana na haki za kibinadamu!

****

Linda alirudi kwenye zile nyaraka nakuanza kuzikagua moja moja!Alipitia hatua kwa hatua hata asijue anatafuta nini!Lakini akiwa ofisini kwake mlango ulifunguliwa akaingia wakala mwingine.Huyu alimpa jukumu lakukagua ile tattoo aliyochora Laredo!

“Ni kweli!Huyu binti ni shushushu!Inawezekana kweli alitumwa kummaliza Masua!”alisema wakala!
 

Attachments

  • UPEPO USIKU.jpg
    UPEPO USIKU.jpg
    51.5 KB · Views: 86
UPEPO WA USIKU-26

BONIFACE BIRAGE

Imethibitika bila hiyana wala visingizio kwamba kuna hati tatu za usajili wa ndoa kati ya Laredo na hawa waume watatu!Haikuingia kichwani zaidi ya kuacha mkururo wa maswali bila majibu ya kuridhisha.

“Aliolewa na wote watatu.”

“Aliwezaje kuwashawishi waume zote nao wakaingia mkenge wa mambo haya?”aliuliza Linda akiwa nazidi kuingiza ukweli huo kwenye ubongo wake!Kugundulika kule kulizidi kutia shaka kuu!

“Niliishi nao wote na wote waliridhika bila hiyana.”alisema Laredo kana kwamba maelezo yale aliyasoma kwenye kitabu.Linda alibaki kutumbua macho kwa mshtuko wa kisa kile.Huyu alifanya kitendo kilichokigeni kwa mwafrika.Wengi hufanya hivyo kwa kujificha bila kujulikana na yeyote lakini huyu katekeleza jambo hilo waziwazi nakuwafanya wanaume wale wacheze ngoma kwa mapigo aliyotaka yeye!Walitibwirika kwa kweli.

“Hukushikwa na hatia kufanya wanaume wote kitendo hicho?”

“Niliwapenda wote nisingeweza kuwaacha.Nisingeishi bila mwingine.They were mine alone to love.”alisema kwa kujiamini huku akihisi uchungu wa kuwapoteza wanaume wale!Alihisi uchungu mkuu wa makiwa yakija kama mawimbi nakuusomba moyo wake wa nyama kisha kuupelekesha kwa mwendo kasi huku pumzi ya kupenda iingiwa vumbi lenye kuleta mafua!

“Tulipendana sana.One happy family.Only us with unconditional love!”alijitetea huku akiwa katika hali yake ya kukumbukia siku za kupendwa kwake.Siku zake za mapenzi zimepotea kabisa kwenye ramani.

“I want to kill you Laredo!”alisema Linda akibubujikwa na machozi.Hali ya kutishiwa ilimfanya Laredo amgeukie mshitaki wake nakumwangalia.

“Nastahili kufa kuwafuata waume zangu ahera.Niishi nao katika ulimwengu wapili.”alisema.Mtu awapo huzuni hutazamia kisichokawaida kuwa kawaida.Linda alizidi kukereka sana na kauli za mwanamke huyu!Alitamani amwadhibu vilivyo kisawasawa.Kumrubuni Masua nikumwingiza mtu huo kwenye himaya isiyokuwa yake.Japo maelezo ya Laredo bado hayakukidhi ushawishi kwa upande wake kwamba hakuhusika na mauaji ya watu watatu waliokufa kwa sumu bado alimuona muuaji.Kama aliweza kuwarubuni wote wamuoe alishindwaje kuwafutilia mbali.Kuwaweka waume watatu nyimba moja na bado ukawa unatembea nao nikununua hatari ambayo ingelipuka muda wowote ule!Hilo lilionekana waziwazi.Japo Laredo hakusema kama anamuhisi Hamza kugusia mambo ya kuuana lakini hata angemtaja bado alimpenda na mapenzi ya ulimwengu wake yalimfanya upofu kiasi kila alichohisi tatizo hakuona sababu ya kukisema.Alimeza siri za mashaka yake.

Wakiwa pale aliingia dokta wake,”Oh Linda afadhali nimekuona.”

Linda alimtizama dokta huku akifuta machozi yaliyokuwa usoni mwake,”Sema dokta.”

“Huyu anatakiwa apelekwe hospitali ya mkoa.Hali yake hainiridhishi kabisa.Nimeshafanya taratibu zote kutoka juu nimepewa maagizo nimpeleke hospitali.”

“Muuaji atibiwe zaidi?’’alihoji Linda.

“Bado katiba inamlinda.Hajapelekwa mahakamani not yet my dear.”

Linda aliongozwa na hasira zake akatoka kwa haraka nakukimbilia ofisini kwake.Alikuwa na ghadhabu sana dhidi ya Laredo.

“Linda najua unataka kulipiza kisasi.Sasa kwanini unalia?”

“Huyu Malaya kaniharibia maisha yangu kaninyang’anya mchumba wangu kamfanya mbwa wake.Yaani Masua niwa kuja kushare mwanamke na afriti huyu?”alitamka kwa kukerwa sana.

“Hutokea mambo kama hayo lakini hatuna budi kuyakubali.Mimi nafurahi akipelekwa hospitali.Huko ni sehemu salama ya kummalizia kabisa.Tutavamia usiku nakummalizia.”alisema James akimfariji Linda.Waliangaliana hali iliyofanya James amsogelee Linda nakumkumbatia kumpooza.Walitumia muda kupanga jinsi watakavyovamia hoaspitali hiyo nakumfutilia mbali Laredo kwa lengo lakulipiza kisasi.Mpango wao ulichukua kikao ccha saa mbili.Baada ya makubaliano hayo walitawanyika nakuendelea na shuguhuli zao.Huku kichwani wakijiuliza tukiop litakavyokuwa.

Masaa yalipita ilipofika mida ya usiku saa tatu walikuwa tayari wamejiandaa kwenda kwenye uvamizi wao.Uvamizi ambao ungehitimisha uhai wa Laredo.

***

Injini ya gari ilisimama baada ya safari kufika tamati.Walishuka katika geti la hospitali.Walivalia kistaarabu wala usingedhani wamekuja kwa shari.Misheni waliyoenda ilikuwa yakujitoa mhanga na kwa namna moja au nyingine isingeishia pazuri lakini msukumo wa kuibiwa penzi na hasira za kumpoteza mchumba wake zilimtuma Linda afanye jambo kinyume na taratibu za kazi!Alidhamiria kwa kweli na angefanikisha.

“Habari sisi ni maafisa usalama tuna mgonjwa wetu tunaomba tumwangalie alisema James akitoa kitambulisho chake hali iliyofanya mlinzi kuwa mwepesi japo kitaratibu za kazi hakutakiwa kuwaruhusu lakini alijikuta akiwaachia bila hata ya kukagua vielezo vyao.Pengine wanajukumu lao aliwaza mlinzi huyo.

“Wakubwa piteni jamani ndani.”alisema mlinzi akiwaruhusu.Walipita wakimwachqa mlinzi Yule akimomonyoa mapande ya mkate pamoja na chai!Mishipa ya shingo ilikaza akitafuna.Linda na James walielekea maana walijua atakuwa wodi namba ngapi.Walielekea moja kwa moja hadi ndani walikatiza korido kadhaa hadi walipofika mlango wa chumba alicholazwa cha binafsi.Walipotokeza kwenye korido ile walishtuka kidogo kusikia kitu kama mtu anakoroma.Ilikuwa sadfa!Wakaangalia kwa kuchungulia nakuona korido ilikuwa pweke isipokuwa afisa wa usalama aliyekuwa anamlinda Laredo alikuwa anakabwa chini na mtu mwenye kushiba aliyepanda hewani!Linda alichomoa bastola yake kwa haraka!Kabla hajafanya lolote alishtukia akisikia kitu kikimgonga James kisogoni na James kuanguka pembeni.Wakati anageuka kwa haraka akahisi kitu cha baridi kikigusa shingo yake!Mwili ukasisimka!Hapo alijua fika ni bomba la bastola ikimaansha kosa moja tu kwisha habari yake!Huwa hapendi kushtukizwa na kuzidiwa akili!Akainua mikono juu akiachia bastola yake iporomoke chini!
 
ivi hapa amna arosto nisije anza kusoma nkaachwa na ham akati imenoga
 
UPEPO WA USIKU-27

BONIFACE BIRAGE

Linda alikasirika sana kushtukizwa huko kwa adui aliye nyuma yake!

Alijaribu kujiuliza atakuwa nani kavamia hospitalini pale na kwa madhumuni gani?Hilo likamzidishia hasira!Ina maana hata hapa sisalama.Na kwanini mlinzi wa Laredo aakabwe.Tayari aliyekuwa akimlinda Laredo aliachiwa huku akiwa atikisiki hakuwa na fahamu!Alikabwa vilivyo.Mkabaji aliinuka kuthibitisha kazi kwisha.Mwili wake ulijaa misuli tinginyaa!

Wakamfuata Linda nakumwangalia usoni kisha akampiga kofi!Linda alichukia kuwekwa chini ya ulinzi alipiga mahesabu ya kuwadhibti akaona hata kama wamzidi lakini nay eye lazima azirushe.Akachepuka kwa teke lililompata bwana mkubwa kwenye tumbo.Kisha akageuka haraka kukabiliana na aliyemshikia bastola!Alirusha teke kumnyang’anya ile bastola kwa kupiga mkono ulioshika bastola kwa nguvu!Hakufanikiwa kuiondoa bastola!Adui yake alichukizwa na kitendo hicho akawataanaelekeza kidole kwenye kishikizo cha bastola tayari kufyetulia risasi ya uhakika!Lakini kufyetua risasi hospitali nikuzusha ghasia ambayokuizima ingekuwa mziki.Lakini pia bora aizushe ilipurukushani ziwape nafasi ya wao kufanza kile walichodhamiria!

Palepale akamtwanga Linda Linda risasi ya tumbo!Moja!Mshindo wa risasi ile ulitikisa hospital nzima!Paa!Linda alijishika tumboni nakuhisi maumivu makali yakipenya kwenye tumbo lake.Alipojishika tumboni kuangalia akakumbana na michirizi ya damu ya moto!Mwili ukaanza kufifia nguvu!Alianguka chini.Wale watu wakaendelea kumnyooshea bastola.Kwa haraka wakaziruidisha bastola zao kwenye viuno vyao.Kwa haraka wakausogelea mlango nakuugonga.

“Tokeni tayari!”alitamka mmoja wao.Waliopo ndani wakatoka wakiwa wamemshika Laredo huku na huku.Laredo alikuwa akitetemeka.Walitoka naye nakukatiza korido zilizoanza kufurika watu wakipiga kelele wengine wakikimbia kufuatilia mlio wa risasi!Tayari utulivu kwa usiku ule uliondolewa na mlio wa bastola!Wengine wakilia wengine wakikimbia maana hakuna aliyejuua ambacho kingefuata.

Laredo alitolewa hadi nje nakuonekana kama moja ya watu wanaokimbia mlio wa risasi.Alitoka moja kwa moja hadi nje ya jingo la hospitali.Walikimbia nakuelekea getini.

“Munaenda wapi?”aliuliza mlinzi mwenye lafudhi ya kimasai.

“Mlio wa risasi nani akae?”alitamka moja ya waliomshikilia Laredo.Mlinzi naye akawaamemeza hilo.Akawaachia wakimbia nje.Walifanikiwa kufuka nje ya geti wakafuata gari lao ambalo lilikuwepo mita chache kutoka walipo.Ni mwendo wa kukimbia.Waakalifikia gari.Mlango ukafunguliwa Laredo akatupwa ndani kisha gari likafungwa wakaondoka mbio.Lilikuwa tukio hatari sana kufanyika.Mtuhumiwa anaondolewa mikononi mwa usalama wa taifa na watu wasiojulikana.Linda kaja kumgeuka Laredo anakutana na watu waliokuja pia kwaajili ya Laredo!Sadfa.

Hilo likawa lina changanya sana.Laredo akapoteza fahamu pasi nakujijua kilichotokea ni kitu gani.

***

Mlio wa risasi katika hospitali uliwatisha wengi hadi polisi wakaitwa.Ndani ya muda mfupi hospitali nzima ilikuwa imejawa na uwepo wa polisi.Ukaguzi uliendelea ikiwa ni pamoja nakusaidia kuwatoa hofu waliopo hosipitalini.Tayari alionekana Linda akiwa amepigwa risasi.James alirejewa na fahamu na wakaogopa kujitangaza kabla ya kujua hatma ya Linda ni nini?Ilibidi Linda afanyiwe matibabu ikiwamo upasuaji mdogo wa kuondoa rasasi iliyozama tumboni.

Kwa kuwa hakuwa haikuwa imegusa sehemu hatari waliweza kuiondoa risasi ile na hali ya Linda ikawa salama.Kazi ilikuwa kuelezea ilikuwaje Linda akapigwa risasi hospitalini usiku.

James alienda kituoni kutoa maelezo kwa kuwa yeye pia alikutwa katika hali ya hatari.

***

“Ilikuwaje mkawa hapo usiku ule?”
“Tulikuwa na mgonjwa wetu?”

“Muda wa kuona wagonjwa ni saa tatu usiku?”aliuliza ofisa wa polisi aliyekuwa anamhoji bwana James.

“Hapana mkuu.”James hakupenda maswali yale.

“Sasa ulikuwa unafanya nini hapo hadi mwenzako akapigwa risasi?”

“Hatuwajui waliotuvamia.”alisema James dhamira ya kumwambia bosi wake aje amtoe pale kituoni na asihojiwe ilimkaba kooni.Alitakiwa kukwepa kitanzi kile haraka sana.Hawezi sema walienda kumuona Laredo maana kazini hakukuwa na lolote lakuwapeleka pale.Hata kama ingekuwa usiku.Pengine angetumia kete kwamba walipata taarifa za kiintelijensia kwamba Laredo angechukuliwa au walichezwa tu na machale.Lazima swali lijibiwe kwanini wamfuate usiku kama ule.Sio tu polisi wangekuwa na maswali dhidi ya Laredo kuchukuliwa hospitali bali hata wao wawili wangetakiwa kusema kwa mabosi wao ilikuwaje.

Ishu hii ya Laredo ilianza kuwagharimu kwa yeye kuchukuliwa mikononi mwa usalama wa taifa tena kwa kutekwa!Hiyo ilimuuzi sana!Alimwangalia polisi halafu kwa ujasiri huku akijua kuna utata mbeleni.

Mkono mmoja uliingia mfukoni akatoa kitambulisho chake nakukiweka mezani.

“Usalama wa taifa tulikuwa katika oparesheni maalum.Sihitaji kuingiliwa tafadhali.”alisema James kw kujiamini.

Afisa wa polisi alionesha kama kumuelewa namna Fulani.

“Naweza kuongea na mkubwa wako?”
Hilo likamtia shaka sana James maana kadri atakavyozidi kuhojiwa watatilia shaka ujio wake na Linda pale kituoni.Hawakwenda kwa shwari walienda kwa shari!

“Natakiwa nimpelekee ripoti tayari mtuhumiwa wetu katekwa.Sihitaji habari hii itoke kwenye vyombo vya habari itaingilia oparesheni zetu.Nahitaji usiri wa hali ya juu.”alisema James akiwa makini.Afisa polisi alimwangalia akijishauri amwachie au la.

“Lakiini nitakuhitaji kwa maswali zaidi.Maana tukio limetoke sehemu ya umma lisipokuwa na majibu nikuchafua jina letu.”alisema afisa wa polisi.Mabishano yaliendelea kwa muda Fulani hadi alipoachiwa.
(POLENI KWA KUICHELEWESHA)
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom